Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

aliyekutwa akimiliki mali na kuishi maisha yasiyolingana na kipato chake halali kusomewa maelezo ya awali (PH) Desemba 6, 2017

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, kesi dhidi ya Afisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi anayekabiliwa na mashtaka mawili ikiwamo la kukutwa akimiliki mali  na kuishi maisha yasiyolingana na kipato chake halali atasomewa maelezo ya awali (PH). Desemba 6 mwaka huu

Jennifer ambaye yuko nje kwa dhamana ameshtakiwa chini ya kifungu cha 27, (1) (a) na (b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11ya mwaka 2007.
Keai hiyo ilikuja leo kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa PH lakini Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter alidai baso hawajamaliza kuiandaa maelezo hayo kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa

Hakimu Shaidi aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 6 mwaka huu.

Katika kesi hiyo mshtakiwa anadaiwa kuwa  kati ya Machi 21, mwaka jana na Juni 30, mwaka huu  jijini Dar es Salaam  akiwa  mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimili magari 19

Magari hayo ni   Toyota RAV4, Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Viz, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota Wish na  Toyota Mark X.

Mengine ni Toyota Regiusage, Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown,  Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na Suzuki Carry yote yakiwa na thamani ya Sh 197,601,207 Mali ambayo hailingani na kipato chake halali.

Pia anadaiwa kati ya Machi  21 ,2012 na  Machi 30,2016 Dares Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akiishi maisha ya kifahari  yenye thamani ya Sh 333,255,556.24 fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali.

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya nchini India wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagonjwa 18 wenye matatizo ya Moyo

$
0
0
Madakatati Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Saifee ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) wakati wa kambi maalum ya upasuaji ya siku sita inayoendelea katika Taasisi hiyo. Hadi sasa jumla ya wagonjwa sita wameshafanyiwa upasuaji wa CABG na kubadilishiwa milango ya moyo (Valve) ambapo hali zao zinaendelea vizuri.
Madakatati Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Saifee ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) wakati wa kambi maalum ya siku sita ya upasuaji wa moyo inayoendelea katika Taasisi hiyo.
Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Saifee ya nchini India wakiendelea na kazi ya kumfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) . Jumla ya wagonjwa 18 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo ya siku inayoendelea katika Taasisi hiyo. Picha na JKCI.

Vigogo wanne Tanesco kizimbani kwa ubadhirifu wa fedha zaidi ya bilioni 2.7

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Maofisa wanne wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco )na watu wengine wawili, leo Novemba 7, 2017 wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka 202 ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 2.7.

Hati ya Mashtaka imesomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi aliyekuwa akisaidiana na wakili wa serikali Gloria Mwende ambapo watuhumiwa wote wanakabiliwa na shtaka moja la kula njama, kutoa taarifa za uongo, kuisababishia hasara serikali na mashtaka 199 ya wizi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa washtakiwa hao ametajwa kuwa ni, Afisa Mapato Mwandamizi, Emmilian Mlowe, Mhasibu wa Mapato msaidizi, Shakira Ngella,  meneja wa fedha mwandamizi Mkama Maira na Mhasibu wa udhibiti wa Mikopo Yaned Jonas.

washtakiwa wengine ni, Bashiru Ngella na Barnabas Massaly.
Imedaiwa kuwa, kati ya Januari 7, 2014 na Januari 31,2015 jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote hao walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka la pili, imedaiwa kuwa, tarehe hizo, katika ofisi ya Tanesco Kinondoni, iliyopo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa, Mlowe,Ngella,  Maira na Jonas wakiwa ni waajiriwa wa Tanesco Kinondoni, wakiwa na uwezo uwezo wa kuingia katika mfumo wa kompyuta unaojulikana kama Tansms33, wakiwa na nia ya kulaghai walifanya maingizo ya uongo katika mfumo huo ya kiasi cha  Sh 2,746,485,545.63 wakijaribu kuwa kuonyesha kuwa fedha hizo zililipwa kwa Tanesco  na mawakala wa tatu (Luku Vendos) kama manunuzi ya umeme wa Luku (unit).

Katika shtaka la 202 washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la kusababisha hasara ambapo wanadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi ,2014 na Machi 31,2016 washtakiwa hao kwa matendo yao waliisababishia Tanesco kupata hasara ya Sh 2,746,485,545.63/-. Washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuongea kitu chochotemahakamani hapo kwa sababu Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi Mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa upande wa Mashtaka, upelelezi wa kesi huyo bado haujakamilika na washtakiwa wamerudishwa rumande hadi Novemba 2, mwaka huu. Hakimu Nongwa amewashauri washtakiwa hao kuomba dhamana katika Mahakama Kuu kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu Mahakama ya Mafisadi.

SERIKALI YAAGIZA MIKOA KUANDAA MAPOKEZI KWA WANAFUNZI WATAKAOJIUNGA KIDATO CHA KWANZA, 2018

$
0
0
Na Fred Kibano
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani S. Jafo (Mb), ameiagiza Mikoa yote nchini kuanza mapema maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2018, kufuatia kuongezeka kwa ufaulu.
Mhe. Jafo ametoa kauli hiyo mjini Dodoma, wakati akiongea na Waandishi wa Habari, juu ya kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka, 2018,
“Wakuu wa Mikoa hakikisheni miundombinu iliyopo inatosha katika mikoa yenu ili watoto wote waliofaulu, wapate nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza hapo Januari, 2018”, ameitaja mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Kagera, Njombe, Tanga, Morogoro, Lindi, Rukwa, Pwani, Mtwara na Songwe kuwa na idadi kubwa zaidi na hivyo maandalizi ya madarasa, vyoo na madawati yatahitajika kwa kiwango kikubwa.
Aidha, amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa, kusimamia zoezi la uchaguzi wa wanafunzi tarajiwa wa kidato cha kwanza ili ifikapo Desemaba 8, 2017 wawe wamekwisha tangaza.
Mhe. Jafo ameagiza kufanyika uchambuzi ili kubaini sababu zilizopelekea watahiniwa zaidi ya asilimia moja kutofanya mitihani katika mikoa ya Geita, Katavi, Mara, Rukwa, Songwe, Dodoma na Manyara kwa lengo la kuondoa mdondoko wa wanafunzi kutoka ngazi moja hadi nyingine.
Pia amezitaka Halmashauri zilizopata ufaulu chini ya asilimia hamsini kujiwekea mikakati ya kupandisha ufaulu wa wanafunzi, Halmashauri hizo ni pamoja na Mkalama, Meatu na Simanjiro.
Matokeo ya darasa la saba, yalitangazwa rasmi hivi karibuni, ambapo jumla ya watahiniwa wapatao 662,035 walifaulu kwa kupata madaraja ya A, B na C, ikiwa ni sawa na asilimia 72.76 ya watahiniwa wote.
Ofisi ya Rais TAMISEMI, yenye dhamana na usimamizi wa Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari imechukua hatua za makusudi, ili kupunguza au kuondoa wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba kutopangiwa shule na kujiunga na kidato cha kwanza mwaka, 2018.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani S. Jafo (Mb), akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Maagizo aliyoyatoa kwa Mikoa kuwapokea wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka, 2018. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda na Mkurugenzi Msaidizi (ELIMU SEKONDARI) OR TAMISEMI.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani S. Jafo (Mb), akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Maagizo aliyoyatoa kwa Mikoa kuwapokea wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka, 2018. 
Wanafunzi (watahiniwa) wa shule ya Msingi Miningani, Halmashauri ya Mji, Kondoa, Dodoma wakifanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIWASIKILIZA MAWAZIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Selemani Jaffo wakati wa Kikao cha kwanza Mkutano wa tisa wa Bunge kilichoanza leo Novemba 7, 2017 mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Umi Mwalimu wakati wa Kikao cha Kwanza Mkutano wa tisa wa Bunge kilichoanza leo Novemba 7, 2017 Mjini Dodoma
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA WADAU WA MASUALA YA AJIRA NA UKUZAJI UJUZI

$
0
0
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisistiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha wadau wa masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kilichofanyika Mjini Dodoma Novemba 7, 2017.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi akisisitiza jambo kuhusu mkakati wa Serikali kuboresha mazingira ya Ajira hapa nchini walipokutana leo Mjini Dodoma katika kikao cha Wadau wa masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw .Geodfrey Simbeye akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akichangia mada kuhusu ushiriki wa watu wenye ulemavu katika programu zinazotekelezwa na Serikali katika masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi ili kujikwamua kiuchumi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

AZAM FC WAACHANA NA MSHAMBULIAJI WAO WA KIMATAIFA YAHYA MOHAMED

$
0
0


Uongozi wa klabu ya Azam FC imeamua kuvunja mkataba na mshambulizi wake, Yahaya Mohammed raia wa Ghana baada ya kuona ameshindwa kuwapatia kile ambacho wanakihitaji kwa muda wote aliokuwa ametumikia kwenye klabu hiyo.

Mwishoni mwa wiki baada ya mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting , Kocha Mkuu wa Azam  Aristica Cioba aliweka wazi mkakati wake wa kutaka kupata washambuliaji  wengine wawili ili kuongeza nguvu ya kikosi chake.

Akitoa ufafauzi wa maamuzi hayo, Msemaji wa Azam Jaffary Idd Maganga alisema kuwa wamefikia uamuzi wa kuvunja mkataba na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 baada ya kuonesha kiwango duni tofauti na matarajio yao walipomchukua mwaka jana wakati wa dirisha Dogo la usajili.

"Nichukue nafasi hii kuwafahamisha kwamba hatutaendelea kuwa naye, uongozi umekutana naye, wamezungumza kuhusiana na suala lake na wamemalizana. Hivi sasa Mohamed sio mchezaji tena wa Azam  baada ya makubaliano kati yake na uongozi," alisema ..

Maganga amesema tayari wameshampatia release letter na pamoja na hayo tayari wameshampatia kila kitu ikiwemo tiketi ya ndege ambapo wanatarajia ataondoka kurudi kwao Ghana Jumanne hii.

"Tutamkumbuka Yahaya, kwa Maana kwamba yale ambayo ameyafanya kwenye timu yetu, ametusaidia kupata ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na pia msimu ndiye aliyefunga bao la kwanza," alisema.

Mbadala wa Yahaya Mohamed kwa mujibu wa Afisa Habari Jaffary Maganga, ni kwamba atatangazwa baada ya benchi la ufundi kufanya tathmini na kuchambua wale wanaowahitaji.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Azam akitokea Aduana Stars ya Ghana, ambayo aliisaidia kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ghana msimu 2015/16, Mohammed pia aliiibuka mfungaji bora namba mbili wa ligi hiyo kwa mabao 15 aliyofunga nyuma ya Latif Blessing wa Liberty Proffesional aliyetupia 17.

Mohammed alikuwa moja ya wachezaji  kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ghana kilichoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizofanyika mwaka juzi nchini Afrika Kusini na timu hiyo kuwa washindi wa pili.

WADAU WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA BIASHARA


"HAKUNA UPUNGUFU MKUBWA WA DAWA NCHINI"-MHE.UMMY MWALIMU

TAMBWE, KAMOSOKU NA NGOMA MATARAJIO NI KUANZA MAZOEZI MEPESI WIKI HII- DR BAVU

$
0
0
Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tz Prison Novemba 19.

Mazoezi hayo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru, Yanga  wamefanya mazoezi bila nyota wao nane walioitwa katika timu za taifa pamoja na mjeruhi watatu ambao ni kiungo Thabani Kamusoko, Washambuliaji Donald Ngoma  na Amissi Tambwe.

Lakini imewakosa wachezaji wake watano walioitwa katika timu za taifa kubwa na ile ya vijana.Walioitwa katika timu ya taifa, Taifa Stars ni Ramadhani Kabwili, Kelvin Yondani, Gadiel Michael, Raphael Daud na Ibrahim Ajibu Migomba.

Kwa mujibu w daktari wa timu Dr Edward Bavu  ameweka wazi kuwa majerehui hao wanaweza kurejea dimabni Novemba 10 kwa ajili ya kuanza mazoezi mepesi na kisha kujiunga na wenzao kwa mazoezi ya pamoja.

Kwa sasa hawajafika asilimia 100 ila sio Ngoma pekee, bali hata kiungo  Kamusoko na Tambwe pia wanaweza kuanza mazoezi wiki. Matarajio yetu hadi wiki ijayo watakuwa wameungana na wenzao kikamilifu."

Ngoma ambaye kwa sasa yupo nchini kwao akiendelea na matibabu atarejea siku yoyote kwa ajii kujiunga na wenzake akianza mazoezi ya taratibu.

Yanga wanaoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 17 wataumana na Tz Prisons wakiwa wametoka kupata sare tasa dhidi ya Singida United mwishoni mwa wiki hii.

Vijiji Vyote Visivyo na Umeme Kupata Umeme Ifikapo 2020/21

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

Serikali imesema itahakikisha vijiji vyote visivyo na umeme vinapata umeme kupitia mradi wa kupeleka umeme vijijini awamu ya Tatu (REA-III) unaotegemewa kukamilika mwaka 2020/21.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni, Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nachingwea Hassan Masala juu ya mpango wa Serikali katika kusambaza umeme katika kata zilizobaki wilayani Nachingwea kupitia REA III.

“Mradi wa REA III utajumuisha vipengele vitatu vya Densification, Grid Extension na Off gridrenewable ambapo Mkoa wa Lindi chini ya miradi ya uendelezaji wa grid (Grid extension) katika Mzunguko wa kwanza unatekelezwa kwa muda wa miezi 24 na Kampuni ya Stategrig & Technical Works Ltd,” alifafanua Naibu Waziri huyo.

Aliendelea kwa kusema, katika wilaya ya Nachingwea mpango wa Awamu ya Tatu utavipatia umeme vijiji 30 ambapo kazi za utekelezaji wa mradi zilianza Julai mwaka huu na zinatarajiwa kukamilika Juni 30, 2019.Mgalu amesema, vijiji vilivyobakia vitapatiwa umeme katika mzunguko wa pili wa REA III utakaoanza Aprili, 2019 hadi Desemba 2021.

Vile vile amesema, kazi ya kupeleka umeme mzunguko wa kwanza itahusisha ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 380, ufungaji wa transfoma 18, ujenzi wa njia za msongo wa kilovoti 0.4 zenye urefu wa kilomita 360 na uunganishaji wa wateja 5,710 katika Mkoa mzima wa Lindi.

Aidha amesema, kwa upande wa Wilaya ya Nachingwea jumla ya wateja 1,200 wataunganishwa, ambapo kwa sasa Mkandarasi anaendelea na upimaji wa njia za umeme na tayari amefikia asilimia 30 na kazi za upimaji zitakamilika mwishoni mwa Novemba 2017.

SERIKALI YALIPA MADAI YA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA TTCL SH. BILIONI 12.7

$
0
0
Benny Mwaipaja, Dodoma
SERIKALI imewalipa pensheni wafanyakazi 245 wa iliyokuwa Kampuni ya Simu ya TTCL, chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kiasi cha shilingi bilioni 12.7.
Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Ludewa Mhe. Deogratias Ngalawa, aliyetaka kufahamu, lini Serikali ingewalipa wafanyakazi wa TTCL wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki madai ya pensheni yao.
Dkt. Kijaji alisema kuwa malipo hayo yamefanyika kwa wafanyakazi 245 ambao wamelipwa fedha zao kwa mkupuo ambapo kati yao wastaafu 54 walifariki dunia na malipo yao kulipwa warithi wao.
“Wastaafu 198 wanaendelea kulipwa malipo ya nyongeza ya pensheni ya kila mwezi” alisema Dkt. Kijaji.Alisema kuwa malipo hayo yanafuatia uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi namba 69/2005 ambapo wafanyakazi hao 254 waliishitaki Serikali kupinga uamuzi wa kusitisha mfuko uliojulikana kama East Africa Non Contributory Pension Scheme.
 “Katika Shauri hilo, Mahakama Kuu iliamua kuwa, uamuzi wa Serikali kusitisha mfuko huo haukuwa sahihi kisheria na hivyo kuamua wafanyakazi 254 waliokuwa katika shauri hilo walipwe madai yao ambayo yalijumuisha malipo ya mkupuo, riba pamoja na pensheni yao ya kila mwezi” aliongeza Dkt. Kijaji.
Alisema kuwa baada ya uamuzi huo wafanyakazi wengine 324 nao walifungua kesi Makahama Kuu wakitaka walipwe pensheni kama wenzao walivyolipwa wakati hawakuwa sehemu ya wafanyakazi waliofungua na kushinda kesi hapo awali.“Mahakama Kuu iliamua kuwa, wafanyakazi waliofungua kesi ya awali ndio walipwe madai yao, na kwamba deed of settlement iliyosajiliwa Mahakamani ilihusisha wafanyakazi hao pekee” alifafanua Dkt. Kijaji.
Alisema wafanyakazi wengine ambao hawakuwa sehemu ya kesi hiyo hawawezi kulipwa kwa kutumia hukumu na tuzo ya kesi ambayo hawakuwa sehemu yake na kusisitiza kuwa, Serikali haiwezi kulipa madai mengine ambayo hayakuthibitika kisheria.

WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII WAJADILI MBINU ZA KUIMARISHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO

$
0
0
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akitoa mada kwa wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuhusu kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo yao katika Mkutano Kazi wa mwaka unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai akiwasilisha mada ya Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa Mkutano Kazi wa Mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi akiwasilisha mada ya kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake nchini wakati wa Mkutano Kazi wa Mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Watoto Bibi Rose Minja akiwasilisha muhtasari wa utafiti wa Shirika la UNICEF kuhusu vichocheo vya ukatili dhidi ya watoto na mabadiliko chanya Tanzania wakati wa Mkutano wa Kazi mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya jamii Unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.
Mratibu wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii kutoka OR TAMISEMI Bi. Mwajina Lipinga wakati wa Mkutano wa Kazi mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya jamii Unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma. 
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma Bw. Deogratias Rwambo akiwasilisha hoja wakati wa siku ya pili ya Mkutano wa Kazi mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya jamii unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma kwa lengo la kuamsha ari ya kufanya kazi na kutokomeza ukatili ili kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha Bibi Janet Mashasi akiuliza swala wakati wa siku ya pili ya Mkutano wa Kazi mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma kwa lengo la kuamsha ari ya kufanya kazi na kutokomeza ukatili ili kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya zote nchini wakifuatilia mijadala ya kuhuisha ari ya wananchi kuitikia kazi za maendeleo yao na kujenga uelewa kuhusu agenda ya kushiriki katika kufikia uchumi wa kati na wa viwanda wakati wa Mkutano wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya jamii unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

…………

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wameendele kujadili jinsia ya kutekeleza kampeni ya Wizara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ya jamii na mbinu mahususi katika kufanikisha utekelezaji wa programu mbalimbali zinazohusiana na maendeleo jumuishi ya jamii zetu. 

Mbinu hii ina wawezesha wataalam wa maendeleo ya jamii katika sekta za umma na sekta binafsi kuhusisha wananchi kubainisha rasilimali na uwezo wa kitaalamu katika kuanzisha miradi ya kimaendeleo na kiuchumi ambayo inalenga kukuza ustawi wa watu wenyewe.

Mpango wa kuamsha ari ya kushiriki kazi za maendeleo ya Taifa unahitaji umuhimu mkubwa wa takwimu katika kupima matokeo ya utekelezaji wa miradi na uwekezaji kuanzia ngazi ya Kata mpaka taifa.

Vipaumbele vinavyotakiwa kuzingatiwa katika utekelezaji wa ari ya watu kushiriki miradi ya maendeleo ya jamii ni ushiriki wa wananchi kuanzia hatua za awali, kujenga hamasa ya jamii kujitambua na kujiamani katika kujiletea maendeleo yao, kuhimiza jamii kuelewa haki zao na fursa zilizopo katika mazingira yao kuwa na uwakilishi maalum wa jamii husika kuweza kusushughulikia vikwazo vilivyopo, na kutumia taarifa za kiutafiti.

Uamshaji wa ari unaweza kufikishwa kwa wananchi na kujenga uelewa wa wananchi wanaohusika na mradi huo katika kutoa mchango wa kufanya kazi za kujitolea.

Njia hii ya kuamsha ari ikitekelezwa ipasavyo, na maafisa maendeleo ya jamii wakawezeshwa itachochea kwa kiasi kikubwa kubadili mitazamo ya hasi na kuwa na mitazamo chanya maana watashiriki ipasavyo katika katika shughuli za maendeleo yao kuanzioa ngazi ya kaya, jamii, na hadi Taifa na hivyo kutoa mchango katika kujenga Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati.

Mkutano huu unatarajia kutoka na mapendekezo ya vikundi/ kanda ambayo yataenda kutekelezwa katika mikoa na halmashauri husika ili kupata uelewa wa pamoja na mchango kufkia uchumi wa kati na viwanda sanjari na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimi 50 ifikapo mwaka 2021/2022.

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA KYAKA-BUGENE WILAYANI KARAGWE

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua rasmi barabara ya Kyaka-Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakipeana mikono baada ya Rais kufungua rasmi barabara ya Kyaka-Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na viongozi wengine wakimsaidia kushika utepe anaoukata kama ishara ya kufungua rasmi barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua rasmi barabara ya Kyaka-Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mzee Nekemia Kazimoto (80) na mkewe Florence Kazimoto baada ya sherehe za kufungua rasmi barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijumuika katika sala na Mzee Nekemia Kazimoto (80) na mkewe Florence Kazimoto na binti yao  Lucy Kazimoto alipomtembelea kumjulia hali baada ya sherehe za kufungua rasmi barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi wa mjini Bukoba waliomsimamisha ili awasalimie wakati akirejea kutoka Karagwe kwenye  sherehe za kufungua rasmi barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017. Picha na Ikulu

MAVUNDE AWAPA NEEMA WAJASIRIAMALI DODOMA MJINI

$
0
0
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini leo amefungua semina ya wajasiriamali wapatao 2000 wa Jimbo hilo.

Semina hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Cavilam wilayani Dodoma ambapo wajasiriamali hao watapata nafasi ya kujifunza juu ya elimu ya Ujasiramali na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.

Aidha amesema kupitia semina hiyo watatoa walimu 205 ambao watazunguka katika kata zote 41 za Dodoma Mjini kwenda kufundisha vikundi vya wakinamama,Vijana na Wazee katika masuala ya utengenezaji bidhaa na kuongeza thamani,Ufugaji wa Kuku, Samaki na Mafunzo ya kilimo Bora.

Mavunde amesema baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo litaandaliwa kongamano lingine kubwa litakalohusisha Taasisi za fedha na Mifuko ya Uwezeshwaji ili wajasiriamali wapate fursa ya kufahamu namna ya kuifikia mikopo na ruzuku zitakazosaidia upatikanaji wa mitaji ya kufanyia shughuli za uzalishaji mali.
 Mbunge wa Dodoma mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akifungua semina ya wajasiriamali Dodoma.
 Mbunge wa Dodoma mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akizungumza na wajasiriamali.
Washiriki wa semina ya ujasiriamali



VIAZI LISHE KUTOLEWA KWA WANAFUNZI SIKONGE MKOANI TABORA

$
0
0

Na Dotto Mwaibale, Sikonge Tabora

WANAFUNZI wilayani Sikonge mkoani Tabora wataanza kunufaika na viazi lishe baada ya kupokea mbegu bora ya viazi hivyo, mihogo na mahindi ya Wema kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

Hayo yameelezwa katika Kijiji cha Kisanga na Mkuu wa Wilaya hiyo, Peres Boniface Magiri wakati akizungumza na wakulima kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na viazilishe kwa ajili ya mashamba darasa katika vijiji vya Isunda, Kisanga, Udongo na Kanyamsenga.

Magiri alisema baada ya kuotesha mbegu hiyo ya viazilishe kwa wingi kitakachofuata ni kuanzisha utaratibu wa wanafunzi katika shule mbalimbali za wilaya hiyo kupata chakula cha mchana badala ya kwenda nyumbani.

Alisema wilaya hiyo kupelekewa mbegu hizo kwao ni fursa kubwa na kwa kushirikiana na wakulima na maofisa ugani atahakikisha mashamba darasa hayo yanatunzwa na kutoa mrejesho.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa (kulia), akimkabidhi mbegu ya mahindi aina ya Wema, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Peres Boniface Magiri wakati wa uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na viazi lishe kwa ajili ya mashamba darasa katika vijiji vya Isunda, Kisanga, Udongo na Kanyamsenga wilayani humo jana.
 Wanakikundi cha Aliselema wakishusha mbegu ya mihogo tayari uzinduzi wa shamba darasa.
 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza kabla ya kuanza uzinduzi huo katika Kijiji cha Isunda kilichopo Kata ya Nkolye.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akielekeza namna ya kupanda mihogo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TIC yafanikiwa kupata uwekezaji kutoka kwa makampuni makubwa duniani ya Ferrostaal ya Ujerumani na Haldor Topsoe ya Demnmark

$
0
0
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kupata uwekezaji kutoka kwa makampuni makubwa duniani ya Ferrostaal ya Ujerumani na Haldor Topsoe ya Demnmark, ambao unatarajiwa kuondoa kwa kiasi kikubwa tatizo la upatikanaji wa mbolea hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya upokeaji wa nyaraka za usajili wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe amesema Mradi huo wa kimkakati unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa katika ukuaji wa sekta ya viwanda na kwamba TIC inatarajia kuwa mradi huo utaleta kasi ya maendeleo na kukuza sekta mbalimbali, kwani mradi huo ni mkubwa na wenye thamani ya dola bilioni moja nukta tisa za kimarekani.

Mwambe aliongeza kuwa mradi huo ni mafanikio makubwa ya Kituo cha Uwekezaji na unatarajia kuongeza wigo wa ajira hapa nchini kwani utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha ajira zipatazo 4500 kwa Watanzania na kuleta chachu katika ukuaji wa sekta ya viwanda haswa uzalishaji wa mbolea ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ni changamoto kwenye ukuaji wa sekta ya kilimo ambapo watanzania wengi wamejiariri.

Katika halfa hiyo fupi ya makabidhiano, Wilfread Wineam ambaye ni Msimamizi wa mradi huo hapa nchini amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mbolea kiasi cha tani milioni moja nukta tatu kwa mwaka na kitauza karibu asilimia 30 ya mbolea hiyo hapa nchini na inayobaki kuuzwa nje ya nchi.
Naye Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Detlet Waecheter ameishukuru TIC kwa makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa kuhusu mradi huo na amesema anatarajia mradi huo utakuwa ni kivutio kwa makampuni mengine makubwa ya Kijerumani kuweza kuja kuwekeza hapa nchini.  

Balozi huyo ameahidi kuleta ujumbe mkubwa wa wawekezaji hivi karibuni kutoka jimbo la Bavaria ili waje hapa nchini kujionea fursa mbalimbali. Mradi huo utasajiliwa hapa nchini kwa jina la Tanzania Mbolea Petrochemicals yaani TAMCO

Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana.

$
0
0
 Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya katika mwaka 2016 imetoa jumla ya Hekta 271,882.86 za ardhi kwa  vijana nchi nzima ili kufanya shughuli za uzalishaji mali na kujipatia ajira.

Hayo yameelezwa leo, Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Anthony Mavunde  alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Mhe. Aida Khenan juu ya mpango wa Serikali kwa vijana wanaomaliza shule za msingi, Sekondarii na Vyuo kwa kuwazesha kujiajiri.

 “Serikali imeendelea kuimarisha utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao unalenga kuwasaidia vijana wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kuweza kujiajiri kwa kuwapa mikopo ya masharti nafuu na mafunzo ya ujasiriamali,” alisema Mavunde.

Aliendelea kwa kusema, katika kipindi cha mwaka 2013/2014 hadi 2016/17, Serikali kupitia mfuko wa Maendeleo ya vijana imetoa mikopo ya masharti nafuu ya Shilingi Bilioni 5.8 kwa vikundi vya vijana 6,076 vyenye wanachama 30,380 katika Halmashauri za Wilaya 157 kupitia SACCOS za Vijana.

Aidha Mavunde amesema, kupitia programu ya kukuza ujuzi wa  nchi Serikali imeanzisha utaratibu maalum wa kutambua ujuzi uliopatikana kupitia mfumo usio rasmi na kuurasimisha kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wale walio tayari kuhitaji na kuwapa vyeti vinavyotambulika.

“Utaratibu huu unawapafursa vijana wetu ya kuendelea na mfumo rasmi wa mafunzo na pia kutambulika na waajiri au watoa kazi,” alifafanua Mavunde.Vilevile amesema, Serikali imerahisisha utaratibu wa uundaji wa Makampuni kupitia BRELA hivyo vijana wengi wanaomaliza vyuo kuweza kuanzisha Makampuni na biashara zinazowezesha kuajiri vijana wengi.

Hata hivyo, Mavunde amewataka vijana wanaomaliza shule za msingi na sekondari kujiunga katika vikundi vya kuzalisha mali na kusajiliwa rasmi kupitia sheria ya usajili wa NGO’s.Aidha mpaka sasa jumla ya vikundi vya vijana vya uzalishaji mali 10, 200 vimesajiliwa.

ZOEZI LA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA LASHIKA KASI MKOANI SINGIDA

$
0
0
Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoani Singida umezidi kushika kasi wananchi wakifika kwa wingi kupata huduma ya Usajili unaohusisha uchukuaji wa alama za Kibiolojia, picha na Saini ya Kielektroniki.

Kwa kushirikiana kwa karibu na Maafisa Usajili, Watendaji wa Kata na Serikali za Mtaa, watumishi wa Mamlaka wamekuwa wafakifanya jitihada kubwa za kuhakikisha Wananchi wanatambua umuhimu wa kuwa na Vitambulisho vya Taifa pamoja na Matumizi yake Msingi na kushiriki kikamilifu kujisajili. 

Pamoja na misururu mirefu wananchi hao wameonyesha kutokata tamaa kwa foleni ndefu badala yake wamekuwa wakihamasishana kushiriki ili kila mmoja kupata haki yake msingi kusajiliwa.

Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa 12 ya Tanzania ambayo zoezi hilo linaendelea kwa sasa ukiwemo mkoa wa Mbeya, Njombe, Songwe, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita na Iringa.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa – NIDA Ndugu Thomas William pamoja na Ndugu Innecent Baraza Meneja Usimamizi wa Majengo (Kushoto) wakifuatilia kwa karibu Uingizwaji wa taarifa za waombaji wa Vitambulisho vya Taifa wakati wa Zoezi la Usajili na Utambuzi linaloendelea Mkoa wa Singida. 
Wanachi katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, wakifanyiwa usajili wa Maombi ya Vitambulisho vya Taifa katika zoezi la Usajili wa Mkupuo (Mass Registration) linaloendela hivi sasa Mkoani humo.
Baadhi ya Wananchi katika kata ya Kindai Halmashauri ya Manispaa Singida wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye chumba cha uchukuaji alama za kibaiolojia, picha na saini ya kielektroniki. 
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Mamlaka ya Vitambulisho Ndugu Thomas William akisimamia zoezi la ugawaji wa fomu za Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images