Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1326 | 1327 | (Page 1328) | 1329 | 1330 | .... | 3286 | newer

  0 0


  Bibi. Mwakawago akimkabidhi Balozi Mulamula zawadi ya picha yake ya kuchorwa.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawsiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni mjumbe wa Umoja wa Wanawake (Nje Women) akitoa neno la shukrani kwa Balozi Mulamula.
  Kikao kikiendelea
  Picha ya Pamoja ya walezi na uongozi wa Nje Women
  Picha ya pamoja. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Following the Israelian Prime Minister Benjamin Netanyahu visit to Africa recently companies from Israel have increased their motives and ambition to expand their investments in Africa. Speaking with the Vice President of the United Republic of Tanzania Hon. Samia Suluhu Hassan the CEO of of Mer  Group  Mr Omer Laviv has mentioned that his company focuses Tanzania as a gateway to Africa and they are planning to expand their investment in Tanzania in order to adhere with Prime Ministers Netanyahu bid to increase investment in Africa.
  Mr .Omer said  Mer a technological company dealing with Telecommunication, Security and Green Technology solutions .that came to Tanzania in a year. 2006 is in its way to move next level hence request for support from the Tanzanian government and other local partners. He told the Tanzanian VP that Mer has received the announcement made by President John Magufuli that he plans to shift the Tanzanian capital to Dodoma With great gesture and it plans to be part of that move in expanding its services once the government of Tanzania agrees to provide them with the opportunity to offer Communication  and other technological works

  0 0

  Na Mama Bishanga
   Rukia mtoto wa marehemu Sheikh Yahya Hussein aliangusha bonge ya white party kusherehekea miaka 50 ya birthday yake kwenye hoteli babu kubwa ya Marrioti, jijini Cleveland Ohio. Mambo yalikuwa mambo haswaaa!
  Rhumba lilinoga kwa nyimbo za nchi mbali mbali za Africa na hasa za maarufu home TZ za Bado, Number one, Bora uende, Colors of African, na Nasema nae taarabu ambao mume wa Rukia ilibidi awekwe kitini na kukatiwa mauno kisawasawa na mkewe na waalikwa akina Mama Bishanga, Prisca Zenda, Michelle Mujuni nk walipotupia mduara wa nguvu! Wapendwa angalieni picha mpate picha ya mambo yalivyokuwa bam bam!         
            HAPPY BIRTHDAY RUKIA MUNGU AKUONGEZEE UMRI, MAFANIKIO, NA
                                FURAHA YA MAISHA YAKO NA NDOA NA FAMILIA YAKO!
   Birthday girl na Mama Bishanga na mdau
   Mambo mseto
  Birthday girl Rukia

  0 0


   Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe  akipokea ripoti ukaguzi  wa asasi za kiraia kutoka kwa  Naibu  Katibu  Mkuu wa Wizara ya Waziri wa Katiba na sharia Mhe. Amon Mpanju  jijini Dar es Salaam. Serikali tayari imepanga kuzifuta Asasi za kiraia takribani 5,000 kutokana na Sababu Mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa asasi hizo usiofuata taratibu za Usajili.
   Kaimu Afisa Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA)  Bi. Emmy Kalomba Hudson akifafanua jambo akiwa na  Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe  jijini  Dar es Salaam.
  Waziri wa Katiba na sheria Dkt.Harrison Mwakyembe  akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano wa kupokea ripoti ya ukaguzi kutoka kwa Taasisi zote zinazofanya usajili wa asasi za kiraia leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu  Katibu  Mkuu wa Wizara ya Waziri wa Katiba na sharia Mhe. Amon Mpanju.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

  0 0  0 0

  UPIMAJI AFYA KWA WALIOKUWA 
  WAFANYAKAZI WA MGODI WA BULYANHULU

  Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) utaendesha zoezi maalum la upimaji afya za waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu ambao waliachishwa kazi na mgodi huo mnamo mwaka 2007 bila kupimwa afya zao kinyume na Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.
  Baada ya ukikwaji huo wa sheria kuripotiwa kwa Wakala, hatua stahiki zilichukuliwa ikiwemo kufanya kaguzi maalum za usalama na afya katika eneo la mgodi na kutoa onyo kali kwa mwajiri wa walalamikaji pamoja na kugharimia upimaji afya za waathirika wote.
  Katika kushughulikia tatizo hilo, vikao vya mashauriano vilivyojumuisha serikali, mwajiri (Mgodi wa Bulyanhulu) na waathirika kupitia chama chao, TAMICO, vilifanyika na utaratibu wa kushughulikia suala hilo ukawekwa. Katika utaratibu huo, TAMICO ilipewa jukumu la kuwatafuta waathirika wote popote walipo na kuwasilisha majina yao kwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi.  Wakala ulikuwa na jukumu la kuyapeleka majina hayo kwa mwajiri kwaajili ya uhakiki na kuratibu upimaji afya wa waathirika hao baada ya majina yao kuhakikiwa. 
  Hadi kufikia sasa tayari waathirika 315 kati ya 371 ambao mwajiri alithibitisha kwamba walikuwa wafanyakazi wake wameshapimwa afya zao. 
  Waathirika 56 waliobaki hawakujitokeza wakati wa upimaji afya licha ya kupewa taarifa juu ya zoezi hilo.  
  Waathirika watakaopimwa kwasasa ni wale ambao vipimo vyao vya awali vilionesha kwamba wanahitaji vipimo zaidi kutoka kwa madaktari bingwa. 
  Maandalizi ya upimaji huu yamekamilika na zoezi hili litafanyika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili siku ya Jumamosi tarehe 20/08/2016 na katika hospitali ya rufaa ya Bugando mnamo tarehe 22/08-15/09/2016. Katika zoezi hili waathirika ambao orodha ya majina yao imeambatanishwa katika taarifa hii wataonana na madaktari bingwa wa magonjwa ambayo wana dalili nayo ili kubaini kama wana matatizo kiafya na hatimaye kuweza kutazama kama matatizo waliyo nayo yametokana na kazi walizokuwa wakifanya mgodini. 
  Kwa waathirika ambao madaktari watathibitisha kwamba matatizo yao ya kiafya yamesababishwa na kazi walizokuwa wanafanya, Wakala utashauri namna ambavyo wanapaswa kufidiwa kwa mujibu wa sheria za nchi. 
  Waathirika ambao watakutwa na matatizo ya kiafya ambayo hayatokani na kazi, watashauriwa kuendelea na matibabu katika hospitali zilizopo karibu nao.
  Aidha kwa waathirika ambao hawatakutwa na matatizo yoyote ya kiafya watapatiwa vyeti vyao (certificate of fitness) ambavyo hutolewa kwa wafanyakazi wanaopimwa afya zao baada ya kukoma kwa ajira zao kwa mujibu wa kifungu Na.24 (2) cha Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.
  Ikumbukwe kwamba, upimaji huu ni mwendelezo wa hatua mbali mbali zinazochukuliwa na serikali katika kushughulikia tatizo hili ambalo lilitokea mwaka 2007 ambapo waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu waliachishwa kazi na mwajiri wao baada ya kugoma kufanya kazi. 
   Hata hivyo mwajiri wao (Mgodi wa Bulyanhulu) haukuweza kuwapima afya zao kama Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 inavyomtaka.
  Mwisho, kwakuwa suala hili ni la kisheria na serikali ina nia ya dhati ya kulishughulikia, tunaomba ushirikiano kutoka pande zote (waathirika na mwajiri) ili kuhakikisha kwamba zoezi hili linatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.
  Imetolewa na;
  Dkt. Akwilina Kayumba

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya tukio la Kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wa kwanza (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa  na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo wa kwanza (kushoto).
   Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Picha na IKULU. KWA PICHA ZAIDI OFYA HAPA.

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Zahanati na vituo vya Afya katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara ambapo ametoa maagizo mbalimbali yafanyiwe kazi huku suala la watumishi likibainika kuwa ni tatizo katika Wilaya hiyo.


  Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea Zahanati ya Hunyari iliyopo Kijiji cha Hunyari, Zahanati ya Kihumbu, Maliwanda, Kituo cha Afya Mugeta, Zahanati ya Sanzate, Kituo cha Afya Ikizu.

  Aidha, amewataka watendaji na Halimshahuri hiyo kuhakikisha wanakamilisha maboresho na utekelezaji mwingine ikiwemo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya kupanga safu ya ufanyaji wa kazi kwa kuwapeleka watalaamu katika Zahanati hizo ili kuwahudumia wananchi walio pembezoni.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, Mh. Boniface alipongeza ziara hiyo kwani wameweza kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili sehemu ya utoaji wa huduma za Afya hivyo ujio wake huo kwenye maeneo hayo ya Vijijini yamewafungua macho.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitembelea kukagua shughuli za ufanyaji kazi wa Zahanati ya Hunyari
  Jengo maalum la wodi ya Wazazi la Zahanati ya Hunyari ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo kutoka Mkurugenzi wa Wilaya ya Bunda namna watakavyoisaidia Zahanati hiyo.


  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Oysterbay jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) na kewe Fatma Mganga Ndugai wakati wakati walipokwenda nyumbani kwa Spika Salasala jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016 kumjulia hali.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakiagana na Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia) na mkewe Fatma Mganga Ndugai (wapili kushoto) wakati walipokwenda nyumbani kwa Spika, Salasala jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016 kumjulia hali.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomjulia hali jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomjulia halijijini Dar es salaam Agosti 19, 2016.

  0 0

  Habari za kusikitisha zimetufikia muda huu kuwa malkia wa Tarabu nchini Bi. Shakila Saidi amefariki dunia jioni ya leo muda mfupi baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar es salaam. 
  Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw. Addo November, Bi Shakila hakuwa anaumwa ila baada ya kumaliza kuswali alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali alikokimbizwa  alikutwa amekwishafariki. Taarifa kamili  ya mipango ya mazishi 
  tutawaletea mara tu tutapozipata.
  MOLA AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMINA
  ------------------------------
  Kipindi cha DANGA CHEE cha MICHUZI TV kilipata bahati ya kuongea na marehemu Bi Shakila enzi za uhai wake takriban miezi sita iliyopita.
  Sikiliza mahojiano hayo hapa chini:

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Serikali imeazimia kuachana na biashara ya kuingiza nguo za mitumba kutoka nje ya nchi ifikapo mwaka 2018.

  Maazimio hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika uzinduzi wa mafunzo ya uanagenzi ya ushonaji nguo katika kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Company, Ltd.

  Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana kwamba ifikapo mwaka 2018 soko la Afrika Mashariki halitaingiza nguo za mitumba kutoka nje. 
   Ameongeza kuwa kwa kutekeleza azimio hilo Serikali imeandaa  mafunzo ya kuhakikisha vijana wengi wanapata stadi za kushona nguo nchini ili kuwawezesha kufanya kazi katika viwanda vilivyopo na vitakavyojengwa kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zetu wenyewe na kuacha kutegemea bidhaa kutoka nje.

  “Tumejipanga kutekeleza azimio hili na kwa kushirikiana na kiwanda hiki tunategemea kutoa mafunzo ya uanagenzi kwa vijana 2,000 kwa mwaka katika stadi za kubuni mitindo, kukata, kushona na kumalizia nguo” alisema Mhe. Jenista.

  Aidha Waziri huyo amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo kwani mafunzo hayo yatawasaidia kuendana na viwango vya soko la kimataifa na mahitaji ya soko la nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika kubuni mitindo, kukata na kushona nguo zenye ubora wa kimataifa.

  “Imani yangu kuwa wataalamu waliopo katika kiwanda hiki watawapa ujuzi wa kutosha na wengine wataweza kupata ajira katika kiwanda hiki tumieni fursa hii mliyoipata ni ya pekee kwani mmebahatika kuwa miongoni mwa wanafunzi wa kwanza kupata mafunzo chini ya Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini. 
  Mhe Jenista amesisitiza kuwa mafunzo hayo yatawezesha vijana kupata ajira katika Viwanda, kujiajiri na hata kutoa ajira kwa wengine hivyo vijana watumie fursa hiyo kutengeneza mtaji na kujiunga katika vikundi vitakavyowawezesha  kufungua viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza nguo na kuendelea kukuza ujuzi waliopata. 

  Pia Waziri Jenista ametoa wito kwa viwanda vingine kushirikiana na Serikali kukuza ujuzi kwa vijana kupitia mafunzo ya uanagenzi na kuwahakikisha kuwa Serikali itaendelea kuwawezesha Vijana kupata mafunzo ya aina hiyo.

  “Napenda niwahakikishie kuwa Serikali iko bega kwa bega nanyi, fungueni viwanda vingi sehemu mbalimbali katika nchi yetu, sisi kama Serikali tutashirikiana kwa pamoja kuhakikisha rasilimali watu ya kuendesha viwanda hivi inapatikana” 

  Mbali na hayo Serikali inayo mipango na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na kuwa na uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

  Serikali iliingia makubaliano na kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Co. Ltd kutoa mafunzo ya uanagenzi kwa vijana 2,000 kwa mwaka katika stadi za kubuni mitindo, kukata, kushona na kumalizia nguo jumla ya vijana 1,089 waliomba nafasi ya kupata mafunzo hayo yatakayoendeshwa kwa awamu tatu na kwa sasa jumla ya vijana 430 wanapata mafunzo hayo.

  0 0

  Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wa wakiwa moja ya maozezi yao ya kupasha viungo kabla ya kuanza mazoezi ya kutuliza ghasia.
  Askari Polisi wa kikosi maalum cha polisi (CRT) wa mkoa wa Iringa wakiwa katika mazoezi ya utayari wa kukabiliana na matukio yoyote yatakayojitokeza katika maeneo mbalimbali.
  Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa mikoa mbalimbali wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kupambana na matukio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali.
  Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kutuliza ghasia na kukabiliana na matukio yoyote ya uhalifu na wahalifu.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0


  Kwa mujibu wa familia marehemu Bi. Shakila Saidi anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi Agosti 20, 2016 saa 10 alasiri katika makaburi ya Uwanja wa Ninja huko Mbagala Charambe jijini Dar es salaam  

  Namna ya kufika msibani nyumbani kwa marehemu kwa kutumia daladala. Unapanda magari ya Mbagala Rangi Tatu, ukifika mwisho unachukua basi la Nzasa na unashuka Mnara wa Voda hapo unauliza kwa Bi Shakila utaonyeshwa.
  Bi Shakila alifariki jana baada ya kuanguka nyumbani kwake mara baada ya kuswali swala ya Magharibi. Kwa mujibu wa binti yake, Shani, mkongwe huyu wa taarabu hakuwa anaumwa wajati mauti yanamkuta.

  KALALE PEMA PEPONI KIPENZI CHETU BI. SHAKILA

  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Msanii wa muziki wa taarab Bi. Shakila Said kilichotokea ghafla nyumbani kwao Mbagala jijini Dar es Salaam jana Ijumaa ya tarehe 19/08/2016.

  Shakila ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa na mchango mkubwa katika kukuza muziki wa taarab nchini hasa katika kubuni kazi za Sanaa za muziki mbalimbali ambazo zilikuja kupata umaarufu mkubwa. Moja ya kazi alizobuni na kupata umaarufu mkubwa ni pamoja na 'Macho yanacheka' na 'kifo cha mahaba'.

  Mchango wake katika muziki wa taarab hasa katika kubuni na kutunga nyimbo zenye ubora, ujumbe na maadili kwa jamii hautasahaulika kamwe. Ni mwanamuziki aliyeacha misingi katika sekta ya muziki na alijitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki wa taarab mahali ulipo leo.

  Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu Shakila hasa katika kupenda kujitolea muda mwingi katika kukuza muziki wa taarab na sekta ya muziki kwa ujumla.

  Baraza linatoa pole kwa ndugu wa marehemu, shirikisho la muziki, wasanii na wadau wote wa Sanaa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

  Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen

  0 0

  Hasa kwa wale wanaonunua magari kwa mara ya kwanza, na hawana uzoefu wa kuendesha gari, na pia wale wote ambao wanaweza wakawa wana uzoefu wa kuendesha gari mijini, lakini hawana uzoefu wa kuendesha gari kwenye bara bara kuu za kwenda mikoani. Lakini ni vema kila mtu aliye dereva akasoma ninachoeleza hapa. Inaweza kuokoa maisha yako ya familia yako, na wengine wanaoendesha magari au kuwa abiria. 

  Ndugu zangu, ukiweza kuendasha gari hapa Dar, au hata mikoani mijini, haina maana utaweza kuendesha gari pasipo tatizo kwenye barabara kuu. Nimeshuhudia watu wengi sana waliokufa kwa sababu baada ya kununua gari walikuwa na mchecheto wa ku-drive kwenda kwao kijijini. Kuendesha gari kwenye barabara kuu ni tofauti sana na kuendesha gari mijini. Kwenye barabara kuu challenge zake ni kubwa sana kwa sababu gari zinaenda kwa kasi, na pia kuna mambo mengi ya ghafla yanayoweza kujitokeza ambayo kama huna uamuzi wa haraka kama dereva utakufa tu kabla ya kufika mwisho wa safari yako. 
  Ukifanya kosa hata dogo barabara kuu unaweza kufa, tofauti na mijini. Kwa mfano, ku-overtake katika barabara kuu ni jambo linatakiwa lifanywe kwa makini sana. Na pia kila unapoingia kona kali au blind spot kwenye barabara kuu weka akilini kwamba unaweza kukutana na kitu upande wako, basi linaloenda kasi, lori au trekta liloharibika, mifugo, shimo kubwa, mawe yaliyoporomoka, ajali nk. Pia unaweza kukutana ghafla na dereva mzembe anae-overtake kwenye kona na yuko upande wako. Usithubutu ku-overtake sehemu ambayo huoni mbali mbele, na usikaribie sana gari unayotaka ku-overtake kabla ya kui-overtake. Na unapo-overtake kama una gari manual gear, rudi gia za chini kwanza ili kujenga spidi ya ku-overtake. 

  Kama una gari automatiki, ikibidi itoe gari kwenye overdrive (unabonyeza kiswitch cha Overdrive na kuna kataa katawaka kwenye dashboard kuonyesha Overdrive iko off), hasa kama ulikuwa umepunguza mwendo. Mara nyingine toa gia kwenye "D" na rudi kwenye "2" ili kujenga spidi ya ku-overtake, na ukishamaliza rudi kwenye D na Overdrive. Hili ni muhimu sana kwa gari ambazo ukikanyaga accerator gari inakawia kuchanganya. 
  Overtake kwa haraka, sehemu ambayo iko salama, na ni vizuri gari unayoi-overtake dereva wake ajue unamu-overtake. Unaweza kumpigia honi kidogo ya kuibia kama kuomba - usipige kwa nguvu ukamuudhi. Epuka kuovertake sehemu ya barabara yenye mashimo, maana dereva wa mbele anaweza kurudi upande wako ili akwepe shimo wakati tayari unamu-overtake. Siri moja ya ku-overtake salama ni uvumilivu - overtake nzuri haitaki haraka. 

  Na pia kosa linaloua watu wengi sana ni ku-overtake kwa kukisia kwamba hakutakuwa na gari inayokuja upande wa pili zile sehemu ambazo huoni vizuri mbele. Hata kama barabara haina magari mengi usithubutu kukisia kwamba hakutakuwa na gari (gambling overtake). Na pia katika barabara kuu kuna suala la uchovu - fatigue. Hili ni jambo jingine linaua sana watu wasio na uzoefu wa kuwa katika barabara kuu. Ni mbaya hata zaidi ikiwa utakaposimama mahali kwa chakula ukanywa bia - hata moja tu, kwa sababu itakuletea sana usingizi. 

  Epuka kula vyakula vizito kama ugali na maharage, au kula hadi ukashiba sana! Ukisikia usingizi simama upumzike, toka ndani ya gari, tembea kidogo, kabla ya kuendelea na safari. Kama ikibidi tumia Redbull (sio zaidi ya moja). Na jambo jingine muhimu sana la kukumbuka ni kwamba ukiingia barabara kuu, ukaendesha kwa muda fulani, akili yako inazoea spidi kali kiasi kwamba huoni tena kama unaenda spidi kali. Unaweza ukawa unaenda 140km/h ukaona kama unaenda 80km/hr. 

  Hili huwa mara nyingi linasababisha kuacha njia na kupinduka, au kuingia kona ukiwa na spidi kubwa na gari kupinduka. Nadhani umesikia sana ajali zinazosemwa zilitokea kwa sababu dereva alishindwa kumiliki gari - ni kwa sababu akilini dereva aliona haendi spidi. 
   Na pia jambo jingine muhimu sana kukumbuka ni kwamba, unapoenda safari yoyote ya mbali ambayo utaendesha gari mfululizo kwa zaidi ya masaa manne, au kwa spidi zaidi ya 100km/hr, hakikisha tairi zako hazina umri zaidi ya miaka mitano, la sivyo utapata basti hata kama tairi inaonekana bado mpya kwa kuitazama. Tairi ikizidi miaka mitano haifai kusafiria safari ya mbali, japo unaweza ukaendelea kuitumia kwa safari za mijini. Nimeona niseme haya kwa sababu nawapenda ndugu zangu.

   Sitaki mufe barabarani, au mniue mie na familia yangu. Wapeni taarifa wengine ili tuzidi kuepuka vifo hivi vya barabarani ambavyo vingi vinazuilika. Neno langu la mwisho, ili uendeleee kuwa salama barabarani ni kwa lugha ya kiingereza; BE PATIENT kwa lolote unalotaka kufanya ukiwa unaendesha gari. Zingaitia hilo, utakuwa salama.

  0 0


  Hii ni zawadi ya heshima (tuzo) iliyotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na kukabidhiwa kwa mshindi wa kwanza,Mwanafunzi wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent.


  Mkurugenzi Mkuu kutoka kampeni ya Puma Energy Tanzania Ltd,Philippe Corsaletti akimkabidhi tuzo/zawadi ya Begi na cheti mwanafuzi wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.

  Mashindano hayo yalihusisha shule kumi kwa upande wa Dar Es Salaam ambazo ni    Mwananyamala,Kisutu,Bunge,Kisiwani,Mchangani,Mnazini,Mwananyamala B,Mikocheni,Mtendeni,Kisutu,Kisiwani na Ugindoni,Shule nyingine tatu ni kutoa mkoa wa Geita ambazo zitashiriki na mchakato wa kuwapata washindi,matokeo ya washindi wa mwisho yatatangazwa wakati wa kilele cha cha wiki ya Usalama barabarani ambayo inatarajia kufanyika hivi karibuni
  Mwanafuzi wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent akilia kwa furaha mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga pamoja na Waandaji kutoka kampuni ya Puma Energy Tanzania na AMEND wakitafuta washindi watatu wa shindano la uchoraji katika masuala mazima ya kuhamasisha usalama barabarani 2016.
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga akimkabidhi Mwanafunzi wa darasa la sita,Shaaban zawadi ya Begi na Cheti,kutoka shule ya msingi Bunge baada ya kuibuka mshindi wa tatu katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga akimkabidhi Mwanafunzi wa darasa la sita Antonia Anthony zawadi ya Begi na Cheti,kutoka shule ya msingi Mwananyamala baada ya kuibuka mshindi wa pili katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake Ilala,jijini Dar wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo ambapo uchunguzi wa wanafunzi wengine hewa bado unaendelea.
  Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akisisitiza jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo, Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Edward Mpogolo.
  Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo.

  .............................................................
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema ametangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya ya Ilala ambazo hakuzitaja, Mjema amesema baada ya uchunguzi huo kufanyika,wamebainika wanafunzi idadi hiyo,ambapo wahusika wote watachukuliwa sheria ikiwamo na hatua za kinidhamu,kwani hayo ni makosa kama yalivyo makosa mengine

  Wilaya ya Ilala ina shule za sekondari za serikali 46 na za sekondari 49 ukiacha shule za taasisi binafsi ,zoezi la ukaguzi bado linaendelea katika shule zote za msingi wilayani humo mpaka Septemba mosi mwaka huu ndiyo litamalizika.

  Akizungumzia suala la Madawati mkuu wa wilaya huyo, amewapongeza wadau wote waliochangia madawati mpaka kuhakikisha uhaba wa madawati katika wilaya ya Ilala unakwisha, huku kukiwa na ziada ya madawati 2821

  Ameongeza kuwa kazi kubwa inayofuatia kwa sasa ni kuongeza vyumba vya madarasa ambapo kazi hiyo inaendelea vizuri .

  Mh. Sophia mjema pia amemshukuru Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuanzisha mkakati wa wadau kuchangia madawati, jambo ambalo limesaidia tatizo hilo kushughulikiwa kikamilifu na wadau mbalimbali, lakini pia akampongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kwa usimamizi thabiti wa utekelezaji wa mkakati huo. jambo ambalo limesaidia wilaya ya Ilala kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa madawati katika shule za zake za msingi

  0 0

  Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Shiza Kichuya akiachia shuti lililopelekea kuipatia Timu yake bao la tatu dhidi ya Timu ya Ndanda, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 3-1.
  Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Shiza Kichuya akishangilia Ushindi sambamba na Mashabiki wa Simba baada ya kuipatia timu yake bao la tatu dhidi ya Timu ya Ndanda, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 3-1.
   Mshambiaji wa Simba, Laudit Mavugo akiondoka na kijiji cha wachezaji wa Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 3-1.
  Kipa wa Simba, Vincent Agban akiruka na kuusindikiza kwa macho mpira ukiingia wavuni baada ya kupigwa kichwa safi kabisa na Mshambuliaji wa Timu ya Ndanda, Omary Mponda na ikiwa ni goli la kufutia machozi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 3-1.
  Beki wa Simba, Mohamed Hussein akiondoka na mpira.


  0 0
 • 08/20/16--09:21: Article 7


 • 0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwapungia wananchi wa Mkoa wa Katavi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara ya kikazi mkoani humo leo Agosti 20, 2016. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Vijana wa CCM baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara  ya kazi mkoani Katavi leo Agosti 20, 2016. 
     Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya  wananchi wa mkoa wa Katavi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara ya kazi mkoani humo leo Agosti 20, 2016.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya  wananchi wa mkoa wa Katavi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara ya kazi mkoani humo leo Agosti 20, 2016.
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

older | 1 | .... | 1326 | 1327 | (Page 1328) | 1329 | 1330 | .... | 3286 | newer