Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAWASILISHA MAKADIRIO YA BAJETI KWA MWAKA 2017/2018

$
0
0
Waziri wa Mambo ya NdaniyaNchi, Mwigulu Nchemba akiwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapo aliliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali yaliyoulizwa na Wabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Mhandisi Hamad Masauni.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali yaliyoulizwa naWabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kushoto ni Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na makamanda wa Jeshi la Polisi muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge la Bajeti ambapo wizara yake iliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akifurahia abaadhi ya wabunge mara baada ya kumaliza kuwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapoa liliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjiniDodoma.PichanaWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI 

FRIENDS OF OCEAN WAUNGA MKONO KAMPENI YA KIMATAIFA YA KUTUNZA FUKWE ZA BAHARI

$
0
0
Wakazi wa Mikocheni B wanaounda Chama cha FRIENDS OF OCEANS wakisafisha fukwe ya Escape One katika uzinduzi wa kampeni ya OKOA BAHARI ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT ,na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita. 
Friends of oceans wakiendelea na usafi wa fukwe ya Escape one ikiwa kama uzinduzi wa kuanza usafi huo kwa kila mwezi na pia kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na rasilimali za bahari 
Usafi ukiendelea katika fukwe ya Escape One ambapo kulikutwa chupa za bia,makopo ya maji, sindano na vingi ambavyo ni hatari kwa afya ya watumiaji wa fukwe hiyo mapema mwishoni wa wiki iliyopita . 
Friends of Ocean wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza usafi katika fukwe ya Escape One Mikocheni B kama uzinduzi wa kampeni ya OKOA BAHARI yenye lengo ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT 

RAIS MSTAAFU JK AENDELEA NA JUHUDI ZA USULUHISHI WA MGOGORO WA LIBYA

$
0
0
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Libya ameendelea na juhudi zake za usuluhishi wa mgogoro wa Libya kwa kushiriki katika Kikao cha 11 cha Mawaziri wa Nchi Jirani na Libya kilichofanyika jijini Algiers, Algeria tarehe 8 Mei, 2017.

Katika Kikao hicho, Rais Mstaafu amepongeza juhudi zinazoendelea za kupatanisha pande zinazogombana nchini Libya na mafanikio yanayopatikana ikiwemo kuimarika kwa hali ya usalama, kudhibitiwa kwa vitendo vya kigaidi, kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji wa mafuta na kufufuliwa kwa mawasiliano kati ya pande zinazohasimiana.
 
 Ameunga mkono jitihada zinazochukuliwa na nchi za Algeria, Misri, Tunisia na UAE katika kuhimiza mazungumzo ya Amani. Amesisitiza umuhimu wa pande mbili za mgogoro kuheshimu Makubaliano ya Amani ya Libya (Libya Political Agreement) na kutekeleza vipengele vyake bila ajizi.

Akiwa jijini Algiers, Rais Mstaafu amefanya pia mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo anayemuwakilisha Mwenyekiti wa Kamati wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika kuhusu Libya Mhe Jean-Claude Gakosso na Balozi Martin Kobler, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Mgogoro wa Libya (UNSMIL).

Rais Mstaafu anatarajiwa kumalizia ziara yake nchini Libya kukutana na viongozi wakuu wa pande zinazotofautiana nchini humo.
Rais Mstaaafu Dkt Jakaya Kikwete akifuatilia Mkutano wa Nchi Majirani wa Libya
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Mgogoro wa Libya Balozi Martin Kobler jijini Algiers
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akitoa msimamo wa Umoja wa Afrika kuhusu Mgogoro wa Libya .

Rais Mstaafu katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo na Mwenyekiti wa AU Mhe. Jean-Claude Gakosso. Kushoto ni Mkuu wa Ofisi ya Uwakilishi wa AU kwa Libya Bi. Wahida Ayari 

KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA AFANYA ZIARA YAKE YA KWANZA BABATI-MKOANI MANYARA

$
0
0
aimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, akifafanua jambo.

 Kaimu Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof.Ibrahim Juma (wa tatu kushoto), Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi (wa tatu kulia), Katibu wa Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, Mhe. Eliazar Luvanda (wa pili kulia) na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Mkoa Manyara, Mhe. Devotha Kamuzora (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wa Mahakama wa mkoani Manyara.

 Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama walioshiriki katika kikao cha Watumishi na Mhe. Kaimu Jaji Mkuu.

Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama walioshiriki katika kikao cha Watumishi na Mhe. Kaimu Jaji Mkuu.

Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu aliowahi kuwafundisha chuoni, wa kwanza kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.

Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akikagua jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi/Wilaya Manyara lililopo katika ujenzi, kukamilika kwa ujenzi wa Mahakama hiyo kutasaidia kuondokana na changamoto ya uchakavu wa jengo wanayokabiliana nayo katika Mahakama ya sasa. 
(Picha zote na Mary Gwera wa Mahakama)

Article 3

$
0
0
Taasisi na Asasi Zisizokuwa za Kiserikali za Tanzania (NGOs) taasisi za serikali zinazoshughulikia uwajibikaji na wadau wengine kadhaa walikutana hivi leo  ili kufanya tathmini ya hatua zilizopigwa na mafunzo yaliyopatikana wakati wa uhai wa mradi wa Pamoja Twajenga  unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID). Toka mwaka 2013, watendaji wa mradi wa Pamoja Twajenga wamekuwa wakifanya kazi bega kwa bega na asasi za kiraia na taasisi za serikali ya Tanzania zinazoshughulikia masuala ya uwajibikaji ili kuimarisha mahusiano kati ya asasi za kiraia na serikali. Mradi huu ulitoa mafunzo na msaada kwa jumla ya asasi zisizo za Kiserikali 16 na taasisi tatu za serikali zinazojihusisha na uwajibikaji katika mikoa ya Mtwara, Iringa, Dodoma, Morogoro na  Zanzibar kwa lengo la kukuza uwazi na uwajibikaji wa serikali kwa raia wa Tanzania. 
Kutokana na msaada huu, hivi sasa asasi za kiraia na taasisi za uwajibikaji zilizoshiriki zina uwezo zaidi wa kushiriki katika mijadala kuhusu masuala mahsusi yanayozigusa jamii (issue-baseddialogue).
Raia katika mikoa lengwa ya mradi – ikiwa ni ni pamoja na vijana, wanawake na makundi mengine ya watu wanaowekwa pembezoni wana uwezo zaidi wa kujadiliana na serikali zao kuhusu kero zao, jambo ambalo limeongeza uwajibikaji na uwazi katika usimamizi wa rasilimali za umma na katika ufanyaji maamuzi
. Asasi za kiraia zilizosaidiwa na mradi wa Pamoja Twajenga zinafanya kazi katika masuala yanayohusiana moja kwa moja na mahitaji ya msingi ya raia ikiwa ni pamoja na huduma za afya, elimu, usalama wa chakula na usimamizi wa rasilimali. 
 Majadiliano ya jumuiya katika kata ya Mpapula mkoani Mtwara, mwanajamii akielezea uzoefu wao kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanywa dhidi ya wanawake na watoto. Majadiliano hayo yaliandaliwa na asasi ya kiraia ya Wanasheria Wanawake Katika Maendeleo Afrika (Women in Law and Development in Africa - WiLDAF), mojawapo kati ya asasi za kiraia zilizopokea msaada kutoka mradi wa Pamoja Twajenga uliokuwa ukifadhiliwa na USAID. (Picha kwa hisani ya: Rhoda Nashon/WiLDAF)
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA ZIZINGATIE SHERIA KATIKA UNUNUZI WA HUDUMA KWA UMMA

$
0
0
Na Ismail Ngayonga, MAELEZO

KATIKA  kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2015/16,  Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ilifanya ukaguzi wa manunuzi ya umma na uhakiki wa ukaguzi uliofanyika Mwaka wa Fedha 2014/15.

Ukaguzi huo ulilenga kuangalia iwapo mikataba ya manunuzi iliyoingiwa katika kipindi husika ilitekelezwa au inatekelezwa kwa mujibu wa vigezo na masharti yaliyoainishwa kwenye mikataba husika inalingana na thamani ya fedha za umma zilizotumika. 

Katika ukaguzi wa uhakiki wa mwaka 2014/15, jumla ya ya taasisi nunuzi 70 zilifanyiwa ukaguzi wa ukidhi uliongalia namna taasisi hizo zilivyozingatia sheria na kanuni za manunuzi pamoja na matumizi ya nyaraka za miongozo na mifumo iliyoandaliwa na PPRA. 

Taasisi zilizoguswa na ukaguzi huo uliofanyika kati ya mwezi Aprili na Septemba, 2016 ni pamoja na taasisi 15 zilizo kwenye kundi la Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa 25; na mashirika ya umma 30.

Jumla ya mikataba 21,313 ya manunuzi yenye thamani ya Tsh Trilioni 1.05 ilifanyiwa ukaguzi huo, ambapo kati yao mikataba 118 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 55.34 ilikaguliwa katika halmashauri za serikali za mitaa.

Aidha taarifa hiyo inaongeza kuwa katika mikataba 122 ya ukusanyaji wa mapato iliyokaguliwa katika Malmaka tisa za Serikali za Mitaa, kumebainika mapungufu kadhaa katika usimamizi wa mikataba hiyo ambapo kumesababisha halmashauri hizo kushindwa kukusanya kiasi cha shilingi 761.54 milioni.

Inaelezwa kuwa pamoja na hasara hiyo, ukaguzi unaonesha kuwa halmashauri hizo hazikuchukua hatua zozote dhidi ya wazabuni waliopewa jukumu hilo kwa mujibu wa mikataba waliyoiingia.

Katika kutekeleza sera ya ugatuaji (upelekaji) wa madaraka kwa wananchi, Serikali iliamua kuwa na programu za maboresho ya Serikali za Mitaa zinazolenga kuongeza ufanisi kwa Watendaji ili waweze kutoa huduma bora na endelevu kwa wananchi likiwemo suala la ununuzi wa vifaa, kandarasi za ujenzi na huduma mbalimbali.

 Chini ya Sera ya Serikali ya ugatuaji wa madaraka, rasimali fedha zinaelekezwa moja kwa moja katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambapo sehemu kubwa ya matumizi yake huelekezwa katika masuala ya manunuzi.

Miongoni mwa Miradi inayotekelezwa kupitia programu hizo ni Mradi wa Kujengea Uwezo Serikali za Mitaa kwenye Ununuzi wa Umma (MKUSEMU) ulioanza kutekelezwa kuanzia mwezi Juni 2012 na kukamilika Desemba 2017.

 Aidha mradi huo umelenga kuwajengea uwezo maafisa watendaji wa Kijiji au Mtaa kuelewa masuala muhimu yanayohusu usimamizi wa fedha kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa namba 9 ya Mwaka 1982; na Sheria ya Ununuzi Namba 21 ya Mwaka 2004 pamoja na kanuni za Ununuzi za Serikali za Mitaa za Mwaka 2007.

 Wadau wakuu wa mradi huo ni Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ikishirikiana na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kikiwemo chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo). 

Mikoa iliyopo katika mradi huo na halmashauri zake katika mabano ni pamoja na Dodoma (Kondoa na Kongwa), Iringa (Kilolo na Mufindi), Tanga (Lushoto na Muheza);, Kigoma (Kasulu na Kigoma vijijini), na Pwani (Mkuranga).

 Katika utafiti wa awali uliofanyika katika miradi ya maendeleo ya mikoa hiyo na vituo vya kutolea huduma ya ununuzi (shule, ujenzi wa madarasa, hospitali) ilibainika kuwa taratibu zinatofautiana kati Halmashauri moja na nyingine, Kata moja na nyingine, hali kadhalika kati ya Kijiji kimoja na kingine.

Uanzishaji wa mradi huo umekuja kufuatia mapungufu yaliyopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweza kufanya ununuzi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.

Katika kaguzi mbalimbali zilizofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG)  na PPRA imeonesha kiwango cha uelewa wa taratibu za ununuzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni mdogo hususan kwenye kuandaa na kutekeleza mpango wa ununuzi wa mwaka, kuendesha michakato ya zabuni, utunzaji wa kumbukumbu.

Kuwepo mradi huo, kutawezesha kuwepo ufanisi katika Ununuzi wa umma, na hivyo kuiwezesha jamii kupata taarifa za ununuzi na kuweza kuzifuatilia na kutoa taarifa ya  kuhusu utekelezaji wa mikataba, kuimarisha mfumo wa kusimamia na kuhakikisha ubora wa manunuzi.

Askofu Gadi atuma salamu za rambirambi Shule ya Lucky Vincent Arusha, aomba mvua zinazoendelea zisiwe na madhara kwa jamii

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Good News For All Ministry Dkt. Charles Gadi (mwenye miwani)akifanya maombi maalum  pamoja na Wachungaji wa kanisa hilo ya kuomba mvua zinazoendelea nchini zisiwe na madhara kwa jamii.
·         Askofu Gadi 01: Askofu wa Kanisa la Good News For All Ministry Dkt. Charles Gadi akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa wa wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent ya Jijini Arusha pamoja na kumpongeza Rais john Magufuli kwa kuzindua miradi mikubwa ya kimaendeleo hivi karibuni, kushoto ni Mchungaji wa kanisa hilo Mchungaji Andrew Thomas na kulia ni Mchungaji Palemo Massawe. Picha na Eliphace Marwa -Maelezo

Mradi wa Hakuna Wasichoweza wazidi kuleta faraja kwa watoto wa kike mkoani Lindi

$
0
0
Mradi wa “Hakuna Wasichoweza” unaoendeshwa kupitia taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation na kutekelezwa kwa ushirikiano wa Shirika lisilo la Kiserikali la T-Marc katika mkoa wa Lindi unazidi kuleta faraja kwa watoto wa kike ambapo kwa mwaka huu wasichana wapato 2,000 tayari  wamenufaika nao.

Mradi huu ni mwendelezo wa program ya Hakuna Wasichoweza uliozinduliwa miaka ya nyuma-Mtwara, umewafikia wanafunzi na walimu 10,000 mashuleni kupatiwa elimu ya afya ya uzazi na huduma ya vifaa vya kujisitiri (pedi) wakati hedhi kwa watoto wa kike.

Akiongea na mtandao huu Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald alisema tangu mradi huu uanze umekuwa na mafanikio makubwa kwa kufikia idadi kubwa ya walengwa wanaosoma katika shule mbalimbali mkoani Lindi ambapo wameweza kupatiwa elimu kuhusiana na mabadiliko ya miili yao katika mchakato wa makuzi na wamewezeshwa kwa kupatiwa taulo za hedhi, Alisema Oswald.

Naye mmoja wa wanafunzi walionufaika na mradi huu, Riziki Athuman (14) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Tandangongoro akiongea kwa niaba ya wenzake kuwa “Hivi sasa wanaelewa kuhusina na suala zima la hedhi na jinsi ya kukabiliana nalo hususani kujiweka katika hali ya usafi na kutumia taulo za kisasa ambazo zinatuwezesha kuendelea na masomo tofauti na awali ambapo wasichana wenzangu wengi walishindwa kuhudhuria vipindi shuleni wanapokuwa kwenye hedhi kutokana na kutokuwepo na mazingira rafiki.

Suala la hedhi lilikuwa halizungumziwi kabisa tofauti na sasa ambapo linajadiliwa na kutafutiwa suluhisho la kukabiliana na changamoto zake hususan kujenga vyoo na miundombinu ya maji mashuleni ya kuwasaidia watoto wa kike wanapokuwa kwenye hedhi”. Alisema Riziki.

RC NDIKILO AMALIZA ZIARA YAKE KIMKOA NA KUSISITIZA MAMBO MAKUU MANNE

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani 

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,amemaliza ziara yake ya kutembelea wilaya sita kimkoa,ambapo amehimiza mambo makuu manne ikiwemo ulinzi na usalama,uwekezaji,kilimo cha matunda na korosho.

Aidha amekemea migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikigharimu maisha ya watu na wengine kujeruhiwa pasipo sababu za msingi.

Akimaliza ziara yake wilayani Kibaha,mhandisi Ndikilo,alieleza mkoa wa Pwani una viwanda vitatu vikubwa vya kusindika matunda kwa sasa ambavyo endapo wakulima watavitumia watanufaika kwa kiasi kikubwa.

Alisema,kiwanda cha Bakhresa ambacho kipo Mwandege -Mkuranga kimeshaanza kazi na kile cha Elven Agri co.ltd kilichopo kata ya Mapinga -Bagamoyo huku cha Sayona kinachojengwa kata ya Mboga kikiwa kwenye hatua za mwisho za ujenzi.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa kina uwezo wa kusindika tani 350 za matunda kwa siku na uwekezaji wake umegharimu sh.bil.261.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, akiwa ametembelea shamba la mfano la zao la biashara la korosho lililopo Ruvu JKT, wilayani Kibaha. (picha na Mwamvua Mwinyi) . 

HaloPesa, Selcom kupanua wigo wa huduma za kifedha

$
0
0
  Katika kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel imeendelea kuunganisha huduma yake ya Halopesa na huduma nyingine zaidi ili kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania .

Katika kulifanikisha hilo Halotel imeingia makubaliano ya mkataba wa utoaji wa huduma na kampuni ya Selcom, ushirikiano utakaowawezesha mamilioni ya wateja wa mtandao huo kutoa na kutuma pesa, kununua vocha za muda wa maongezi na kufanya manunuzi mbalimbali.

Hatua hii itawawezesha watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ikiwa ni sehemu ya kufanikisha azma ya serikali ambayo inazitaka taasisi mbalimbali za kifedha kuwafikia wananchi na huduma zao hasa kwa maeneo ya vijijini.

Akizungumza wakati wa makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Bw. Le Van Dai amesema kuwa ni hatua nyingine kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi nchini Tanzania. Sasa kupitia huduma ya Halopesa itakuwa imewezesha kupanua wigo kwa wateja wa mtandao huo kuweza, kutoa na kuweka fedha, pamoja na kufanya malipo mbalimbali kwa urahisi zaidi.

“Ushirikiano huu ni wa kipekee katika kurahisisha maisha ya watanzania ambao wamekuwa wakipata tabu kupata huduma za kifedha kutokana na maeneo wanayoishi. Sisi kama Halotel hadi sasa tumewafikia watanzania kwa zaidi ya asilimia 95. Hivyo ni dhahiri kwamba wateja watakaojiunga nasi wataweza kutoa au kuweka fedha huko huko waliko kupitia kwa mawakala wetu ambao wameenea nchi nzima,” alisema Dai. 
  Mkuu wa Halotel, Le Van Dai (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango wa Selcom, Benjamin Mpamo wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kibiashara baina ya kampuni hizi yatakayo wawezesha wateja wa  Halopesa kutoa na kuweka pesa, pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia mawakala wa Selcom nchi nzima.

  Mkuu wa Halotel, Le Van Dai (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango wa Selcom, Benjamin Mpamo wakitia saini mikataba ya makubaliano ya kibiashara baina ya kampuni hizi yatakayo wawezesha wateja wa  Halopesa kutoa na kuweka pesa, pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia mawakala wa Selcom nchi nzima, Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa kampuni hizo.

SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI

$
0
0

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. 

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imesema itajenga daraja la juu kwa ajili ya kivuko cha waenda kwa miguu(Over head Pedestrian Bridge) eneo la Kawe Bondeni. 

Hayo yamesemwa Bungeni leo na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe aliyekuwa akijibu swali la Mbunge wa Kawe Mhe.Halima Mdee kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano. 

“Tatizo la kivuko cha waenda kwa miguu eneo la Kawe Bondeni hadi Jeshini Kata ya Mbezi Juu na Kawe Tayari limeshapatiwa ufumbuzi”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe. 

Amesema kwa sasa Mkandarasi wa kujenga daraja hilo yupo kwenye hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi katika eneo hilo muhimu. 

Aidha Serikali ina mpango wa kuweka taa za kuongozea magari katika Barabara ya Mwenge-Tegeta ambapo Mkandarasi ameshapatikana wa kuweka taa hizo katika makutano ya Afrikana na anatarajia kuanza kazi wakati wowote. 

Mbali na Hayo tatizo la Udogo wa mapokeo na matoleo ya maji ya mvua yanayosababisha kero katika eneo la Makonde hadi Mbuyuni,Serikali inakamilisha taratibu za kusaini mkataba wa ujenzi wa mtaro mkubwa eneo la Mbezi Samaki ambao utatatua kero ya barabara kujaa maji nyakati za mvua. 

“Serikali ya Awamu ya Tano ni makini sana na itahakikisha changamoto hizi inazifanyia kazi ili wananchi waweze kutumia barabara zetu vyema”Aliongeza Mhe.Kamwelwe.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe

TFF YAVITAHADHALISHA VYOMBO VYA HABARI KUACHA KAMPENI CHAFU

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limevionya Vyombo vya Habari ambavyo vinaripoti habari zenye lengo za kuichafua shirikisho hilo na viongozi wake .

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa TFF Alfredy Lucas alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,  juu ya tuhuma zilizotolewa na moja ya gazeti la kila siku.

“Navitaka baadhi ya vyombo vya habari nchini kuacha mara moja kampeni za upotoshaji zenye lengo la kuwachafua viongozi wa juu wa shirikisho la soka hapa nchini.Amesema Alfred Lucas.

Amesema TFF imeshtushwa na taarifa inayoendelea kutolewa kwenye gazeti moja la kila siku ikidai kuwa kuna ufisadi ndani ya shirikisho wakati madai hayo ni ya uongo na yenye lengo la kujenga mtazamo hasi dhidi ya shirikisho na viongozi wake.

Ametaja kuwa Gazeti hilo la kila siku limetumia taarifa ya ukaguzi wa fedha iliyofanywa na wakaguzi kutoka TAC kujenga picha kuwa ni ushahidi tosha wa kuwepo kwa ufisadi ndani ya shirikisho.

Ameweka wazi kuwa taarifa ya ukaguzi wa fedha ya TAC haikuwahi kuituhumu TFF kwa ufisadi. Taarifa ilibaini maeneo ya kiuhasibu ambayo yalihitaji maelezo ya ziada ya namna baadhi ya malipo yalivyofanyika (audit queries), na ufafanuzi ulitolewa kwa ufasaha na watendaji wa shirikisho na kupelekwa mbele ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho.

Amesema hata hivyo gazeti hilo ambalo limeonekana kuweka kando kabisa misingi ya uandishi wa habari, limechapisha taarifa bila hata kutoa nafasi kwa wanaotuhumiwa kujibu na kutoa ufafanuzi stahiki.

“Rais na katibu mkuu wa shirikisho wanahudhuria mikutano ya CAF nje ya nchi wakati gazeti hilo likiendelea kuporomosha mlolongo wa tuhuma bila kutoa haki ya kusikilizwa kwa wanaoandikwa vibaya, TFF inaliangalia suala hili kama kampeni chafu inayofanywa ili kushawishi matokeo ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Agasti mwaka huu.” Amesema Alfredy Lucas.

Pia taarifa hii potofu inalenga kulihamisha taifa kutoka kwenye masuala ya msingi kama kuiunga mkono Serengeti Boys kwenye mashindano ya Afrika na kuanza kujadili masuala yanayohusiana na siasa za uchaguzi wa TFF.

TFF kwa sasa inatafakari hatua za kisheria za kuchukua dhidi ya vyombo vya habari husika na inachukua nafasi hii kuvisihi vyombo vya habari kuacha mara moja kujihusisha na kampeni ya kuchafuana ambayo ni kinyume na misingi ya maadili ya uandishi wa habari.

Afisa habari wa TFF Alfredy Lucas
Waandishi wakifatili akatika mkutano huo

MBEYA WAANZA SAFARI YA KUJA KUIVAA YANGA WIKIENDI HII

$
0
0
KIKOSI Mbeya City Fc , leo kimeanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wenyeji Yanga uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki hii. 

Afisa habari wa kikosi hicho Dismas Ten amesema kuwa jumla ya nyota 18 na viongozi 10 watakuwa kwenye msafara huo kwa ajili ya kuhakikisha City inafanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu na kujiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi. 

Ligi iko kwenye hatua za mwisho, huu ni mchezo muhimu na matarajio yao ni kushinda na kupata matokeo muhimu kwenye mchezo wa jumamosi, kwani wanafahamu Yanga ni timu nzuri na iko kwenye mbio za ubingwa lakini hilo haliwapi hofu kwa sababu wana kikosi kizuri. 


Ten amesema katika duru ya kwanza waliweza kupata matokeo mazuri na sasa wanakwenda Jijini Dar kuhitimisha dhamira yao ya kupata pointi sita msimu huu kutoka kwao

Akiendelea zaidi Ten alisema City imekuwa na wiki nne za kujindaa vizuri ili kuikubali Yanga kwa kufanya mazoezi mazito ikiwa ni pamoja na kucheza michezo zaidi ya mitano ya kirafiki ambayo imesaidia kuimarisha uwezo wa nyota wa kikosi kiuchezaji na kuwaongezea Morari ya kutaka kushinda kwenye uwanja wa Uhuru. 

"Tumekuwa na wiki nne za kujindaa, hatukucheza mchezo wowote baada ya sare ya 1-1 na African Lyon kwenye uwanja wa Sokoine April 13,hivyo nguvu zetu zote tunaziweka siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa,".amesema Ten. 

Miongoni mwa nyota waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Mrisho Ngassa,Hassan Mwasapile,Tumba Lui na Zahoro Pazzi 

Kwa upande wake kocha mkuu Kinnah Phiri amesema hana wasiwasi na mchezo huo wa jumamosi kwa sababu anaifahamu vyema Yanga hasa baada ya kuifuatilia kwenye michezo kadhaa na tayari ameandaa mbinu za kuhakikisha vijana wake wanapata ushindi. 

"Sina wasiwasi,wakati huu ambao sikuwa na mchezo wa ligi nilikuwa nawafuatilia, najua mbinu zao na nimewandaa vijana wangu vizuri ni wazi tutashinda tena dhidi yao kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa duru ya kwanza".

SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA WABUNGE WA BUNGE LA UMOJA WA ULAYA

$
0
0



Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya Mhe. Alojz Peterle (kulia) pale ugeni wa Wabunge kutoka Bunge la Umoja wa Ulaya ulipomtembelea leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
A
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza jambo pale ugeni wa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya ulipomtembelea leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
A 1
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza  jambo pale alipopata ugeni wa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, katika Kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
A 4
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wanne kulia) akipiga picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Mhe. David Martin (wanne kushoto) baada ya kumalizika kikao kilichofanyika  leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
A 3
Wageni wa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ambao ni Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wakifwatilia Vikao vya Bunge vinavyoendelea leo Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE) 

RAIS JACOB ZUMA KUHUDHURIA KONGAMANO LA BIASHARA NCHINI MEI 11.

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma anatarajiwa kuhudhuria Kongamano la Biashara litakalofanyika kesho May 11 katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika Kongamano hilo, Mhe. Zuma ataongozana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, pamoja na Wafanyabiashara wakubwa kutoka nchi hizo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari amesema kuwa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia kituo hicho wameandaa Kongamano hilo, na kutoa wito kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza kwa wingi kukutana na Wafanyabiashara wenzao wa nchi hiyo ya Afrika Kusini.

Tandari amesema kuwa Sekta kubwa zitakazojadiliwa katika Kongamano hilo ni Sekta ya Nishati, Viwanda, Miundombinu, Uchukuzi, Usafirishaji, Huduma ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Maji na Madini.

Pia amesema Afrika Kusini ni Taifa ambalo lipo katika nchi kumi bora zilizowekeza kwa wingi hapa nchini, hivyo ni fursa kuchamshana kiuchumi, pia wameandikisha miradi 63 ambayo imeajiri vijana wengi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam kuhusu Kongamano la Biashara litakalofanyika May 11 mwaka huu jijini Dar na kuhudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli.


TFF YAMPONGEZA TENGA KUPATA UBOSI CAF

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limempongeza Rais wa Heshima wa shirikisho hilo, Leodegar Chilla Tenga kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Kamati ya Usimamizi wa Leseni za Klabu katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Afisa Habari wa TFF ,Alfredy Lucas amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya CAF, Tenga atasaidiwa Dany Jordaan wa Afrika Kusini katika kusimamia mpango huo muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika.

“Uteuzi wake ulitangazwa na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad Jumatatu Mei 8, 2017 mara baada ya Kikao cha Kamati ya Utendaji CAF, chini uongozi mpya kilichofanyika katika Hoteli ya Sheraton, Manama, Bahrain.Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, Rais wa TFF Jamal Malinzi alimpongeza Tenga akisema: “Hii ni fursa nzuri inayojenga taswira ya thamani na uwezo viongozi wetu wa mpira wa miguu nchini na kutambulika nje ya nchi katika taasisi za kimataifa kama CAF.

“Kwa niaba ya Kamati ya Wanafamilia wote wa mpira wa miguu, Wajumbe wa Kamati Utendaji, nachukua nafasi hii kumpongeza sana sana Rais wa Heshima wa TFF, Mzee wetu, Ndugu Leodegar Tenga kwa nafasi nyeti ya kusimamia Kamati ya Leseni za Klabu. Tunamtakia kila la kheri tukiamini nafasi hiyo ana uwezo nayo na bila shaka Mwenyezi Mungu, atakuwa pamoja na Tenga,” amesema Tenga.

Katika katika mkutano wa Bahrain, Rais wa CAF alipendekeza majina ya viongozi wawili kuwa Makamu wa rais, wa kwanza ni Kwesi Nyantakyi kutoka Ghana na wa pili ni Omari Selemani kutoka DR Congo na pendekezo hili lilipitishwa na kamati.

Uteuzi wa wajumbe wawili wa ushirikiano wa Kamati ya Utendaji. Kwa mujibu wa masharti ya sheria, Rais wa CAF alifanya mapendekezo ya wanachama mawili wa ushirikiano kwenye kamati ya utendaji ya CAF ambako wanachama waliopitishwa ni Moses Magogo (Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Uganda na Ahmed Yahya – Rais wa Shirikisho la Mpira wa Maurtania.

Muundo wa Kamati ya dharura, Mwenyekiti ni Rais wa CAF, Ahmad Ahmad na wajumbe wake ni Kwesi Nyantakyi (Ghana), Omari Seleman (DR Congo), Fouzi Lekjaa (Morocco), Souleiman Waberi (Djibouti) na Musa Bility (Liberia).

MKURUGENZI MKUU WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU AFANYA KIKAO NA WAFANYAKAZI WA OFISI HIYO NA KUWATAKA KUFANYA KAZI KWA BIDII

$
0
0
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Dkt.Chuwa amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu rasmi nchini. (Picha na Veronica Kazimoto)
  Kaimu Mkurugenzi wa Utawala, Fedha na Masoko Bi. Lilian Karumuna wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akifafanua jambo wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania tawi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (TUGHE) Bi. Raya Mikidadi akifafanua jambo wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. (Picha na Veronica Kazimoto)

WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA YA BIASHARA YA MENO YA TEMBO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Watu wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali za Meno ya Tembo vipande sita ambavyo vilivyokamatwa Chanika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Somon Sirro amesema kuwa  vipande hivyo vilikamatwa wakati polisi wakifanya operesheni kupata taarifa ya watu wanataka kufanyabiashara ya kuuza vipande sita vya meno ya tembo na kwenda kuwatia hatiani nje ya nyumba ya moja ya watuhumiwa hao.

Watuhumiwa hao ni Mfanyabiashara Senei Abbas (36) pamoja na  Juma Mkong’wa (33) Fundi Ujenzi Mkazi wa Gongolamboto  jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo cha St. Joseph, Lewis Mbise (23) kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya Luger CZ yenye namba za usajili C 4122 ikiwa na risasi 13 ndani ya magazine .

Mwanafunzi huyo alipohojiwa alivyopata silaha na kukiri kuwa aliiba kwa baba yake pamoja na fedha Tasilimu sh.800,000.
Jeshi polisi limeagiza kukamatwa kwa baba wa manafunzi kwa kukosa kutunza silaha mpaka mwanae anapata nafasi ya kwenda kuiiba.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi inawashilikilia watu watatu kwa tuhuma za kuvujisha mtihani wa kidato cha Sita ambao unafanyika hivi sasa.

Watuhumiwa hao ni Mwalimu  Mussa Elius , Mwalimu Innocent Mrutu pamoja na mwanafunzi wa Kidato  cha Sita, Ritha Mosha .
Kamanda Sirro amesema wanaaendelea na mahojiano kuhusiana na mtihani  wa kidato cha sita unaoendelea kufanyika.

Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa watatu ambao ni walinzi kituo cha Mafuta cha Camel Kurasini kwa kula njama za wizi wa mauta lita 36000 zenye thamani ya sh. Milioni 72.

Walinzi hao Hamis Peter (49) mkazi wa Charambe, Jumanne Hamis (35) pamoja na Huruka Ramadhan (37).
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dar es Salaam  leo. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionyesha vipande vya meno ya tembo vilivyokamtwa na jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionyesha silaha waliokamata kwa mwanafunzi ambayo aliiba kwa baba yake  leo jijini Dar es Salaam.

RAIS WA ZANZIBAR AREJEA NCHINI AKITOKEA DJIBOUTI.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Moahammed Mahmoud mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Wakuu wa Vikosi vya SMZ mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein wa kwanza kulia akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na wabunge Mussa Ntimizi wa Igalula na Felista Bura wa Viti Maalum, bugeni mjini Dodoma Mei 10, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, George Simbachawene kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Mei 10, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge, Kange Lugora wa Mwibara (kushoto)  na Katani Ahmed Katani wa Tandahimba (katikati) kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10,2017.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images