Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1580 | 1581 | (Page 1582) | 1583 | 1584 | .... | 3283 | newer

  0 0  0 0


  Benny Mwaipaja, WFM, Zanzibar

  MAMIA ya wastaafu wa Taasisi za Muungano kutoka visiwa vya Pemba na Unguja-Zanzibar, wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamejitokeza kwa wingi kuhakikiwa huku wakiiomba Serikali iwaongezee pensheni kutokana na wengi wao kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.

  Wakizunguza katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, iliyoko katika eneo la Vuga, wastaafu hao wamepongeza hatua ya Serikali ya kuwahakiki ili kufahamu hali zao na kwamba hatua hiyo itasaidia kuwabaini watu wasio na sifa ya kupata malipo hayo kutoka Serikalini

  Wastaafu Bi Sauda Ramadhani Mpambalyoto na Abuu Ali Hamisi, wameiomba Serikali iangalie namna ya kuwaongezea pensheni wataafu ambao wengi wao ni wagonjwa hawajiwezi na wengine wana afya njema, wanalima, lakini wanahitaji kuwezeshwa na Serikali ili waweze kumudu maisha ambayo wamesema yamepanda.

  Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Bw. Stanslaus Mpembe, amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inaendesha zoezi la kuhakiki wastaafu wanaolipwa pensheni na wizara hiyo ili kuhuisha taarifa za wastaafu kwa lengo la kupata kanzidata (database) iliyo ili kuiwezesha Serikali kuwalipa wastaafu wanaostahili.
  Mkaguzi wa Ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Bara, Bw. Paison Mwamnyasi (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo kwa wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waliofika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, eneo la Vuga, kwa ajili ya uhakiki.
  Zoezi la uhakiki likiwa linaendelea katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, kulia ni mstaafu Bw. Amir Apacho akifanyiwa uhakiki na Mkaguzi Bi. Mary Mauki.
  Mchambuzi mwandamizi wa mifumo ya kompyuta Bi. Magreth Ambrosi Akipokea namba kutoka kwa mstaafu (aliyeko dirishani) aliyopewa kwa ajili ya uhakiki. Uhakiki wa Wastaafu unafanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, katika eneo la Vuga.
  Baadhi ya wastaafu ambao ni wagonjwa wakisubiri kupata huduma wakiwa wametengewa sehemu maalumu kwa ajili ya kupata huduma hiyo ya uhakiki.
  Afisa Tehama wa Wizara ya Fedha na Mipango akimfanyia uhakiki Bw Uleja Edward katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, zilizoko eneo la Vuga visiwani humo.
  Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko-Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali, alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki. Aliyesimama mbele yake ni Mkaguzi wa Ndani Bw. Nicholaus Jalane.  0 0
 • 02/21/17--08:30: SBL yaanza kuuza bia Kenya
 • Kwa mara ya kwanza, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeanza kuuza nje ya nchi bidhaa zake katika soko la kikanda, eneo la kwanza likiwa ni nchi jirani ya Tanzania kwa upande wa Kaskazini, Kenya.

  Shehena ya kwanza ya bia inayofahamika kama Allsopps ilisafirishwa kwenda Kenya wiki iliyopita na hivyo kukiweka kiwanda cha SBL kuwa mmoja wachangiaji wakubwa katika soko la kanda.

  Akizungumzia kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha alisema; “Hii ni hatua nyingine ya kufurahisha katika kampuni yetu na kimsingi kwa bidhaa zetu. Ukweli unabakia kwamba kumudu kupenyeza ndani ya soko la Kenya kunaonesha kuwa ubora wa bidhaa zetu sio tu kwamba unakubalika na wateja wetu wa ndani bali pia zinakubalika katika soko kubwa la kikanda.”

  Wanyancha alisema kuwa SBL inaangalia uwezekano wa kupanua mauzo ya biashara katika masoko mengine ya kikanda, hatua ambayo iko katika mkondo wa kuhamasisha Jumuia ya Afrika Mashariki na kada nyingine za kiuchumi kuongeza biashara yake ya kuvuka mpaka ndani ya ukanda huo.

  SBL imekuwa inazalisha aina za bidhaa zinazotambulika kimataifa kama vile Pilsner Lager,Tusker Lager, TuskerLite, Kibo Gold, Guinness Stout, Uhuru, The Kick pamoja na bidhaa kuu ya Serengeti Premium Lager-ambayo peke yake imeshajizolea medali kumi zinazotambuliwa kimataifa. 

  0 0  Kaimu katibu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akimuonyesha ofisi mbalimbali Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga mara baada ya kuwasili Ofisi Ndogo Makao Makuu ya UVCCM Taifa

  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akitoa ufafanuzi na kumkaribisha Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga kuzungumza na wajumbe Wa Sekretariet Ya UVCCM TAIFA pamoja na wafanyakazi Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.

  Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu
  Ngemela Lubinga akizungumza Wajumbe Sekretariet Ya UVCCM TAIFA pamoja na wafanyakazi Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.

  picha ya Pamoja ya Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga pamoja na Wajumbe wa Sekretariet Ya UVCCM TAIFA Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.  0 0


  Benny Mwaipaja, WFM, Tunduma

  KITUO cha Pamoja cha Forodha cha mpaka kati ya Tanzania na Zambia (Tunduma/Nakonde) kimeanza rasmi kutumika licha ya kukabiliwa na msongamano mkubwa wa magari unaotakiwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

  Kituo hicho kimeanza kufanyakazi tangu Februari mosi mwaka huu, ambapo watumiaji wa mpaka huo watakuwa wakihudumiwa upande mmoja wa mpaka badala ya utaratibu uliokuwa ukitumika awali ambapo watumiaji walilazimika kukaguliwa mizigo yao kila upande hatua iliyokuwa ikichelewesha biashara katika mpaka huo

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, wameeleza kuridhishwa na kazi inayofanyika mpakani hapo kupitia mfumo huo mpya.

  Hata hivyo baadhi ya madereva wanaosafirisha bidhaa kupitia mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, pamoja na kupongeza utaratibu huo mpya, wameiomba Serikali iwasiliane na upande wa Zambia, ili waongeze kasi ya kuruhusu malori kuendelea na safari yanapofika mpakani hapo bila kucheleweshwa ili kwenda sambamba na kasi ya upande wa Tanzania, ambao umeboresha kwa kiwango kikubwa utoaji wa huduma.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na watoa huduma katika mpaka huo yalikuwa ni kuwahudumia wadau wanaotumia mpaka huo kwa muda usiozidi siku moja na kuwataka madereva wa malori wanaokwazwa kuwasiliana na mamlaka zinazohusika.
  Kaimu Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha mpakani Tunduma/Nakonde, Bw. Tabaran Mzee, (aliyevaa sare za uhamiaji), akieleza namna idara hiyo ilivyoanza utekelezaji wa uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja cha Forodha kati ya Tanzania na Zambia, ambapo wafanyakazi wa idara hizo kutoka nchi hizo mbili wanafanyakazi katika jengo moja kila upande wa nchi ili kuboresha ufanyaji biashara mpakani.
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (anayeshughulikia biashara na uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda, akionesha kibao chenye namba za simu kilichowekwa Idara ya Forodha katika mpaka wa Tunduma/Nakonde zitakazotumiwa na wadau endapo watakuwa na malalamiko yoyote, lengo likiwa ni kuboresha huduma katika mpaka huo ambapo huduma ya pamoja ya forodha kati ya Tanzania na Zambia imeanza kutolewa rasmi tangu Februari mosi mwaka huu.
  Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, Viwanda, na Mambo ya Ndani, wakizungumza na Afisa Forodha wa Zambia aliyeko katika Kituo cha Forodha cha Tunduma upande wa Tanzania, baada ya Ujumbe huo wa Serikali kutembelea mpaka huo kukagua shughuli za biashara ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuanza rasmi kwa huduma ya Kituo cha Pamoja cha Forodha katika mpaka huo wa Tunduma/Nakonde (Tanzania na Zambia).
  Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Mbeya Bw. Juma Irando (aliyenyoosha kidole) akieleza jambo baada ya ujumbe wa Serikali ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea mpaka huo kukagua shughuli za biashara baada ya kuanza rasmi kwa huduma za Kituo cha Pamoja cha Forodha mpakani Tunduma/Nakonde.
  Kituo cha Uhamiaji na Forodha cha Tanzania kilichoko kwenye jengo la Zambia upande wa Nakonde, baada ya kuanzishwa kwa Kituo cha pamoja cha Forodha cha Mpakani mwa Tanzania na Zambia (Tunduma/Nakonde).


  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, alipomtembelea kujadili masuala mbalimbali yaliyohusiana na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam.Katikati ni msaidizi wa Katibu huyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga,akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa mazungumzo mbalimbali yaliyohusiana na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita.Mazungumzi hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akifafanua jambo kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, alipomtembelea kujadili masuala mbalimbali yaliyohusiana na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita.Mazungumzi hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  Mzazi wa mtoto Catherine anaomba msaada wako wa hali na mali kumuweza mtoto huyu mwenye ulemavu aweze kulipa ada yake ili aendelee na masomo . Mtoto huyu anasoma shule ya St. Bernard, lakini kutokana na mama yake kutokuwa na uwezo hivi sasa wa kulipa ada mtoto yuko nyumbani. Mama wa mtoto huyu Flora anaomba wasamaria wema kuweza kumsaidia kulipa ada ya mtoto ili aweze kurudi shuleni. Kwa wale walioguswa mnaweza kutuma msaada kwa kupitia akaunti ya Evelyn Kamukuru 0112014797900 CRDB BANK

  0 0

  Naibu wa Waziri wa Afya Dkt. Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza kwenye kituo cha kuwahudumia watu wanaotibiwa kuacha dawa za kulevya kwa kutumia methadone kilichopo Hospitali ya Mwananyamala ili kuona namna huduma zinavyotikewa. 

  Ameamua kufanya ziara hiyo sababu kuna ongezeko kubwa la wateja siku za hivi karibuni kutokana na kuongezeka udhibiti. Na kuna taarifa kwamba wanaouza dawa za kulevya (drug dealers) wameathiriwa sana kwa kupoteza mapato ya sh bilioni 70 kwa uwepo wa vituo hivi ambavyo kwa sasa vinahudumia wateja 3351, na hivyo wameanza kubuni mbinu za kuwarudisha kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa mbinu mbalimbali ikiwemo kudai kuwa methadone haifanyi kazi.

  Dkt. Kigwangalla ameagiza:

  1. Hospitali zote za kanda zianzishe vituo vya rehab ndani ya miezi 6

  2. Hospitali zote za mikoa nchini zianzishe kliniki ya kutoa methadone ndani ya miezi 6

  3. Katibu Mkuu afya ahakikishe kuna Daktari bingwa wa afya ya akili kwenye kila mkoa ili kuanzisha na kusimamia vituo vya kutoa tiba ya methadone

  4. Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni aongeze eneo la kliniki sambamba na watumishi kwenye kituo hiki 

  5. Kamishna wa polisi wa operesheni maalum afuatilie wateja (exit follow-up) wanaotoka kliniki ili kudhibiti mkakati wa drug dealers wanaolenga kuwarubuni na kuwarudisha kwenye dawa za kulevya wateja wa vituo hivi. 

  Msafara wa Dkt. Kigwangalla umeelekea Temeke Hospitali kwenye kituo kingine kama hiki.

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0
 • 02/21/17--11:42: Article 6


 • 0 0


  0 0

  Pichani ni Mpendwa wetu Jennifer Livigha maarufu aliyekuwa Mmiliki wa Libeneke la CHINGA ONE  na Mwanachama mwanzilishi wa  Tanzania Bloggers Network  (TBN) enzi za uhai wake. Marehemu alizaliwa 25.01.1979 Nachingwea, alifariki nyumbani kwake Kinyerezi 18.02.2017 Jijini Dar es salaam. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ini. Atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao Nachingwea.
  Ndugu, jamaa na mafafiki pamoja na wanachama wa TBN wakiwa wanawaaga wanaosafiri na mwili kuelekea Nachingwea
   Baadhi ya wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN) wakiwa wanaaga mwili wa aliyekuwa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer 'Chinga One' 
  Baadhi ya wanachama wa TBN , ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wanapeleka mwili wa Marehemu Jennifer katika Gari tayari kwa safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi
  Baadhi ya wanafunzi wakilia kwa uchungu 
   Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (Aliyevaa T-Shirt ya Mistari) akiongea jambo kabla ya safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi.
  Baadhi ya wana TBN wakiwa katika Msiba wa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer.

  0 0

  Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 20 Februari 2016 amekutana na kufanya mazungumzo  na Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu yake jijini N'Djamena, Chad. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu wa Chad Mhe. Ahmat Ghazali Acyl na Waziri wa Fedha Mhe. Diguimbaye Christian.
  Ziara hiyo ya Rais Mstaafu nchini Chad ni muendelezo wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu ya kuwafikia viongozi wa nchi 14 za Afrika za kipaumbele katika kutekeleza mapendekezo ya Ripoti ya Kizazi cha Elimu (The Learning Generation).
  Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Deby wamezungumzia janga kubwa linaloinyemelea dunia na hasa nchi za uchumi wa kati na chini ikiwa hakutafanyika mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu. Viongozi hao wamezungumzia haja ya nchi za bara la Afrika kuchukua hatua z amakusudi kufanya maboresho na mageuzi makubwa katika sekta ya elimu katika nchi zao ili kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea. Azma hiyo inatokana na stadi kuwa nchi za uchumi wa kati na chini zko nyuma kielimu kwa miaka 50 hadi 70. Aidha, lipo tishio kuwa ifikapo mwaka 2050, kazi na ajira takribani bilioni 2 zitakuwa zimefutwa kutokana na maendeleo na matumizi ya teknolojia (automation).
  Rais Deby amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete uthabiti wa azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.
  Mbali na mkutano wake na Rais wa Chad, Rais Mstaafu amekutana pia na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake N'Djamena. Rais Mstaafu amempongeza Mhe. Fakhi kwa kuchaguliwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja huo na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya. Viongozi hao wawili wamekuwa pia na mazungumzo yaliyohusu mipango ya Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu barani Afrika na masuala ya hali ya usalama ya Libya.
   Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu ya nchi hiyo  jijini N'Djamena, Chad.
   Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu ya nchi hiyo  jijini N'Djamena, Chad.
   Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena
    Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena
   Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena.

  0 0


  0 0
 • 02/22/17--00:00: UJUMBE KUTOKA IKULU


 • 0 0

  AWAPA SIKU 14, WAFANYA BIASHARA NJE YA SOKO KUHAMIA NDANI YA SOKO

  Na Anthony John Glob Jamii. 
  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameendelea na ziara ya kutembelea Kata za wilaya ya kinondoni, ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkuu wa wilaya ametembelea kata Mzimuni, akiwa katika soko la Magomeni, ametoa siku 14 kwa uongozi wa soko hilo kuhakikisha wanaondoa baa na ghala vilivyopo katikati ya soko hilo.

  Akiwa ndani ya soko hilo, Hapi alisema inasikitisha kuona hata wamiliki wa ghala hizo hawafahamiki.Alisema uwepo wa ghala na baa katikati ya soko hilo inasababisha kuwanyima fursa wafanyabiashara walio wengi hasa wale wadogo.

  "Ninatoa siku 14 kwa viongozi wa soko na manispaa kuhakikisha wanaaondoa maghala haya kwani inaonyesha ni ya wafanyabiashara wakubwa hivyo waende kwa wenzao hapa hapawafai,"alisema Hapi.

  Sambamba na hilo mkuu huyo ametoa siku 14 nyingine kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya soko hilo kurejea ndani ya.soko.Alisema sheria zipo wazi na hakuna aliyejuu ya sheria zaidi ya kuzingatia sheria hizo.

  "Hakuna aliyeruhusu wafanyabiashara wengine kufanya biashara nje ya soko,  hivyo naagiza ndani ya siku 14 wote mhamie ndani kwa sababu mnaleta usumbufu kwa wengine na kuleta malalamiko,"alisema Hapi.

  Baadae mkuu wa wilaya alifanya mkutano wa adhara katika shule msingi Mikumi, katika mkutano huo wananchi waliuliz maswali mbali mbali lakini kero kubwa imeonekana kuwa viongozi wao sio waaminifu hukusanya pesa kwa wananchi lakini hafanyi yaliyokusudiwa, mkuu wa wilaya akijibu hoja hiyo ameagiza viongozi wote kutoa risit za EFD kwa kila malipo yanapofanyika

   MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza na Wananchi mapema leo kwenye muendelezo wa ziara yake jijini Dar
    MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akisikiliza kero mbalimbali za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
  Wanachi wa Mzimu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi 

  0 0

  Wakazi wa mtaa wa NAMANYINGU kata ya MSHANGANO Manispaa ya Songea Mkoani RUVUMA, wamewalazimisha mume na mke kuchimba kaburi la mtoto wao aitwaye DANROAD MAHUNDI mwenye umri wa miaka 36 ambaye inasemekana wazazi wake wamemuua kwa njia za kishirikina,


  0 0

older | 1 | .... | 1580 | 1581 | (Page 1582) | 1583 | 1584 | .... | 3283 | newer