Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MAJALIWA AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa katika  ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa katika  ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa  Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa baada ya kufungua mafunzo hayo katika  ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya  Rais, Selemani Jafo na kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja. Aliyekaa kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa  katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na  Mkuu wa Wilaya  ya  Dodoma Mjini, Christina Mndeme baada ya kufungua Mafunzo ya  Wakuu wa Wilaya  na Wakurugenzi wa Halmashauri za Seriklali za Mitaa katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Balozi Seif akutana na Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akikiongoza Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar akiwa Mwenyekiti  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad akitoa taarifa ya tathmini ya awali ya athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Kanda ya Zanzibar Nd. Mohamed  Khamis Ngwali akitoa tathmini ya hali ya Mvua zinazoendelea kunyesha katika ukanda wa Pwani katika Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi , Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Nd. Mustafa Aboud Jumbe akitoa ufafanuzi wa hatua zilizochukuliwa na Wizara yake za kurekebisha baadhi ya miundombinu iliyoharibiwa na Mvua za Masika zinazoendelea kunyesha. Picha na – OMPR – ZNZ. 

MAELEZO TV: SERIKALI IMETENGA SHILINGI BILIONI 30 KUKAMILISHA MALIPO YA FIDIA KWA WAKAZI WA KIPUNGUNI

MUFINDI YAENDELEA KUTEKELEZA SERA YA KUWA NA ZAHANATI KILA KIJIJI.

$
0
0
Na Afisa Habari Mufindi
Halmashauri ya Wilaya ya Maufindi imeendelea kutekeleza sera ya serikali ya kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na Zahanati kwa kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye  zahanati za Vijiji vinne kati ya vitano zilizopo kata ya Ihalimba Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
 Uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi umetekelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh. Festo Mgina, Diwani wa kata Ihalimba Mh. Award Mahanga sanjari na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri Prof. Riziki Shemdoe.
Taarifa hiyo imevitaja vijiji vilivyo nufaika na huduma hiyo muhimu kwa usatawi wa afya ya jamii kuwa, ni pamoja na Kijiji cha Wamimbalwe uwekaji wa Jiwe la msingi, uzinduzi wa Zahanti ya Kijiji cha Vikula, uzinduzi wa zahanati ya Kijiji cha Nundwe pamoja na uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye azahanati tarajiwa ya Kijiji cha Ihalimba.  
 Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe, akizindua Zahanati ya  ya kijiji cha Vikula halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
 Mwenyakiti wa Halmashauri Mh. Festo Mgina, akizindua Zahanati ya Kijiji cha Nundwe Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

Mwenyekiti wa halmashauri akiwahamasisha wakazi wa Kijiji cha Ihalimba kuchangia Mfuko wa CHF kabla ya kuweka jiwe la Msingi kwenye jengo la zahanati ya Kijiji hicho.​​ Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

SERIKALI KUBORESHA KIWANGO CHA VYOO BORA KUFIKIA 2025

$
0
0
 Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akizungumza mbele ya wabunge na wadau mbalimbali wa afya na mazingira hwapo pichani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ya utunzaji wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” iliyofanyika leo mjini Dodoma.

 Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa kampeni ya ya utunzaji wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” uliofanyika mjini leo mjini Dodoma.

 Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu katikati akiwa amebeba nembo inayoashiria uzinduzi wa kampeni ya kutunza mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” uliofanyika mjini Dodoma , wengine ni wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na baadhi ya wabunge.

Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ya utunzaji wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” uliofanyika mjini leo mjini Dodoma.
Picha na Ally Daud-WAMJW DODOMA. 

DC SHINYANGA APONGEZA WANANCHI KUJENGA KITUO CHA POLISI ISELAMAGAZI

$
0
0


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua jengo la kituo cha Polisi kata ya Iselamagazi ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na mbunge wao wa Solwa Ahmed Salimu.

Ukaguzi wa jengo ukiendelea
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akiteta jambo na viongozi wa serikali pamoja na baadhi ya madiwani wa halmashauri kabla ya kuingia kwenye mkutano wa viongozi wa Sungusungu na watendaji wa vijiji,kata na vitongoji kujadili ajenda mbili za ulinzi na usalama pamoja na kuunda ushirika wa vyama vya kuuza mazao ili kuinua wakulima kiuchumi sambamba na kuhifadhi chakula cha akiba ili kukabiliana na janga la njaa hapo baadae.
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akizungumza na viongozi wa Sungusungu,baadhi ya watendaji wa kata ,vijiji,vitongoji na Madiwani wa halmashauri hiyo juu ya kudhibiti uhalifu kwenye tarafa hiyo ya Nindo pamoja na kuwafichua wahalifu ambao huhatarisha hali ya amani. 




SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

WANANCHI KILOLO MKOANI IRINGA WATAKIWA KUUZA MAZAO YAO KWA VIPIMO SAHIHI

$
0
0
 Mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  mkoani  Iringa  Asia  Abdalah  akiwataka  wananchi wa  kijiji  cha Irindi na Magana  kata ya  Mahenge  kuachana na uuzaji mazao kwa  vipimo batili
Mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  Asia Abdalah  akiwahutubia  wananchi  mwenye   kilembe  cha madoa mekundu ni meneja  wa  vipimo  mkoa wa Iringa Zainabu Kafungo. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

MAELEZO TV: JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA TAREHE 09.05.2017.

BALOZI FATMA AWASILISHA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO NCHINI QATAR

$
0
0
Mhe. Fatma Mohammed Rajab, Balozi  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar akiwa katika mazungumzo na Mhe. Sultan bin Saad Al Muraikhi, Waziri wa Nchi, Mambo ya Nje wa Qatar. Mazungumzo hayo yalifanyika baada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho. Wawili hao walizungumza masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar.
Balozi  wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Mohammed Rajab akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Sultan bin Saad Al Muraikhi, Waziri wa Nchi, Mambo ya Nje wa Qatar ofisini kwa Mhe. Waziri. Mhe. Fatma Rajab anakuwa Balozi Mkazi wa kwanza kuiwakilisha Tanzania katika Taifa la Qatar. Mhe. Balozi alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Doha alipokelewa na Idara ya Itifaki ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar. Aidha, wawakilishi wa Watanzania wanaoishi nchini humo walifika Uwanja wa Ndege kumlaki
Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab, akiwa na viongozi wa Watanzania wanaoishi nchini Qatar.

MAZUNGUMZO YA BAINA YA MAWAZIRI WA TANZANIA ZANZIBAR NA DJIBOUTI

$
0
0
 Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakizungumza na Mawaziri wa Serikali ya Djibouti (hawapo pichani) walipokutana katika kujadili mambo mbali mbali  masuala ya ushirikiano wa kiuchumi baina pande mbili hizo ikiwemo Tanzaniz na Djbouti katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 Waziri wa Ujenzi,Usafirishaji na Mawasiliano mhe,Balozi Ali Abeid Karume (kushoto) na Waziri wa Afya mhe mahmoud Thabit Kombo walipokuwakatika kikao cha pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Djiboutiambapo walizungumzia zaidi ushirikiano katika nyanja za kiuchumi walipokuwa katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Mawaziri wa Serikali ya Djibouti wakizungumza naMawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  (hawapo pichani) walipokutana katika kujadili mambo mbali mbali  masuala ya ushirikiano wa kiuchumi baina pande mbili hizo ikiwemo Tanzaniz na Djbouti katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Picha na Ikulu.

Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wakabidhi Vifaa Kwa Shughuli za Kijamii Jimboni

$
0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza nas Wananchi wa Shehia tatu za Bungi, Ubago na Tunguu wakati wa kukabidhi vifaa kwa ajili ya shehia hizo tatu kwa matumizi ya Kijamii wakati wa shida na raha, Vifaa walivyokabidi majiko ya gesi 3, sinia 800  mitungi ya gesi 6 na mabusati. kwa ajili ya matumizi yao katika shughuli za kijamii, hafla hiyo ya makabidhiani imefanyika katika Tawi la CCM Tunguu Wilaya ya Kati Unguja. Na kuhudhuriwa na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mbunge wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Khalifa Salim Suleiman akizungumza na wananchi wa jimbo lake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii katika jimbo lao ikiwa ni kutimiza ahadi kwa wananchi wa jimbo lao walioitowa wakati wa kampeni ya uchaguzi.hafla hiyo imefanyika katika tawi la CCMTunguu Wilaya ya Kati Unguja.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu wakikabidhi vifaa mbalimbali waliohidi kwa wananchi wa jimbo lao wakikabidhi vifaa hivyo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdallah na Uongozi wa jimbo hilo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Tawi la CCM Tunguu Unguja. wakikabidhi mabusati na sinia.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar wakikabidhi majiko ya gesi kwa ajili ya shia tatu kila shehia imepata jiko moja na mitungi ya gesi miwili. na sinia 200, kwa ajili ya matumizi ya kijamii katika shehia zao.Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Tawi la CCM Tunguu Unguja. 

Eckobank Tanzania yawahakikishia wateja wake kuendelea na shughuli zake nchini Tanzania

$
0
0

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict amefanya mkutano na waandishi wa habari leo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, na kueleza kwamba hawana dhamira ya kusitisha shughuli zao nchini kutokana na ahadi na malengo makubwa waliyojiwekea ya kuleta maendeleo ya kiuchumi Tanzania.

“Hii ilikuwa ni ahadi yetu tangu tulipoanza kufanya shughuli zetu hapa nchini miaka saba iliyopita na itaendelea kuwa ahadi yetu mpaka hivi sasa,” alisema Benedict.

Licha ya kukiri kwamba kumekuwapo na ongezeko la wateja kushindwa kurejesha mikopo yao mwaka jana, alisema benki hiyo imejiwekea utaratibu mzuri na hatua sahihi za jinsi ya kukabiliana na hali hiyo.

Alisema, “Tumechukua hatua muhimu ili kuwezesha urejeshaji wa mikopo mbalimbali ndani ya miezi mitatu iliyopita na tunaamini kwamba mfumo tuliouanzisha utatuletea mafanikio makubwa ndani ya miezi michache ijayo.”

Aliongeza kuwa, nguvu ya msingi ya benki hiyo ina ungwa mkono na wanahisa wakubwa ambao wanaifanya benki kuwa imara, madhubiti na kuaminika na hivyo kuwa moja ya chombo cha fedha kinachoweza kuendana na hali yoyote ya dhoruba.

Washirika wakubwa wa Ecobank ni pamoja na Nedbank ya Afrika Kusini( asilimia 21), Qatar Nation Bank (asilimia 20), Public Investiment Corporation ya Afrika Kusini ( asilimia 14) na International Finance Corporation iliyopo chini ya Benki ya Dunia (asilimia 14).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwahakikishia wateja wa benki hiyo na umma wa ujumla kuhusu dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kutoa huduma zake hapa nchini. Kushoto Mkuu wa kitengo cha Wateja wa rejareja wa benki hiyo, Ndabu Lilian Swere.
Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa EcoBank Tanzania Raphael Onyango akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake hapa nchini kutokana na ahadi na mikakati madhubuti waliyojiwekea. Wa pili kushoto ni Ndabu Lilian Swere, Mkuu wa kitengo cha Wateja wa rejareja, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzania, Raphael Benedict (wa pili kulia) na Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Respige Kimati (kulia).
Mkuu wa kitengo cha biashara wa Ecobank Tanzania, Respige Kimati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake nchini kutokana na ahadi na malengo yake. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za biashara za ndani Ndabu Lilian Swere.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MAY 10,2017


WAZIRI MWAKYEMBE AKIONGELEA UHURU WA HABARI NCHINI

TAARIFA KUTOKA KWA WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO

PUMA ENERGY YAGAWA FULANA MAALUM KWA BODABODA ZINAZOAKISI MWANGA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

$
0
0
 Mratibu  wa Masuala ya Usalama wa Afya, Mazingira na  Udhibiti wa Ubora kutoka Kampuni ya Puma Energy, Rehema Madoffe akimvisha Abubakar Selemani mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Ungindoni iliyopo Kigamboni Dar es Salaam moja ya fulana inayoakisi mwanga ikiwa ni sehemu ya shehena iliyotolewa kwa shule hiyo kwa  ushirikiano na Taasisi ya Amend Tanzania kusaidia kampeni ya kupunguza ajali za barabarani hususani kutetea maisha ya watoto wa shule jana  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Usalama barabarani ya Umoja wa Mataifa(UN-Global Road Safety Week)

 Ofisa Mipango wa Taaasi ya Amend Tanzania, Neema Swai akigawia fulana maalum zinazoakisi mwanga kwa waendesha bodaboda wa Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam, jana, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Usalama barabarani ya Umoja wa Mataifa(UN-Global Road Safety Week)



BALOZI SYLEVESTER MABUMBA,AWASILISHA NAKALA YA HATI ZAKE ZA UWAKILISHI KWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KOMORO

$
0
0
Mhe. Sylvester Mabumba Balaozi wa Tanzania ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Komoro jana tarehe 09 Mei aliwasilisha nakala za hati zake za uwakilishi kwa Mhe. Mohambed Baccar Dossar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Komoro. Hafla hiyo ilifanyika siku hiyo hiyo ambayo Mhe. Balozi aliwasili Visiwani Komoro jambo ambalo linaonesha jinsi gani nchi hizi mbili zimedhamiria katika kuboresha na kukuza mahusiano yaliopo baina yao.
Katika hafla hiyo Mhe. Dossar alichukua fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Balozi Mabumba Visiwani Komoro na kumtakia kila la kheri katika kipindi chake ambacho atakuwa Balozi Visiwani hapa. Aidha Mhe. Waziri alimuahidi Mhe. Balozi Mabumba kuwa nchi yake itampatia ushirikiano maradufu na kwamba milango yake ipo wazi muda wowote ambapo Mhe. Balozi atakuwa na shida ya kuonana nae na kufanya mazungumzo.
 
Kwa upande wake Mhe. Balozi Mabumba alionyesha furaha yake kwa kumuelezea Mhe. Waziri kuwa amejiskia faraja sana kwa kuchaguliwa kuwa Balozi wa Pili kuiwakilisha Tanzania Visiwani Komoro na kwamba anaimani kuwa Serikali ya Komoro itampatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake.  
Aidha Mhe. Balozi Mabumba alieleza kuwa uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Komoro ni wa Kihistoria na unapaswa kudumishwa. Mhe Balozi alimueleza Mhe. Waziri kuwa moja ya agenda zake za mwanzo ambazo anataka kutekeleza ni ile ya utiaji saini wa Mkataba wa Kudumu wa Ushirikiano baina ya Tanzania na Comoro (Joint Permanent Commission).

MNADA WA HADHARA: UBALOZI WA MAREKANI, SWEDEN, UNICEF & ELZABETH GLASER PEDIATRIC AIDS FOUNDATION

$
0
0
 UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na Ubalozi wa Marekani,  Sweden, UNICEF na Elzabeth Glaser Pediatric Aids Foundation  watauza kwa mnada wa hadhara  AVR,Magari , Generator na Fanicha  tarehe 13 Mei, 2017 Jumamosi saa 4.00 asubuhi. Mnada utafanyika Golden Resort Sinza,  Lion Street.
MAGARI, GENERATOR NA AVR ZITAKAZOUZWA:

Idadi

Aina

Model

Mwaka

Hali yake

Ushuru

2

Toyota L/Cruiser GX S/Wagon

1HZ Diesel Engine

2003/2007

Nzuri

Bado

2

Toyota L/Cruiser Prado

5L Diesel Engine

2008

Nzuri

Bado

6

Nissan Patrol S/Wagon

TD 42 Diesel Engine

2008/2010

Nzuri

Bado

3

Toyota Rav4   S/Wagon

1AZ Petrol Engine

2002/2004

Nzuri

Bado

1

GMC Terrain  

2CTF Petrol Engine

2011

Nzuri

Bado

1

HINO Truck 5 Tons Tanker

1521 Diesel Engine

2009

Nzuri

Bado

1

Toyota Rush

3SZ  Petrol Engine

2007

Nzuri

Umelipwa

1

Isuzu ELF  Truck 3Tons

NKR Diesel Engine

2001

Nzuri

Umelipwa

6

Digital Voltage Stabilizer ( AVR)

 80KVA

-

Nzuri

Bado

4

Generator Honda /Yamar Diesel

8,12,16 & 27 KVA

2005/2010

Nzuri

Bado

MALI ZITAKAZOUZWA: Sofa, Dining Table, D.Chairs, Book shelve, Office Desk/Chair, Reception counter, Vitanda /Magodoro, Fridge, Freezer, Washer/ Dryer, Computer sets, Laptop, 12 pcs. Photocopy m/c Canon IR3245,3300,3080,7pcs. Kyocera KM 2550,1635 Photo copy m/c, HP Plotter (Large format color printer Q6654A), Safe, File cabinet, UPS,GYM equipment,  A/c split units na vingine vingi.


Mali zote zinaweza kukaguliwa Golden Resort Sinza,Lion Street tarehe 10 mpaka 12  Mei,  2017  kuanzia saa 4.00. asubuhi mpaka saa 10:00 jioni.

MASHARTI YA MNADA:

  1. Mnunuzi  wa fanicha na AVR atatakiwa kulipa malipo yote pale pale. Na mnunuzi wa gari na Generator atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 7 ukishindwa kulipa kwa muda huo gari/Generator litauzwa tena na dhamana haitarudishwa.
  2. Mali zote zitauzwa kama zilivyo. 
  3. Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru. 
  4. Mali yote iliyouzwa itatakiwa kuondolewa siku hiyo hiyo  baada ya kulipia malipo yote pamoja na ushuru

Kwa maelezo zaidi waone:

UNIVERSAL AUCTION CENTRE                     ( LION STREET SINZA)

SIMU  NO:  0754 284 926, 0757 284 926            E-mail: universalauction@hotmail.com

DAR ES SALAAM



Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images