Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA

$
0
0
Na Mary Gwera, Zanzibar

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim H. Juma ashauri juu ya uwezekano wa kuwa na Kanuni za pamoja za Sheria ya Biashara na Uwekezaji ‘Trade Investment Regulations’ kati ya Tanzania na China zitakazowezesha ukuaji wa uchumi ambao utasaidia kuleta maendeleo baina ya nchi hizi mbili.

Aliyasema hayo, Desemba 1, katika maongezi maalum na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa China, Mhe. Zhao Dacheng, pindi alipotembelewa na Naibu Waziri huyo Mahakama Kuu-Zanzibar ambapo Mhe Jaji Mkuu anaendelea na Vikao maalum vya Mahakama ya Rufani ‘court session’

Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa; China ni nchi ambayo tayari imeshapiga hatua kubwa kiuchumi na kimaendeleo, hivyo kuwepo kwa Kanuni wezeshi za Biashara Uwekezaji baina ya nchi hizi mbili (2) utasaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania pia.

“Ni vyema kuangalia juu ya uwezekano wa nchi zetu; Tanzania na China kuwa na kanuni zinazofanana zitakazotoa muelekeo wa jinsi ya kuwekeza kwa manufaa ya pande zote mbili,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa China, Mhe. Zhao Dacheng aliafiki ushauri huo uliotolewa na Mhe. Jaji Mkuu na kumtaka kuendelea na hatua za awali za uwasilishaji wa pendekezo hilo kwa taratibu zinazotakiwa kufanyika ili kufanikisha utekelezaji wa ushauri uliotolewa.
Mhe. Jaji Mkuu akifurahia zawadi ya picha aliyopatiwa na Mgeni wake.
Picha ya pamoja baada ya Majadiliano: wa nne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, katikati ni Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga pamoja na Wajumbe waliombatana na Naibu Waziri.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akimkaribisha Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng pindi alipowasili katika Ofisi ya Jaji Mkuu-Mahakama Kuu Zanzibar.
Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng (katikati) akiongea jambo na Mhe. Jaji Mkuu pindi alipomtembelea Desemba 01, 2017.


RC Wangabo achangia Milioni Moja kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya cha Waislamu

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amechangia shilingi milioni moja kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kusaidia ujenzi wa kituo cha afya cha Waislamu kinachoendelea kujengwa katika Tarafa ya Kirando, Kata ya Kirando Wilayani Nkasi.

Amesema kuwa Taasisi za kidini kwa muda mrefu zimekuwa zikisaidia juhudi za serikali katika kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi jambo ambalo pia linasaidia utekelezaji wa Ilani ya chama tawala inayoongoza serikali hiyo.

“Naendelea kuzishukuru taasisi za kidini kwa kuisaidia serikali katika kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi kwani kwa uopande wa sekta ya Afya Mkoa una zahanati kumi, vituo vya afya vinane na Hospitali mbili zinazomilikiwa na taasisi za kidini na mmeniambia kuwa mnaendelea na ujenzi wa vituo viwili vya afya ambavyo vikikamilika vitaongeza upatikanaji wa huduma,” Alielezea Mh. Wangabo.

Ametoa mchango huo kuzindua harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya katika siku ya maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika Kimkoa katika Kijiji cha Kabwe, Kata ya Kabwe Wilayani Nkasi ambapo Mgeni rasmi wa shughuli hiyo alikuwa Mh. Joachim Wangabo.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa nasaha katika  maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika kimkoa Kijiji cha kabwe Wilayani Nkasi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiitikia dua ya kuliombea taifa na serikali ya awamu ya tano, Dua iliyosomwa na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Shekh Hassan Kiborwa katika maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W).
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akiongozana na Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Sumbawanga Mh. Adam Mambi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akipanda mti kuhamasisha upandaji miti kwa waisalamu na wanachi kwa ujumla hasa kipindi hiki cha mvua.

WAJASIRIAMALI JIJI LA ARUSHA WAPATIWA MKOPO WA MILIONI 605

$
0
0

Na Mahmoud Ahmad,Arusha.

Jumla ya Shilingi milioni 605 zimetolewa kama mkopo wa kuwanufaisha wajasiriamali walioko kwenye vikundi vya kinamama na vijana pamoja na walemavu waliopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Akizungumzia mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Arusha, Hanifa Ramadhani amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa ili kuwawezesha kinamama na vijana kuondokana na hali ngumu za kiuchumi zinazowakabili ili kuinua uchumi .

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amewataka Vijana ambao ni wasomi kujiunga katika vikundi hivyo na kupata mikopo ili kujiendeleza kiuchumi badala ya kusubiri ajira serikalini ile hali nafasi ni chache na wahitimu wa vyuo ni wengi.

Kwa upande wao Wanufaika wa Mikopo hiyo kwa niaba ya Walemavu Mwajuma Juma na Patrick Petro wameishukuru serikali kwa kutoa mikopo hiyo yenye masharti nafuu ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.
 Kinamama na vijana waliokusanyika katika ukumbi wa Arusha School kupewa mafunzo kabla ya kupatiwa mikopo ya halmashauri. Picha na Ferdinand Shayo

 Kinamama na vijana waliokusanyika katika ukumbi wa Arusha School kupewa mafunzo kabla ya kupatiwa mikopo ya halmashauri. Picha na Ferdinand Shayo 
Mkuu wa Wilaya ya Arusha  Gabriel Daqqaro akikabidhi hundi ya shilingi milioni 500 ya mkopo wa kinamama iliyotolewa na Halmashauri ya Jiji la Arusha .Picha na Ferdinand Shayo

WAZIRI MHAGAMA AKABIDHIWA VIFAA VYA WATU WENYE ULEMAVU CHUO CHA UFUNDI CHA YOMBO IKIWA NI MSAADA KUTOKA SERIKALI YA KUWEIT

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya watu wenye ulemavu katika Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu, Dar es Salaam jana , kulia ni Balozi wa Kuweit nchini Tanzania,  Jasem Al-Najem. 
  Balozi wa Kuwait nchini,  Jasem Al-Najem akizungumza jambo na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa kwanza kushoto), wakati mmoja wa mwanafunzi wa Chuo hicho, Lenah Sauli alipokua akishona nguo
 Mkufunzi Mkuu Msaidizi  Regina Makotha (kulia) akizungumza kwa kuwapa ishara yale aliyokuwa akizungumza Waziri Mhagama
 Wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu wakiashiria kupiga makofi wakati walipokuwa wakipewa ishara na Mwalimu wao, Mkufunzi Mkuu Msaidizi  Regina Makotha (pichani hayupo) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza nao.


SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU YAWAWEZESHA WANANCHI WA VIJIJI VYA CHILONWA NA MSANGA WILAYANI CHAMWINO KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA.

$
0
0
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Idara Kuu ya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sylivia Siriwa  akizungumza na wanakijiji wa vijiji vya Chilonwa na Msanga wakati wa Semina ya uwezeshaji wananchi kupambana na ukatili wa kijinsia katika muendelezo wa Siku 16 za Kupambana na Ukatili huo.
 Mwanasheria kutoka Idara Kuu Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Denis Bashaka akitoa ufafanuzi wa masuala ya kisheria  na jinsi sheria inavyoweza kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanakijiji wa vijiji vya Chilonwa na Msanga Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma katika muendelezo wa Siku 16 za Kupambana na Ukatili huo. 
 Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Idara ya Ustawi wa Jamii Idara kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Amina Mafita akielezea nafasi na wajibu wa maafisa Ustawi wa Jamii katika katika kuisaidia jamii kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo yao kwenye Semina na kuwawezesha wananchi wa vijiji vya Chilonwa na Msanga Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma kupambana na ukatili wa kijinsia katika muendelezo wa Siku 16 za Kupambana na Ukatili huo.
 Wananchi wa vijiji vya Chilonwa na Msanga Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wataalam kutoka Serikalini na Mashirika Yasiyoya Kiserikali jinsi ya  kupambana na ukatili wa kijinsia katika muendelezo wa Siku 16 za Kupambana na Ukatili huo.  Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SAVE THE CHILDREN YATOA MSAADA WA GARI,PIKIPIKI KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA WATOTO SHINYANGA

$
0
0

Shirika la Kimataifa la Save The Children limetoa msaada wa gari aina ya Toyota Landcruiser katika Halmashauri ya Mji Kahama mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kusaidia ufuatiliaji wa matukio ya ukatili na unyanyasaji wa watoto. 



Mbali na kukabidhi gari hilo, Save The Children pia imekabidhi pikipiki mbili aina ya Boxer, Kompyuta mpakato moja (Laptop) na Ipad moja kwa shirika la KIWOHEDE linalotekeleza mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama. 


Hafla fupi ya makabidhiano hayo imefanyika leo Ijumaa,Desemba Mosi,2017 katika viwanja vya Halmashauri ya Kahama Mji wilayani Kahama,mkoani Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi,gari,pikipiki,laptop na Ipad, Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima alisema vifaa hivyo vitasaidia katika utendaji kazi kupambana na ukatili dhidi ya watoto. 
“Leo ni siku ya Ukimwi duniani na sisi tumeona tushiriki katika siku hii ili kuonesha kwamba ukatili ni njia mojawapo ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Mradi wetu umeisha lakini mapambano dhidi ya ukatili kwa watoto yanaendelea, kwa hiyo tunakabidhi gari hili ili mapambano yaendelee”,alisema Malima. 
“Vifaa hivi likiwemo gari hili vitakwenda kufanya kazi za mapambano dhidi ya ukatili wa watoto,tunaomba likafanye kazi kama ilivyokusudiwa ili kuhakikisha kuwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinaisha mkoani Shinyanga”,aliongeza Malima. 
Aidha alisema tangu mwaka 2014 walikuwa wanatekeleza mradi wa Ukatili dhidi ya watotokatika halmashauri ya Mji Kahama,Manispaa ya Shinyanga na Shinyanga Vijijini na baada ya mradi kuisha mwaka huu wametoa gari hilo kwa halmashauri ya Kahama Mji kwani imekuwa mstari wa mbele katika mapambano ya ukatili dhidi ya watoto. 
“Tunawapongeza sana halmashauri ya Kahama Mji kwa kuwa mfano mzuri katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia na watoto,wameonesha hatua za ziada,waliamua kuubeba mradi huu na kuufanya wao,tunaamini wataendeleza mapambano”,alisema Malima. 
Hata hivyo,Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Kahama Mji,Robert Kwela aliuhakikishia uongozi wa shirika hilo kuwa watalitunza na kulitumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa. 
“Mradi wa wenzetu Save the Chidren kuisha muda wake, wamekabidhi vifaa hivi ili shughuli za mapambano ya ukatili dhidi ya watoto ziendelee”,alisema. 
“Baada ya mradi kuisha,ili shughuli zilizokuwa zinatekelezwa ziweze kuendelea,utaratibu huwa ni lazima mashirika husika yaendelee kuona namna ya kujenga uwezo kwenye taasisi ambazo walikuwa wanafanya nazo kazi ili shughuli zilizokuwa zimeanzishwa ziweze kuendelezwa”,alifafanua Kwela. 
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija alilishukuru shirika hilo kwa ushirikiano ambao limekuwa likiwapa na kuongeza kuwa suala la ukatili dhidi ya watoto linapaswa kufanywa kwa vitendo kama vile Save the Children walivyoonesha kwa kutoa vifaa hivyo vya kutendea kazi. 
Naye Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE, Lulu Makwale alilishukuru shirika la Save the Children kwa kuwapatia msaada wa pikipiki mbili,laptop na Ipad vifaa ambavyo vitasaidia katika utekelezaji wa mradi huo katika Halmashauri ya Ushetu.
Makabidhiano hayo pia yalishuhudiwa na Katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela alilishukuru shirika hilo kwa msaada wa gari na kuongeza kuwa litasaidia katika kupunguza changamoto ya usafiri katika halmashauri hiyo.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza wakati akikabidhi gari katika halmashauri ya Kahama Mji na pikipiki,laptop na Ipad kwa shirika la KIWOHEDE leo katika viwanja vya Kahama Mji,wilayani Kahama.Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija. Kulia ni Mratibu wa ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala shirika la Save The Children,Alex Enock akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Kahama Mji,Robert Kwela.
Gari na pikipiki zilizotolewa na shirika la Save The Chilren vikiwa nje ya ofisi za halmashauri ya Kahama Mji.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BODI YA USAJILI WA GAZETI NA VIJARIDA YAZINDULIWA

$
0
0
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma katikati kushoto akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Bodi ya Idara ya Habari Maelezo ya Usajili wa Gazeti na Vijarida katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Unguja.kulia yake ni Naibu Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Chumu Kombo Khamis.
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dk,Juma Mohammed Salum kushoto akitoa hotuba ya makaribisho katika hafla ya Uzinduzi wa Bodi ya Idara ya Habari Maelezo ya Usajili wa Gazeti na Vijarida katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Unguja
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi waliohudhuria katika Uzinduzi wa Bodi ya Idara ya Habari Maelezo ya Usajili wa Gazeti na Vijarida katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Unguja
Mwenyekiti wa Bodi ya Idara ya Habari Maelezo ya Usajili wa Gazeti na Vijarida Yussuf Omar Chunda akizungumza machache kuhusiana na Uzinduzi wa Bodi hio katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Unguja.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MAKAMU WA RAIS APIGA KURA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA CCM MKOA WA KUSINI UNGUJA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akipiga kura kuchagua viongozi wa CCM mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye Hoteli ya Coconut Tree, Marumbi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdallah Juma Abdalla Sadalla(Mabodi)kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye Hoteli ya Coconut Tree, Marumbi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akiwasalimu wajumbe kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye hoteli ya Coconut Tree, Marumbi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA WA KUSINI UNGUJA LEO.

$
0
0
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Coconut Marumbi Wilaya ya Kusini Unguja.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Abdallah Juma Mabodi akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeri rasmin Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein kufungua Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa coconut marumbi Unguja.(Picha na Ikulu)
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipiga kura yake kuwachagua Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Marumbi Wilaya ya Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)

 WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika ukumbi wa mkutano katika hoteli ya coconut marumbi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano huo.(Picha na Ikulu)

TAASISI YA HER INITIATIVE 'PANDA' WATOA SEMINA SHAWISHI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MWANZA LEO.

$
0
0
  Mchekeshaji na Mshindi wa Big Brother Afrika 2014,Idrisa Sultan akizungumza leo katika semina ya kuwashawishi wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza.
Msemaji na innovator katika fursa za kimataifa, Banji Fernandes akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya jijini Mwanza kwaajili ya kuwavutia kwa njia mbalimbali kutokana na aliyoyapitia katika maisha ya shule pamoja na maisha ya Kawaida.Pia amewashauri wanafunzi hao wa vyuo vikuu vya jijini Mwanzakusoma kwa bidii pamoja na kuwa wavumilivu kwenye vikwazo mbalimbali wanavyokutana navyo. Hayo yamesemwa katika semina fupi ya kuwashawishi iliyoandaliwa na Taasisi ya her initiative Present PANDA iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza leo.
  Msanii wa Bongo Muvi na Majasiliamali na mshawishinkatika upande wa sanaa, Rose Ndauka akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza katika semina iliyofanyika leo katika chuo kikuu cha Makatifu Agustino jijini humo.
Mwanzlishi wa Taasisi ya Her Initiative Presents PANDA, Moureen akizungumza na katika semina ya kuwashawishi wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza Leo.
Baadhi ya wananfunzi wa vyuo vikuu vya jijini Mwanza wakiwasikiliza watoa maada katika semina iliyofanyika katika chuo cha Mtakatifu Augustino jijini Dar es Salaam leo.

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO DECEMBER 3,2017

MAHAFALI YA 11 YA CHUO KIKUU ARDHI (ARU) YAFANA DAR ES SALAAM

$
0
0

Sehemu ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakishangilia katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017. (Imendaliwa na Robert Okanda Blogs)

Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifuatilia matukio katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017

Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifuatilia matukio katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017 


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Serikali haitawafumbia macho Wezi wa kazi za Sanaa:Dkt Mwakyembe.

$
0
0

Na Shamimu Nyaki-WHUSM

Serikali imesema itaendelea kuwachukulia hatua wote watakaobainika kusambaza kazi za sanaa kinyume na utaratibu ili kuondoa kero ya muda mrefu ya wizi wa kazi za Sanaa uliolalamikiwa na wasanii wote hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akizindua Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment itakayohusika na usambazaji wa kazi za Sanaa kuanzia kesho.

“Serikali haitaendelea kuwafumbia macho wezi wa kazi za Sanaa,tutawashughulikia kama ambavyo tumeanza na mafanikio yameanza kuonekana yeyote anaetaka kusambaza kazi hizi aende Barazani Entartainment watamsaidia.”Alisema Dkt Mwakyembe.

Aidha amewataka wasanii wote hapa nchini kutumia Kampuni hiyo kwa manufaa ili waweze kupiga hatua ambapo pia amewahakikishia kuwa ndani ya kipindi kifupi kijacho sekta ya Sanaa itakuwa na mageuzi makubwa.

Kwa upande wake Katibu wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amewahakikishia wasanii hao kuwa Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Wilaya wapo tayari kushirikiana na Kampuni ya Barazani Entartainment katika kuleta mafanikio ya kazi zao.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw.John Kalaghe ameishukuru Serikali kwa ushirikiano ilioupatia kampuni hiyo tangu ilipoanzisha wazo hilo ambalo leo limefanikiwa na wasanii wataanza kunufaika na kazi zao kwani Kapuni hiyo itasambaza kazi zao kwa urahisi na salama zaidi.

Kampuni ya Tyeeo Barazani Entartainment itakuwa ndio wakala wa kusambaza kazi za sanaa ikiwemo Filamu za nje na ndani,Muziki,masomo ya watoto,na makala za kielimu kupitia simu ya mkononi kwa mitandao yote kwa malipo nafuu.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) na viongozi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment wakionyesha Filamu ya “Queen of Masai”itakayoanza kusambazwa na Kampuni hiyo kuanzia kesho. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Tyeeo Entartainment Bw.John Kalaghe wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fissoo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi.Joyce Fissoo akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini.

MEYA MWITA ASHANGAA WATU WA KISIWA CHA MAYOTTE WAKIZUNGUMZA KISWAHILI

$
0
0
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa watu 10 kutoka Kisiwa cha Mayotte kilichopo Nchini Ufaransa.

Ujumbe huo ulikuwa umeambatana na wabunge watatu kutoka Nchini humo, Rais wa Shirikisho la wafanyabiashara wa Mayotte pamoja na wajumbe wengine ambao ni wawakilishi kutoka kampuni mbalimbali kisiwani humo.
Katika mazungumzo hayo, Mstahiki Meya Mwita na wageni wake wamejadili mambo mbalimbali ya maendeleo jijini hapa hususani masuala ya kibiashara ambapo amewakaribisha na kuahidi ushirikiano kwao.

Aidha Meya Mwita pia ameshangaa kuona ugeni huo kutoka Kisiwa cha Mayotte wakizungumza Kiswahili jambo ambalo alidai kuwa ni la kihistoria kutokana na historia ya Nchi hiyo.

Kutokana mshangao huo, ambao uliambatana na furaha ndani yake, aliwakabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili kwa lengo la kuendelea kujifunza zaidi Lugha ya Kiswahili pindi watakaporejea nchini kwao.
“ Nimefarijika na kushangaa baada ya kusikia asilimia 40 ya wananchi wakisiwa cha Mayote wanazungumza lugha ya Kiswahili, hii ni ajabu, lakini inaonyesha ninamna gani ambavyo watu wanaipenda Lugha yetu” amesema Meya Mwita.

Awali jumbe huo ulikutana na kufanya mazungumzo na Shirikisho la wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania.
Imetolewa leo Desemba 1 na Christina Mwagala, Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto, akimsikiliza Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda Hamidani Magoma mwenyemiwani walipokutana katika ofisi za Mastahiki Meya jiji.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Saalam Isaya Mwita akimkabidhi Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda wa Mayotte Hamidani Magoma Kamusi ya Kiswahili baada ya kuzungumza Kiswahili.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita watatu kulia mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka Kisiwa Cha Mayotte kilichopo Nchini Ufaransa walipomtembelea ofisini kwake.
Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda wa Mayotte Nchini Ufaransa Hamidani Magoma akimuelekeza jambo kwenye kwenye dokomenti Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita walipomtembelea ofisini kwake na kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya biashara jijini hapa.

MAKAMU WA RAIS APIGA KURA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA CCM MKOA WA KUSINI UNGUJA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akipiga kura kuchagua viongozi wa CCM mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye Hoteli ya Coconut Tree, Marumbi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdallah Juma Abdalla Sadalla(Mabodi)kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye Hoteli ya Coconut Tree, Marumbi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akiwasalimu wajumbe kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye hoteli ya Coconut Tree, Marumbi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein wakati alipowasili kwenye kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye hoteli ya Coconut Tree, Marumbi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MBUNGE WA KINONDONI CUF AJIUZULU UBUNGE NA KUJITOA UANACHAMA WA CUF.

SHIRIKA LA AGPAHI LIKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA VVU KATIKA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA

$
0
0
Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Care Initiative (AGPAHI) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga wameendesha zoezi la upimaji vya virusi vya Ukimwi kwa wakazi wa Jiji hilo huku zaidi ya wakazi 1900 wakijitokeza kupima na kupatiwa ushauri wa namna ya kuweza kujikinga na maambukizi ya VVU .

Upimaji huo ulifanyika kwenye vituo vya Afya Makorora, Ngamiani, Pongwe na Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani inayoadhimishwa kila mwaka hapa nchini. Zoezi hili la upimaji lililenga wanafamilia wa watu wanaoishi na VVU katika jiji la Tanga. Upimaji huo ulianza siku ya Jumatano hadi Ijumaa (29 Novemba – 01 Disemba) ambayo ndiyo siku ya Ukimwi duniani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupima afya zao mkazi mmoja wa Donge Jijini Tanga, Zilipa Elangwe alisema zoezi hilo limekuwa ni zuri kwa sababu linasaidia watu kuweza kujua afya zao na namna ya kujikinga.

Alisema wanapokuwa wakijua afya zao inawasaidia kuweza kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kupelekea kuingia kwenye maambukizi ikiwemo kujiepusha na ngono zembe.

Aidha alisema huduma hiyo ya upimaji wa VVU ambayo imetolewa na Shirika la AGPAHI likishirikiana na halmashauri ya jiji la Tanga imewasaidia kujua afya zao kutokana na baadhi ya familia kutokuwa na uwezo wa kifedha kwenda kupima mara kwa mara hivyo ni jambo nzuri.

“Kwa kweli tunalishukuru sana Shirika la AGPAHI kwa kutuletea huduma hii ya upimaji wa VVU maana imetusaidia kujua afya zetu lakini pia kuchukua tahadhari ya kuhakikisha tunaepukana na maambukizi mapya “Alisema.
Kushoto ni Muuguzi wa kituo cha Afya Ngamiani Lea Kakunya akichukua maelezo ya mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alijitokeza kupima VVU wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani.
Wakazi wa Jiji la Tanga wakiingia kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Ngamiani kwa ajili ya kupima VVU katika zoezi ambalo liliendeshwa na Shirika la AGPAHI katika vituo vya Afya vya Makorora,Ngamiani ,Pongwe na Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo ambapo zaidi ya wananchi 1900 walijtokeza kupima.
Kushoto ni Ochieng Makaranga ambaye ni Mratibu wa Huduma na Tiba kwa watu wenye VVU Kituo cha Afya Ngamiani Jijini Tanga akichukua maelezo ya mkazi wa Jiji hilo wakati wa zoezi la Upimaji wa VVU jana Desemba Mosi 
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga wakiwa kwenye kituo cha Afya Makorora wakisubiri huduma ya kupima VVU. 

Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6

$
0
0


Hussein Makame-NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya Uchaguzi Mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika tarehe 13 Januari mwaka 2018.

Akitoa taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Mhe. Jaji Mkuu (Mst. Zanzibar) Hamid Mahmoud Hamid, alisema Tume imetangaza uchaguzi huo kufuatia kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwepo nafasi wazi ya jimbo la Singida Kaskazini kufuatia kuvuliwa uanachama wa CCM mbunge wa jimbo hilo Lazaro Nyalandu na hivyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge.

Kwa upande wa Jimbo la Songea Mjini, Jaji Mst. Hamid alisema kuwa Spika aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi ya jimbo hilo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Leonidas Gama huku Tume ikipokea Hati ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ikithibitisha kuwa Jimbo la Longido kuwa wazi baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo.

Aliongeza kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata sita Tanzania Bara.

Mhe. Jaji Mst. Hamid alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandolu (Halmashauri ya Jiji la Arusha), Kihesa (Halmashauri ya Manispaa ya Iringa), Bukumbi (Halmashauri ya Wilaya ya Uyui), Kurui (Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe), Keza (Halmashauri ya Wilaya ya Ngara) na Kwagunda (Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe).

AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema kuwa anakerwa na wakandarasi wasio na uwezo, ambao wamekuwa wakitekeleza miradi bila kuzingatia mikataba, ama kutoikamilisha kwa wakati au kutekeleza chini ya kiwango kwa kukosa thamani halisi ya fedha iliyotumika

Aweso alisema hayo wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya maji katika Wilaya ya Songea Vijjini, katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma na kusikitishwa na mwenendo wa utekelezaji usioridhisha wa baadhi ya miradi.

Naibu Waziri alisema kuwa ipo haja ya kufutiwa usajili na kutokupewa kazi yoyote nchini wakandarasi wote wababaishaji, baada ya kutoridhishwa tendaji wao katika baadhi ya miradi wilayani humo.

‘‘Hatutawavumilia wakandarasi wasio na uwezo ambao wanatuangusha, tutawafuatilia na ikiwezekana wafutiwe usajili kabisa nchini ili wasiendelee kufanya kazi mahali popote nchini, tubaki na wakandarasi wenye uwezo’’, alisema Aweso.

Akiwa mkoani Ruvuma, Aweso ametembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa katika wilaya za Tunduru, Namtumbo, Songea Mjini, Songea Vijijini na Madaba lengo likiwa ni kuweka msukumo katika utekelezaji wa miradi kwa nia ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati na wananchi wa mkoa huo wanapata huduma ya maji ya uhakika.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiangalia kilula cha maji cha mradi wa Liula, Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoa maagizo kwa watendaji mara baada ya kukagua Tenki la maji la mradi wa Parangu katika Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoka kukagua chanzo cha maji cha Masimeli, kinachotumika kuzalisha maji kwa ajili ya mradi wa Lipaya katika Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa kwenye tenki la mradi wa Matimila, Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA NDANI YA SIKU 30 KUJITOKEZA WAMILIKI WA MAGOGO YALIKAMATWA BANDARINI DAR

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ametoa muda wa siku 30 kwa wahusika ambao ni wamiliki wa magogo yaliyokamatwa katika bandari ya Dar e s Salaam (TPA) ambayo yalikuwa yasafirishwe nje ya Nchi, kujitokeza haraka kueleza wameyato wapi na walikuwa na lengo gani baada ya kuyatelekeza bandarini hapo kwa muda wa miaka 10 sasa huku mengine yakitelekezwa pasipo kuwa na vibali maalum.
Dk.Kigwangalla ametoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini hapo kukagua mali na bidhaa zinazoshughulikiwa na Wizara yake hiyo ambapo katika zkukagua kwake huko alibaini uwepo wa makontena hayo 55 ambayo yapo kwa miaka 10 sasa yakihifadhiwa huku wahusika wakishindwa kujitokeza.
“Naagiza mamlaka zilizo chini ya wizara yangu kuhakikisha wanahakiki magogo yote yalipo hapa bandarini. Mwenye huu mzigo lazima ajulikane hasa haya magogo 938, Ndani ya siku 30 mwenye haya magogo atangaziwe na ajitokeze vinginevyo itabaki kuwa mali ya Serikali” alisema Dk. Kigwangalla.
Hata hivyo aliagiza pia kontena 55 zilizokutwa bandarini hapo zenye magogo pia nazo wahusika wajitokeze na nyaraka zao kamili ili waeleze kama kweli wameyatoa Zambia magogo hayo ama sehemu gani hivyo wajitokeze na wasipofanya hivyo ndani ya siku hizo 30, magogo hayo yatataifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa uongozi wa bandari ya TPA.
Baadhi ya magogo hayo yaliyokutwa katika makontena bandarini hapo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakiwa katika eneo la bandari ya nchi kavu ya Malawi Cargo. wakati wa kukagua magogo hayo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa nyaraka ya idadi ya makontena katika eneo la Malawi Cargo.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images