Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1579 | 1580 | (Page 1581) | 1582 | 1583 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Baada ya kukaa kimya kwa miezi mingi bila kuachia wimbo, Hussein Machozi anatarajia kuachia wimbo mpya wiki chache zijazo. Wimbo huo unajulikana kwa jina la ‘Nipe Sikuachi.’
  Wimbo huo umetayarishwa na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa Bongo Flava katika miaka tofauti, Man Walter kupitia studio zake za Combination Sound.

  “Combination ya mimi na Man Walter, sidhani kama kuna kitu cha mchezo hapo,” anasema Machozi ambaye amethibitisha kuanza kufanya kazi rasmi kwa uangalizi wa label ya mtayarishaji huyo mashuhuri nchini Tanzania.

  “Man Walter ni mshkaji kitambo, tumekutana tukakubaliana kufanya kazi na tukaona kabisa kwamba sisi tukifanya kazi wawili itakuwa kazi na ndicho kilichofanyika japo tuna makubaliano ya kusaini. Kwahiyo ni mimi tu nirudi Tanzania tuje tukae tusaini, lakini ukweli ni kwamba mimi nafanya kazi chini ya uongozi wa Kombinega,” amesema.

  “Video pia imefanyika Italy, Gressoney Italy. Kuna mabadiliko makubwa ukiangalia location ambazo tumezizoea, ukiangalia video ambazo kila siku tunaziona Tanzania za magari na majumba,” amesisitiza muimbaji huyo.

  Machozi ambaye anafahamika kwa vibao vingi vilivyowahi kufanya vizuri kwenye vituo vya redio na runinga ndani na nje ya Tanzania vikiwemo ‘Utaipenda’, ‘Kwaajili Yako’, ‘Addicted’ na zingine, amedai kuwa ukimya wake ulitokana na majukumu mengine ya kimaisha.
  “Kama unavyojua, hakuna mtu anapenda kuwa kimya, na ukifuatilia vizuri kuna kazi kadhaa nilishawahi kuziachia lakini hazikufika nilikotarajia nadhani kwasababu ya ukosefu wa management.

  Kwa sasa Hussein anaishi nchini Italia baada ya kuwa ameenda kusoma, lakini hiyo haimaanishi kuwa ameupa kisogo muziki, kitu anachoamini alizaliwa kukifanya.

  “Ilikuwa ni kozi fupi ambayo kwa sasa imeisha na nafanya shughuli za kawaida kujipatia riziki,” anaeleza.
  Machozi anakikisha kuwa ujio wake mpya utakuwa wa tofauti.

  “Kinachokuja kuonekana sasa hivi, hakijawahi kuonekana katika macho ya watu na nimejaribu kufanya hivyo kwasababu mimi mwenyewe nahitaji mabadiliko, nifanye kitu ambacho ni kipya zaidi hata kwenye macho yangu mimi, kwahiyo nimekikubali kwamba  ni kipya, video ni mpya, audio ni mpya kabisa.”

  Anasema tarehe rasmi ya kutoka kwa video na wimbo itatangazwa hivi karibuni. 

  KUFAHAMU ZAIDI KUHUSU HUSSEIN MACHOZI MFUALITIE KWENYE MITANDAO  YA KIJAMII:


  0 0


  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na Makamu wa Rais  wa Kampuni ya Landes SportBund Niedersachsen e.v ya nchini  Ujerumani  Bw.Reinhard Rawe   kuhusu jinsi wanavyoweza kushirikiana katika Sekta ya Maendeleo ya Michezo hapa nchini walipokutana jana Jijini Dar es Salaam.

   Makamu   wa Rais  wa Kampuni ya Landes SportBund Niedersachsen e.v ya nchini  Ujerumani  Bw.Reinhard Rawe  akimueleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kushoto) namna ambavyo kampuni yake inaweza kushririkiana na Wizara katika Sekta ya Maendeleo ya Michezo hapa nchini walipokutana jana Jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (katikati) akiangalia zawadi aliyopewa na Ujumbe wa  Kampuni ya Landes SportBund Niedersachsen e.v ya nchini  Ujerumani baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu maendeleo ya Sekta ya Michezo  hapa nchini yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

   Mjumbe wa Kampuni ya Landes SportBund Niedersachsen e.v ya nchini  Ujerumani Bibi Angie (wa kwanza kulia) akimueleza jambo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye wakati wa mazungumzo baina yao kuhusu maendeleo ya Sekta ya Michezo hapa nchini yaliyofanyika jana Jijjini Dar es Salam.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja  na ujumbe kutoka  Kampuni ya Landes SportBund Niedersachsen e.v ya nchini  Ujerumani baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu maendeleo ya Sekta ya Michezo  hapa nchini yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 02/21/17--01:01: Article 4
 • 0 0

  Na.Vero Ignatus, Monduli.

  Halmashauri ya wilaya ya Monduli imeendelea kuungana na vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi katika kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya .

  Hayo yamebainika katika taarifa iliyosomwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Steven Ulaya kwa mkuu wa mkoa Mrisho Mashaka Gambo, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo katika halmashauri hiyo ambapo taarifa hiyo imesema kuwa Mirungi imekuwa ikiingizwa kutoka nchi ya jirani ya Kenya kupitia mpaka wa Namanga.

  Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa jeshi la polisi lilefanya operesheni maalum na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya madawa hayo,ambapo takwimu za mwaka 2016 hadi januari 2017 kesi za bhangi 11 dhidi ya 8 mwaka 2015 na mirungi ni kesi 12 kwa mwaka 2016 dhidi ya 10

  Aidha ripoti hiyo imeonyesha kuwa halmashauri inaendelea na zoezo la uhakiki wa watumishi hewa limewabaini 24 ambapo kiasi cha shilingi 54,798,300 kilihojiwa kwa watumishi hao,kiasi cha shilingi 32,988,963.19 kilirejeshwa hazina baada ya kuzuia mishahara ilitolewa na baadhi ya watumishi walirejesha fedha hizo walionufaika nazo ambapo makato ya mishahara kiasi cha shilingi 21,809,336.81 yaliyokuwa yanalipwa moja kwa moja na wizara ya fedha ikiwa ni kodi ya mishahara ya watumishi husika na makato ya mifuko ya pensheni tayari mfuko umeandikiwa barua za kurejesha fedha hizo .

  Sambamba na hayo halmashauri hiyo ina jumla ya watumishi 1,867 sawa na asilimia 71.3 ya mahitaji halisi ya watumishi 2,615,ikiwana upungufu wa watumishi 723 katika mchanganuo ufuatao :Idara ya elimu ya msingi walimu 191,elimu ya sekondari (walimu wa sayansi 54)Mmaendeleoa jamii watumishi 18,Utawala (watendaji wa vijiji na kata 20)Kilimo (watumishi 25)Mifungo (watumishi(21)Afya watumishi 391.

  Wilaya ina jumla ya watumishi 295 wa sekta ya Afya ambapo ni sawa na asilimia 43 tu ya mahitaji ya watumishi wote 686,upungufu mkubwa upo katika kada ya Tabibu,wauguzi,wateknolojia ,,mahabara,Dawa na Daktari wasaidizi.

  Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mapato ya halmashauri hiyo kwa mwaka 2016/2017 imekasimia kukusanya jumla ya shilingi 2,457,310,003 kutoka katika mapato ya ndani hadi kufikia januari 2017,halmashauri iliuwa imekusanya jumla ya shilingi 1,120,7147,542.32 sawa na 46% makisio ya mwaka mzima.

  Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Monduli miezi ya hivi karibuni ilipatwa na matukio 4 kuungua moto kwa badhi ya mabweni na shule za sekondari 1.Lowassa Sekondari tarehe 27/01/2016 na 31/7/2016,Nanja Sekondari tarehe 2/8/2016 na Ole Sokoine Sekondari tarehe 11/8/2016 ambapo matukio haya ya moto yalileta athari kubwa kwa jamii ikiwemo baadhi ya wanafunzi kurejeshwa majumbani kwa muda kwa mahitaji ya shule .

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na watumishi katika wilaya ya Monduli ,alipofanya ziara ya kukagua maendeleo katika halmashauri hiyo,aliyeko pembeni yake ni mkuu wa wilaya Monduli Idd Kimanta.
  Mkuu wa mkoa akipokea kadi ya CHF wilaya ya Monduli kutoka kwa mkuu wa wilaya hiyo Idd Kimanta,ili kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo.
  Baadhi ya watumishi katika halmashauri ya wilaya ya momduli wakifuatilia  yaliyokuwa yanaendelea kwa makini.
  Mkutano unaendele wadau pamoja na watumishi wa wa halmashauri hiyo wakifuatilia yale yanayoendelea.Picha na Vero Ignatus Blog

  0 0

  Mfuko wa pensheni wa PPF ulifanya kikao cha Baraza la Wafanyakazi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Katika kikao hicho moja ya mada iliyojadiliwa ni uwekezaji katika kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari katika eneo la Mkulazi mkoani Morogoro ambayo iliwasilishwa na Mkurugenzi wa Muda wa Kampuni ya Mkulazi Holdings Co. Ltd, Nicander Kileo.

  Uwekezaji huo unafanyika chini ya Kampuni ya Mkulazi Holdings Ltd ambayo ni Kampuni Tanzu ya Mfuko wa Pensheni wa PPF na Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Uwekezaji wa kiwanda hiko cha sukari upo katika eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari 63,000 na upo katika hatua za awali ambapo unatarajiwa kuzalisha tani 200,000 za sukari utakapokamilika. Mradi huo utapunguza uhaba wa sukari nchini na kutoa fursa za ajira kwa Watanzania.

  Katika kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi wa PPF Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio alimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mkulazi Holdings Co. Ltd kuelezea mradi wa ubia kati ya PPF na NSSF.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa PPF (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi ambapo katika kikao hicho PPF walimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara kuelezea mradi wa ubia kati ya PPF na NSSF, katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa PPF kilichofanyika mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara akitoa ufafanuzi juu ya uwekezaji katika viwanda cha Mkulazi ambapo aliwapongeza wafanyakazi wa PPF kwa kuupokea mradi huo.
  Kutoka Kushoto, Mkurugenzi Mkuu Wa Mfuko Wa Pensheni Wa PPF Ndg. William Erio, Mkurugenzi wa Muda wa Kampuni ya Mkulazi Holdings Co. Ltd. Ndg. Nicander Kileo ambayo ni Kampuni Tanzu ya Mfuko wa PPF na NSSF na Mkurugenzi Wa Shirika la Taifa Wa Hifadhi Ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara wakijadiliana wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa PPF mwishoni mwa wiki.

  0 0  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Bashnet wilayani Mbulu wakati aliposimama kijijini hapo akitoka Mbulu kwenda Hanang Februari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Mwakilishi wa Dar es Salaam kutoka Benki ya Exim ya Korea Bw. Lee Hyonjong (wa pili kushoto), ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Mwakilishi wa Dar es Salaam kutoka Benki ya Exim ya Korea Bw. Lee Hyonjong, kuhusu uwekezaji wa miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo, ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.
  Moja ya mradi uliokuwa ukijadili na ugeni kutoka Mwakilishi wa Dar es Salaam kutoka Benki ya Exim ya Korea Bw. Lee Hyonjong na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa leo, jijini Dar es Salaam.


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Na Ismail Ngayonga .

  MAAFISA Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri nchini wametakiwa kutumia njia za haraka na za kisasa katika mawasiliano ikiwemo matumizi ya tovuti na mitandao ya kijamii ili kutangaza shughuli na mafanikio ya sera na mipango ya Serikali kwa wananchi.

  Hayo yamesemwa jana Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas wakati wa uzinduzi wa tovuti za halmashauri 35 za mikoa 5 ya kanda ya ziwa inayojumuisha Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga na Simiyu.

  Dkt. Abbas alisema pamoja na kuwepo kwa vyombo mbalimbali vya habari vinavyotumika kufikisha taarifa za habari kwa wananchi ikiwemo magazeti na redio, bado mitandao mitandao ya kijamii ikiwemo barua pepe imendelea kutumia na wananchi wengi zaidi ulimwenguni kwa sasa. 

  “Kwa sasa nusu ya watu duniani wapo mtandaoni na hapa nchini kwa mujibu wa ripoti ya TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Nchini) inaonyesha kuwa Watanzania zaidi ya Milioni 19 wapo mtandaoni aidha kwa kutumia barua pepe au kutembelea kurasa za facebook” alisema Dkt. Abbas.

  Kwa mujibu wa Dkt. Abbas alisema sifa za Afisa Habari na Mawasiliano wa karne ya sasa ni mwenye uwezo wa kutumia njia za kisasa za mawasiliano, ambazo zitamwezesha kujibu hoja mbalimbali kwa haraka zaidi badala ya kusubiri Serikali kulalamikiwa na wananchi.

  Aidha Dkt. Abbas alisema uzinduzi wa tovuti katika mikoa na halmshauri hizo ni kigezo muhimu kitakachotumiwa na Serikali katika kupima wa utendaji kazi wa Maafisa Habari katika kushughulikia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

  Akifafanua zaidi Dkt. Abbas alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa tovuti za mikoa na halmashauri za Wilaya nchini zinaendelea kuwa hai na zenye taarifa zilizozingatia muda na wakati na hilo litawezekana iwapo Maafisa Habari watatimiza malengo wanayopaswa kujiwekea katika maeneo yao ya kazi.
   Mkurugenzi wa Habari na  Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza na Maafisa Habari na Tehama wakati wa Mafunzo elekezi ya matumizi ya tovuti kutoka Mikoa 5 na Halmashauri 35 za Mikoa ya Kanda ya Ziwa  yaliyofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekaani (USAID) na kusimamiwa na Ofisi ya      Rais- TAMISEMI,  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA). Mafunzo hayo yalianza tarehe 9-20 Februari, 2017, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Rebecca Kwandu. 

  0 0

  Hatimaye baraza la Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limepitisha na kulitambua rasmi eneo lililopo kata ya Igowole kuwa ndipo zitakapojengwa Ofisi za makao makuu ya halmshauri hiyo hivyo, kuruhusu kuanza kwa ujenzi wa mradi wa kwanza wa hospitali ya halmshauri ya Wilaya katika eneo teule.

  Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Ofisa habari na mawasilino wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ndimmyake  Mwakapiso, amesema baraza hilo limefanya uamuzi huo wa  kihistoria wakati wa kikao cha baraza maalum lililoitishwa kwa mujibu wa kanuni  kwa agenda maalum ya kuridhia mapendekezo ya kamati teule ya wataalamu iliyopendekeza maeneo katika   vijiji vya Ibatu na Nzivi vilivyopo kata ya Igowole.

  Ofisa habari huyo, ametaja baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa wakati wa kulipitisha eneo hilo, kuwa ni pamoja na utayari wa wananchi na halmshauri za vijiji kulitoa eneo bure bila kudai fidia, Eneo kuwa ubali wa km 13 kutoka barabara kuu, eneo  kupendekezwa kwa asilimia 29 wakati wa mchakato wa kusaka maoni katika kata 27 za halmshauri, likifuatiwa na Nyololo kwa asilimia 25 sanjari na Ukubwa wa eneo lenyewe likiwa na ekali 127.

  Uamuzi huo umefikiwa ikiwa ni takribani mwaka mmoja baada ya kuzaliwa kwa halmshauri mpya ya Mji wa Mafinga ambao kwa sasa ndiyo wenye mamlaka kamili ya kuuendesha mji huo. Aidha, uongozi wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi umewashukuru wenyeviti wa kamati za kata na wanamufindi kwa ujumla wao kwa ushirikiano waliounesha wakati wa  kupendekeza eneo la ujenzi wa  makao makuu ya halmshauri.
   Mkurugenzi wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa eneo la ujenzi wa makao makuu.
  Mwenyekiti wa kamati  iliyokuwa imeundwa kwa ajili ya kutafuta eneo la ujenzi Bw. Ubisimbali Jeswald akiwasilisha kazi yao kwa baraza la Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
  Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindiwakimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa kamati wakati anawasilisha kazi walioifanya na kamati hiyo.


  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo amezindua Mafunzo ya  namna ya Kutengeneneza Taa na Chaja zinazotumia mwanga wa jua kwa vijana 20  katika Kata ya Nyegina Mkoa wa Mara.

  Akifungua mafuzo hayo Profesa Muhongo amewataka vijana hao kuwa mabalozi wazuri wakati wanapohudhuria mafunzo na kueleza kuwa, yatakuwa chachu katika kupanua wigo wa  wa ajira ikiwemo wahitimu kujiari wenyewe.  Profesa Muhongo amewataka vijana na wananchi mkoani humo kuweka nguvu kubwa katika elimu kutokana na umuhimu  na mchango wake kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.  Akizungumzia kuhusu Mradi wa Usambazaji Vijijini Awamu ya Tatu, Profesa Muhongo ameeleza kuwa, awamu hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa, mradi huo utafanywa kwa Awamu na kusisitisza kuwa, adhma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa, ndani ya kipindi cha miaka mitano vijiji vyote nchini viwe vimeunganishwa na nishati hiyo.  " Vijiji vyote vitaunganishwa na nishati ya umeme. Tutasambaza  awamu kwa awamu na lengo letu ni kuhakikisha kuwa, vijiji vyote chini vinaunganishwa na umeme ndani ya kipindi cha miaka mitano. Wale ambao hawajafikiwa awamu ya kwanza na ya pili tutawafikia awamu ya tatu vivyo hivyo mpaka tufikie lengo letu," amesisitiza Prof. Muhongo.  Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung ambaye nchi yake imefadhili mafunzo hayo, amesema kuwa,  uwepo wa taa hizo utasaidia upungufu wa umeme hususan maeneo ya vijijini na ambayo bado hayajaunganishwa na nishati hiyo.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akionesha mfano wa Taa zinazotumia mionzi ya jua ambazo vijana 20 katika Kata ya Nyegina watafundishwa namna ya kuzitengeneza baada ya kuzindua mafunzo hayo. Kulia ni Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi.
   Mkufunzi wa mafunzo ya kutengeneza Taa na Chaja zinazotumia mionzi ya jua, Dkt. Dkt. Hong- Kyu Choi, akiwaleza washiriki wa mafunzo namna mafunzo hayo yatakavyoendeshwa.
   Mkuu wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Dkt. Vicent Naano, (wa tatu kushoto) akiongea jambo mara baada ya uzinduzi wa mafunzo ya Kutengeneza taa na chaja zinazotumia mionzi ya jua. Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muongo (katikati), Balozi wa Korea Kusini nchini,Song Geumyoung   Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi (wa pili kulia) na baadhi ya wawakilishi wa vijana wanaoshiriki mafunzo.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akiweka tofali katika moja ya vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika Shule ya Msingi Kata ya Bwasi, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo. Wengine ni Viongozi wa Vijiji, Halmashauri na wananchi wa Kijiji cha Kome.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Shirika la ndege Tanzania ATCL linatarajia kutoa huduma za usafiri wa anga kutoko Dar Es salaam kuja Songea mkoani Ruvuma.Bonyeza play kupata undani wa habari hii.


  0 0

  Na Georgina Misama – MAELEZO.

  Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limejipanga kumaliza kero ya makazi ya nyumba kwa watanzania ifikapo mwaka 2025.

  Hayo yamesemwa na Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) Bw. Erasto Chilambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

  Ili kutimiza azma hiyo,Chilambo alibainisha kuwa nyumba zisizopungua elfu 30 zitajengwa kwa ajili ya kuuzwa na kupangishwa ambapo katika nyumba hizo watu wa kipato cha chini, kati na juu ndio walengwa.

  “Katika mkakati huu, Shirika limekusudia kujenga nyumba 12000 kwa ajili ya watu wa kipato cha chini, nyumba 13500 kwa ajili ya watu wenye kipato cha kati na nyumba 2700 kwa ajili ya watu wenye kipato cha juu.” Alisema Chilambo.

  Aidha, Shirika linajenga majengo 1800 ya kibiashara katika maeneo mbalimbali nchini, ambayo yanatazamiwa kukamilika ifikapo 2025.

  “Katika kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhamia Dodoma, shirika linajenga nyumba za makazi 300 zitakazouzwa kwa watumishi wa Serikali, ambazo zina ukubwa tofauti zenye vyumba 3 kila moja.” Alisema Bwn.Charahani.

  Tangu kuanzishwa kwake Shirik la Nyumba limekuwa likimiliki na kuuza majengo mbalimbali. Hivi sasa shirika linamiliki MAJENGO 2483 yenye sehemu 18121 za makazi na biashara katika Mikoa ya Tanzania Bara.
  Meneja Mauzo wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Bw. Erasto Chilambo akizungumza na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mkakati wa shirika hilo kujenga nyumba 300 zitakazouzwa kwa watumishi wa umma Mkoani Dodoma ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa makazi kwa watumishi wanaohamia Mkoani humo na kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamia mkoani humo.kushoto ni Afisa Habari wa Shirika hilo Bi Edith Nguruwe.

  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa NHC leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye amekutana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala aliemtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujifunza na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.

  Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa.

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ametembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la ushirika - mnazi mmoja jijini Dar es salaam, mapema leo asubuhi na alipata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kuwa na mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo. “Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt Anna Makakala.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mapema leo asubuhi (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyekaa katikati mbele akiwatambulisha Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala na kumueleza ni jinsi gani Jeshi la Zimamoto linavyoendesha shughuli zake.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akimkabidhi zawadi ya bendera ndogo ya mezani Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ikiwa ni ishara ya umoja, ushirikiano na ukumbusho juu ya ziara yake alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jengo la ushirika – mnazi mmoja mapema leo asubuhi.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) mapema leo asubuhi alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala na Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto mapema leo asubuhi. (PICHA NA FC GODFREY PETER)

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya filamu (hawapo pichani) wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitolea ufafanuzi maoni yaliyotolewa wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wadau wa sekta ya filamu wakisikiliza hoja zilizokua zikiendelea kutolewa wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa jiji.

  Tatizo la wimbo wa Taifa na dua katika mkutano wa baraza la madiwani wa mkoa wa jiji la Dar es Salaam umeweza kuzua mjadala kwa zaidi ya dakika kumi katikati ya mkutano huo.

  Mjadala huo ambao uliibuliwa na mtoa hoja, Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ambaye alitoa hoja ya kukiukwa kwa kanuni za uendeshwaji wa baraza hilo.
    
  Mara baada ya kutoa hoja mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam,Sipora Liana alimuomba mwanasheria wa halmashauri kutoa ufafanuzi juu ya swala hili na kusema kuwa hakuna kitu kilichoharibika jambo ambalo lilipingwa vikali na madiwani wote.

  Mara baada ya madiwani kumpinga mwanasheria huyo na Mstahiki meya waliamuliwa na madiwani hao kurudia kuimba wimbo wa taifa kisha kufuatiwa na dua jambo ambalo liliridhia kuanza kwa mkutano huo bila mgogoro.

  Hoja nyingine aliyoibua kubenea ilikuwa ni kitendo cha kuanzishwa kwa mkutano huo bila ya akidi kutimia na kumlazimu kurudia tena kuhesabu watu ili kujiridhisha kuwa akidi imetimia.

  Hata hivyo dakika chache baadae mkutano ulivyoanza ulikuwa kwa majibizano ya hoja mbalimbali ikiwemo juu ya namna uwasilishaji wa taarifa hiyo.

  Hata hivyo baraza hilo lilimalizika kwa Meya wa jiji Isaya Mwita kuairisha mkutano mpaka kesho.
   Mbunge wa Ubungo na Diwani wa Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam , Saed kubenea akizungumza wakati wa kikao cha baraza
   Diwani wa kata ya Kibonde Maji , Abdalah Mtinika akitoa hoja katika kikao cha baraza la Madiwani kilichafanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
  Mayor wa Halmashauri wa Manispaa ya Temeke, Abdalah Chaurembo akitoa hoja katika kikao cha baraza la Madiwani wa jiji la Dar es Salaam
  Madiwani wakiwa katika kikao baraza la Madiwani wa jiji la Dar es Salaam katika ukumbi wa Karimjee.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Katesh wilayani Hanang, Mkoani Manyara leo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifanya uzinduzi wa madarasa ya shule ya Msingi ya Mogitu Wilayani Hanang Mkoani Manyara leo, wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoa wa Manyara. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa Hanang Mkoani Manyara baada ya kuzindua madarasa ya shule ya Msingi ya Mogitu.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ngoma ya asili.

  0 0


  SGT Weston Paul Ngaponda akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati akijibu maswali yaliyoulizwa na Bw. Fadhiri Aticki Mr Pengo kutoka Michuzi Blog na Michuzi Tv.

  Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Mbeya limetoa Takwimu ya Ajali za Moto zilizotokea ndani ya miaka 6 kuanzia 2011 mpaka 2016.
  Akizungumza na waandishi wa habari Sajenti Weston Paul Ngaponda kwa niaba ya Mkuu wa Operesheni Zimamoto Mkoa wa Mbeya amesema Jeshi la Zimamoto na Uokozi Mkoani Mbeya linafanya majukumu yake kwa weredi mkubwa na kwa mafanikio makubwa.


  SGT Ngaponda ametoa Takwimu za Ajali za moto kwa muda wa miaka sita na zipo kama ifuatavyo:-
  1.Mwaka 2011,Matukio ya Moto yalikuwa  jumla 54 kwa wastani wa Matukio matano kwa mwezi.
  2. Mwaka 2012, kwa mwaka mzima matukio yalikuwa jumla 88, kwa wastani wa matukio 7 kila mwezi.
  3. Mwaka 2013, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 50, kwa wastani wa matukio manne kila mwezi.
  4. Mwaka 2014, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 52, kwa wastani wa matukio manne kila mwezi.
  5. Mwaka 2015, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 74, kwa wastani wa matukio 6 kila mwezi.
  6. Mwaka 2016, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 65, wastani wa matukio matano kila mwezi.
  SGT Ngaponda akiongea na wanaHabari amesema kwa tathmini zao ni kwamba matukio ya ajali za moto yanazidi kupungua Mkoani Mbeya huku akiwasifu wananchi kwa ushirikiano wanaowaonyesha pindi majanga ya moto yatokeapo. Aidha,SGT Ngaponda amesema Jeshi la Zimamoto limekuwa likitoa elimu kuhusu majanga ya moto pindi litokeapo tatizo sehemu ili kusaidia kupunguza hatari hizi kwa siku za usoni. Pia amesema vyanzo vya moto daima husababishwa na binadamu kwa mitazamo tofauti, inaweza kuwa kwa Ujinga, Uzembe na Uhujumu.
  Akitolea maelezo jinsi ya kuepuka majanga ya moto amesema, kwa wale wazembe basi Umakini unahitajika sana pindi watumiapo vitu vinavyoweza kusababisha moto kama mishumaa, taa ya kandiri, matumizi ya umeme na kwa upande wa Ujinga Elimu pekee inaweza kusaidia kuifanya jamii kuwa salama zaidi. SGT Ngaponda amewaomba wananchi wa Mkoa wa Mbeya kujitahidi kutoa taarifa mapema majanga yatokeapo bila kuchelewa kwani wapo wananchi ambao huchelewa kutoa taarifa.
  Akihitimisha Taarifa hiyo ametoa wito kwa wananchi hasa waiishio Mbozi kwani wamekuwa na tabia ya udanganyifu kwa kuwapigia simu Jeshi la Zimamoto kuwa kuna janga la Moto kumbe sio kweli na baadhi ya wananchi kuzitumia namba za Zimamoto kwa matumizi yasiyostahiki.
   Wanahabari wakimsikiliza kwa makini SGT Ngaponda wakati akitoa Ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Jeshi la Zimamoto
  MAELEZO NA: THOBIAS OMEGA
  PICHA NA: MR PENGO MMG...

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhiwa hekali 1500 na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate Mohamed Iqbal kwa ajili ya viwanda vidogo.

  Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo  eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni Mkurugenzi huyo amesema wameamua kumkabidhi eneo hilo RC Makonda kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuijenga Tanzania ya viwanda ili kuwakomboa wananchi wenye uchumi wa kati.

  Kwa upande wake RC Makonda ameeleza kuwa dhamira ya viwanda ya Rais Magufuli inabidi itafsiriwe kwa vitendo, hivyo eneo hilo litatumika kwa ajili ya ufugaji, kilimo, usindikaji, utengenezaji wa sabuni na eneo hilo litatumika na wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

  Pia RC  Makonda ameongeza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unajengwa na wana Dar es Salaam wenyewe hivyo kama kuna watu wanataka kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya Dar es Salaam wafanye hivyo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul  Makonda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makabidhiano hayo  eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul  Makonda akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul  Makonda akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa wakiangalia ramani ya eneo hilo, leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda  (watatu kutoka kulia)  akiwa amefuatana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate,Mohamed Iqbal    wakikagua eneo hilo
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa,
  Muomoneke wa  eneo hilo alilokabidhiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii. 

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz P. Mlima, akifungua Mkutano cha Makatibu Wakuu nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Kamati Ndogo ya Mawaziri ya Siasa na Diplomasia ya SADC (Inter State Politics and Diplomacy Sub Committee-ISPDC) unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 na 24 Februari, 2017. Mkutano wa Makatibu Wakuu unafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
  Sehemu ya wajumbe wa Mkutano kutoka katika mataifa ya nchi wanachama wakifuatilia mkutano. 
  Kaimu Mkuu wa Mabalozi Mhe. Balozi Edzai Chimonyo (wa kwanza kushoto) na wajumbe wengine wakifuatilia mkutano.
  Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Tax (wa pili kushoto) na wa kwanza kulia ni Balozi Simba Yahya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia mkutano. 
  Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia Mkutano. 

older | 1 | .... | 1579 | 1580 | (Page 1581) | 1582 | 1583 | .... | 3284 | newer