Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wa pili kutoka (kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Serikali kuashiria ufunguzi rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi hao mara baada ya ufunguzi wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya ufunguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald kuashiria ufunguzi wa wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wanne kutoka kushoto waliokaa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kukagua chumba cha abiria uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mke wake Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge, viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Dini mara baada ya ufunguzi wa uwanja huo wa Ndege.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na kumshukuru Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya shughuli za ufunguzi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba.
Wananchi wakishangilia wakati wa Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya ufunguzi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi huo wa uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera. PICHA NA IKULU

DK. KIGWANGALLA, "SIWEZI KUJARIBIWA NA SIWEZI KUCHEZEWA, SIKO HAPA KWA BAHATI MBAYA"

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Hamdun Mansur (katikati) na Afisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Ndugu Bajuta wakisoma ramani ya Pori Tengefu Loliondo na mpaka wake na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Ngorongoro muda mfupi kabla ya kuaza ziara ya kukagua maeneo hayo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana, pamoja na mambo mengine alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Prof. Alexander Songorwa kwa tuhuma za rushwa na kuhujumu jitihada halali za Serikali za kumaliza mgogoro huo. Aliagiza Mkurugenzi huyo afikishwe TAKUKURU kwa uchunguzi wa tuhuma hizo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana.
Dk. Kigwangalla (kulia) akimuhoji mmoja ya wananchi jamii ya wafugaji alipotembelea Pori Tengefu Loliondo jana.
Waziri Kigwangalla (kushoto) akioneshwa  mpaka wa Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori Tegefu Loliondo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Hamdun Mansuri wakati wa ziara yake ya kukagua iwapo mifugo inaingizwa katika hifadhi ya Serengeti kama ilivyoripotiwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari. 

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

TAFITI ZA KILIMO ZAWAFIKIA WAKULIMA WA WILAYA YA URAMBO KWA MARA YA KWANZA

$
0
0

Na Dotto Mwaibale, Urambo Tabora

TAFITI za kilimo zinazofanywa hapa nchini na wataalamu zimewafikia wakulima wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora kwa mara ya kwanza.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo Adamu Malunkwi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109 na mihogo kwa ajili ya mashamba darasa kwa wakulima wa vijiji nane vya Isongwa, Ussoke, Usisya, Kapiluka, Vumilia, Kamalendi, Muungano na Songambele.

Alisema mara nyingi tafiti zilizokuwa zikifanyika zilikuwa zikibaki kwenye makabati bila ya kuwafikia walengwa na jambo lililofanywa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kuwafikishia wakulima matokeo ya tafiti hizo ni jambo zuri na limefurahiwa na kwa hapa kwetu ni mara ya kwanza kutokea.

"Tuna amini kuwa hivi sasa uchumi utastawi kuanzia ngazi ya familia, wilaya na hadi taifa na tutakuwa na chakula cha kutosha" alisema Malunkwi.
 Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro, akionesha uchimbaji wa mashimo kabla ya kupanda mbegu hiyo ya mahindi.
 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Isongwa, Shabani Rajabu Mkokoteni , akichimba mashimo.
 Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro, akionesha, akionesha namna ya kuweka mbolea kwenye mashimo yaliyochimbwa.
  Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba, akipanda mahindi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ESRF YAWEZESHA WARSHA YA ANDIKO THABITI LA UTAFITI

$
0
0
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewezesha warsha ya siku 3 kuwajengea uwezo watafiti wa ndani waweze kuandika andiko bora la kuombea fedha kwa ajili ya tafiti. Warsha hiyo iliyofadhiliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (International Development Research Centre-IDRC) kupitia Jukwaa la Wanazuoni Wabobezi (Think Tank Initiatives), ilifanyika makao makuu ya ESRF, Dar es salaam. 

Akizungumza Jijini hapa, Mtalaamu Mwandamizi wa Programu ya Think Tank Initiatives anayeshughulikia Sera za Uchumi, Dkt. John Okidi kutoka (IDRC), amesema kwamba watafiti kutoka nchini za Senegali, Tanzania, Uganda, Ghana na Kenya walikutana kwa siku tatu kujadili na kubadilishana mawazo namna ya kujenga uwezo katika kuandika maandiko thabiti ya kuomba fedha kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa. Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko bora ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Wanazuoni (Think Tank Initiatives-TTI) na kumalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Alisema kuna umuhimu wa kufanya andiko linaloeleweka ili kuweza kushawishi watoa ruzuku kutoa fedha za utafiti ili kuharakisha mapinduzi ya viwanda nchini. “Watafiti lazima wawe mstari wa mbele katika kushawishi wanasiasa na viongozi kutegemea zaidi tafiti katika kuleta matokeo chanya kwa wananchi na kusukuma umuhimu wa kutumia tafiti katika kufanya maamuzi kwenye ngazi zote za maamuzi,” aliongeza Dkt. Okidi Alisisitiza umuhimu wa utafiti katika utungwaji wa sera za maendeleo ya kiuchumi hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania inafanya mageuzi makubwa ya kuingia kwenye uchumi wa viwanda. Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance akifungua warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

 Aliongeza kwamba Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo-IDCR ina programu ya miaka kumi ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2019. Alisisitiza kwamba bila tafiti bora na makini ni vigumu kuwa na sera bora zaidi katika utatuzi wa changamoto za binadamu katika maeneo mbalimbali hasa maeneo ya vijijini. Dkt. Okidi amesema kwamba watafiti wana umuhimu mkubwa sana katika kushiriki kwenye ukuaji wa sekta nyingi kama vile gesi, mafuta, biashara na maeneo mengine ya uwekezaji katika kuongeza tija na mafanikio ya uhakika baada ya matokeo ya utafiti. 

MAGAZETI YA JUMANNE LEO NOVEMBA 7,2017

JAFO: TAARIFA ZA WATUMISHI WALIOAJIRIWA 2058 IMEKAMILIKA.

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) amesema jumla ya watumishi wa Sekta ya Afya wapatao 2058 wamekwisha pangiwa vituo vya kazi kuanzia leo 06/11/2017 na taarifa zote zinapatikana kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais TAMISEMI.

“Taarifa ya watumishi 2058 imekamilika na itarushwa kwenye mtandao wa OR TAMISEMI leo tarehe 6/11/2017 jioni, hivyo Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wanatakiwa kujiandaa kuwapokea watumishi hao ikiwemo kuwapatia stahiki zao”

Amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waajiri kuhakikisha wanachukua taarifa za watumishi walioripoti na kuwaingiza kwenye Mfumo wa Mishahara na kuwapangia katika maeneo ambayo ya uhitaji mkubwa ili kuboresha huduma za afya nchini.

Pia ameekeza watumishi wanaopangiwa vituo, kuripoti katika vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 tangu tangazo hili kutolewa.

Aidha, Waajiri wote watoe taarifa juu ya kuripoti kwa watumishio haa wapya na vituo walivyopangiwa siku 14 baada ya kuripoti kwao. Taarifa za Watumishi hao na Vituo vyao vya kazi, inapatikana katika Mtandao wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) wa www.tamisemi.go.tz

HOTUBA YA RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA UFUNGUZI WA UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA

AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA

$
0
0
Imeandikwa na Rais wa Taifa la Palestina, Mheshimiwa Mahmuud Abbas
Waingereza wengi hawamjui “Sir.Arthur James Balfour”ambae aliwahi kuwa Waziri Mkuu mwanzoni mwa karne ya ishirini, lakini jina lake ni maarufu sana kwa Wapalestina wapatao milioni kumi na mbili. Katika kumbukumbu ya azimio la Balfour,serikali ya Uingereza inalazimika kutumia fursa hiyo ili kurekebisha makosa ya kihistoria iliyoyafanya dhidi ya wananchi wetu wa Palestina.

Mnamo Novemba 2,1917 akiwa ofisini kwake mjini London,“Sir.Arthur James Balfour”alisaini barua akiliahidi shirika la kizayuni, kuanzisha taifa lao ndani ya ardhi ya Palestina. Ameahidi kutoa ardhi hiyo wakati sio yake, huku akifumbia macho haki za kisiasa za Wapalestina walioishi katika ardhi hiyo kwa miaka mingi. Kwa Wapalestina ambao ni raia wangu, matukio yaliyosababishwa na barua hii yamekuwa na uharibifu mkubwa, huku pia yakiacha madhara ya muda mrefu kwa wananchi wetu.

Sera ya Uingereza iliyounga mkono uhamaji wa Wayahudi kwenda Palestina, ikiwa ni mbadala wa kukataa kwao haki ya Kiarabu ya Palestina ya kujipangia mustakabali wao, sera hiyo imeleta mvutano mkali kati ya wahamiaji wa Kiyahudi wa Ulaya na wakazi wa asili wa Kipalestina. Palestina iliyokuwa ajenda ya mwisho ya kumaliza ukoloni, inasumbuka kama tunavyosumbuka wananchi wake kutafuta haki yetu isiyo badilika katika kujipangia mustakabali, jambo ambalo ni janga kubwa mno kushuhudiwa na historia ya sasa.

Mnamo mwaka 1948, wanajeshi wa kizayuni waliwafukuza kwa mabavu kutoka katika miji yao, watu wanaofikia milioni moja wakiwemo wanawake na watoto, huku wakifanya mauaji ya kutisha na kubomoa kabisa vijiji kadhaa. Wakati tulipofukuzwa kwa mabavu kutoka mji wa Safad, umri wangu ulikuwa miaka kumi na tatu, wakati Israel ikisherehekea kuasisi taifa lake, sisi Wapalestina tunakumbuka siku ya giza zaidi katika historia yetu. 

Azimio la “Balfour” kwa hakika sio tukio la kusahaulika, kwani wananchi wangu leo wanaofikia zaidi ya milioni kumi na mbili wamesambaa duniani kote, baadhi yao wakilazimishwa kwa nguvu kuacha miji yao mnamo mwaka 1948, huku zaidi ya Wapalestina milioni sita bado wanaishi uhamishoni hadi leo hii, waliosalia katika miji yao ni milioni (1.75) ila wao wanaishi chini ya mfumo wa kibaguzi uliopangika nchini Israel.

Aidha, Wapalestina zaidi ya milioni (2.9) wanaishi Ukingo wa Magharibi wakiwa chini ya uvamizi wa kijeshi na wa kinyama uliogeuka kuwa ni ukoloni. Miongoni mwao wapo wakazi wa Jerusalem ambao ni wa asili kabisa wapatao laki tatu (300,000), bado wanapambana na sera za kivamizi za Israel zinazowahamisha kwa nguvu kutoka katika mji wao. Huku wapalestina wengine wapatao milioni mbili wapo katika Ukanda wa Gaza, ambayo ni gereza la wazi linaloharibiwa mara kwa mara na vifaa vya jeshi la Israel.

MOI:WAGONJWA KULALA CHINI IMEBAKI HISTORIA

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) imekuwa na uwezo wa vitanda 340 ya kulaza wagonjwa na kuachana na kulaza wagonjwa chini ya sakafu iliyokuwa inatokana na ukosefu wa vitanda katika taasisi hiyo.

Uwezo wa MOI kuwa na vitanda hivyo imetokana na jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli kutoa maelekezo ya kutaka watanzania wasipate huduma katika taasisi hiyo wakiwa wamelazwa chini ya sakafu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa MOI, Jumaa Almas, amesema kuwa suala la wagonjwa wanaofika katika taasisi ya MOI kulazwa chini ya sakafu limebaki kuwa historia.

Jumaa amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli alichukua jitihada na kununua vitanda ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora katika hospitali hiyo.

Meneja huyo amesema taasisi ya MOI mazingira ya kutolea huduma katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Dk. Pombe Magufuli, yameboreshwa na kuanza kutumika kwa mradi wa awamu ya tatu ya kupeleka mazingira ya kazi ya kuwa rafiki kwa watoa huduma na wagonjwa.

Jumaa amesema mazingira katika kipindi cha nyuma yalikuwa hatarishi kwa watumishi na wagonjwa kupata maambukizi kutokana na kuwa nafasi finyu ya kuwa na idadi kuliko uwezo wa nafasi.

Amesema awali wodi yenye vitanda 33 ilikuwa inalaza wagonjwa 90 hadi 100 hali ambayo ilikuwa ni wakati mgumu kwa utoaji huduma kwa watumishi kwa nafasi kuwa finyu ambapo idadi ya wagonjwa wa upasuaji imeongezeka hadi kufikia waonjwa 600 hadi 700 kwa mwezi.
Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Jumaa Almas akizungumza na waandishi habari juu ya mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha Rais Dk. John Pombe Magufuli kutoa maelekezo ya kboresha huduma kwa kununua vitanda leo, jijini Dar es Salaam.

SERIKALI IMETOA BURE MBEGU NA VIUATILIFU KWA AJILI YA KILIMO CHA PAMBA KWA MKOA WA SINGIDA.

$
0
0
Serikali imeahidi kutoa bure pembejeo za kilimo kwa wakulima mbali mbali wa zao la pamba mkoani Singida kuanzia msimu huu wa kilimo ikiwa ni moja ya juhudi za kuhamasisha na kufufua kilimo hicho mkoani hapa.  

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga ameeleza hayo juzi katika vijiji vya Kinyangiri na Lyelembo wilayani Mkalama katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku mbili kuhimiza Kilimo cha pamba mkoani Singida. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Kampuni ya Biosustain iliyopo mjini hapa imepewa jukumu la kuleta na kusambaza mbegu na madawa yote yahusuyo kilimo cha pamba bure na kwamba gharama ya pembejeo hizo italipwa na Serikali. 

Kutokana na hilo, Mkurugenzi huyo amewataka Wakulima kutumia vyema fursa hiyo kwa kulima mashamba makubwa zaidi lakini pia kwa kuzingatia tija na ubora wa pamba. Amesema kuwa Wakulima wataweza kufanya hivyo tu iwapo pia watawatumia kikamilifu wataalamu wao wa kilimo na kufuata Kanuni na Taratibu za kilimo bora. 
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi mmoja kati ya wa wakulima wa Pamba wa kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama kilo kumi za mbegu za zao la pamba zilizotolewa bure na Serikali kwa wakulima hao. Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga.
 Mkulima wa Pamba Bi Johari kutoka kijiji cha Kinyagiri Wilayani Mkalama akibeba mbegu za Pamba kilo kumi alizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi, mbegu hizo zimetolewa bure kwa wakulima wa Pamba Mkoa wa Singida.
 Mama Devid Mkulima wa Pamba wa Kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama akijifunza kwa vitendo namna ya kuandaa kamba inayotumika kuonyesha vipimo vya upana na urefu katika kupanda pamba badala ya kilimo cha mazoea cha kumwaga mbegu bila kufuata kipimo chochote.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
  Waziri wa  Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamad Rashid Mohamed (katikati) alipowasilisha Muhtasari wa  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017, wakati wa kikao cha siku moja cha  Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)wengine ni  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa BLM pia Kaimu Katibu Mkuu  Kiongozi Nd,Salum Maulid Salum (kulia) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Nd. Lulu Msham Abdalla.
Katibu Mkuu  Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi alipokuwa akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika kikao cha siku moja  cha  Wizara hiyo  kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo p ichani),akiwepo na Naibu Katibu Mkuu Maryam Juma Abdulla Saadalla (kulia)
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi,wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),alipozungumza na Uongozi wa Wizara  hiyo  katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja (Picha na Ikulu)

Raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu ailalamikia Mahakama

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan ameilalamikia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juu ya mashahidi kutofika mahakamani licha ya kesi inayomkabili kupangwa kusikilizwa mfululizo na kuuliza iko wapi kauli ya Rais Magufuli ya hapa kazi tu.

Feng anakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi anadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889 zenye thamani ya Sh 13 bilioni  bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori. 
Katika kesi hiyo anashtakiwa pamoja na watanzania wawili Salvius Matembo na Philemon Manase.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, mshtakiwa Feng amedai kuwa alimsikia Jaji Mkuu akisema kesi zote za zamani zimalizike kwa Haraka, lakini kesi yake imekuwa ikipangiwa kusikilizwa mfululizo mara lakini shahidi anayetakiwa kutoa ushahidi hajawi kwenda mfululizo hata mara moja.

"Magufuli anasema hapa kazi tu, nikasema sasa mahakama ile kazi haipo kwa haraka, nipo mahabusu naumwa moyo, misuli inauma, kidole kimekufa ganzi, lakini najitahidi nakuja". aliomba kesi ikipangwa tarehe nyingine mashahidi waje na kuuliza kama shahidi mmoja anaumwa je wengine wote wanaumwa?

Mshtakiwa Feng amedai hayo baada ya wakili wa serikali, Wankyo Simon kuieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa kusikilizwa lakini shahidi aliyetarajiwa kutoa ushahidi anaumwa, hali yake bado siyo nzuri.

Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko, aliomba mahakama iliangalie hilo na kuwa waendelee na mashahidi wengine wa upande wa Mashtaka katika kuokoa muda.

Wakili Wankyo alidai kuwa katika hali ya kawaida ni lazima shahidi huyo amalizie kutoa ushahidi wake. Hakimu Shaidi aliutaka upande wa Mashtaka kupelekwa mashahidi  kama huyo hatakuwa hajatengemaa.

Kesi hiyo imeahirishwa na itasikilizwa Mfululizo, Novemba 21,24,27,28,29,30 na Decemba Moja.

Driving cost-effective African broadband adoption with WTTx

$
0
0
Despite the rapid advancement in information communication technologies (ICT) globally, the vast majority of people across Africa remain either unconnected, or only have access to slow internet connections. On the continent, the average broadband penetration rate sits at less than 1%, while 80% of connected households have to make do with bandwidth of less than 2Mbp/s. While approximately 20-million households in the region are in dire need of access to broadband.

While copper cables and/or optical fibre is often used to deliver stable and fast home broadband (HBB) services in cities with favourable economic conditions, providing similar infrastructure beyond urban areas is more challenging.  Wired access deployment is costly, time-consuming and expensive to maintain, while sparser populations and lower disposable income levels in rural areas results in a poor return on investment (ROI), and it becomes clear that an alternative is needed.

Fibre-like experience

Huawei’s Wireless to the X (WTTx) broadband is the ideal solution for operators looking to expand coverage beyond urban centres. Based on 4.5G wireless broadband technologies, including massive MIMO and carrier aggregation, WTTx significantly improves spectral efficiency and provides bandwidth of over 1 Gbp/s, giving home users a fibre-like experience. High-gain plug and play customer premise equipment (CPE) - a wireless household gateway - is used to provide the entire range of mobile broadband (MBB) services for end users, including video broadcasts, VoIP, enterprise networks, and even VR movies, and gaming. 

Unlike copper or fibre, which requires trenching and/or pole installations, operators can leverage existing 4G base stations for WTTx, significantly reducing network deployment time and costs, while also helping operators to increase their monthly average revenue per user (ARPU).
ITU statistics show that 148 countries around the globe have proposed national broadband strategies to enhance the broadband penetration rate and internet experience. Many operators in sub-Saharan Africa consider WTTx as a top priority, and have provided WTTx broadband access to over 1 million households by 2017. 

Complementary technologies

WTTx can be deployed during initial stages of broadband service development to understand local broadband requirements; if user has higher experience requirement, operators are advised to focus on FTTx to improve user experience and increase revenue.  In villages and towns with FTTx networks and close to large cities, operators can provide WTTx-based differentiated products to develop a competitive edge, boasting both complementary fixed and mobile networks. WTTx+FTTx hybrid networking mode allows operators to quickly gain broadband users, shorten ROI periods, and improve ROI.

International successes of the innovative WTTx solution has help operators to develop and gain revenue in a blue ocean market, and the technology is expected to be a key contributor to increasing broadband penetration and connecting ‘the next billion’.

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO, AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO YA TAIFA KWA MWAKA 2018/19 NA MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2018/19

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, akiwasilisha Bungeni Mjini Dodoma, Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2018/2019 na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/2019.

SAFARI YA NDEMLA YASOGEZWA MBELE, SASA KUONDOKA ALHAMIS

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tunapenda kuwafahamisha kuwa safari ya mchezaji wetu Hamis Said Juma Ndemla iliyokuwa ifanyike leo Jumanne imesogezwa mbele.

Ndemla ambaye amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden ,sasa ataondoka nchini siku ya Alhamis ya tarehe 9 ya mwezi huu.

Mabadiliko haya ya safari hayataathiri muda wake wa majaribio katika klabu hiyo,ambapo atakuwa huko kwa siku 14.

Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,

Simba Sports Club.



Haji S.Manara.

7/11/2017

Simba Nguvu Moja..!!!

DKT. NDUMBARO AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUZINGATIA UADILIFU, KUJITUMA NA KUWAJIBIKA KWA WANANCHI

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa maelekezo mbalimbali ya masuala ya kiutumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri ya Wilaya ya Madaba Bw. Shafi Mpenda na kushoto kwakwe ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bw. Bwai Biseko.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bw. Biseko Bwai akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo mkoani Ruvuma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Ibrahim Mahumi akitoa maelekezo kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini kuhusu taratibu zinazohusu menejimenti ya Rasilimaliwatu serikalini, wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ya kuhimiza uwajibikaji.
Baadhi ya watumishi wa Hamashauri ya Wilay ya Songea Vijiji wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya katibu mkuu huyo ya kuhimiza uwajibikaji katika Hamashauri hiyo.

WASHINDI WA DROO YA KWANZA WA PROMOSHENI YA ZALI LA MWANASPOTI WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

$
0
0
KAMPUNI ya Mwananchi Communications Limited kupitia Gazeti la Michezo la Mwanaspoti, imekabidhi zawadi za droo ya kwanza ya Promosheni ya Zali la Mwanaspoti ikiwa ni zawadi kwa wasomaji kuelekea mwisho wa mwaka.

Zawadi hizo mbalimbali sita zikiwemo simu mbili(Smartphone), Tv mbili nchi 32 zikiwa na vinga’amuzi vyake vya Azam huku zikiwa zimelipiwa mwzi mzima,Pikipiki moja na ticketi moja ya kwenda kushohudia moja ya mechi kubwa nchini Wingereza.

Makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.   
Mshindi wa Pikipiki, Joachim Gibson akikabidhiwa Kadi na Funguo wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa droo ya kwanza ya Promosheni ya Zali la Mwanaspoti iliyofanyika Viwanja vya Taifa.
Meneja Masoko wa Mwananchi Communications Limited, Sarah Munema (kushoto) akimkabidhi Aristides Alphonce, zawadi ya ticketi ya Uingereza mara baada ya kuibuka mshindi wa droo ya kwanza ya Zali la Mwanaspoti katika hafla fupi iliyofanyika Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.
Meneja wa vipindi vya Michezo wa Azam TV, Baruani Mhuza(kulia) akimkabidhi Mkombozi Mubanga, zawadi ya TV nchi 32 ikiwa na king’amuzi cha Azam TV kikiwa kimelipiwa mwezi mzima mshindi wa droo ya kwanza ya Zali la Mwanaspoti katika hafla fupi iliyofanyika Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Masoko wa Mwananchi Communications Limited, Sarah Munema.

SAMATTA NJE WIKI SITA, AUMIA GOTI SASA KUWAKOSA BENIN NOV 12

$
0
0
NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ anayekipiga na KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta atakuwa nje ya uwanja kwa majuma sita akiuguza majera ya goti aliyopata katika mchezo wa ligi kuu uliomalizika kwa sare tasa dhidi ya Lokeren.

Samatta alishindwa kuendelea na mchezo baada kuumia dakika ya 40 nafasi yake ikachukuliwa na Nikos Karelis aliyerejea hivi karibuni baada ya kukaa nje kwa muda mrefu pia kutokana na majeraha.

Ripoti ya daktari iliyotokana na majibu ya vipimo alivyofanyiwa straika huyo jana inasema amepata jeraha dogo katika misuli ya goti inayofahamika kitaalamu kama ‘Literal Ligament’ huku pia maungio ya mfupa wa paja na wa ugoko (meniscus) yakionekana kuathirika pia.





“Literal ligament imechanika kidogo, hiyo itapona yenyewe lakini pia wamegundua tatizo kwenye meniscus ambalo inabidi lifanyiwe upasuaji mdogo ili lisije kuleta shida hapo baadae,” alisema Samatta

Upasuaji huo mdogo utamlazimisha Samatta kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita akipata tiba na mazoezi huku timu yake ikiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Ubelgiji baada ya kukusanya pointi 19 pekee.

Samatta ndiye mshambuliaji tegemeo klabuni hapo akiwa amejihakikishia nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza licha ya kuwepo kwa wakali kadhaa.

By Boiplus Media.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images