Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

BODI YA WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR WATEKETEZA DAWA ZA MENO

$
0
0
Na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Wafanyakazi kutoka Bodi ya Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar wameangamiza Tani tisa za Dawa ya meno aina ya Aloe zilizoharibika katika jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja

Dawa hizo ziliingizwa nchini na Kampuni ya Bacelona Interprises Limited zikiwa zimeharibika baada ya kontena lilikuwa na dawa hizo kuinga maji wakati wa kusafirishwa kuja Zanzibar .

Mkaguzi Mkuu wa Wakala wa Chakula Dawa Zanzibar Mwadini Ahmadi Mwadini alisema walibaini kuwa dawa hizo zimeharibika wakati wa kuzitoa bandarini na kumshauri mmiliki wa dawa hizo kuzirejesha zilikotoka au kuziangamiza na alikubali ziangamizwe ili kujiepusha na gharama nyengine.

Mwadini alisema Bodi inaendelea kufanya ukaguzi kwa bidhaa zinazoingizwa bandarini na  maduka mbali mbali ili kuhakikisha zinakuwa salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

Aliwataka wafanyabiashara kuwa waangalifu wanapoagiza Bidhaa na kujenga ushirikiano wa karibu na Bodi yake kwa kutowa taarifa wanapoona bidhaa zao zinamashaka kuuzwa kutokana na kuharibika au kupitwa na muda wake wa matumizi.Aidha aliwaomba wananchi wanaponunua bidhaa madukani  na kuzigundua kuwa hitilafu watowe taarifa katika Bodi ili hatua zinazofaa ziweze kuchukuliwa kwa usala wao.       

“Kama mukigundua kunafanyika udanganyifu kwa bidhaa mnazonunua kama kuharibika au kupitwa na wakati musisite kutoa taarifa kwetu, tupo kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi.” alisema Mkaguzi Mkuu.  
 Wafanyakazi wa Bodi ya Wakala na Dawa Zanzibar  wakiteremsha dawa za msuaki tani tisa zilizoharibika katika jaa la kibele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kuangamizwa.
 Maboksi yaliyokuwa na dawa za msuaki zilizoharibika yakichomwa moto na wafanyakazi wa Bodi  ya Wakala na Dawa Zanzibar katika jaa la Kibele, Wilaya ya Kati Unguja.
 Gari aina ya kijiko likisaga dawa zilizoharibika ili kuziangamiza baada ya kuingia maji wakati wakusafirishwa katika jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.Picha na Ramadhani Ali – Maelezo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Embassy of Kuwait in Tanzania Committed to Support Educational Projects in Zanzibar

$
0
0
The Ambassador of Kuwait to Tanzania HE Jassim Al-Najim handing over the computers and printers to the guest of honour, Deputy Minister of Education in Zanzibar Hon Mmanga Mjengo Mjawire at the center. Seen on the right, is the member of the House of Representative of Tunguu Hon Simai Mohammed Said
Happy faces, The Ambassador of Kuwait with various leaders from Tunguu Constituency and government officials as he officially hands over the 20 Computers and 10 printers worth 23,287,000/- SHS
As a token of appreciation, the teachers and students of Tunguu rewarded MADAFU (Coconut Juice) as a present on behalf of the people of Tunguu to the Ambassador. 
Member of the Union Parliament and House of Reps for Tunguu Constituency Khalifa Salim Suleiman ( MIMINA ) and Simai Mohammed Mohammed Said ( MPAKABAS) bidding farewell to the guest of honour from the Revolutionary Government of Zanzibar Hon Mmanga Mjengo Mjawire


WAHITIMU WA MAFUNZO YA MGAMBO GAIRO WATAKIWA KUISHI KIAPO CHAO CHA UTII KWA MATENDO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe amewataka wahitimu wa mafunzo ya mgambo kukiishi kiapo cha utii kwa matendo na si maneno. 

Hayo ameyazungumza leo Disemba 16, 2017 wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya mgambo ambayo yalifanyika katika Kata ya Rubeho halmashauri ya wilaya ya Gairo ambapo mgeni rasmi aliwaasa wahitimu kutii yale yote waliyofundishwa ili kujenga uchumi wa Taifa. 

Katika hotuba yake Mhe. Mchembe aliongeza kuwa mgambo wanapaswa kutumia elimu waliyoipata ili kuinua uchumi wao na jamii inayowazunguka bila kuwaonea au kuwatesa wananchi. "Nawaombeni sana ndugu zangu mafunzo mliyoyapata ni muhimu sana katika taifa letu ni vyema sasa na nyie mkayaishi yale yote mliyofundishwa kwa kipindi cha miezi mitatu mliyoshiriki," alisema Mhe. Mchembe. 

Aliongeza kuwa ni vyema mgambo wakawa mabalozi wema wa amani na si wao wawe mstari wa mbele katika vitendo vya rushwa, unyanyasaji wa wananchi na kuepuka kujihusisha kwenye uharifu kwa kukodisha magwanda yao. Mhe. Mchembe aliwataka viongozi wa wilaya kufanya usaili tena kwa wale mgambo wote ambao wameshapitisha miaka 10 ili waweze kurudi kupata mafunzo zaidi.

"Kazi hii ya mgambo inahitaji kuendelea kujifunza mara kwa mara hivyo nawaomba viongozi wote fanyeni upya usaili wale wote ambao muda wa miaka 10 umepita warudie katika mafunzo waweze kuongeza ujuzi zaidi," alisema Mhe. Mchembe. 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Rubeho akikagua gwaride. 
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo. 
Mshauri Jeshi la Akiba Gairo, Major Balitoga akitoa machache mbele ya mgeni rasmi. 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Rubeho akikagua gwaride. 
Wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo wakipita mbele ya mgeni rasmi kwa gwaride la kutoa heshima. Na Kajunason/MMG. 



RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA MISA YA JUMAPILI KANISA KUU LA MT. PAULO WA MSALABA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na Mapadri baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
 Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU MJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha kikao KAmati Kuu ya chama hicho ukumbi wa mikutano wa White House mjini Dodoma leo Desemba 17, 2017.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Dkt John Pombe Magufulia akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho  (Zanzibar),Dkt Shein
Katibu MKuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akizungumza jambo kabla ya kikao cha Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi kuanza ndani ya ukumbi wa mikutano wa white House mjini Dodoma leo Desemba 17,2017.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Kamani Kuu ya CCM wakipiga makopi ya kumkaribisha Mwenyekiti wa chama hicho,Rais Dkt John Pombe Magufuli kabla ya  kuanza kwa kikao cha Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi ndani ya ukumbi wa mikutano wa white House mjini Dodoma leo Desemba 17,2017.

PICHA NA IKULU

WAKAGUZI MIGODI KUPUNGUZA AJALI MIGODINI

$
0
0
Wakaguzi wa Migodi Nchini wameagizwa kutembelea mara kwa mara kwenye migodi hususan ya wachimbaji wadogo kwa ajili ya kukagua hali ya usalama na kuwasaidia Wachimbaji kuepusha ajali wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.

Agizo hilo limetolewa Desemba 14, 2017 Mkoani Tabora na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alipotembelea kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilaya ya Kaliua ili kujionea shughuli zinazofanywa mgodini hapo na kuzungumza na wachimbaji.

Baadhi ya Wachimbaji walimueleza Naibu Waziri Nyongo kuwa wamekuwa wakifanya shughuli zao katika mazingira magumu bila kuwa na elimu ya namna bora ya uchimbaji wa madini.

Nyongo alisema ni jukumu la Maafisa Madini wakiwemo Wakaguzi wa Migodi (Mining Inspectors) kuhakikisha wachimbaji hususan wadogo wanapatiwa elimu ya mara kwa mara kuhusu afya, uchimbaji salama na uhifadhi wa mazingira ili kuepusha magonjwa na ajali zinazosababishwa na uelewa finyu wa uchimbaji bora.

“Wachimbaji wadogo wanapaswa kutembelewa na kuelimishwa mara kwa mara na hili ni jukumu lenu, msisubiri hadi kutokee madhara ndio mfike kutoa elimu,” alisema.Aidha, Nyongo aliagiza wamiliki wa machimbo kuhakikisha wanawapatia vitendea kazi wachimbaji kwenye maeneo yao ili kuwalinda na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza kwenye mkutano na Wananchi na Wachimbaji Wadogo kutoka Kata ya Silambo Wilayani Kaliua (hawapo pichani).
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akielekea kwenye machimbo ya dhahabu yaliyopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kutoka kulia) akitazama moja ya shimo la dhahabu lililoko katika Mgodi wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele) akiongoza ujumbe wake kukagua shughuli za uchimbaji wa dhahabu kwenye mgodi wa dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.

HABARI ZAID BOFYA HAPA

Ukoo wa Patel wachangia shilingi 22,500,000/= kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi ya JKCI

$
0
0
Ukoo wa Patel umekabidhi kiasi cha shilingi 22,500,000/= fedha ambazo zitatumika  kwaajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Akikabidhi fedha hizo leo Mwenyekiti wa Ukoo huo Harish Patel alisema watoto wengi wanazaliwa na ugonjwa wa moyo na wengi wao hawana fedha za kulipia matibabu wameona kwa kidogo walichokipata kisaidie kulipa gharama za matibabu ya wagonjwa hao.

“Kila wakati, kila mwaka kutokana  na kipato tunachokipata tumekuwa tukisaidia jamii katika mambo mbalimbali ikiwemo  elimu na afya na leo hii tumeona furaha zaidi kusaidia watoto”,  alisema.

Akipokea fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI  Prof. Mohamed Janabi aliushukuru Ukoo wa Patel kwa kuona umuhimu wa afya ya mtoto na kusaidia kulipia gharama za matibabu na kuziomba Taasisi, Mashirika na watu binafsi wenye uwezo wajitokeza  kulipia matibabu ya watoto.

Prof. Janabi alimalizia kwa kusema kuwa  watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo ni wengi   kati ya watoto milioni mbili wanaozaliwa asilimia moja (1%) wanazaliwa na matatizo ya Moyo hivyo bado fedha zaidi zinahitajika kwa ajili ya matibabu.
 Mwenyekiti wa Ukoo wa Patel,  Harish Patel akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= fedha zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na ukoo wa Patel pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo mara baada ya kukabidhiwa  mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
  Ukoo wa Patel ukiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  kukabidhi  mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Mkurugezi Mtendaji wa Taasisis ya Moyo Jakaya Kikwete (JKI) Prof. Mohamed Janabi akongea na waandishi wa Habari mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi shilingi 22,500,000/= na Ukoo wa Patel , fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Picha na JKCI.

DC GONDWE:AWATAKA WAZAZI KOROGWE KUCHANGAMKIA MPANGO WA TOTO AFYA KADI

$
0
0
KAIMU Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa Toto Afya kadi uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mazoezi wilayani humo kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Tafa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe,Rehema Kwasi
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza katika uzinduzi huo kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni anaye fuatia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe,Rehema Kwasi
Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe,Rehema Kwasi akizungumza wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Godwin Gondwe kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe,John Nyarongo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Mji,Jumanne Shauri akizungumza wakati wa uzinduzi huo.


WASAMARIA WEMA WAKITOA MSAADA KWA MWENDESHA BODABODA

$
0
0
Wasamaria wema wakimsaidia mwendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda yenye nambari MC307 BPG (jina halikupatikana) amabaye alidondoka chini baada ya kuganga kwa nyuma gari dogo aina ya Toyota RAV 4 nambari T924 BPG kwenye eneo la Kanisa Kuu Katoliki la Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Dodoma, Desemba 17, 2017. Wasamalilia Wema hao walimpeleka kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa matibabu. (Picha na Hilary Bujiku wa Ofisi ya Waziri Mkuu)

DK. KIGWANGALLA AFUNGA MAFUNZO YA 15 YA JESHI USU KWA MAAFISA WANYAMAPORI WA TAWA, TANAPA NA NGORONGORO MKOANI KATAVI

$
0
0


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaongoza Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kupiga gwaride la ukakamavu muda mfupi baada ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi. 

Na Hamza Temba-  Mlele, Katavi
...........................................................................

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza wahifadhi wote nchini kushirikiana na wadau wengine hasa mamlaka za Mikoa na Wilaya katika maeneo yenye uvamizi wa mifugo na migogoro ya mipaka ya hifadhi ili kutatua changamoto hizo kwa namna shirikishi ikiwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.


Ametoa agizo hilo jana Disemba, 16, 2017 katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wakati akifunga mafunzo ya 15 ya mabadiliko ya kuelekea mfumo wa Jeshi Usu kwa Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.


“Kazi ya ulinzi wa rasilimali zetu za asili ni yetu na tutaiendeleza, Falsafa yetu ni kuwashirikisha wadau wote, kama kuna taasisi za kiraia kwenye eneo lako la kazi, taasisi za kijamii, mamlaka za mikoa na wilaya, wananchi, halmashauri husika mshirikiane nao ili kupunguza madhara ya operesheni zetu, na zoezi hili la uhifadhi liwe endelevu,” alisema Dk. Kigwangalla.


Aidha, alitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuheshimu Sheria za nchi na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuingiza mifugo, kuanzisha kilimo, makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na matumizi mengineyo.


Awali akizungumzia mafunzo hayo alisema, lengo ni kubadilisha utendaji katika sekta ya uhifadhi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu ambao utaongeza nidhamu, uwajibikaji, uadilifu na maadili kwa watumishi wote wa sekta hiyo ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili za taifa.


MWENYEKITI RAIS DKT, MAGUFULI, PHILIP MANGULA NA DKT. SHEIN WAPITISHWA CCM

MAVUNDE AYATAKA MAKAMPUNI KUFADHILI MCHEZO WA KARATE NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde ameyataka makampuni,viwanda na Taasisi mbalimbali nchini kusaidia kufadhili mchezo wa Karate nchini ambao umeanza kukua kwa kasi hivi sasa.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifungua mashindano ya kitaifa ya Karate katika ukumbi wa Kilimani Dodoma yanayojumuisha Timu za Karate kutoka Mikoa mbalimbali nchini na baadhi ya timu waalikwa kutoka Kenya.

“Wafadhili wengi hivi sasa wameweka nguvi kubwa katika kusaidia michezo ya mpira miguu,pete,wavu na kikapu,ni muda sasa muafaka sasa kuangalia aina mingine ya michezo kama huu wa karate ambao unaweza kutuletea sifa katika medani za kimataifa”Amesema Mavunde.

Awali, akimkaribisha Mavunde, Kiongozi wa Karate nchini Kitte Mfilinge amemuomba Waziri Mavunde kusaidia kuutangaza na kuukuza mchezo huu kwa kushirikiana na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili upate uzito unaostahili kama ilivyo michezo mingine.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde akifungua mashindano ya Karate.

HALMASHAURI 174 ZAPATA DAWA ZA KUANGAMIZA MBU WAENEZAO MALARIA

$
0
0

Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kuzalisha Dawa ya Viuadudu vya Mbu waenezao Malaria Tanzania (TBPL), Mhandisi Aggrey Ndunguru (katikati) akitoa taarifa ya utekelezaji mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu baadhi ya Halmashauri zilizopatiwa dawa ya viuadudu vya mbu waenezao malaria, Wilayani Kibaha Mkoani Pwani 17 Desemba, 2017.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Masoko wa Kiwanda cha Kuzalisha Dawa ya Viuadudu vya Mbu waenezao Malaria Tanzania (TBPL), Bi. Upendo Ndunguru (kushoto) akifafanua masuala mbalimbali mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mikakati wa kiwanda hicho katika kutafuta masoko ndani na nje ya nchi, Wilayani Kibaha Mkoani Pwani, 17 Desemba, 2017.(PICHA ZOTE NA MAELEZO)


Na Mwandishi Wetu, Kibaha-Pwani.

Kiwanda cha kuzalisha Dawa ya Viuadudu vya Mbu waenezao Malari Tanzania (TBPL) kimefanikiwa kusambaza dawa katika Halmashauri zaidi ya 174 nchini zenye viwango vikubwa vya malaria ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali katika kupambana na ugonjwa wa malaria.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa leo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani na Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Mhandisi Aggrey Ndunguru, usambazaji wa dawa hizo umefuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 22 mwaka huu.

Akifafanua kuhusu agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mhandisi Ndunguru alisema kwamba, Rais alizitaka halmashauri zote nchini kununua dawa hizo kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kwasababu kiwanda hicho kimejengwa na Serikali kwa lengo la kupambana na ugonjwa wa malaria.

“Moja ya mambo ambayo Mhe. Rais alituagiza ni kuhakikisha kwamba kiwanda hiki kinatumika kutengeneza dawa za kuua mbu waenezao malaria na pia alituagiza kwamba halmashauri zote nchini zihakikishe zinanunua dawa hizi, na kwamba Serikali ilitenga shilingi bilioni 250 kwa ajili ya kununulia madawa mbalimbali nchini kwa mwaka huu wa fedha”, alisema Ndunguru.

TANESCO yahamasisha Wananchi kutunza Miundombinu ya Umeme

$
0
0
Wananchi Wilayani Igunga mkoani Tabora Wametakiwa Kujenga Tabia na mazoea ya Kutunza miundombinu ya Umeme, kwani kwa Kufanya hivyo kutaifanya Tanzania kuwa nchi yenye Uchumi wa Kati Kupitia Sekta ya Viwanda kutokana na Umeme wa Uhakika.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Tabora na Meneja wa Njia kuu za Umeme, Mhandisi Amos Kaihula, ambapo amesema ni Jukumu la Wananchi Kwenye maeneo yao Kuhakikisha kwamba Miundo mbinu ya Umeme inakuwa Salama wakati wote.

Sambamba na wito huo, Mhandisi Kaihula amewaasa wananchi kukemea kwa nguvu viashiria na Matukio yenye mrengo wa Kuhujumu Miundombinu ya Umeme." Mtu mmoja mwenye dhamira mbaya anaweza kuleta hasara kubwa kwa jamii yote na nchi nzima pale hujuma na wizi wa vyuma unapofanyika katika njia kuu ya umeme na kupelekea nguzo kubwa ya grid ya taifa kuanguka" alisema Mhandisi Kaihula.

“Ndugu zangu, miundombinu hii ya Umeme mnayoiona, imetengenezwa kwa gharama na jitihada kubwa mno za serikali, lakini inapotokea mtu amejaribu kuisogelea miundombinu hiyo, madhara yake ni makubwa ikitokea lile tower (muundo mbinu) limeanguka, umeme wake ni mkubwa mno, na inaweza kuleta maafa makubwa na athari kubwa kwa nchi kiuchumi na kiusalama” aliongezea mhandisi Kaihula.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Igunga Robert Mwagala amekemea vitendo hivyo vya Uhujumu wa miundombinu ya umeme, na kusema Serikali ikishirikiana na TANESCO itafanya zoezi la kubaini wahujumu hao, na watachukuliwa hatua za kisheria.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Igunga Robert Mwagala akizungumza na Wananchi wa Kata hiyo wakati wa Kampeni ya Utoaji Elimu Kwa Wananchi Kuhusu Kulinda Miundombinu ya Umeme ya Tanesco, katika Kijiji cha Mgongolwa Wilayani Igunga mkoani Tabora.

Wakazi wa Kijiji cha Mgongolwa wakisikiliza kwa umakini elimu iliyokuwa ikitolewa na Maofisa wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, kuhusiana na umuhimu wa Kulinda miundombinu ya Shirika hilo.
Baadhi ya miundombinu ya njia kuu ya umeme za Msongo wa Kilovolti 220 na Kilovolti 400 zinazopita katika mikoa ya Singida na Tabora.

UZIKWASA YAZIPA ZAWADI KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI PANGANI

$
0
0
Shindano hilo ambalo lililokuwa linashirikisha vijiji 33 kutokea wiayani humo, limehudhuriwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi.

Awali akitangaza kamati tatu bora zilizofanya vizuri kwa mwaka huu mbele ya mgeni rasmi, mkurugenzi msaidizi kutokea shirika la UZIKWASA Bwana Novatus Urassa alisema, mchakato wa kupata washindi hao ulikuwa mgumu kwa kuwa mwaka huu kamati zote zilionesha ushindani wa hali ya juu katika kutekeleza mipango kazi yao waliyojiwekea.

"Mheshimiwa mgeni rasmi, takribani vijiji vyote 33 vilivyoshiriki shindano hili kwa mwaka huu vilikuwa moto, kwa maana kila kijiji kilikuwa na mpango kazi wake, na kwa asilimia kubwa wote wamefanikiwa kutekeleza mipango kazi hiyo, lakini wapo waliotekeleza vizuri zaidi na tukaona hao ndio watakuwa mfano mzuri kwa wenzao, hivyo mpaka kupata kumia (10) bora haikuwa kazi rahisi, hivyo hivyo mpaka kupata hizi tatu (3) bora pia haikuwa rahisi" alisema Bwana Urassa.

Bwana Urassa alizitaja kamati hizo zilizofanya vizuri kuwa ni kamati ya kijiji cha Msaraza ambacho ndicho kiliibuka na ushindi na kukabidhiwa zawadi ya hundi ya shilingi laki saba, mshindi wa pili ni kijiji cha Mwera ambacho kilipewa hundi ya shilingi laki sita na mshindi wa tatu ni kijiji cha Mkwajuni ambapo walikabidhiwa hundi ya shilingi laki tano.

Mheshimiwa Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Hamidu Awesso akitoa ngao ya ushindi kwa mjumbe wa kamati ya kudhibiti Ukimwi, Jinsia na Uongozi ya kijiji cha Msaraza wakati wa tamasha hilo

Mheshimiwa Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Hamidu Awesso akitoa zawadi kwa kijana bora wa mfano wa kuigwa kwa mwaka 2017 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na kijana Selemani Hamisi kutokea kijiji cha Kimang'a(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Mheshimiwa Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Hamidu Awesso akitoa zawadi kwa mama bora wa mfano kwa mwaka 2017 ambapo nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Mama Hadija Mrisho wa kijiji cha Kwa-Kibuyu pichani

Hatimae shindano la kutafuta kamati bora za kudhibiti Ukimwi, Jinsia na Uongozi vijijini lililokuwa linaratibiwa na shirika la UZIKWASA wilayani Pangani limemaliza kwa kishindo huku kamati ya kijiji cha Msaraza kikiibuka na ushindi.


Dk. Salim Ahmed Salim aaga Kamati Kuu ya CCM.

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Salim Ahmed Salim leo amewaaga wajumbe Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano.

Katika salamu zake mwishoni mwa kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma Mhe. Dk. Salim amewashukuru Wajumbe wa Kamati Kuu na Viongozi wakuu wa chama kwa kushirikiana nao katika kipindi chote cha ujumbe wake na pia amempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli kwa uongozi uliokiwezesha chama kuimarika.

Mhe. Dk. Salim amesema kazi nzuri inayofanywa na Mhe. Dk. Magufuli imeonesha dhahiri kuyaenzi mambo muhimu aliyoyasimamia Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Mhe. Dk. Salim ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kuwa mtiifu kwa Chama na Serikali.

kampeni ya upigaji chapa mifugo yazinduliwa wilayani Ngorongoro

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mh Mrisho Gambo kwa Ushirikiano na Naibu Waziri wa Mifugo (Mhe Ulega) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,mapema leowa wamezindua zoezi la Upigaji Chapa Mifugo Kata ya Nainokanoka Wilayani Ngorongoro. 
 
Mh Mrisho Gambo aliesma kuwa kampeni hiyo itasaidia Ku-Control movement ya mifugo kutoka ndani na nje ya nchi, kuipa serikali uwezo wa kuwatambua na kuwahudumia wafugaji wetu. Mtu yoyote atakaye hujumu zoezi hili hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake! Deadline ya kuhitimisha zoezi hili ni tarehe 30 Januari 2018 kwa mkoa wa Arusha!

Uongozi unao acha alama!

 
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mh Mrisho Gambo kwa Ushirikiano na Naibu Waziri wa Mifugo (Mhe Ulega) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,mapema leo akishiriki kuzindua kampeni ya Upigaji Chapa Mifugo Kata ya Nainokanoka Wilayani Ngorongoro.

Article 0

TPB YAFUNGUA TAWI JIPYA KWA MROMBO - ARUSHA

$
0
0

Leo Ijumaa, 15 Desemba 2017, Benki ya TPB tumeendelea kusogeza huduma zetu karibu zaidi na wateja kwa kufungua tawi jipya maeneo ya Kwa Mrombo, Mkoani Arusha.

Lengo la kufungua tawi hili ni kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na pia kupata fursa ya kutoa huduma kwenye mazingira bora na ya kisasa zaidi, ili wakazi wa mkoa wa Arusha, hususan waishio maeneo ya Kwa Mrombo, waendelea kufaidika na huduma bora zenye gharama nafuu.

Akizungumza wakati wa kuzindua tawi hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya alisema tawi hilo jipya litaongeza idadi ya wateja kwenye benki hiyo.

Alisema pia wakazi wa Kwa Mrombo, watafaidika na mikopo mbalimbali inayotolewa na TPB inayokidhi mahitaji ya vikundi, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, mikopo ya wafanyakazi na hata wastaafu.

‘Ni furaha kubwa sana kwetu sisi TPB kuweza kufikisha huduma zetu hapa Kwa Mrombo. Ni matumaini yangu kuwa tawi hili litaongeza idadi ya wateja watakaofika kupata huduma mbalimbali tunazozitoa, kwani TPB tunatoa huduma bora na zenye kukidhi matakwa ya kila mwananchi katika jamii ikiwemo mikopo kwa vikundi visivyo rasmi,’ alisema Profesa Rutashobya.

Alisema kwa sasa lengo lao kubwa ni kuendelea kutoa huduma bora zaidi ili kuwanufaisha wananchi wa kipato cha chini. ‘TPB inaendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi kwani mbali na kufungua tawi hili, katika kipindi cha mwaka huu tumeweza kufungua matawi yetu huko Mwanjelwa Mkoani Mbeya, Mto wa Mbu wilayani Monduli na Temeke,’ alisema.

Kwa upande wake, Meneja wa tawi la Kwa Mrombo Hussein Jalala alisema mwitikio wa wakazi wa maeneo ya Kwa Mrombo umekuwa mzuri, tangu walipoanza kutoa huduma zake maeneo hayo. Alisema tawi lake limejipanga vizuri kuhakikisha kuwa huduma zitakazotolewa kwa wateja wao ziwe za kuridhisha na zenye kukidhi mahitaji yao. Jalala alizitaka taasisi mbalimbali vikiwemo vyuo, mashirika na hata shule kufungua akaunti za taasisi na TPB ili kupata huduma za kisasa na zenye gharama nafuu. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobya akifurahia  baada ya kufungua rasmi tawi jipya la benki hiyo maeneo ya  kwa Mrombo ,huko Mkoani Arusha. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi .
Mwenyekiti wa Bodi ya Waurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa, akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw. Tate Looboye Koole, wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi la benki hiyo lililopo maeneo ya  Kwa Mrombo, Mkoani Arusha. Katikati ni Meneja wa tawi hilo Hussein Jalala.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa (wa pili kushoto), akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw. Elias John Malisa, wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi la benki hiyo lililopo maeneo ya  Kwa Mrombo, Mkoani Arusha. Kushoto  ni Meneja wa tawi hilo Hussein Jalala na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo pamoja na baadhi ya wakurugenzi, kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo lililopo maeneo ya kwa Mrombo, Mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa tawi la benki hiyo lililopo maeneo ya kwa Mrombo, Mkoani Arusha.

NAIBU WAZIRI ULEGA ASHIRIKI UHAMASISHAJI WA UPIGAJI CHAPA MIFUGO NGORONGORO MKOANI ARUSHA

$
0
0

Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na uvuvi Mhe.Abdalla Hamisi Ulega amefanya ziara mkoani Arusha katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa lengo la kuhamasisha upigaji chapa mifugo.

Akizungumza na baadhi ya wafugaji katika halmashauri ya Ngorongoro, Ulega amempongeza mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo, kwa utendaji mzuri wa kazi hususani katika kuhamasisha upigaji chapa mifugo mkoani humo.

Aidha Mhe Ulega amezijata baadhi ya halmashauri zilizofanya vizuri katika zoezi la upigaji chapa kuwa ni pamoja na Chemba,Kondoa,Maswa,Mafinga na Misungwi.

Mh.Ulega amewahimiza wafugaji kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upigaji chapa mifugo linaloendelea nchi zima.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizindua zowezi la upigaji chapa mifugo katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, (wa kwanza kulia) akizungumza na wananchi wanoishi katika hifadhi ya Ngorongoro jana baada ya kushuhudia zowezi la upigaji chapa mifugo mkoa wa Arusha.katikati ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na kushoto, Naibu Muhifadhi Dkt.Maurus Msuha
Naibu Muhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Dkt Maurus Msuha  akishiriki zowezi la upigaji chapa mifugo mapema jana mkoani Arusha.

Zowezi la upigaji chapa mifugo likiendelea mkoani Arusha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG Arusha)
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images