Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1416 | 1417 | (Page 1418) | 1419 | 1420 | .... | 3284 | newer

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia Oktoba mwaka huu, Serikali imekwishapeleka zaidi ya sh. bilioni 177 kwenye halmashauri mbalimbali nchini ili kutekeleza miradi ya maendeleo.

  Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 3, 2016) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Bibi Munde Tambwe aliyetaka kupata kauli ya Serikali kuhusu ucheleweshwaji wa fedha za bajeti ya maendeleo katika halmashauri mbalimbali nchini.

  “Kwa kuwa Serikali ina mifumo, miongozo, sheria na taratibu za kupeleka fedha kwenye halmashauri mara baada ya kikao cha bajeti. Mheshimiwa Waziri Mkuu unatoa kauli gani kuhusu ucheleweshwaji wa fedha hizo katika halmashauri nchini zikiwemo za mkoa wa Tabora? Alihoji Mheshimiwa Munde.

  Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu amesema: “Baada ya Bunge kuridhia na kutoa mamlaka ya matumizi ya fedha, Serikali ilianza kujiridhisha uwepo wa mfumo sahihi ya makusanyo na mapato na matumizi yake. Ni kweli kwamba Serikali yetu baada ya kikao cha bajeti inawajibika kutekeleza maamuzi ya Bunge kwa kupeleka fedha zilizopangwa.”

  Waziri Mkuu amesema Serikali ilianza kupeleka watumishi watakaosimamia ukusanyaji mapato katika halmashauri zote nchini. Kutathmini miradi yote iliyoanza ambayo haijaendelezwa pamoja na mipya ili kutambua thamani na kisha kupeleka fedha.

  Amesema Serikali itaendelea na upelekaji wa fedha kwenye halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Amezisisitiza halmashauri hizo kuendelea kukusanya mapato ndani ili kuongezea bajeti kwa fedha wanazopelekewa na watumie mfumo wa kielektroniki ili kudhibiti mapato hayo.

  Aidha, Waziri Mkuu amezitaka halmashauri zote nchini zihakikishe fedha zinazopelekwa katika maeneo yao zinatumika kama ilivyokusudiwa kwa miradi husuka. Amewasihi Wabunge wafuatilie na wasimamie matumizi ya fedha hizo ili miradi iliyopangwa iweze kukamilika.

  Wakati huo huo; Waziri Mkuu amesema Serikali haijafilisika na kuhusu suala la mfuko wa jimbo bado unatambulika na fedha zitapelekwa kwenye majimbo na wabunge watajulishwa kiasi kilichopelekwa ili waweze kuratibu miradi yao ya maedndeleo.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Ukonga Mheshimiwa Mwita Waitara aliyetaka kupatiwa kauli ya Serikali kuhusu kutopelekwa kwa fedha za mfuko wa jimbo.

  Pia Mheshimiwa Waitara alilalamikia kitendo cha jimbo lake kutengewa fedha kidogo katika mgawo wa mfuko wa jimbo ambazo ni sh. milioni 16 licha ya kuwa na wananchi wengi huku jimbo la Segerea alilosemma lina watu wachache likitengewa sh. milioni 33. Ameiomba Serikali ingalie upya ugawaji huo kulingana na mazingira ya jimbo husika.

  Waziri Mkuu amesema kumejitokeza matatizo kwenye halmashauri zenye majimbo zaidi ya moja na Serikali inaendelea kufanya sensa kutambua idadi ya wananchi kwenye majimbo hayo ili itakapopeleka fedha iweze kuzingatia idadi hiyo na kuwawezesha wabunge kupanga miradi ya maendeleo.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  ALHAMISI, OKTOBA 3, 2016.

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho, Dodoma.

  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wamefanikiwa kuhamasisha baadhi ya wawekezaji kuwekeza katika sekta ya dawa za binadamu na vifaa tiba ili kupunguza uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi.

  Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la Mhe. Khadija Ali (Viti Maalum) aliyehitaji kufahamu mpango wa Serikali wa kutumia malighafi zilizopo kuzalisha baadhi ya dawa na vifaa tiba.

  Waziri Mwijage amesema kuwa Serikali inaendelea na Mkakati Unganishi wa Maendeleo ya Viwanda (IIDS) pamoja na Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Miaka Mitano ambayo yote inalenga kuondoa changamoto ya kununua dawa na vifaa tiba kutoka nje ya nchi.

  “Serikali kupitia mashirika yake ya MSD, TIRDO, NHIF, TIB na TFDA wamepewa jukumu la kuandaa mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya dawa za binadamu pamoja na vifaa tiba kwa hiyo kupitia wizara yangu na TIC tayari tumefanikiwa kuwahamasisha wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani”, alisema Mwijage.

  Baadhi ya wawekezaji hao ni JSN Solution ambao watajenga kiwanda cha kuzalisha IV Fluid, China Dalian International Economic Development Group Co. Ltd ambao watajenga kiwanda cha kutengeneza vifaa tiba, Zinga Pharmaceuticals Ltd pamoja na Hainan Hualon ambao watatengeneza madawa mbalimbali ya binadamu.

  Waziri Mwijage amesema kuwa kupitia Ubalozi wa Korea nchini, Kampuni ya Boryung Pharmaceuticals Co. Ltd itatengeneza madawa ya Penicilin Orals Solids Antibiotics, wakati Agakhan Foundation Network watazalisha dawa mbalimbali.

  Waziri Mwijage ameongeza kuwa kujengwa kwa viwanda vya dawa za binadamu na vifaa tiba kutakuwa na fursa pana ya kuwahakikishia Watanzania nafasi za ajira kwa vijana nchini kipindi kifupi kijacho.

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akijibu swali leo Bungeni mjini Dodoma 

  0 0


  Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungunguza na wabunge wa Bunge hilo, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ili umsalimia na kupata mawazo kutokana na uzoefu wake hasa alipokuwa Spika wa Bunge hilo la Afrika Mashariki. Wa Kwanza kulia upande wa mstari wa kushoto, ni Mwenyekiti wa Wabunge hao, Makongoro Nyerere, Shayrose Bhaji, Yves Nsabimana, Maryam Ussi, Twaha Tasilima, Wilime Asheri ambaye ni mratibu EALA, na kutoka kulia, mstari wa kulia ni, Katibu wa NEC Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib, na Wabunge wa EALA, Adam Kimbisa, Bernard Murunya, Abdulla Mwinyi,Angela Kizigha na mwisho Msemaji wa CCM, Christopher Sendeka..
  Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib (kulia), akiwa na Wabunge wa Bunge la Afika Mashariki, Adam Kimbisa, Bernard Murunya, na Abdulla Mwinyi, wakati wakimsubiri Kinana kuingia ukumbini
  ukumbini
  Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzungunguza na wabunge wa Bunge hilo, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ili umsalimia na kupata mawazo kutokana na uzoefu wake hasa alipokuwa Spika wa Bunge hilo la Afrika Mashariki.


  0 0

  MSHAMBULIAJI kinda mwenye asili ya kitanzania anayekipiga nchini Kenya ameweka wazi msimamo wake wa kutamani kucheza ligi ya Tanzania hasa baada ya mkataba wake kumalizika na timu ya Agro Chemical iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la Kwanza ijulikanayo kama National Super League.

  Akizungumza na mtandao wa Michuzi Globu, kinda huyo kutoka zao la Copa Coca Cola Jerome Nturukindo amesema kuwa mkataba wake umeisha na anachokitamani kwa sasa ni kuja kucheza ligi ya nyumbani kwani anajua ni moja ya ligi yenye ushindani sana Afrika Mashariki na Kati.

  Nturukindo amesema kuwa, toka alivyoondoka nchini mwaka 2013 akitokea timu ya vijana ya chini ya miaka 20 African Lyon ambapo walimchukua kutoka mashindano ya Copa Colachini ya miaka 17 kutoka timu ya Temeke na tayari amechezea timu ya St Joseph na Agro Chemical za nchini humo.

  Kutokana na mapenzi yake makubwa ya mpira na kutaka kuisaidia timu yake katika Nturukindo amesema kuwa kwa sasa anarejea nchini rasmi na yupo tayari kufanya mazungumzo na timu yoyote itakayohitaji huduma yake kwani yeye mpira ndio kazi.

  Mwaka jana alifanikiwa kwenda kwenye majaribio nchini Serbia na alifanya vizuri na wakamuahidi kuwa katika dirisha dogo la mwezi Januari watamuita ila akaona kimya na hawakumpa taarifa yoyote mpaka mda huu.

  Katika msimu wa 2015/2016 Nturukindo ameweza kuifungia timu yake goli 16 kati ya mechi 25 na ligi inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Novemba na itakapomalizika tu anarejea Tanzania kuja kutafuta timu.


  0 0

  Na Theresia Mwami TEMESA Mtwara.

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu amesema kuwa hajaridhishwa na ukusanyaji wa mapato na madeni katika kituo cha Mtwara katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo karakana imekusanya asilimia 20% tu ya kiasi cha pesa ilichozalisha.

  Dkt Mgwatu amesema kuwa hatovumilia uzembe wowote utakaojitokeza katika suala la ukusanyaji wa mapato na madeni katika vituo vyote vya TEMESA nchini.“Hatuwezi kuendesha vituo na karakana zetu kwa mwendo huu hivyo inatupasa kuongeza juhudi katika kufuatilia madeni” alisema Dkt. Mgwatu.

  Kwa upande wake Meneja wa TEMESA Mtwara Mhandisi Said Mongomongo amesema kuwa kuna changamoto za Taasisi nyingi kutolipa kwa wakati gharama za matengenezo ya magari na mashine mbalimbali katika karakana yake.Mhandisi Mongomongo amewataja baadhi ya wadaiwa sugu kuwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Ofisi ya Katibu Tawala mkoani Mtwara.

  Akiwa mkoani Mtwara, Dkt Mgwatu ametembelea Kivuko cha MV. Mafanikio kinachotoa huduma ya usafiri kati ya Msangamkuu na Msemo pamoja na Kivuko cha MV. Kilambo kinachotoa huduma kati ya Kilambo (upande wa Tanzania) na Namoto (upande wa Msumbiji).

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara kuangalia utendaji kazi wa vituo hivyo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kushoto) akiongea na Meneja wa TEMESA Mtwara Mhandisi Said Mongomongo alipotembelea ofisi hiyo, ili kujionea hali halisi ya kituo hicho pamoja na utendaji kazi wake.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kulia) akisikiliza malalamiko ya abiria wa MV. Mafanikioalifanya ziara Mkoani Mtwara.
  Kivuko cha MV. Kilambo kinachotoa huduma ya uvushaji katika Mto Ruvuma, unaozitenganisha nchi za Msumbiji na Tanzania katika eneo la KIlambo (TANZANIA) na Namoto (Msumbiji). . Kivuko hiki kinasimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme ( TEMESA) Dkt Mussa Mgwatu akikagua kitabu kinachoonyesha taarifa za safari zinazofanywa na kivuko pamoja na hali ya kivuko kinapokuwa safarini.Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Mtwara.

  0 0

  Serikali ya Tanzania imeishukuru Jamhuri ya watu wa China kwa ushirikiano katika maeneo mbalimbali yanayolenga kuleta ustawi kijamii na kukuza uchumi.Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru ametoa shukrani hizo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ofisi ya masuala ya biashara na uchumi ya jimbo la Jiangsu la nchini China hapa nchini.

  Mbali na kuushukuru uongozi wa jimbo la Jiangsu kwa hatua hiyo, Dr. Meru alisema hatua hiyo ni muhimu katika kuinua uchumi wa viwanda na kusimamia mpango wa uwekezaji wa viwanda kutoka jimbo hilo la China kuja Tanzania.“Tunatambua kuwa jimbo la Jiangsu limeendelea sana kiviwanda, hivyo kufunguliwa kwa ofisi hii kutasaidia sana katika kuhamasisha maendeleo ya viwanda hapa nchini,” alisema Dkt. Meru ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

  China ni moja ya wadau wakubwa wa maendeleo wa Tanzania katika masuala ya biashara na uwekezaji.Akizungumza wakati wa tukio hilo, Kamishna wa Biashara wa Jimbo la Jiangsu, Bw. Zhao Jin alisema ofisi hiyo ni ya 17 duniani na ya pili kwa bara la Afrika.Ofisi hiyo imefunguliwa kwa ushirikiano kati ya idara ya biashara ya jimbo la Jiangsu, manispaa ya Changzhou na Jiangsu Overseas Group Corporation.Manispaa ya Changzhou ndiyo inayomiliki asilimia 51 ya kiwanda cha nguo cha urafiki, China Friendship Textile.

  “Kiwanda cha Urafiki na reli ya TAZARA ni alama za urafiki wa enzi kati ya Tanzania na China,” alisema Katibu wa Chama cha Kikomunisti katika jimbo la Changzhou, Bw. Yan Li.Eneo jipya la viwanda lijulikanalo kama "Jiangsu-Shinyanga Agricultural Industrial Zone” lililowekezwa na Jiangsu Overseas Group Corporation hapa nchini ndio uwekezaji mkubwa unaotaka kutekelezwa na jimbo la Jiangsu hapa nchini.Uwekezaji katika eneo hilo utafikia Dola za Kimarekani milioni 200.

  Ofisi ya biashara na uchumi ya Jiangsu hapa Tanzania itashughulika pamoja na mambo mengine, kuimarisha hadhi ya jimbo hilo hapa nchini; kuhamasisha uwekezaji wa viwanda na kuimarisha njia za biashara kati ya nchi hizo mbili.Pia, ofisi hiyo itashirikiana na ubalozi wa China hapa nchini kufanya tafiti za ushirikiano zaidi katika maeneo ya uchumi na biashara.

  Tukio hilo lilishuhudiwa na Bw. Yan Li, Muwakilishi wa masuala ya Uchumi na Biashara wa China hapa Tanzania, Bw. Lin Zhiyong na Mwenyekiti wa CCM mkoani Singida, Bi. Martha Mlata.
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Dkt.Adelhelm Meru (katikati)akipiga makofi muda mfupi)) baada ya kuzindua Ofisi ya uwakilishi wa biashara na Uchumi wa Jimbo la Jiangsu la China hapa nchini (Dar es Salaam) juzi. Wengine ni wakilishi wa jimbo hilo.

  0 0
  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe amezindua Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) jijini Dar es Salaam
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe akielezea majukumu ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) kwenye uzinduzi huo.

   Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wakisikiliza Hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (hayupo pichani).

  Kutoka kushoto Kaimu Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Ally Samaje, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania. (TMAA), Mhandisi Dominic Rwekaza pamoja na Watendaji wengine kutoka Wakala huo, wakisikiliza maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (hayupo pichani).

   Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Charles Sabuni akieleza jambo katika uzinduzi huo.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (kulia) akimkabidhi mwongozo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Charles Sabuni (kushoto) mara baada ya kuzindua Bodi hiyo.


  0 0

  East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, November 3rd, 2016: Preparations are in high gear at the East African Community Secretariat for it to effectively take part in the 22nd Session of the Conference of Parties (COP22) to the United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC) and the 12th Meeting of Parties to Kyoto Protocol (CMP12) to be held from 7th to 18th November, 2016 in Marrakech, Morocco.   

  The first session of the Conference of the Parties serving as the Meeting of the Parties to the Paris Agreement (CMA1) will also take place in Marrakech in conjunction with COP 22 and CMP 12. The main purpose of these sessions is to review the progress in the implementation of decisions and directives of COP 21/CMP11 and agree the way forward on the implementation of the Paris Agreement.

  The EAC delegation will be lead by the Deputy Secretary General in charge of Finance and Administration, formerly of Productive and Social Sectors, Hon. Jesca Eriyo.

  As part of the preparations for the COP22/CMP12, the EAC Secretariat with support from US Government, undertook national climate change consultative meetings from 12th September to 4th October, 2016 in all Partner States seeking to identify national climate change priorities with a view to developing the common regional position to guide negotiations during the COP22/CMP12 and CMA1 sessions. Furthermore, the national consultations aligned countries’ road map for implementation of the Paris Agreement to the roadmap proposed by the EAC Secretariat.


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0
  0 0


  0 0

   Are you in Dar ? Do you want a car to hire for town trips only in Dar es salaam ? I have a Toyota Corolla x model (Corolla Police) in good condition for as cheap as 25,000/= per day. Full AC,GPS monitored ,paid all goverment certificates and all car traffic requirements. PLEASE CALL ME ON 0766 112445/0712 627848


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Novemba, 2016 amekutana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird na kuzungumzia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania yenye thamani ya jumla ya Dola za Marekani Bilioni 1.6 zikiwa ni mkopo kutoka benki hiyo.

  Akizungumza baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Magufuli, Bi. Bella Bird amesema mikopo hiyo inalenga kusaidia juhudi za maendeleo nchini Tanzania na itatolewa katika sekta mbalimbali zikiwemo nishati, usafirishaji, elimu na maji.

  "Miradi hii yote imelenga zaidi kuharakisha maendeleo na kuleta matokeo katika maisha ya Watanzania, ni miradi ambayo inahitaji uongozi na msukumo mzuri kutoka Serikalini na tunafurahi kwamba Rais Magufuli ni kiongozi ambaye ana dhamira ya dhati ya kusimamia maendeleo" amesema Bi. Bella Bird.

  Kwa upande wake Rais Magufuli ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo na ametoa wito kwa Benki hiyo kuharakisha utoaji wa mikopo kwa ajili ya kutekeleza miradi.

  "Tunataka kuona mambo yanatokea badala ya kutumia muda mwingi kuzungumza, miradi hii ina manufaa makubwa kwa watanzania na tungependa utekelezaji wake ufanyike haraka, na ili ufanyike haraka Benki ya Dunia inapaswa kutupatia mikopo kwa wakati unaofaa" amesisitiza Rais Magufuli.

  Aidha, Rais Magufuli amemhakikishia Bi. Bella Bird kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano imejipanga kusimamia utekelezaji wa miradi yote inayotekelezwa sasa na itakayoanza kutekelezwa katika siku zijazo kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia.

  Kwa hivi sasa miradi 26 yenye thamani ya Jumla ya Dola za Marekani Bilioni 4.5 inatekelezwa hapa nchini kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia.  Gerson Msigwa

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Dar es Salaam

  03 Novemba, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird Ikulu jijini Dar es Salaam 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU. 

  0 0
  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkalama waliojitokeza kuunga mkono kampeni ya ujenzi wa  vyumba vya madarasa iliyozinduliwa hivi karibuni wilayani humo. 
  Baadhi ya Kina mama wakishiriki shughuli ya usombaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa madarasa katika shule mpya ya Kilima Mswaki iliyopo katika kijiji cha Mkalama wilayani Hai. 

  Afisa tawala wa wilaya ya Hai,Julieth Mushi akishiriki katika zoezi la ubebaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi katika shule hiyo. 


  0 0
  0 0


  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB), (kushoto), akijibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma

  Baadhi ya Wabunge wakiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (Kulia) na Naibu Waziri wake Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati), baada ya kujibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimpongeza Naibu Waziri wake, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya kuwasilisha kwa umahili mkubwa majibu ya serikali kutokana na hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb), akizungumza na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri (kulia) pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Tume hiyo baada ya kuwasilishwa kwa majibu ya hoja mbalimbali za Waheshimiwa Wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
  Kamisha wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Cheyo (kulia), akibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (katikati) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba, nje ya ukumbi wa Bunge baada ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) na Naibu Waziri wake Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb), kujibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma. (Picha zote na Benny Mwaipaja-Wizara ya Fedha na Mipango) 


older | 1 | .... | 1416 | 1417 | (Page 1418) | 1419 | 1420 | .... | 3284 | newer