Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

WANANCHI SIMIYU WAENDELEA NA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
 Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikao 12 ya Tanzania inayoendelea na zeozi la kuwasajili wananchi kwa lengo la kuwapatia Vitambulisho vya Taifa.

Kwa sasa zoezi hilo limeingia kwenye awamu ya pili ya Usajili katika wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Bariadi, Meatu, Busega, Maswa na Itilima huku mwitikio wa watu ukiwa mkubwa.


wanaoshiriki kwenye zoezi hilo ni wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wageni na Wakimbizi.

Pichani ni Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiwachukua alama za Kibaiolojia wananchi wa mkoa wa Simiyu Kijiji cha Mwakiboro wakati zoezi la Usajili likiendelea .
Zoezi la Usajili likiendelea katika Kijiji cha Kilulu wilayani Bariadi

Wananchi wa Kijiji cha Mwakiboro mkoani Simiyu wakisubiri kupatiwa huduma ya Uandikishwaji Vitambulisho vya Taifa.
  

NAWAOMBA WATANZANIA MNIPIGIE KURA NIWEZE KUSHINDA TUZO YA MISS AFRICA USA-LYLIAN MUTTAKYAWA

$
0
0

Habari

Naitwa Lylian Muttakyawa, ni Mtanzania

Nimeleta ujumbe huu kuwaomba Watanzania wote kunipigia kura niweze kushinda tuzo ya Miss Africa USA kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzania

Kupiga kura ni rahisi, tafadhali bofya kiunganishi(Link) ifuatayo kisha utabonyeza VOTE kura hii inapigwa mara moja kwa kila siku na mwisho wa kupiga kura ni tarehe 10/11/2017. 



DC KIBONDO AWAAGIZA MADIWANI KUHAMASISHA WANANCHI KUIBUA VITUO VYA AFYA KATIKA KATA ZAO.

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WILAYA ya Kibondo inakabiliwa na upungufu wa vituo vya Afya, ambapo katika Wilaya nzima kuna vituo vya afya viwili hali inayopelekea Wananchi wa Wilaya ya Kibondo kukosa vituo vya kwenda kutibiwa na kupelekea ongezeko la vifo kwa Wananchi kutokana na kukosa huduma.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Bura amewaagiza Madiwani kuhakikisha wanawahamasisha Wananchi katika kata zao kuibua vituo vya Afya kwa kuanzisha ujenzi Wa vituo hivyo na Halmashauri kumalizia ujenzi huo ili kuhakikisha vituo vya Afya katika Wilaya hiyo vinaongezeka.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani Juzi Mkuu huyo alisema jambo la aibu sana kwa Wilaya hiyo kuwa na vituo vya Afya viwili na halmashauri isipochukua hatua ya kurekebisha vituo hivyo vitarudi kuwa zahanati, na amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kuhakikisha anaongeza mbinu ya kuibua vituo hivyo angalau Wilaya hiyo kuwa na vituo 10 kwa kuanzia.

Aidha Bura alisisitiza Madiwani kupatiwa Vitambulisho vya bima ya afya ili na wao waweze kuwahamasisha wananchi kuchangia mfuko wa bima ya Afya (CHF) na waweze kupatiwa matibabu bure na kupunguza gharama za matibabu.

DC WA HANDENI MH GODWIN GONDWE APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI WA ZAHANATI WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 14.7

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe amepokea msaada wa vifaa vya ujenzi wa zahanati wenye thamani ya Shilingi Milioni 14.7 za Kitanzania kutoka Darworth Ltd, Mwekezaji wa kiwanda cha usindikaji matunda, kama shukurani baada ya kupewa ardhi yenye ukubwa wa ekari 10 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho Kitongoji cha Mkomba katika Kijiji cha Michungwani Wilayani Handeni..

Akizungumza wakati wa mapaokezi ya vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya amewataka Viongozi ngazi ya Kata kuhakikisha wanasimamia na kutumia vifaa kwa kadri ilivyokusudiwa na kwamba asitokee mtu yeyote kupindisha matumizi au kusimamisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Ameongeza kuwa yote hayo yanafanywa kwaajili ya wananchi wa Handeni na kwamba maendeleo hayana itikadi, hivyo roho ya maendeleo iliyopo waishikilie ili wasonge mbele kwa pamoja kwakuzingatia kuwa wanatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

Gondwe amesema kuwa Mh.Rais ameagiza kuwepo kwa maeneo yanayotengwa rasmi kwaajili ya viwanda , na sisi kama viongozi tumejumuika kwa pamoja kusimamia agizo la Mh.Rais, kwa Handeni ni wajibu wetu kuhakikisha tunaendelea kutenga maeneo kwaajili ya viwanda kama ambavyo kiwanda hiki kitakavyojengwa.

“Asitokee mtu akauondoa umoja huu, huu ni mwanzotu, viongozi tunakazi ya kuhakikisha vifaa hivi vilivyoletwa vinafanye kazi yake na wananchi waone matunda ya rasilimali yao” amesema Gondwe

Kadhalka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe ameahidi kusimamia na kuhakikisha vifaa vyote vinatumika ipasavyo na kutoa ushirikiano kwa mwekezaji ili kufikia malengo ya ukamilishaji wa kiwanda cha kusindika matunda. 
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni MH. Godwin Gondwe  (mwenye koti jeusi akipokea nondo kutoka kwa mwekezaji John Kessy kwa ishara ya kupeana mikono na viongozi wengine wakishuhudia
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni  kulia name Mwekezaji upande wa Kushoto akipokea mfuko wa saruji kuwakilisha mifuko mingine  ,pembeni ni viongozi mbalimbali wa Halmashauri
 Mapokezi ya mabomba kwa ajili ya kusambazia maji,  Mkuu wa Wilaya ya Handeni  mwenye koti jeusi akipokea kutoka kwa mwekezaji John Kessy, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza na uongozi wa Kata kwenye ofisi ya Kijiji cha Michungwani.

wataalam wa Michezo nchini watakiwa kuleta matokeo Chanya katika sekta hiyo

$
0
0
Na Lorietha Laurence-WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wakufunzi 128 ambao ni wataalam wa michezo kuzingatia kwa makini yote waliojifunza na kuyafanyia kazi ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya michezo nchini.

Akizungumza katika ufungaji wa mafunzo hayo  Wilayani   Kyela Mkoani Mbeya ambapo Mhe. Dkt. Mwakyemba alieleza kuwa sekta ya michezo ni ajira na chanzo kikubwa cha mapato hivyo wakufunzi hao wakasimamie vyema waliyojifunza na kuyafanyia kazi kwa ajili ya maendeleo ya michezo nchini.

“Michezo ni ajira na chanzo kikubwa cha mapato hivyo msimamie vyema yote mliyojifunza na kuyafanyia kazi ipasavyo ili kuleta matokeo chanya kwa jamii yetu kwa kuwa na wacheza bora wa kimataifa”amesema Mhe. Mwakyembe.

Aidha ameongeza kwa kueleza kuwa mbali ya kuwa michezo ni ajira pia  ni kinga bora inayosaidia katika kuimarisha afya na hivyo kujiepusha na maradhi mbalimbali jambo ambalo ni muhimu kwa jamii.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja  ameeleza kuwa Baraza lake limejipanga  kutoa mafunzo ya wataalam wa michezo hayo kwa nchi nzima na hivyo kuzishauri Halmashauri kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiandaa na kuwasilisha maombi mapema ili kuyafanyia kazi.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyela. Dkt. Hunter Mwakifuna alimshukuru Waziri Mwakyembe kwa mchango wa hali na mali katika kukamilisha mafunzo hayo na kuahidi kuwatumia wakufunzi hao katika  kufundisha michezo Wilayani hapo.

Nao Wahitimu wameishukuru serikali kwa jitihadi iliyofanta ya  kuwaandalia mafunzo hayo na kuahidi kuwa walimu na mabalozi bora katika sekta ya michezo kwa kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji katika ngazi mbalimbali.

Mafunzo hayo yalifanywa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ilianza tarehe 23 hadi 28 Oktoba huku awamu ya pili ikiwa ni kuanzia 29 Oktoba hadi tarehe 4 Novemba mwaka huu chini ya uratibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Chuo cha Michezo Malya cha Mkoani Mwanza lengo ikiwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na wataalam wa kutosha katika sekta ya michezo.

Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo

$
0
0
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amempa maelekezo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuunda Kamati ya kuchunguza uvamizi wa viwanja vya Gereza Isanga uliofanywa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) mjini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi katika Gereza hilo, Masauni alisema eneo hilo ambalo lina ukubwa wa ekari zaidi ya 150 lazima lirudishwe katika himaya ya Jeshi la Magereza kama lilivyokua awali. “Eneo hili linalimilikiwa na Jeshi la Magereza tangu mwaka 1946, haiwezekani watu watokee na kuchukua ardhi hii kiholelaholela, hii haiwezekani hata kidogo, lazima uchunguzi ufanyike haraka iwezekanavyo na eneo lote lilrudi mikononi mwa jeshi,” alisema Masauni na kufafanua;

“Serikali ilishahamia hapa mjini Dodoma, hivyo shughuli za magereza zitaongezeka kwa kasi, na umuhimu wa maeneo utakua mkubwa zaidi kutokana na umuhimu wa jeshi hili katika kukuza uchumi.” Aliongeza kuwa, jeshi hilo linahitaji kujenga nyumba za askari kwa kasi na kutokana na changamoto hiyo ya uvamizi uliofanywa ujenzi waweza kusuasua hivyo eneo hilo lahitajika kurudishwa haraka sana.

Masauni alifafanua kuwa, tayari amemuelekeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali, Projest Rwegasira kulichunguza suala hilo kwa kina kwa kuwa kuna taarifa ambazo bado hazijathibitishwa kuwa kati ya wamiliki wa viwanja hivyo walikua ni viongozi waandamizi wa CDA, Jeshi la Magereza pamoja na viongozi wakubwa mbalimbali.

Hata hivyo, Masauni alipiga marufuku mtu yeyote kuendeleza ujenzi wa eneo hilo hata kama ana vibali vyote vya kumiliki eneo. Aidha, Mkuu wa Gereza Isanga, Keneth Mwambeje, akizungumzia suala hilo, alisema jeshi lake lina nyaraka za mawasiliano kati ya viongozi wa gereza hilo ambao walikua kwa wakati huo pamoja na wa CDA.

CDA ambayo ilivunjwa na Rais John Magufuli, ndio inahusika kugawa viwanja hivyo kwa wananchi zaidi ya mia moja ambao baadhi yao wamejenga na wengine wanaendelea na ujenzi katika eneo.

Miaka Miwili ya Rais Magufuli, Mageuzi Makubwa Yafanyika

MAAMUZI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YA RUFAA 15 ZA WAGOMBEA WA UDIWANI

$
0
0
Kwa kuzingatia Kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ikisomwa pamoja na Kanuni ya 28(1)(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa kumi na tano (15) kutoka kwa Wagombea Udiwani wa Halmashauri mbalimbali zenye Uchaguzi Mdogo wa Madiwani.

Kati ya Rufaa hizo kumi na tano (15), Rufaa 9 ziliwasilishwa na Wagombea ambao hawakuridhishwa na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi waliowaengua kutoka katika orodha ya wagombea wa Udiwani katika Kata mbalimbali.

Aidha, Kati ya Rufaa kumi na tano (15), Rufaa sita (6) ziliwasilishwa na Wagombea ambao hawakuridhishwa na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi ya kuwaruhusu wagombea wenzao kuendelea kugombea udiwani katika Halmashauri mbalimbali.

Kuanzia tarehe 03 hadi 04 Novemba, 2017, Tume kwa mujibu wa Kanuni ya 29 ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015, ilipokea, ilijadili na kufanya maamuzi ya Rufaa hizo. Yafuatayo ndiyo maamuzi ya Tume:

Kuhusu Rufaa tisa (9) za wagombea waliokata Rufaa kupinga maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi kuwaondoa katika kugombea Udiwani, Tume imekubali Rufaa zao na kuwarejesha katika kugombea udiwani katika Kata husika kuanzia tarehe ya leo 04 Novemba, 2017.

Kuhusu Rufaa sita (6) za wagombea waliokata Rufaa kupinga maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi ya kuwaruhusu wagombea wenzao wa Udiwani kuendelea na Kampeni za Udiwani, Tume imezikataa Rufaa na imekubaliana na Maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi. Hivyo, wagombea sita (6) waendelee kuwa wagombea.

Taarifa rasmi za maamuzi ya Tume zimetumwa kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ili wawapatia wahusika maamuzi ya Tume.

Imetolewa leo tarehe 04 Novemba, 2017 na;

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU ATEMBELEA MIRADI YA UMEME CHAMAZI-DOVYA NA MBANDE WILAYANI TEMEKE

$
0
0
Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (kulia), akizungumza jambo mbelke ya viongozi wa Tanesco mkoa wa Temeke na wa serikali ya Mtaa, alipotembelea miradi ya umeme huko Cghamazi, Dovya, Mbagala jijini Dar es Salaam, leo Jumapili Novemba 5, 2017.


NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu leo Jumapili Novemba 5, 2017 amefanya ziara ya kutembelea miradi 7 ya umeme inayotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), huko Chamazi-Dovya kwa Mzala 1-3, Mbande kwa Masister na Chamazi Vigoa, Mbagala jijini Dar es Salaam.


Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri amefuatana na Kaimu Mkurugenzi, TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka na viongozi wengine wa Shirika hilo.

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Uhusianom wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, miradi hiyo saba ni pamoja na ule wa Chamazi Dovya ambao unajumuisha miradi mitatu, (3), Mbande kwa Masister, Miradio 4 na hivyo kufanya jumla ya miradi saba lengo likiwa ni kuwapatia umeme Wananchi wote wa Chamanzi Dovya ambao hawajapata umeme.

“Miradi hii imekamilika na na kila mradi tumefunga transfoma mbili (2).” Alisema Bi. Leila.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (wapili kushoto), Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mgaya, (wakwanza kushoto) wakimsikilzia Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula, wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Naibu waziri Mgalu, akiangalia ripoti ya utekelezaji wa miradim hiyo, iliyokuwaikisomwa na Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula Maendeleo.

Waziri Mwakyembe awataka wataalam wa Michezo kuleta matokeo Chanya katika sekta ya Michezo nchini.

$
0
0
Na Lorietha Laurence-WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wakufunzi 128 ambao ni wataalam wa michezo kuzingatia kwa makini yote waliojifunza na kuyafanyia kazi ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya michezo nchini .

Akizungumza katika ufungaji wa mafunzo hayo Wilayani Kyela Mkoani Mbeya ambapo Mhe. Dkt. Mwakyemba alieleza kuwa sekta ya michezo ni ajira na chanzo kikubwa cha mapato hivyo wakufunzi hao wakasimamie vyema waliyojifunza na kuyafanyia kazi kwa ajili ya maendeleo ya michezo nchini.

“Michezo ni ajira na chanzo kikubwa cha mapato hivyo msimamie vyema yote mliyojifunza na kuyafanyia kazi ipasavyo ili kuleta matokeo chanya kwa jamii yetu kwa kuwa na wacheza bora wa kimataifa”amesema Mhe. Mwakyembe.Aidha ameongeza kwa kueleza kuwa mbali ya kuwa michezo ni ajira pia ni kinga bora inayosaidia katika kuimarisha afya na hivyo kujiepusha na maradhi mbalimbali jambo ambalo ni muhimu kwa jamii.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja ameeleza kuwa Baraza lake limejipanga kutoa mafunzo ya wataalam wa michezo hayo kwa nchi nzima na hivyo kuzishauri Halmashauri kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiandaa na kuwasilisha maombi mapema ili kuyafanyia kazi.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyela. Dkt. Hunter Mwakifuna alimshukuru Waziri Mwakyembe kwa mchango wa hali na mali katika kukamilisha mafunzo hayo na kuahidi kuwatumia wakufunzi hao katika kufundisha michezo Wilayani hapo.

Nao Wahitimu wameishukuru serikali kwa jitihadi iliyofanta ya kuwaandalia mafunzo hayo na kuahidi kuwa walimu na mabalozi bora katika sekta ya michezo kwa kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji katika ngazi mbalimbali.

Mafunzo hayo yalifanywa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ilianza tarehe 23 hadi 28 Oktoba huku awamu ya pili ikiwa ni kuanzia 29 Oktoba hadi tarehe 4 Novemba mwaka huu chini ya uratibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Chuo cha Michezo Malya cha Mkoani Mwanza lengo ikiwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na wataalam wa kutosha katika sekta ya michezo.

WAZAZI MBURAHATI SACCOS YAIVA, KUPATA HATI YA USAJILI HIVI KARIBUNI

$
0
0
 Mwenyekiti wa muda wa Wazazi Mburahati Saccos, John Mapunda akifungua mkutano wa wanachama wa Saccos hiyo, uliofanyika kwenye ukumi wa Jengo la Kitegauchumi la CCM, Mburahati, Dar es Salaam, jana.

Amesema ameamua yeye na wenzake kuanzisha ushirika huo wa Akiba na mikopo siyo kwa maslahi ya kisiasa bali kuwasaidia kuwasaidia kiuchumi wanachama wa Jumuiya ya Wazazi katika Kata ya Mburahati ili nao waweze kuwa na maisha bora wakiwa ni miongoni mwa Watanzanaia wenye mahitaji hayo. Kushoto ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo ambaye alifika kwenye mkutano huo kutoa mafunzo ya namna bora ya kuanzisha na kuendesha Saccos. Kulia ni Mhazini wa muda Boniface Chigenda na Katibu wa muda Sofia Kiroboto.
 Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akitoa mafunzo ya namna bora ya kuanzisha Saccos na kuifanya idumu wakati wa mkutano huo. Amesema Saccos hiyo kwa sasa imeshatimiza masharti yote ya kupatiwa usajili na inapatiwa usajili huo hivi karibuni, alisema katika Kadirio lake Saccos hiyo inatarajia kupata zaidi ya Sh. milioni 13 kutokana na ada na michango ya wanachama ambao hadi sasa wamefikia 68, pia kufanya matumizi ya zaidi ya Sh. milioni 13 na kubaki na ziada ya zaidi ya Sh. milioni 29.
 Kitabu au Masharti ya Saccos hiyo
 Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo, akionyesha orodha ya wananchama 68 waliokwishajiunga na Saccos hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa muda John Mapunda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Kata ya Mburahati.

VODACOM TANZANIA PLC YAFANIKISHA NDOTO ZA WANAWAKE KUPITIA M-PESA

$
0
0
 Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, Hawa Hamis (kushoto)akimwelewesha jambo Mwanakomba Shabani,Kuhusiana na huduma ya M-Pesa wakati wa mkutano wa akina mama uliojulikana kama"Atukuzamu  Women of Conference" uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa Udhaminiwa na  Vodacom Tanzania PLC.
 Meneja wa  kitengo cha M-PESA wa Vodacom Tanzania PLC,Noel Mazoya (kushoto) akiongea na wanawake wajarisiliamali kuhusiana na huduma  M-Pesa  inayotolewa na kampuni hiyo wakati wa Kongamona la wanawake la"Atukuzamu  Women of Conference"uliofanyika katika ukumbi wa City Christian Center( CCC) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC,Anayeshuhudia kulia ni mshereheshaji wa mkutano huo,Jimmy Byamungo.

DC URAMBO: WAKULIMA 4,268 WAJIANDIKISHA KULIMA PAMBA MSIMU UJAO.

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT-RS –TABORA

JUMLA ya wakulima 4,268 wilayani Urambo wamejiandikisha kulima zao la Pamba katika msimu wa kilimo unatarajia kuanza wakati wowote mwezi huu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa wakati akitoa taarifa ya maandalizi ya kilimo hocho kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey ambaye anazungukia vijiji mbalimbali vinavyolima pamba kwa ajili ya utoaji wa elimu juu ya ulimaji bora.Alisema kuwa idadi ya wakulima wanatoka Kata 15 ambao wamo katika vijiji 49 wameleta makisio yao ya kulima zao hilo na kuongeza wakifanikiwa kulima zinaweza kupatika zaidi tani 2000.

Kwingwa alisema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri ambapo wanatarajia kupata mbegu ambazo zimependekezwa na Bodi ya Pamba zisizokuwa na Manyoa tani 31.2 kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima kwa ajili ya kuanza kilimo hicho.Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri aliwaonya wakulima na wafanyabiashara kutoingiza mbegu za manyoya ambazo zimepigwa marufuku na kuongeza kuwa mkulima atakayepanda mbegu hizo atalazika kuzing’oa.

“Hapa mbegu tutakayopanda ni UKM08 na sio nyingine …nikikutana mtu amepanda mbegu iliyopigwa marufuku ya manyoa nitavuruga shamba lake na kuwachukulia hatua watu ambao watakuwa wamebainika kuingiza mbegu hiyo” alisisitiza Mwanri.

NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU ASEMA VIJIJI 54 MKOANI PWANI KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME WA REA AWAMU YA TATU

$
0
0

NA VICTOR MASANGU, PWANI

VIJIJI vipatavyo 54 katika mkoa wa Pwani ambavyo wananchi wake walikuwa katika hali ya sintofahamu kutokana na kukaa gizani kwa kipindi cha muda mrefu hatimaye wanatarajia kupata na kunufaika na nishati ya umeme wa uhakika ifikapo mwezi machi mwaka 2018 baada ya kukamilika kwa mradi wa kusambaza umeme vijiji (REA) awamu ya tatu.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa wizara ya nishati Subira Mgalu baada ya kufanya ziara yake ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Bagamoyo pamoja na Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya kutembelea baadhi ya miradi ya REA ambayo inatekelezwa kwa awamu ya tatu pamoja na kujionea changamoto mbali mbali zinazowakabili.

Pia Magalu amesema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha inapeleka huduma ya uhakika kwa wananchi wake pamona na maeneo mengine yenye kutoa huduma za kijamii na kubainisha kuwa wanatarajia ifikapo mwaka 2021 vijiji vtote nchini view vimefikiwa na huduma ya nishati ya umeme.

Aidha Naibu Waziri huyo alipotembelea kituo cha uzalishaji wa umeme kilichopo maeneo ya Mlandizi aliliagiza Shirika la ugavi wa umeme Tanesco kuhakikisha wanajipanga vizuri ili kuweza kupunguza malalamiko ambayoyamekuwa yakitolewa na baadhi ya wananchi kuunguza vitu vyao majumbani kutokana na tatizo la kukatika katika umeme kila mara bila ya kutoa taarifa.
Naibu Waziri wa Wizara mpya ya nishati Subira Mgalu akizungumza na watendaji wa shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani pamoja na wakandarasi baada ya kukagua mradi wa REA awamu ya tatu uliopo maeneo ya sofu mlandizi Wilayani Kibaha mkoani Pwani alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kujionea mwenendo mzima wa ujenzi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu wa kati kati akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani Martin Madulu wa kushoto katika alipotembelea kituo cha usambazaji wa umeme kilichopo Mlandizi.
Naibu Waziri wa Wizara mpya ya nishati Subira Mgalu akipata ufafanuzi kutoka kwa wakandarasi wa mradi wa umeme wa REA awamu ya tatu katika eneo la Msufini Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
Naibu waziri mpya wa Nishati Subira Mgalu akisikiliza kwa umakini maelezo kutoka kwa Meneja wa tanesco Mkoa wa Pwani Martin Madulu wa kushoto mara baada ya kutembelea kituo cha umsambazaji wa umeme kilichopo Mlandizi ikiwa ni ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua miradi ya nsihati ya umeme 


RC RUVUMA AMWAGIZA MKANDARAS KUMALIZA UJENZI WA GHALA LA KOROSHO.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA, CHRISTINE MNDEME amemwagiza Mkandarasi SKYCITY LIMITED, anayejenga ghala la kuhifadhia korosho wilayani TUNDURU kumaliza ujenzi huo mapema ili kupisha ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho.

MAMENEJA TEMESA WAHITIMU MAFUNZO USIMAMIZI WA MANUNUZI NA MIKATABA

$
0
0
Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle (katikati) akitoa msisitizo wakati alipokua akizungumza na Mameneja na wakuu wa vituo kutoka wakala huo (hawapo pichani) kabla ya kuwatunuku vyeti baada ya kumaliza mafunzo ya Manunuzi na Usimamizi wa Mikataba yaliyomalizika mwishoni mwa wiki, Kulia ni Mhandisi Dkt Ramadhan Mlinga aliyeendesha mafunzo hayo na kushoto ni Mhandisi Aurelia Ngopa kutoka Temesa. Mafunzo hayo yalifanyika katika chuo cha Uhandisi na Teknolojia (COET) Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya Mameneja na wakuu wa vituo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Mhandisi Aurelia Ngopa alipokua akisoma risala kwa mgeni rasmi wakati wa sherehe ya kuwatunuku vyeti Mameneja hao baada ya kuhitimu mafunzo ya Manunuzi na Usimamizi wa Mikataba zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo cha Uhandisi na Teknolojia (COET) Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya Mameneja na wakuu wa vituo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza mgeni rasmi Mhandisi Japhet Maselle alipokua akizungumza nao wakati wa sherehe ya kuwatunuku vyeti Mameneja hao baada ya kuhitimu mafunzo ya Manunuzi na Usimamizi wa Mikataba zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo cha Uhandisi na Teknolojia( COET) Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RC MNYETI AKAGUA UJENZI UKUTA UNAOZUNGUKA MIGODI YA MADINI YA TANZANITE MIRERANI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, ameanza rasmi kazi Mkoani humo kwa kukagua ujenzi wa ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli. 

Mnyeti alitembelea eneo hilo na mwenyeji wake mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo. Alipongeza kasi ya maandalizi ya ujenzi huo kwani kila sehemu aliyokagua ambapo ukuta utapita aliwakuta vijana hao wa JKT wana ari na hamasa ya utendaji kazi. 

"Kwa namna vijana wetu wanajeshi wanavyoonekana kwenye maeneo yote niliyopitia wanaonyesha wataimaliza kazi hii ndani ya muda mfupi tofauti na agizo la miezi sita lililotolewa na Rais Magufuli," alisema Mnyeti.Aliwaahidi kutoa ushirikiano kwa jambo lolote lile watakalokuwa wanalitaka kwenye serikali ili kuhakikisha agizo hilo la Rais Magufuli linatekelezeka kwa wakati husika. 

Kamanda wa operesheni ukuta Mirerani, Kanali Festus Mang'wela alimhakikishia mkuu huyo wa mkoa kuwa vijana wote wanaojenga ukuta huo watafikishiwa ujumbe huo wenye lengo la manufaa ya kulinda afya zao. Kanali Mang'wela alisema ukuta huo wenye kilometa 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu unatarajiwa kuanza kujengwa rasmi Novemba 6 mwaka huu. 

Alisema wanatarajia mkuu wa JKT Meja jenerali Michael Isamuhyo ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo wa ukuta wanaotarajia kuujenga kwa muda usiopungua miezi sita. Alitoa shukrani kwa serikali ya wilaya ya Simanjiro kwa ushirikiano mkubwa wanaowapa askari hao wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo la maandalizi ya ujenzi wa ukuta huo.   
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (kushoto) akimsikiliza msimamizi wa ujenzi wa ukuta unaojengwa kuzunguka madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, Kanali Festus Mang'wela, (katikati) baada ya kutembelea zahanati ya kijiji cha Naisinyai ambapo madaktari wa JWTZ wanatoa huduma za afya. 
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (kulia) akikagua maandalizi ya ujenzi wa ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (kushoto) akikagua maandalizi ya ujenzi wa ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (kushoto) akikagua ramani ya ujenzi wa ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA 

SEMINA YA WABUNGE WA KAMATI TATU ZA BUNGE YAFANYIKA MJINI DODOMA

$
0
0
 Ndugu Serafine Tamba akitoa mada kuhusu Mchakato wa Utungaji Sheria katika Semina ya Wabunge wa Kamati ya Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati Mambo Nje, Ulinzi na Usalama.
 Wajumbe wa Kamati tatu za Bunge wakifuatiliana mada kuhusu mchakato wa Utungaji Sheria kutoka kwa Ndugu Serafine Tamba  katika Semina ya Wabunge iliyofanyika Mjini Dodoma. Wajumbe wa Kamati zilizohudhuria Semina hiyo ni Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati Mambo Nje, Ulinzi na Usalama.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Bunge zilizoshiriki Semina kuhusu Mchakato wa Utungaji Sheria wakifuatilia mada katika Semina iliyofanyika Mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mheshimiwa Andrew Chenge akitoa mchango wake Katika Semina ya Wabunge iliyofanyika Mjini Dodoma. Wajumbe wa Kamati zilizohudhuria Semina hiyo ni Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati Mambo Nje, Ulinzi na Usalama.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Balozi Adadi Rajabu akizungumza katika Semina ya Wabunge wa Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati Mambo Nje, Ulinzi na Usalama iliyofanyika Mjini Dodoma.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria Mohamed Mchengelwa 

WAZIRI MKUU AHIMIZA LINDI WAJIPANGE MAANDALIZI YA BARAZA LA MAULID KITAIFA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wana-Lindi na wana-Ruangwa watumie fursa zilizopo ili kufanikisha maandalizi ya sherehe za Maulid na Baraza la Maulid Kitaifa mwaka huu.

Ametoa wito huo leo (Jumapili, Novemba 5, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Lindi na wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja.

Waziri Mkuu amesema sherehe hizo zitafanyika Desemba mosi kwa mkesha wa Maulid na kufuatiwa na Baraza la Maulid litakalofanyika Desemba 2, saa 3 asubuhi kwenye viwanja vya shule ya msingi Likangale.

Aliwataka wana-Ruangwa waharakishe kujenga nyumba za kulala wageni na sehemu za kula ili waweze kupokea ugeni huo mkubwa wa kitaifa. “Kila mmoja anayeona hapo kuna fursa, ni lazima aitumie vizuri,” alisisitiza.

“Kwa niaba ya wana-Ruangwa, tunamshukuru Mheshimiwa Mufti na Baraza la Maulamaa kwa kuridhia sherehe hizi zifanyike kitaifa hapa wilayani kwetu. Nitumie fursa hii kuwaomba Waislamu wote tuungane katika sherehe hizi licha ya tofauti za madhehebu yetu tuliyonayo,” alisema.

LUSINDE "KIBAJAJI" AKITIFUA KITWIRU KAMPENI ZA UDIWANI MKOANI IRINGA

Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images