Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

DC SHINYANGA ATEMBELEA VITUO VYA HUDUMA YA MTOTO VYA MAKANISA YENYE USHIRIKA NA COMPASSION KLASTA YA SHINYANGA

$
0
0
Mkuu huyo wa wilaya amefanya ziara hiyo leo Jumamosi Disemba 2,2017 kwa ajili ya kujionea stadi za maisha na miradi mbalimbali inayofanywa na watoto wanaopata huduma katika vituo hivyo.Vituo vilivyotembelewa ni vituo vya Kanisa la ACT Shinyanga Mjini,AICT Kolandoto,TAG Shinyanga Mjini,PAG Shinyanga Mjini,KKKT Shinyanga Mjini. 

Akiwa katika ziara hiyo,Matiro amejionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na watoto kama vile utengenezaji skonzi,biskuti,keki,nguo,mafuta,sabuni pamoja na ususi,ufumaji,saluni,ufyatuaji wa matofali,uchomeleaji wa vyuma,useremala,masomo ya kompyuta na mambo mengine kadha wa kadha. 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,mkuu huyo wa wilaya alilipongeza shirika la Compassion kupitia makanisa yanayosimamia vituo hivyo ambavyo vimekuwa msaada mkubwa kwa watoto ambao wanajengewa uwezo wa kujiajiri. 

“Nimegundua tuna jeshi kubwa la vijana wenye ujuzi wa aina mbalimbali,vijana tumieni fursa hii ya Compassion kujinufaisha kwa ajili ya maisha yenu,sisi kama serikali tunafarijika sana kuona vijana wakijengewa uwezo wa kujiajiri ili kuleta maendeleo katika jamii”,alieleza. Matiro alieleza kufurahishwa kuona jinsi vijana hao wanavyojengewa uwezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuwashauri kuongeza jitihada ili kutengeneza viwanda kamili vya kutengeneza bidhaa. 

“Sera ya serikali ni kuwa na viwanda,nimeona vijana wanatengeneza skonzi,biskuti kwa kutumia mashine za kisasa kabisa katika kituo cha AICT Ngokolo,hiki ni kiwanda,naomba kanisa na Compassion kwa kushirikiana na serikali tuangalie namna ya kupanua kiwanda hiki ili kuleta mabadiliko katika jamii na kitasaidia vijana kujikwamua kiuchumi”,alisema Matiro. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ametembelea vituo sita vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga yenye vituo tisa.
Vijana wakimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro keki walizotengeneza.Vijana hao walisema wamepatiwa ujuzi wa kutengeneza keki katika kituo hicho. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia jinsi wanavyochomelea vyuma katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini.


WAZIRI MKUU MAJALIWA AMFARIJI MOHAMMED CHILAMBO AMBAYE NYUMBA YAKE ILICHOMWA MOTO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwafariji Katibu wa CCM wa Kata ya Mnacho , Mohammed Chilambo (kushoto kwake) ambaye nyumba yake imechomwa moto kwa sababu zinazodaiwa kuwa za kisiasa katika kijiji cha Chimbela B wilayani Ruangwa Desemba 2, 2017.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Global complacency threatens the lives of children and adolescents as world set to miss global AIDS target - UNICEF

$
0
0
NEW YORK/DAR ES SALAAM, 02 December 2017 – In 2016, 120,000 children under the age of 14 died of AIDS related causes, and 18 children were infected with HIV every single hour. If current trends persist, there will be 3.5 million new adolescent HIV infections by 2030, according to projections from the 2017 UNICEF Statistical Update on Children and AIDS released today.

“It is unacceptable that we continue to see so many children dying from AIDS and so little progress made to protect adolescents from new HIV infections,” said Dr. Chewe Luo, Chief of HIV for UNICEF (pictured) . “The AIDS epidemic is not over; it remains a threat to the lives of children and young people and more can and should be done to prevent it.”

A UNICEF analysis of demographic trends and new HIV data reveals that targets set in the 2020 Super-Fast-Trackframework developed in 2016 to end AIDS among children, will not be achieved.  
There has been some progress in the fight against AIDS, notably in preventing mother to child transmission of HIV. Around 2 million new infections among children have been averted since 2000. However, UNICEF warns that such progress must not lead to complacency as the Statistical Update highlights that children aged 4 and under living with HIV face the highest risk of AIDS-related deaths compared to other age groups. 
Globally paediatric HIV testing and treatment is lagging, with only 43 per cent of HIV exposed infants being tested within the recommended first two months of life, and the same percentage of children living with HIV receiving lifesaving antiretroviral treatment. 
UNICEF says progress in preventing new HIV infections among adolescents and improving testing and treatment in adolescent populations has been unacceptably slow. Globally, in 2016 alone, 55,000 adolescents (age 10-19) died from AIDS-related causes, 91 per cent of them in sub-Saharan Africa. The data also reveals a worrying gender disparity: for every five adolescent boys living with HIV, there are seven girls of the same age.
Preliminary findings of the Tanzania HIV Impact Survey 2016-17 state that the annual incidence of HIV among people aged 15 to 64 years was0.29 percent. There are gender disparities. Women have a higher rate of new infections (0.4 per cent) was much higherthan in men (0.17 per cent). 
Prevalence of HIV among people aged 15 to 64 years in Tanzania stands at 5 percent and is two-times higher in women (6.5 percent) thanmen (3.5 percent). The disparity is most pronounced among younger adults, with women in the age group of 15 to 19 years, 20 to 24 years and 25 to 29 years, all having a higher prevalence than men in the same age group.
In order to achieve the 2030 goal of ending the AIDS epidemic in Tanzania, efforts need to be intensified by:
• Investing in and utilizing emerging innovations such as HIV self-testing, pre-exposure prophylaxis and new paediatric drugs;
• Scaling-up response for children,including expanding treatment programmes, and investing in new technology for point-of-care diagnostics;
• Strengthening capacity in the collectionof comprehensive, disaggregated testing and treatment data, especially on adolescents, to help inform programming;
• Prioritizing interventions for adolescent girls.
The AIDS epidemic must remain a public health concern, according to UNICEF. Innovative solutions must be adopted to speed upprogress in preventing HIV infection of children and ensuring those living with HIV get the treatment they need

Article 4

$
0
0
Baba  tunakumbuka umefikisha miaka 30 tangu ulipotwaliwa siku ile ya tarehe 2 desemba 1987. 

Unakumbukwa na mke wako Margaret. watoto wako Emily. Leonard. Martha. Enid. mMtilda na Sia. Pia unakumbukwa na kaka zako na dada zako, wakwe zako pamoja na wajukuu na vitukuu. 

Pumzika kwa amani Baba.

COUNCIL OF EAST AND CENTRAL AFRICA FOOTBALL ASSOCIATIONS (CECAFA) UPDATES

$
0
0

The CECAFA Congress convening here at Four Point Hotel in Nairobi City this Saturday December 2nd 2017 has elected the five new Executive Committee members to run the region’s top football office for the next two calendar years. 


The five who have been unanimously elected will now join CECAFA President Eng. Mutasim Gafar (Sudan) whose constitutional term runs till November 2019. 

These include Abdiqaani Arab Said (Somalia), Aimable Habimana (Burundi), Juneid Basha Tilmo (Ethiopia), Wallace Karia (Tanzania) and Doris Petra a woman representative hailing from Kenya.
The race that had earlier attracted eight candidates had Eng. Moses Magogo (Uganda), Vincent Nzamwita (Rwanda) and Kourecha Ali Gued from Djibouti withdrawing their candidature just minutes before the polls.

CECAFA COMPETITIONS:
The Congress emphasized the need to have annual tournaments and the following member federations have offered to host the 2018 events as below. 
No.TOURNAMENT - COUNTRY
01Beach Soccer & Women - Uganda
02Kagame Cup - Djibouti
03Youth U17- Tanzania
04Youth U20- Sudan/Kenya

This year’s delayed CECAFA WomenCup will still take place in Rwanda early next year. The hosts for the Senior Challenge Cup 2018 will be decided at a later date.  Ten out of twelve countries participated except Sudan and Eritrea.

Mkutano wa 47 wa Kimataifa wa kuwaandaa Watafiti Chipukizi wa Bara la Afrika wafunguliwa Arusha

$
0
0
Na Othman Khamis Ame
Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Muhamed Shein alisema Kiwango duni cha uwajibikaji katika misingi ya kuendesha Utawala Bora Kisiasa na Kiuchumi miongoni mwa Nchi za Bara la Afrika kimekuwa kikichangia na kusababisha migogoro isiyokwisha ambayo huwaathiri Wananchi walio wengi ndani ya eneo kubwa la Bara hilo. 

Alisema hicho ni moja ya kitu hatari kinachosababisha kuporomoka kwa Uchumi, Maendeleo na Ustawi wa Jamii Barani Afrika changamoto inayopaswa kutoa fursa kwa Waafrika wenyewe kutafakati kwa kina njia gani yenye muelekeo wa mafanikio katika masuala ya kufanikisha Maendeleo na Utawala Bora. 
Dr. Ali Muhamed Shein alisema hayo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati alipokuwa akiufungua Mkutano wa 47 wa Kimataifa wa kuwaandaa Watafiti Chipukizi wa Bara la Afrika katika dhana nzima ya kusaidia mataifa yao Kitaaluma uliofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Maunt Meru Mkoani Arusha. 

Mkutano huo unaofanyika kila baada ya Miaka Miwili katika Mataifa Wanachama huandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika { AERC } kwa lengo la kuwandaa Vijana waenye vipaji katika masuala ya Tafiti mbali mbali zikiwemo Uchumi, Kilimo, Uhandisi na Afya. 

Rais wa Zanzibar alisema Mataifa mengi Barani Afrika yamekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya Watu hasa Vijana kasi ambayo inahitaji nguvu kubwa zitakazozaa maarifa za Kiutafiti katika masuala ya Uchumi ili itoe afueni ya Maendeleo ya muelekeo wa matumaini. 

Alisema uwajibikaji wa pamoja katika umuhimu wa kuandaa nguvu za kiutendaji kwa kuwashirikisha Wananchi na hasa Vijana wenye Vipaji vya Utafiti wa kawaida ndani ya Taasisi za Kitaaluma unaweza kuzinyanyua Kiuchumi Nchi za Afrika katika kipindi kifupi. Dr. Shein alisema Warsha na Mikutano hiyo ya kuwakusanya Vijana Watafiti Chipukizi inasaidia kuamsha hamasa ya mijadala ya Maendeleo, namna ya uendeshaji wa Utawala pamoja na Mahusiano yenye muelekeo wa kujenga mazingira bora ya uwajibikaji. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alisema katika mfumo wa kulikwamua Bara la Afrika Kiuchumi ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika  (AERC) Kutafuta mbinu na maarifa zaidi ya kuona Mikutano, Mijadala na hata Warsha za kuwakutanisha Watafiti wa Uchumi wa Bara hili inafanyika mara mbili kwa Mwaka. 

Alisema mpango huo unaweza kuhamasisha chachu ya Utafiti kwa Wanataaluma hao wa mambo ya Uchumi jambo ambalo linaweza kufungua njia ya haraka za kupunguza au kuondosha kabisha Changamoto zinazolikabili Bara la Afrika hasa katika masuala ya Ajira. 

Dr. Shein alisema hatma njema ya mafanikio ya Maendeleo ya Kiuchumi kwa Wananchi waliomo ndani ya Mataifa ya Bara la Afrika inaweza kuchomoza hatua kwa hatua iwapo Wanataaluma hao 100 wa Utafiti wa Uchumi kutoka zaidi ya Nchi 25 za Afrika wataamaua kutumia vyema Kizalendo ujuzi wao. Rais wa Zanzibar aliupongeza na kuushukuru Uongozi mzima wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika { AERC } kwa uamuzi wake wa kuwakusanya Wataalamu Watafiti wa Masuala ya Kiuchumi Barani Afrika kwa nia ya kusaidia Uchumi wa Bara la Afrika na Watu wake. 

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika  (AERC)  Prosefa Lemma Denbet alisema Watafiti wa Taasisi hiyo wamekuwa wakifanya utafiti kwa kushirikiana na Taasisi nyengine ya Kimataifa takriban kwa Miaka 30 sasa. 
Profesa Lemma alisema ushirikiano huo kwa kiasi kikubwa umesaidia kuibua Watafiti Chipukizi Barani Afrika ambao kwa sasa wamekuwa cheche wa muelekeo wa Matumaini kwa Mataifa wanayotoka. 

Alisema katika dhana nzima ya nguvu za uwajibikaji katika sekta ya Utafiti AERC imeweka utartibu maalum wa kuwatumia Wataalamu mbali mbali waqzoefu waliobobea katika fani hiyo ili kusaidi maarifa yanayoweza kuongeza nguvu na kasi ya uvumbuzi hasa katika masuala ya Kiuchumi. 

Akimkaribisha Mgeni rasmi kuufungua Mkutano huo wa 47 wa Kimataifa wa kuwaandaa Watafiti Chipukizi wa Bara la Afrika Gavana wa Benki ya Kuu ya Tanzania Profesa BennoNdulu alisema kinachohitajika kwa Watu wa Afrika wakati huu ni kuangalia muelekeo wa namna gani Mataifa ya Bara la Afrika yanavyojikita katika uimarishaji wa uchumi kwa kuzingatia Utawala Bora.

Profesa Benno alisema kutokana na mabadiliko ya Dunia yanayokwenda kwa kasi kupitia mfumo wa kisasa wa Teknolojia ya Mawasiliano, Jamii za Waafrika wanalazimika kubadilika kwa haraka ili waende na wakati huo.

 Alitahadharisha kwamba changamoto za Rushwa, migomo ya mara kwa mara , uhabawa vyombo vya usafiri zinazooneka kuzielemea Bara la Afrika iwapo hazikutizamwa na kuchukuliwa hatua zinazofaa zinaweza kuviza maendeleo ndani ya Nchi za Bara la Afrika. 

Utafiti wa Uchumi Afrika {AERC } iliyoasisiwa Mwaka 1988 ina Wanachama kutoka Mataifa ya Ghana, Kenya, Malawi, Msumbiji, Nigeria,Rwanda, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Tanzania.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiingia ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru Arusha kwa ajili ya kuufungua Mkutano wa 47 wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika (AERC) kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika  (AERC) Profesa Lemma Senbet akitoa Taarifa ya Taasisi yake kwenye Mkutano wa  Watafiti Chipukizi wa Afrika hapo Mount Meru Arusha.

Sehemu ya Washiriki wa Mkutano wa 47 wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika { AERC } wakifuatilia matukio
mbali mbali yaliyokuwa yakitendeka ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru kwenye Mkutano wa Watafiti Chipukizi wa Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya AERC.


Sehemu ya Washiriki wa Mkutano wa 47 wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika  (AERC) wakifuatilia matukio
mbali mbali yaliyokuwa yakitendeka ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru kwenye Mkutano wa Watafiti Chipukizi wa Afrika ulioandaliwa na Taasisi hiyo

Mwenyekiti wa Mkutano wa 47 wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika  (AERC) Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania {BOT} Profeza Benno Ndulu akiuendesha Mkutano wa 47 wa Taasisi hiyo. Picha na OMPR

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AONGOZA ZIKU YA KIMATAIFA YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa kikundi cha Walemavu kutoka Mwembe Makumbi kinachojishughulisha na kutengeneza viatu wakati alipotembelea maonyesho ya walemavu katika uwanja wa Skuli ya Uzini.

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani na ambapo Kitaifa siku hii inaadhimishwa Mkoa wa Kusini Unguja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akifafanua jambo kwa kikundi cha Walemavu kutoka Mwembe Makumbi kinachojishughulisha na kutengeneza viatu wakati alipotembelea maonyesho ya walemavu katika uwanja wa Skuli ya Uzini.

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani na ambapo Kitaifa siku hii inaadhimishwa Mkoa wa Kusini Unguja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni mgeni rasmi.

SPIKA JOB NDUGAI MGENI AFUNGUA MASHINDANO YA NANE YA MABUNGE YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifanya usajili wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam.
 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiteta jambo wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam. Wakiongozwa na Mhe. Ritta kabati (kulia)
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Ndg. Rwigema Celestin (katikati) wakielekea kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson na wa pili kushoto ni katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Ndg. Edwin Rutageruka
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (aliesimama) akiwatambulisha  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam.
 Mgeni Rasmi Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Ndg. Benard Konga (kulia) wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam. NHIF ni watoaji huduma ya afya kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Wageni Mbali mbali kutoka nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam.
 Wageni Mbali mbali kutoka nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam.
Spika waBunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi Mbali mbali kutoka Afrika ya Mashariki wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam. watatu kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai

Michuzi TV: RC Paul Makonda akizungumza kwenye Dar Freshers Party Mlimani City

RC MAKONDA ATANGAZA DISCOUNT YA 20% HADI 70% KWA WANANCHI WOTE WATAKAOFIKA MADUKA YA MLIMANI CITY.

$
0
0

Maelfu ya Wanafunzi waliojitokeza katika hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa Vyuo vikuu Mwaka wa Kwanza DAR FRESHERS PARTY 2017,iliyofanyika jana nje ya Mlimani City katika viunga vya kupaki Magari huku usiku huo ukipambwa na Wasanii mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametangaza Punguzo la Bei (Discount) la 70% kwa Bidhaa zote zinazopatikana Ndani ya Maduka Mlimani City kwa muda wa Wiki moja kuanzia Leo.

Punguzo hilo la bei ni kwa Wananchi Wote ikiwa ni zawadi ya RC MAKONDA Kuelekea Sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya ili kuwapunguzia Wananchi makali ya gharama.

RC MAKONDA amesema hayo kwenye Hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa Vyuo vikuu Mwaka wa Kwanza DAR FRESHERS PARTY 2017,iliyofanyika jana nje ya Mlimani City katika viunga vya kupaki Magari ambapo amesema tamasha hilo litakuwa likifanyika kila Mwaka kwa kushirikisha Wasanii wakubwa kutoka Ndani na Nje ya Nchi.

Ameshukuru Vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo TBC, E. FM na E TV pamoja na Channel Ten kwa kufanikisha Tamasha hilo.

Aidha amewashukuru wasanii mbalimbali wakiwemo WCB, AY, FID Q,  RUBY, KASSIM MGANGA, MWANA FA,  RAY C, LADY JAYDEE, MSAMI, CHRISTIAN BELLA, DULY SYKES na MRISHO MPOTO kwa kujitolea kutoa Burudani bila Malipo.

Amesema Lengo la Tamasha hilo ni kujenga umoja kwa kuwakutanisha wanafunzi wa Vyuo mbalimbali kubadilishana mawazo  na kupatiwa maarifa.
Mmoja wa wasanii kutoka kundi la Mrisho Mpoto akitumbuiza jukwaani kwa madaha,huku pichani kulia Mkali wa kughani Mashari Mrisho Mpoti akichagiza na umahiri wake wa Mashairi.
Baadhi ya Askari wakiwa katikati ya kundi kubwa la Wanafunsi wa Vyuo,wakihakikishiwa ulinzi wao huku wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri jukwani kwa usiku ule
Mmoja wa Wasanii kutoka kundi la WCB akitumbuiza jukwaani.
Ilikuwa ni shangwe,vifijo na nderemo tuu
Mwanadada machachari katika anga ya muziki wa bongofleva kutoka kundi la WCB,Queen Darleen akiimbo wimbo wake aliouachia hivi karibuni ujulikanao kwa jina la 'ntakufilisi'.
Msanii mwingine mahiri kabisa kutoka kundi la WCB,Ray Vann aka Vanny Boy akiwakuna vilivyo maelfu ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali,kwenye pati yao ya ukaribisho iliyofanyika usiku wa kuamkia leo nje ya Mlimani City,jijini Dar Es Salam
Mkali mwingine wa kucheza na sauti Cassim Mganga akitumbuiza
Mzee wa Masauti Christian Bella akiwaimbisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali kwenye siku yao maalum ya kukaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Paul Makonda
Msanii mkongwe katika anga ya bongofleva Rehema Chalamila a.k.a Ray C akitumbuiza jukwaani
Burudani murua kabisa kutoka kwa wasanii mbalimbali ilitolewa

WADAU WATAKIWA KUJITOKEZA KUSAIDIA KITUO CHA ELIMU YA WATU WAZIMA KIGAMBONI

$
0
0
 Mratibu wa Elimu Kata ya Kigamboni Angelina Gaswaswa akipokea maelezo kutoka kwa Mmoja wa waratibu wa kituo cha kutoa elimu ya watu wazima  Mastidia Mbeo.Mratibu huyo wa Elimu amewaomba Wadau kujitokeza kwa kila hali kusaidia kituo hicho cha Elimu ya Watu wazima kilichopo Wilaya ya Kigamboni,jijini Dar.
 Mwenyekiti wa  Serikali ya Mtaa wa Kigamboni, Abdul Habibu  akizungumza wakati alipotembelea kituo hicho cha kutoa elimu ya Watu wazima cha Kigamboni
 Wanafunzi wanaopatiwa elimu ya Watu wazima wakiimba wimbo mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kigamboni akiwa katika picha ya Pamoja na Wanafunzi wa Shule ya elimu ya watu wazima ya Kata ya Kigamboni

Meya wa jiji la Dar Mwita ahudhuria mkutano wa kujadili utawala bora Nchini Marekani

$
0
0
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo ameondoka jijini hapa kuelekea Chicago Nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa Mameya kutoka sehemu mbalimbali duniani utakaofanyika Desemba 4 hadi 7 mwaka huu.

Mkutano huo unatarajiwa kuhusisha Mameya 182 kutoka sehemu mbalimbali Dunia ambapo pamoja na mambo mengine watajadili suala la utawala bora pamoja na utumishi wa viongozi kwa wananchi.

Aidha katika mkutano huo pia wataangalia na kujadili changamoto za majiji makubwa hususani katika sekta ya Afya, miundombinu, Maji safi na salama, Elimu pamoja na mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Desemba 5 Mameya wote waliohudhuria mkutano huo kwa pamoja watashindanisha majiji yaliyofanya vizuri katika sekta ya miundombinu ambapo jiji la Dar es Salaam limeingia kwenye ushindani huo kupitia mradi wa mabasi yaendayo haraka.

Aidha katika ushindani huo, Meya Mwita amesema kuwa ana amini kwamba jiji la Dar es Salaam litaibuka mshindi wa tuzo hiyo kwa kuwa mradi huo umekuwa ukifanya vizuri katika sekta ya usafirishaji na kwamba watanzania wajiandae kwa ajili ya kupokea tuzo hiyo.

Majiji mengine ambayo yanameingia kwenye ushindani huo mbali na jiji la Dar es Salaam ni Mji wa Cape Town, Cairo pamoja na majiji mengine Dunia. Meya Mwita atarajea Nchini Desemba 8 mwaka huu.

Imetolewa leo Desemba 3
Na Christina Mwagala, Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa jiji.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUVUMA ALANI UKABILA UNAOJITOKE KATIKA CHAGUZI ZA VIONGOZI

$
0
0
Mwenyekiti anayemaliza muda wake wachama cha mapinduzi mkoa wa ruvuma ODDO KILLINI MWISHO amesema chama hicho katika mkoa wa ruvuma kimekubwa na ukabila kwa baadhi ya ujumbe wa chama hicho,baada ya kuonekana baadhi ya wilaya zimekuwa na ukabila.hayo ameyasema kabla ya uchaguzi mkuu wa chama hicho mkoa wa RUVUMA kufanyika leo ukisimamiwa na waziri husseni mwishi ambaye pia mlezi katika mkoa huo, huku naye akiomba ridhaa ya kurudi tena madarakani kuweza kukitumikia kwa miaka mitano tena ijayo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA WA LINDI

$
0
0
  Mjumbe wa Kamati Kuu yaTaifa ya  CCM,  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano Mkuu wa CCM wa Mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea Desemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa mkoa wa Lindi wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea, Desemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa mkoa wa Lindi wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea, Desemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa mkoa wa Lindi wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea, Desemba 3, 2017.  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Lindi aliyen'gatuka, Ali  Mtopa baada ya kufungua mkutano mkuu wa CCM wa mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea Desemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAFANYAAKAZI MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB), WAJIPANGA KUBORESHA ZAIDI HUDUMA MWAKA 2018

$
0
0
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.

WAKATI Mwaka 2017 ukifikia ukingoni taasisi mbaliombali nchini zimeanza kuwakusanya watumishi wake na kufanya tathmini ya utendaji na kujadili namna ya kuzikabili changamoto walizokutana nazo ili hatimaye kuongeza ufanisi mwaka ujao 2018.
Miongoni mwa taasisi hizo ni Mwalimu Commercial Bank, (MCB), ambao wamekutana jijini Dar es Salaam, ili kufanya tathmini ya kiutendaji na kuweka mikakati mipya waingiapo mwaka 2018.
Wafanyakazi hao kutoka idara mbalimbali wakiongozwa na Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi pia walipatiwa semina kuhusu masuala mbalimbali ya kiuwajibikaji katika maeneo tofauti kutoka kwa mtaalamu wa kujenga umoja kwa wafanyakazi ili kupata matokeo bora, (Team building consultant), Elizabeth Wachuka.
Ili kuonyesha ushirikiano wafanyakazi hao walibadilishana zawadi mbalimbali ambapo kila mfanyakazi alimuandalia zawadi mfanyakazi anayemvutia zaidi kiutendaji.

 Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
 Wafanyakazi kwa utulizvu kabisa wakisikiliza kilichokuwa kikizunhgumzwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MARY MAJALIWA: WAZAZI WEKEZENI KWENYE ELIMU YA WATOTO

$
0
0
MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewaomba wazazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wahakikishe wanatumia sehemu ya kipato chao katika kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao.

Amesema elimu ndiyo jambo pekee linaoweza kumsaidia mtoto katika kutimiza ndoto zake za maisha pamoja na kumtoa katika kundi la wategemezi.Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumamosi, Desemba 2, 2017), katika maafali ya shule ya awali na msingi ya Wonder Kids, iliyopo wilayani Ruangwa, Lindi.Mke wa Waziri Mkuu alialikwa katika maafali hayo kama mdau wa elimu. Maafali hayo yaliyohusisha watoto wa awali ambao wanaingia darasa la kwanza.

“Walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri, hivyo wazazi watumie kipato chao kuwekeza katika elimu kwani faida watakuja kuiona baadaye.”Alisema kitaaluma yeye ni mwalimu hivyo anatambua kuwa walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri na wanakuwa na tabia nzuri, hivyo wazazi hawana budi kushirikiana nao.

Pia Mama Mary alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi wawatie moyo walimu kwa sababu kazi wanayoifanya ni kubwa. “Wote ni mashahidi watoto wetu tulivyowaleta na sasa ni tofauti.”Alisema ni vizuri wazazi wakashiriki kikamilifu katika suala la elimu kwa watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya masomo yao badala ya kuwaachia walimu peke yao.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mini Ruangwa, Desemba 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza na watoto wakati alipotembelea bwalo la chakula la Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa katika mahafali ya shule hiyo, Desemba 2, 2017. 
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa , Bw. Craig Ferla ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Children in Crossfire akimkabidhi cheti kwa mhitimu wa Mafunzo ya Awali katika shule hiyo, Jasmine Madamba, Desemba 2, 2017.Wapili kuil ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa
Baadhi ya wazazi na waalikwa wa Mahafali ya Kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mjini Ruangwa wakimsikiliza Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa wakati alipozungumza katika Mahafali hayo Desemba 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI JAFO-KUMSOMESHA MTOTO NI IBADA KUBWA KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akizungumza wakati Mahafali ya Shule Mikocheni Islamic ambapo aliwaasa wazazi kuwekeza katika kuwapatia watoto elimu ya Duniani na dini hili waweze kuja kuwa watumishi waadilifu baadae pindi wanapokuja kuwa viongozi wa Umma.
Katibu wa Shule ya Mikocheni Islamic akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo katika mahafali ya shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akikagua Maonesho ya kisayansi ya shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic wakati wa mahafali ya Darasa la Saba ya shule hiyo yaliyofanyika jana.
Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic wakionesha Umahiri wao wa kuimba Kaswida mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kitengo cha Sayansi na walimu wao wa shule ya Msingi Mikocheni Islamic.

DKT MWANJELWA AWATAKA WAJUMBE MKUTANO MKUU CCM MKOA WA MBEYA KUCHAGUA VIONGOZI MAKINI

$
0
0
Na Mathias Canal, Mbeya.

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Leo Disemba 3, 2017 amewasihi Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kuchagua viongozi makini, weledi, wenye nidhamu na kipawa cha uongozi.


Mhe Mwanjelwa ameyasema hayo wakati akitoa salamu za wabunge Wa Mkoa Wa Mbeya kwenye Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya.


Alisema kuwa wajumbe hao hawapaswi kuchagua viongozi kwa sababu ya kufahamiana, Urafiki, Ujamaa au Undugu badala yake wanapaswa kuchagua viongozi wenye maono na mtazamo chanya ili wawe mfano bora katika kukiimarisha na kukijenga Chama Cha Mapinduzi.


Mbele ya wajumbe hao Mhe Mwanjelwa kwa ushirikiano na wabunge wote Wa Mkoa Wa Mbeya wamempatia zawadi ya Pawatila Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi kwa ajili ya Kilimo cha kisasa ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi na ufanisi Wa uongozi wake kama Mwenyekiti katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2012-2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana  na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akifatilia Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.

UZINDUZI WA CHAMA CHA UHUSIANO WA UMMA TANZANIA

$
0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM
Idara ya Habari Maelezo pamoja na Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) wametakiwa  kuungana kwa pamoja na kuandaa Kanuni za Maadili ya Taaluma ya Mawasiliano kwa Umma kwa kuzingatia maslahi ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William alipokuwa akizindua chama cha PRST chenye lengo la kuongeza ueledi kwa wanataaluma ya mawasiliano kwa umma nchini . 
“Ningependa kuona chama hichi kinakuwa mstari wa mbele katika kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanataaluma wake kama lilivyolengo kuwa chama kitajikita zaidi katika kuongeza weledi kwa wanatansia pamoja na kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika sekta ya mawasiliano nchini kwa kulingana na mahitaji ya soko,”Bw.William.
Akiendelea kuzungumza katika uzinduzi huo Naibu Katibu Mkuu huyo alisisitiza kuwa ni vyema wadau wote wa taaluma ya mawasiliano kwa umma watambue umuhimu wa chama hichi kwani wao ndiyo wenye dhamana ya kukikuza,kukiendeleza na kukijengea misingi imara itakayodumu na kuleta tija ndani ya taifa.
Kwa upande wa Mwakilishi wa Msemaji Mkuu wa Serikali kutoka Idara ya Habari Maelezo Bw.Jonas Kamaleki alieleza kuwa serikali inaunga mkono jitihada za kuanzishwa kwa PRST na iko tayari kutoa ushirikiano wakati wote.
“Serikali ingependa chama hichi kuwa na mikakati madhubuti na utekelezaji  wenye tija na hata kuwa mfano kwa Afrika Mashariki bila ya kujali kuchelewa kwa kuanzishwa kwake,”Bw.Kamaleki. 
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Shule ya Habari na Mawasiliano kwa Umma Dkt.Dietrick Kaijanangoma alitoa nasaha kwa Maafisa Uhusiano wa taasisi mbalimbali nchini ya kuwataka kuwa wabunifu na kufanya tafiti ndogo na kubwa kwa ajili ya kuimarisha taasisi zao na zaidi kujifunza kwenda na wakati kwa kutambua mahitaji ya umma. Pamoja na hayo nae Rais PRST Bw.Loth Makuza alitoa shukrani kwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania  Awamu ya Tatu Mhe.Benjamin William Mkapa kwa kuanzisha sekta ya habari nchini.
 Halikadhalika Bw.Makuza alitoa ombi kwa taasisi mbalimbali kuunga mkono uanzishwaji wa chama hicho  pamoja na wanataaluma kujitokeza kwa wingi na kujiunga na chama utaratibu wa kujiunga unapatikana kupitia tovuti ya www.prst.or.tz.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William (watatu kushoto) akikata utepe wa Katiba ya Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) kuashiria kuzinduliwa kwa chama hicho leo jijini Dar es Salaam,aliyeshika Katiba hiyo (kulia) ni Rais wa PRST Bw.Loth Makuza.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William(kushoto) na Rais wa Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST)  Bw.Loth Makuza (kulia) wakionyesha Katiba ya chama hicho kwa wanataaluma ya mawasiliano kwa umma waliyohudhuria uzinduzi wa chama hicho (hawapo pichani)   leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William(wanne kushoto)akimkabidhi cheti  Bw.Innocent Mungy kilichotolewa na uongozi wa chama Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST)  kwa kutambua mchango wake katika kuanzishwa kwa chama hicho mara baada ya uzinduzi  wake leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William(aliyeketi wanne kushoto) mara baada ya uzinduzi wa chama hicho leo jijini Dar es Salaam na  watatu kutoka kulia) ni Rais wa PRST Bw. Loth Makuza.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA ATOA MIEZI MITATU WANANCHI WALIPWE FIDIA WAPISHE ENEO LA HIFADHI

$
0
0
Na Hamza Temba, Mbarali - Mbeya.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kukamilisha malipo ya fidia ya shilingi milioni 771.6 kwa kaya 308 za Kitongoji cha Machimbo ili ziweze kupisha eneo la hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele.

Naibu Waziri Hasunga ametoa agizo hilo jana katika mkutano wa hadhara baada kutembelea kitongoji hicho katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi mkoani humo.

“Kaimu Mkurugenzi (TAWA) kama unavyoona wananchi hawa wapo tayari kupisha eneo hili la hifadhi, wanachosubiri ni malipo yao ya fidia, naagiza mpaka ifikapo mwezi Februari mwakani (2018) wawe wameshalipwa fidia zao, na ikiwezekana hata ndani ya mwezi Januari wawe wameshalipwa,”alisema Hasunga.

Awali akiwasilisha taarifa ya pori hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, David Kenyata alisema wakati pori hilo linaanzishwa mwaka 2002 kwa Tangazo la Serikali Na. 483 wananchi wa kitongoji hicho na vitongoji vingine walikuwa ndani ya eneo hilo la hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele alipotembelea makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wangin'ombe mkoani Njombe. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kanyata na Kaimu Meneja wa pori hilo, Stanslaus Odhiambo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (waliokaa mbele katikati) akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele alipotembelea makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wangin'ombe mkoani Njombe.
Baadhi ya watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (hayuko pichani).
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Machimbo wapatao kaya 308 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ambaye aliwatembelea jana na kuagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania iwalipe fidia ya shilingi milioni 771.6 kabla ya Februari, 2018 ili wapishe eneo la Hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele alipowatembelea.

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images