Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM ISAYA MWITA LEO ALIPOKUWA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 500 YA KANISA L.A. KKKT

$
0
0
 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo,walipokutana leo katika tamasha la maadhimisho ya miaka 500 ya kanisa la KKKT lililofanyika katika Uwanja wa Taifa.Wakwanza kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye .
 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akimsisitizia jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo walipokutana kwenye Tamasha la  maadhimisho ya miaka 500 ya Kanisa la KKKT  lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini hapa.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwa na Waziri Mkuu Mstafu Frederick Sumaye wa kwanza kushoto ,kwenye tamasha la Maadhimisho ya miaka 500 ya kanisa la KKKT lililofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini hapa.

MAGAZETI YA JUMATATU LEO NOVEMBA 6,2017

ASKOFU MALASUSA AONGOZA MAELFU YA WAKAZI WA DAR ES SALAAM KATIKA IBADA YA MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA

$
0
0
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa  akiongoza  Maelfu ya Waumini wa KKKT wa Dayosisi hiyo katika Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa,iliyofanyika jana Uwanja wa Taifa,jijini Dar.


Naibu Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mission na Uinjilisti Mchungaji, Boniface Kombo akiongoza Lutrijia wakati wa Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa.
 Mchungaji Lewis Hiza akisoma somo la pili wakati wa Ibada ya Miaka 500 ya Matengezo ya Kanisa la KKKT iliyoadhimishwa na Dayosisi ya Mashariki  na Pwani katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Mchungaji Muke Najua  kutoka nchini Afrika kusini akitoa mahubiri wakati  Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa hilo iliyofanyika  Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Kundi la watoto zaidi ya 4000 waliopata Ubarikio wa Kipaimara wakati wa Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa la KKKT Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UMOJA WA VIJANA WALIOSOMA NCHINI CHINA (CAAT) WAANZA KUTANGAZA UTALII WA NDANI KUSINI MWA TANZANIA KWA NJIA YA RELI YA TAZARA

$
0
0
Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. Halfa hiyo ilifanyika ijumaa iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (kulia) na Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto). PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG.
Baadhi ya wageni ambao ni wanaumoja wa CAAT wakifuatilia kwa makini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akitoa pongezi kwa umoja wa wanafunzi waliowahi kusoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania - CAAT) kwa kuweza kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam. Katika salamu zake Jaji Mihayo aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii ili waweze kujifunza mengi zaidi. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.

MKUTANO MKUU WA MWAKA 2017 WA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA WILAYA YA KISHAPU VINAVYOSIMAMIWA NA TGNP MTANDAO

$
0
0
Wanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka katika vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga vinavyosimamiwa na TGNP Mtandao wamefanya Mkutano Mkuu mwaka 2017 wa vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na baraza la kituo cha taarifa na maarifa la wilaya hiyo.

Mkutano huo wa siku mbili ulioanza Novemba 4,2017 hadi leo Jumapili Novemba 5,2017 umefanyika katika ukumbi wa Sheli ya BM kata ya Maganzo wilayani Kishapu.Mbali na mkutano huo kuhudhuriwa na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka kata saba,pia umehudhuriwa na maafisa watendaji wa kata pamoja na baadhi ya madiwani kutoka wilayani Kishapu. 

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kupanga mikakati na kuendeleza vituo vya taarifa na maarifa na kuunda baraza la kituo la wilaya ambapo wajumbe wa mkutano huo walichagua viongozi wa mtandao wa wilaya ambao kazi yao ni kusimamia shughuli zote za vituo vya taarifa na maarifa kwa wilaya hiyo ya Kishapu. 

Mkurugenzi wa uchaguzi wa baraza la kituo cha taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu uliofanyika katika mkutano huo,John Myola alimtangaza bi Rahel Madundo (aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo kipindi kilichopita) kuwa mwenyekiti wa baraza hilo kwa muda wa miaka miwili. 
Rahel Madundo akifurahia ushindi baada ya kutangazwa kuwa amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Afisa Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius Temba akiwasisitiza wanaharakati wa masauala ya kijinsia kuongeza nguvu kukabilina na vitendo vinavyokiuka haki za binadamu 
Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini 

RC.MNDEME AMEWATAKA WAKUU WA IDARA KUWA NA NIDHAMU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA, CHRISTINE MNDEME amewataka watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya SONGEA kujituma kufanyakazi kwa kutatua kero za wananchi badala ya kukaa ofisini.

LAPF YACHANGIA SHILINGI MILIONI TANO UJENZI WA OFISI ZA WALIMU MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akipokea Msaada wa Fedha Taslimu Shilingi Milioni tano 5.000.000/= kutoka kwa Bw. James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa ajili ya Kununulia mifuko 500 ya Saruji katika kuchangia kampeni ya ujenzi wa Ofisi za Kisasa za walimu katika shule za Msingi na Sekondari Mko wa Dar es salaam.

Kampeni hiyo imeanzishwa na Mkuu wa mkoa wa Mh.Paul Makonda katika jijini la Dar es salaam, ambapo Ofisi zaidi ya 400 zitajengwa katika shule za jiji la Dar es salaam hivyo kuboresha utendaji kazi wa waalimu hao, Kalia anayeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Kanali Charles Mbuge, Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki ofisini kwa Mkuu wa mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akimsikiliza Bw. James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakati akizungumza kabla ya kukabidhi msaada uliotolewa na LAPF kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za walimu katika shule za sekondari na Msingi katika mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika Ofisini kwake katikati ni Bw. James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF na kulia ni Kanali Charles Mbuge Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisisitiza jambo wakati akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika Ofisini kwake lulia ni Bw. James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF.

UVCCM: UTENDAJI MIAKA MIWILI YA SERIKALI YA JPM KIELELEZO CHA UZALENDO

$
0
0
Kaimu katibu mkuu Shaka Hamdu Shaka akizumgumza kwenye kongamano lilioandaliwa na uvccm kuhusu tathmini ya uchambuzi wa utendaji wa miaka miwili wa serikali ya Rais dk John Magufuli kwenye ukumbi wa bmk Mkoani Tanga jana.
Kaimu katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCM) Shaka Hamdu Shaka (wa tatu kulia)akishiriki kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa kongamano la tathmini ya uchambuzi wa utendaji wa miaka miwili wa serikali ya Rais John Magufuli kwenye Ukumbi wa BKM Mkoani Tanga jana.Kulia ni Mweyekiti wa ccm wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Khamis Mkoba(picha na Fahdi Siraji)
Chipukizi wa CCM Mkoa wa Tanga wakiimbisha Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa kongamano la tathmini ya uchambuzi wa miaka miwili ya serikali ya Rais John Magufuli kwenye Ukumbi wa BKM Mkoani humo.
Sehemu ya washiriki kwenye kongamano lililoandaliwa na uvccm kuhusu tathmini na uchambuzi wa miaka miwili ya utendaji wa serikali ya Rais Dk John Magufuli lilifanyika Mkoani humo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DC SHINYANGA ASHIRIKI CHAKULA CHA PAMOJA NA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA,ASHINDANA NAO KUCHEZA MUZIKI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameshiriki katika hafla fupi kula chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija mjini Shinyanga kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania Limited inayomilikiwa na Crissant Mssipi.

Kabla ya kula cha pamoja na watoto hao,mkuu huyo wa wilaya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya ulinzi walifanya usafi wa mazingira ikiwemo kupulizia dawa ya kuua wadudu kama vile kunguni katika mabweni yanayotumiwa na watoto hao.

Hafla fupi ya chakula cha pamoja iliyohudhuriwa pia na Afisa Mthibiti ubora wa Shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga,imenogeshwa kwa burudani ya muziki ambapo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro aliamua kucheza muziki na watoto hao hali iliyoongeza furaha zaidi kwa watoto hao.

Akizungumza katika kituo hicho,Matiro ameitaka jamii kuondokana na dhana ya kuwabagua na kuwafanyia vitendo vya kikatili ikiwemo kukata viungo na kuwaua akibainisha kuwa watoto wenye ualbino binadamu kama wengine na kinacho watofautisha ni rangi tu ya ngozi yao.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishindana kucheza muziki na watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija wakati wa hafla ya kula chakula cha pamoja kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania Limited-Picha na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akizungumza katika hafla fupi ya kula chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga ambapo aliwahakikishia ulinzi pamoja na kuboreshewa makazi yao.-Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Afisa Mthibiti ubora wa shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga, akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija ambapo aliwataka wadau wajitokeze kuwasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili pamoja na kushiriki kula nao chakula cha pamoja na siyo kusubiri hadi siku za sikukuu.

Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akipika chakula kwa ajili ya watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakila chakula cha pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ,kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD.

UMOJA WA VIJANA WALIOSOMA NCHINI CHINA (CAAT) WAANZA KUTANGAZA UTALII WA NDANI KUSINI MWA TANZANIA KWA NJIA YA RELI YA TAZARA

$
0
0
Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. Halfa hiyo ilifanyika ijumaa iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (kulia) na Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto). PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akitoa pongezi kwa umoja wa wanafunzi waliowahi kusoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania - CAAT) kwa kuweza kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam. Katika salamu zake Jaji Mihayo aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii ili waweze kujifunza mengi zaidi. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto) akitolea ufafanuzi wa masuala mbali mbali jinsi umoja wao ulivyo na lengo kuu la kuweza kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika.  Halfa hiyo iliyofanyika ijumaa iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wageni ambao ni wanaumoja wa CAAT wakifuatilia kwa makini.

DStv kuwazawadia wateja Channel za SuperSport Bure!

$
0
0
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kampuni ya Multichoice Tanzania (DStv) kuanza ofa yake kabambe ya msimu wa sikukuu, imesema inaanza kuwatunuku wateja wake kwa kuwapa chaneli za SuperSport bure kwa siku 7 kwa wateja watakaolipia huduma za DStv kabla ya kukatika

Kwa wateja wa kifurushi cha DStv Compact na DStv Compact Plus watakaofanya malipo ya kifurushi kabla ya kukatika watapata chaneli zote za SuperSport zinazopatikana katika kifurushi cha DStv Premium kwa kipindi cha muda wa siku saba (7)  mfululizo bureeee!!!


Kwa wateja watumiaji wa  kifurushi DStv Bomba  na DStv Family  wao watapata chanel zote za SuperSport zinazopatikana kwenye Kifurushi DStv Compact na hivyo kuweza kushuhudia mechi zote za Ligi ya Uingereza (PL) na mashindano mengine makubwa kwa siku saba (7) mfululizo bureee!!!!

Akizungumzia zawadi hii Meneja wa Wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo amesema hii itaendelea kwa muda na ni chombeza tuu kwani baada ya muda mfupi itaanza ofa maalum ya msimu wa sikukuu. “Mara zote sisi DStv huwa tunawatunuku wateja wetu, na sasa tumeamua kuwatuza wale wote watakaolipia akaunti zao kabla hazijakatika kwa kuwapa chaneli za michezo za vifurushi vya juu” alisema.

“Kuwathamini na kuwasikiliza wateja wetu umekuwa ni utamaduni wetu endelevu. Na tutaendelea kufanya hivyo ikiwemo kurekebisha bei zetu, kutoa tuzo na ofa mbalimbali na la msingi zaidi kuhakikisha kuwa muda wote tunawapa wateja wetu huduma bora kabisa” alisisitiza Hilda na kuwataka Watanzania wote kukaa mkao wa kula kwani kuanzia Septemba 15, DStv itazindua ofa yake maalum ya sikukuu itakayokuwa gumzo hapa nchini. http://thanks.dstv.com/

Wateja wa Tigo mjini Morogoro waliojishindia Tiketi za kushuhudia Tamasha la Tigo Fiesta

$
0
0

Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya, Roma Mkatoliki (kulia) na Zaiid wakimkabidhi mteja wa Tigo, Francis Wamonje (katikati) zawadi ya tiketi ya kwenda kishuhudia Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika jana mjini Morogoro.
Mteja wa Tigo mjini Morogoro, Idrissa Bakari (katikati) aliyejishindia tiketi ya kwenda kushuhudia Tamasha la Tigo Fiesta uwanja wa Jamhuri jana, akipokea tiketi yake toka kwa Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya, Barnaba, Mimi Mars, Maua Sama na Country Boy.
Msanii Barnaba akipiga picha 'selfie' na mfanyakazi wa duka la Tigo lililopo mtaa wa Stand Morogoro jana.

Tarehe mpya ya uchaguzi wa urais yatangazwa DR Congo

$
0
0
Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kwamba uchaguzi mkuu nchini humo sasa utafanyika Desemba 2018.

Hatua hiyo hata hivyo haijaufurahisha upinzani ambao unataka Rais Joseph Kabila aondoke madarakani.

Uchaguzi ulipangiwa kufanyika mwaka huu chini ya makubaliano yaliyoafikiwa mwaka jana, lakini tume ya uchaguzi imechelewa kuandaa uchaguzi.

Awali, ilikuwa imetangaza kwamba uchaguzi unaweza tu kufanyika mwaka 2019.

Lakini sasa tume hiyo imetangaza kwamba uchaguzi wa rais, wabunge na viongozi wa serikali za majimbo utafanyika mnamo 23 Desemba, 2018.

VIGUTA YAWAPIGA TAFU VIJANA PIKIPIKI 15 KIBAHA

$
0
0
Meneja wa Vicoba group union Tanzania (VIGUTA)Mkoani Pwani ambae pia operesheni Meneja Taifa ,Iddi Kanyallu akimkabidhi mwenyekiti wa CHAMAWAPIKI -Mailmoja Kibaha,Ayubu Kijazi pikipiki 15 kwa baadhi ya wanachama wa chama cha madereva wa pikipiki Kibaha ( CHAMAWAPIKI )zilizogharimu milioni 30.Picha na Mwamvua Mwinyi.

Na Mwamvua Mwinyi, Globu ya Jamii - Kibaha

MUUNGANO wa vikundi vya vicoba Tanzania (VIGUTA) umekabidhi pikipiki 15 kwa baadhi ya wanachama wa chama cha madereva wa pikipiki Kibaha mkoani Pwani (CHAMAWAPIKI) zilizogharimu milioni 30. Aidha VIGUTA imevitaka vikundi vya akinamama  vya vicoba kuhifadhi fedha zao kwenye taasisi za kifedha badala ya kutumia mfumo usio rasmi wa kuweka kwenye vibubu.

Akikabidhi pikipiki kwa vijana ambao ni madereva pikipiki Mailmoja-Kibaha ,Meneja Wa Viguta mkoani Pwani, Iddi Kanyallu aliwasihi wananchi wakimbilie fursa zilizopo kwenye muungano huo. Alieleza vijana hao walikopeshwa kwa gharama nafuu vyombo hivyo vya moto na kukabidhiwa ili kujiinua kimaendeleo. Alisema hatua hiyo inalenga kuwawezesha vijana kuendelea kujiajili kupitia wenyewe badala ya kutumika na wamiliki ambao uwabana kimaslahi. Kanyallu alisema ,wamekuwa wakitoa mikopo ya pikipiki kwa wajasiriamali vijana kwa rejesho la wiki sh.46,500 mkopo kwa muda wa mwaka mmoja .

"Tumekuwa tukishuhudia vijana hawa wakipewa Pikipiki na maboss wao ambapo hupeleka hesabu sh.70,000 kwa wiki lakini sisi tunakopesha kwa kuleta 46,500 kwa wiki "

"Sisi pia tunashughulika na vikundi vya akinamama wanatumia mfumo usio rasmi wa kuhifadhi fedha kwenye vibubu badala ya bank" alisema Kanyallu.

Pamoja na hayo ,alielezea kuwa ,Vicoba group union Tanzania inashughulika na NMB ambayo vikundi vyote husajiliwa na kuviunganisha kwa kupatiwa akaunti na kisha vinanufaika kwa kupata mikopo ya pikipiki,nyumba na mashamba. Kanyallu aliwaomba ,waliokabidhiwa kutunza pikipiki zao ili kujiinua kiuchumi.

Nae mwenyekiti wa CHAMAWAPIKI -Mailmoja Kibaha,Ayubu Kijazi alisema chama kiliamua kwenda ofisi za Viguta huko Miembesaba na kupewa taratibu za kupata mikopo ya pikipiki. Alisema kwamba ,kuna mikopo ya mikataba ambayo hutakiwa kurejesha kila siku sh.10,000 ikiwa ni 70,000 kwa wiki na ukitakiwa kumaliza mkopo ndani ya miezi kumi. Kijazi alifafanua ,ipo mikopo ya pikipiki unayotakiwa kutoa asilimia 30 kisha 650,000 uirejeshe kwa mwezi.

Mwenyekiti huyo wa CHAMAWAPIKI aliishukuru Viguta kwa kuwafungua macho kwa kuweza kupata pikipiki zao wenyewe kujitafutia kipato. Mbali ya hayo ,Kijazi alisema zipo changamoto wanazokabiliana nazo madereva bodaboda ikiwemo kuibiwa pikipiki hasa nyakati za usiku suala ambalo wanapambana nalo kwa kushirikiana na jeshi la polisi .

Kwa upande wake ,makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Focus Bundala alisema kwa vijana kupatiwa mikopo mbalimbali itawawezesha kujituma na kuondokana na kushinda vijiweni. Alisema pikipiki hizo wamekuwa wakikopeshwa kupitia watu wengine kwa kulipia sh.mil.3 wakati Viguta imekuwa mkombozi kwani gharama zao ni nafuu. Focus alieleza, halmashauri ya Mji huo inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya asilimia tano kwa vijana na wanawake asilimia tano ili kusukuma mitaji yao .

ALIYEIPAISHA TUSIIME KITAIFA ATAKA KUWA DAKTARI WA MOYO

$
0
0
MWANAFUNZI Ibrahim Shaban wa shule ya Tusiime aliyeibuka mshindi wa kwanza kitaifa kwenye matokeo ya mtihani wa taifa kumaliza elimu ya msingi amesema ndoto yake ni kuwa daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo.

Akizungumzia namna alivyoyapokea matokeo hayo alisema, amefurahi sana na kuahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi akiwa sekondari ili aweze kutimiza ndoto zake.

Alisema siri ya mafanikio yake ni jitihada kubwa za walimu wake akiwa shule ya msingi Tusiime na aliwamwagia sifa wazazi wake ambao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu maendeleo yake ya klitaaluma siku hadi siku.

Ibrahim alisema kuwa ndoto yake ya muda mrefu ni kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo hivyo aliahidi kuwa atasoma kwa bidii hadi ahakikishe ndoto zake zinatimia.

 “Nawashukuru walimu wangu wa Tusiime maana tulikuwa tunasoma usiku na mchana, mafanikio haya hayajaja kwa kubahatisha bali ni jitihada kubwa zimefanyika, nawashukuru wazazi wangu na nawaahidi nitafanya vizuri zaidi hadi niwe daktari wa moyo,” aliahidi Ibrahim ambaye aliongoza kitaifa kwa upande wa wavulana na shule yake kuwa ya kwanza Wilaya ya Ilala na ya a tatu kwa Mkoa wa Dar es Salam.

Mama mzazi wa Ibrahim, Mery Semwenda alisema si mara ya kwanza kwa Ibrahim kupata matokeo mazuri kama hayo kwani aliwahi kuwa wa kwanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam, kwenye matokeo ya darasa la nne.

“Akiwa darasa la nne hapo hapo Tusiime aliongoza katika matokeo ya darasa la nne kwa Mkoa wa Dar es Salaam na alipewa zawadi ya ngao na cheti na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick,” alisema

Alisema mazingira mazuri ya kusoma ya shule hiyo ndiyo yamekuwa yakisababisha wanafunzi wengi wa shule hiyo kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa kuanzia darasa la nne, la saba, kidato cha pili , cha nne na cha sita.

Alipoulizwa anamipango gani ya kuendeleza kipaji cha mtoto wake, aliiomba serikali iwatambue na kuwathamini,iwawezeshe na  iwawekee mazingira mazuri wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani yao.

“Serikali iwaweke pamoja wanafunzi wenye vipaji kama Ibrahim ili waendeleze vipaji vyao kwa faida ya taifa tofauti na sasa ambapo wanatangazwa tu kwenye magazeti lakini hakuna mfumo mzuri wa kuwafuatilia na kuendeleza vipaji vyao,” alisema na kuongeza

“Kwa mataifa mengine wanafunzi wenye vipaji kama hawa wanaangaliwa vizuri na kusaidiwa na serikali na mwishowe wanakuja kuwa wataalamu bingwa kwenye fani mbalimbali hivyo kutoa mchango wao kwa taifa,” alisema.

Ankal akiwa na Wadau wa Habari mjini Bukoba mkoani Kagera

$
0
0
Ankal akiwa na Wadau mbalimbali wa habari mjini Bukoba mkoani Kagera,wakati Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya siku nne mkoani humo,ambapo leo Rais  atazindua Uwanja wa Ndege wa Kagera

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWASALIMIA WANANCHI WA MULEBA NA KEMONDO WAKATI AKIELEKEA BUKOBA MJINI MKOANI KAGERA

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Muleba wakati akiwa njiani kuelekea Bukoba mjini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Muleba wakati walipokuwa wakiwasilisha kero zao mbalimbali.
 Baadhi ya wananchi wa Kemondo mkoani Kagera wakiwa juu ya miti kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akihutubia wananchi wa eneo hilo.
 Wananchi wa Kemondo wakifurahia wakati  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
 Wananchi wa Muleba wakifurahia wakati  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kemondo wakati akielekea Bukoba mjini. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwananchi Maarufu wa Muleba Hassan Milanga mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Muleba.
 Baadhi ya mabango wa Wananchi wa Kemondo mkoani Kagera wakiyanyanyua wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akipita katika eneo hilo. 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum  Kijuu mara baada ya kuwasili mkoani Kagera. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU AWAPOKEA WANACHAMA 37 WA UPINZANI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea wanachama wapya 37 kutoka vyama vya CUF na CHADEMA ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Bw. Barnabas Essau wanachama 35 kati ya hao wametoka CUF na wawili wametoka CHADEMA.Wanachama hao walipokelewa jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mbekenyera, wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Bw. Essau alisema wanachama hao wote wametoka kata za Mbekenyela na Matambalale. Walikabidhiwa kadi mpya za CCM, na kula kiapo cha uaminifu.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake wapya, Bw. Mohammed Issa Ndogoro ambaye amehamia kutoka CHADEMA, alisema wamejiunga na CCM baada ya kuridhishwa na mwelekeo wake. Alisema wameguswa na jinsi Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli inavyofanya kazi ya kutatua kero za wananchi. 

Alisema amekaa upinzani kwa miaka 23 lakini anaikubali CCM sababu ya uwazi wake na ameshangaa kuona akipewa kadi na stakabadhi ya walipo yenye jina lake, jambo ambalo hajawahi kuliona katika vyama vingine vya upinzani.

“Sote sisi tumehamia CCM, uhai wa chama ni michango. Nani aseme hapa kama aliwahi kupewa stakabadhi katika chama chake, na kama yupo nampa sh. 5,000/- sasa hivi,” alisema Bw. Ndogoro na kuamsha kicheko kwenye mkutano huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 - DODOMA.
JUMATATU, NOVEMBA 6, 2017.

WATAKAOKWAMISHA MALIPO YA KOROSHO KUKIONA-MAJALIWA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawashughulikia watu wote watakaokwamisha malipo ya wakulima wa zao la korosho.

“Hatutamuacha mtu yeyote atakayesababisha wakulima kuchelewa kulipwa fedha zao. Tutawakamata wote na kuwachukulia hatua stahiki.”Ametoa kauli hiyo jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mbekenyera wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu alisema wakulima hao ni lazima walipwe fedha zao kwa wakati na asitokee mtu wa kuzitamani fedha hizo.“Mkulima amelima mikorosho mwenyewe, ameokotoa na kukodoa mwenyewe wao wamepewa dhamana ya kuziuza, hivyo wahakikishe wanawapelekea fedha zao na wala wasizitamani.”

Pia Waziri Mkuu amewataka viongozi wa vyama vya Ushirika vya Msingi wahakikishe mkulima hakosi sh. 3,500 katika kilo moja ya korosho atakayoiuza baada ya kukatwa michango.Alisema bei ya juu ya korosho katika minada ya mkoa wa Lindi sh. ni 3,970 na ya chini sh. 3,800. “Vyovyote itakavyokuwa mkulima hawezi kukosa sh. 3,500, viongozi wa AMCOS mnisikie.”

Waziri Mkuu alisema hatua hiyo inatokana na kuongezeka kwa bei ya zao la korosho pamoja na kupungua kwa makato ya mkulima ambapo kwa sasa hayazidi sh. 300 katika kilo moja ya korosho.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATATU, NOVEMBA 06, 2017.

‘RUANGWA INAHITAJI SEKONDARI YA WASICHANA’-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema wilaya ya Ruangwa inahitaji kuwa na shule ya sekondari ya wasichana ambayo ni ya bweni ili kupunguza tatizo la wasichana kukosa elimu.

Ametoa wito huo jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ng’au, kata ya Mnacho wilayani Ruangwa mkoani Lindi ambako alienda kukagua ujenzi wa shule mpya ya msingi ambayo ujenzi wake ulianza wiki mbili zilizopita.

“Mpango wetu ni kujenga shule ya msingi mpya hapa kijijini Ng’au ili watoto wanaotoka ng’ambo hii wasome hapa hapa. Wakati wa masika nyote mnajua taabu wanayopata watoto wetu kukatisha kwenda ng’ambo ile,” alisema.

“Nimefurahi kukuta msingi wa vyumba tisa uko tayari na hii idadi inaweza kuongezeka. Wanakijiji tushirikiane kujaza kifusi ili kazi ya ujenzi iende haraka,” alisema.Waziri Mkuu alisema ng’ambo ya pili kuna shule ya msingi Mnacho ambayo ina madarasa 11 na wanafunzi waliopo ni karibu 500, na ndoto yake ilikuwa ni kuona ile shule inabadilika na kuwa ya sekondari.

“Ile shule ina historia na wakazi wengi kutoka Nandagala, Namahema, Chimbila ‘A’ na Chiemeka wamesoma pale. Mimi mwenyewe nimesoma pale kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Shule ilishazeeka, ndipo tukatafuta fedha ili ifanyiwe ukarabati na sasa ina miundombinu mizuri ndiyo sababu inaonekana inafaa kuwa ya sekondari,” alisema.

“Kwa vile shule ina miundombinu ya kutosha, ni vema ikawa ya bweni ambayo ni mahsusi kwa wasichana wa wilaya hii kwani tunalo tatizo la watoto wa kike kupata elimu, na wanahangaika sana,” alisema.

“Ujenzi wa hii shule ukikamilika, watoto wale 500 watahamia hapa na walimu wao na ile pale itapokea wanafunzi sekondari za wilaya hii ili tuwe na kidato cha kwanza hadi cha nne na ianze mara moja,” alisema.

Alisema shule hiyo itaitwa Lucas Malia kwa heshima ya mwalimu mkuu wa zamani wa shule hiyo ambaye alisomesha watu wengi katika wilaya hiyo na wengine sasa hivi ni viongozi Serikalini na jeshini. Mwalimu Malia hivi sasa ni marehemu.

Waziri Mkuu amerejea Dodoma leo asubuhi kuendelea na vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza kesho (Jumanne, Novemba 7, 2017).


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 - DODOMA.
JUMATATU, NOVEMBA 6, 2017.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa shule ya msingi Ng’au, katika kata ya Mnacho, Wilayani Ruangwa, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya msingi Ng’au, iliyopo kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule ya msingi Ng’au iliypo Wilayani Ruangwa, Daniel Chilemba kwa kusimamia ujenzi kikamilifu, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa shule, Novemba 5, 2017.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images