Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1327 | 1328 | (Page 1329) | 1330 | 1331 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mkutano wa kazi na watendaji wa ofisi yake ya Idara ya Mazingira kujadili kwa kina namna ya kukabiliana na hali tete ya uharibifu wa mazingira unaoendelea nchini.

  Katika mkutano huo uliofanyika leo, Ikulu, Dar es salaam ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba, Makamu wa Rais ameawaagiza watendaji wa idara hiyo waache kukaa ofisini na badala yake waende kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.

  Alisema hali ya uharibifu wa mazingira ikiachwa iendelee kama ilivyo inaweza ikasababisha madhara makubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla, hivyo ni muhimu kwa makundi yote wakiwamo wataalam wa mazingira na wadau wa maendeleo kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na tatizo hilo.

  Alisema baadhi ya watendaji wamekuwa ni sehemu ya uharibifu wa mazingira na kuonya wataobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali ili kukomesha tabia hiyo.Baadhi ya watendaji waliotoa taarifa kuhusu hali ya mazingira nchini wamekiri kuwa hali ya uharibifu wa mazingira siyo nzuri hasa kwenye mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Manyara, Geita, Singida na Kilimanjaro.

  Inakadiriwa kuwa takribani hekta 400,000 za misitu zinaharibiwa kila mwaka hali ambayo inapelekea baadhi ya wanyama kutoweka.Watendaji hao wameiomba serikali iongeze bajeti ya kutosha ili waweze kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi.Makamu wa Rais ametumia siku ya mapumziko ili kujadiliana na kuweka mipango na mikakati ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini. Mkutano huo wa kazi unaendelea tena hapo kesho.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira mara baada ya kupata taarifa za maendeleo, mipango na mikakati ya Idara hiyo, kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo kwenye mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Watendaji wa Idara ya Mazingira (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira, kushoto ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kulia ni Katibu Mkuu Oisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbaraka Abduwakil Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Msaidizi Idra ya Mazingira Bi. Esther Makwaia akiwasilisha taarifa ya hali ya Mazingira nchini kwenye mkutano na Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu, Ikulu jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Aliyekuwa msanii mahiri wa Taarab, marehemu Shakila Said wakati wa uhai wake akipongezwa na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Tamasha la wasanii la kumuaga Mhr. Kikwete  baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa chama hicho, mjini Dodoma Julai 23, mwaka huu. 
   Shakila akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana
  Aliyekuwa msanii mahiri wa Taarab, marehemu Shakila Said wakati wa uhai wake  akiwa kwenye hafla hiyo
  (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
   KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
  0 0


  0 0  0 0

  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2016.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye akiweka udongo kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
  Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar,wa pili kushoto aakishuhudia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye na Katibu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw. John Kitime.
  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam. Kushoto ni  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye.
   Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said  huko nyumbani kwa marehemu  Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam.
  Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kulia) na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye (pili kushoto) wakishiriki maziko ya aliyekuwa Mkongwe,mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarabu hapa nchini,Bi Shakila Saidi ambaye mazishi yake yamefanyika leo huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.


  0 0

   Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.

  SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litatumia fursa ya tukio la kupatwa kwa jua kama njia mojawapo ya kutangaza hifadhi za taifa hususani zinazopatikana katika mikoa ya nyanda za juu kusini na Magharibi mwa Tanzania.

  Tukio la kupatwa kwa jua linataraji kuonekana vizuri ukilinganisha na maeneo mengine Duniani katika eneo la Rujewa wilayani Mbarali mkoani hapa,eneo ambalo liko jirani na Hifadhi za taifa za Ruaha,Kitulo na Katavi.

  Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete  alisema maandalizi kwa ajili ya kupokea wageni wanao tarajia kufika nchini kwa ajili ya tukio hilo ambalo limekuwa likitokea kwa nadra.

  “ Wataaam na wanasayansi wa kitaifa na kimataifa wathibitisha kuwa  eneo pekee ambalo tukio hilo litaonekana vizuri kuliko maeneo yote duniani ni Tanzania katika mikoa ya nyanda za juu kusini,eneo ambalo lina vivutio utalii vinavyopatikana katika hifadhi zetu za Katavi.Kitulo na Ruaha”alisema Shelutete .

  “Shirika limejipanga kuhakikisha kuwa wageni wanoukuja kwa ajili ya tukio hilo pia wanapata fursa ya kuingia katika moja ya hifadhi zetu,niwaomba wadau wa sekta ya utalii nchini kutumia nafasi hii adhimu kukutana na wageni wanaokuja ili kuuza bidhaa zao za utalii”aliongeza Shelutete.
   
  Naye mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha Christopher Timbuka alisema kituo kikubwa ambacho kimethibitishwa kutumika kwa ajili ya watu kujionea vizuri tukio hilo ni katika eneo la rujewa wilaya ya mbarali ambako maandalizi yote muhimu yamefanyika.

  Kwa upande wake mhifadhi wa idara ya  utalii Tutindaga Mdoe alisema baada ya tarifa za tukio hilo kuthibitishwa idadi ya wageni imeanza kuongezeka na kwamba wameandaa mahema na eneo la vyakula na vinywaji kwa wageni watakaofika kushuhudia tukio hilo katika eneo la Bonde la Ihefu lililopo katika hifadhi ya taifa ya Ruaha.

  Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti hili katika eneo hilo maarufu kwa kilimo cha mpunga umebaini asilimia kubwa ya nyumba za kulala wageni tayari zimejaa kwa tarehe ya tukio hilo.

  0 0  Na Adili Mhina
  Tume ya Mipango imekamilisha zoezi la kuandaa wataalamu wanaotarajiwa kutoa mafunzo juu ya usimamizi na utayarishaji wa miradi ya uwekezaji katika sekta ya umma kwa maofisa wa serikali walio chini ya Idara za Sera na Mipango na zile za Uwekezaji katika Wizara, Mikoa, Halmashauri, Mashirika pamoja na Taasisi mabalimbali za Umma hapa nchini.

  Akifunga mafunzo hayo mwishoni mwa juma, Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe alisema kuwa katika awamu hii ambapo Shilingi trilioni 59 kati ya trilioni 107 zinatarajiwa kutolewa na Serikali pekee katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Serikali imeamua kujipanga upya ili kuhakikisha miradi yote itakayoanzishwa inaleta tija kwa wananchi.

  “Tumeamua kujiandaa mapema kwa sababu tunatarajia miradi mingi mikubwa itaanzishwa katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP II). Hivyo, ni muhimu huko mtakapoelekea kutoa mafunzo mhakikishe mnatoa mbinu sahihi za kukabili changamoto zinazojitokeza katika kutayarisha, kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo”, Alisema Bw. Sangawe.

  Sangawe aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo kuwafikia walengwa wote hakutakuwa na sababu kwa maofisa wa serikali kushindwa kuandaa, kutekeleza, kusimamia au kutoa ushauri sahihi pale serikali inapofanya uwekezaji kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

  Akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Tume ya Mipango kwa niaba ya wahitimu wote, Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Sauda Ponda alisema kuwa wahitimu wote walipata fursa ya kujadili, kuuliza na kufanya mazoezi mbalimbali katika vikundi kwa lengo la kuongeza uelewa na kuimarisha uwezo kwa ajili ya kwenda kutoa mafunzo kwa wahusika.

  “Kwa niaba ya wenzangu wote napenda kutoa shukrani za pekee kwa Tume ya Mipango kwa kuandaa mafunzo haya, waalimu wetu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wametufundisha vizuri na wametupa mazoezi ya kutosha na sote tuko tayari kwenda kutoa elimu hii kwa wenzetu,”. Alisema Bi. Ponda.

  Wataalamu hao waliotumia siku tano kuchambua kwa kina Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma ambao ndio unaopaswa kufuatwa katika kutekeleza miradi yote ya serikali, wanatarajiwa kugawanyika katika makundi mbalimbali yatakayotoa mafunzo kikanda ambapo zoezi hilo litaanza tarehe 22 mwezi huu.

  Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Sauda Ponda akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Tume ya Mipango kwa niaba ya wahitimu. 
  Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe akifunga mafunzo ya kuandaa wataalamu wa kufundisha masuala ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma, pembeni yake ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Uchumi Jumla, Dkt. Lorah Madete.
  Wajumbe wa mafunzo wakimsikiliza Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe wakati wa kufunga mafunzo hayo.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (katikati) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumzia maboresho yanayofanywa na mamlaka hiyo.  kulia ni Mkurugenzi wa Utekelezaji (TRL), Bw. Focus makoye na Mkurugenzi wa Biashara na Masoko (TPA), Bibi. Fransisca Muindi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumzia maboresho yanayofanywa na mamlaka hiyo. 
   

  0 0

  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) imezitunuku kampuni 86 leseni na vyeti vya ubora baada bidhaa wanazozalisha kukidhi matakwa ya viwango vya shirika.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dkt. Egid Mubofu amesema mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa sasa kampuni hizo zina fursa zaidi ya kupanua masoko ndani na nje ya nchi.
  “Alama hizi hutolewa kwa bidhaa zilizopimwa na kuthibitishwa na kukidhi matakwa ya viwango,” alisema Dkt. Mubofu.
  Kampuni zilizopatiwa vyeti hivyo ni za wazalishaji wakubwa, kati na wadogo.  Alama hiyo ni uthibitisho kuwa bidhaa zao  ni salama kwa mlaji na uhifadhi wa mazingira.
  Kampuni zilizopata alama hiyo zinatoka katika sekta mbalimbali zikiwemo za usindikaji wa vyakula, uhandisi mitambo na umeme, kemikali, ujenzi na nguo.
  Alisema hatua hiyo ni mwendelezo wa kuona wazalishaji wadogo na wa kati nao wanakuwa ni sehemu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
  Alitoa wito kwa wazalishaji ambao bado hawajapata leseni na vyeti vya ubora waendelee kufuata taratibu za shirika ili nao waweze kupata alama hiyo kwa ajili ya usalama wa mlaji na kuyafikia masoko ya ndani na nje.
  Afisa Masoko wa Kampuni ya Waja Mabati, Bw. Donasian Massawe alisema cheti cha ubora ni fursa kwao. 
  “Alama yetu tumeipata bila ya usumbufu kutokana na huduma nzuri za shirika hili,” alisema Massawe.  Kiwanda hicho kinachomilikiwa na Watanzania kiko eneo la Kisemvule wilayani Mkuranga, mkoa wa Pwani.
  Alifafanua kwamba uchumi wa viwanda unawezekana na kwamba jambo la msingi ni kwa wajasiriamali kujitokeza na kufuata taratibu za kiserikali ili kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi.
  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Nafaka Nzima Bakery LTD, Bi. Hesperance Kilonzo alilishukuru shirika hilo kwa kumpatia alama ya ubora na kusema kuwa ataweza kuzalisha na kuyafikia masoko kwa urahisi zaidi.
  “Natumia nafaka zisizokobolewa kuzalisha bidhaa kama mikate na keki ambayo ni muhimu kwa afya na maendeleo bora ya ubongo kwa watoto na kujenga afya kwa ujumla,”alisema.
  TBS ina jukumu la kuandaa viwango vinavyotakiwa kufikiwa na wazalishaji mbalimbali kabla ya kuingiza bidhaa zao sokoni.

   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango (TBS), Dkt. Egid Mubofu (wa pili kushoto) akimkabidhi cheti cha ubora Afisa Masoko wa kampuni ya Waja Mabati, Bw. Donasian Massawe (kulia) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Udhibiti Ubora, Mhandisi Tumaini Mtitu na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora, Bi. Ashura Katunzi.  Jumla ya kampuni 86 zilikabidhiwa vyeti vya ubora. 
  Wazalishaji wa bidhaa mbalimbali wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Egid Mubofu katika hafla fupi ya kukabidhiwa vyeti vya ubora kwa kampuni 86 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0

  KWAMBA TAREHE 21.08.2016 MAJIRA YA 10:00 USIKU KATIKA ENEO LA CLUB YA VILLA PARK RESORT KATA YA KIRUMBA WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, ASKARI NAMBA G.5092 PC JOHN NYANGE WA OFISI YA MKUU WA UPELELEZI NA MAKOSA YA JINAI MKOA WA MWANZA (RCO), ALIUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI ENEO LA SHINGONI NA MTU ALIYEKUWA ANAUGOMVI NAE.


  INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUA NA UGOMVI WA MUDA MREFU NA MTU ALIYEJULIKANA KWA JINA MAGINA HUSSEIN MIAKA [27] FUNDI COMPUTER MSUKUMA NA MKAZI WA MTAA WA KIGOTO, AMBAPO MAREHEMU ALIKUWA AKIMDAI BWANA MAGINA HUSSEIN COMPUTER AINA YA LAPTOP.  NDIPO USIKU WA LEO MAJIRA TAJWA HAPO JUU WALIKUTANA ENEO LA CLUB YA VILLA PARK HUKU MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO IKISEMEKANA KUWA ALIKUWA NA WENZAKE WATANO NDIPO WALIMVAMIA NA KUMCHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI SHINGONI NA KUFARIKI DUNIA NJIANI WAKATI AKIPELEKWA HOSPITALI.


  MAREHEMU KWA SASA ALIKUWA NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA STEFANO MOSHI MEMORIAL UNIVERSITY COLLEGE CHA MJINI MOSHI, ALIKUWA ANASOMEA SHAHADA YA SAYANSI YA HABARI NA MAWASILIANO MWAKA WA PILI, AIDHA ALIREJEA MWANZA BAADA YA KUPATA LIKIZO KUJA KUIANGALIA FAMILIA YAKE NDIPO UMAUTI UKAMKUTA.


  WATUHUMIWA SITA AKIWEPO MAGINA SELEMANI AMBAYE ALIKUWA NA UGOMVI NA MAREHEMU PAMOJA NA WENZAKE WATANO WAMEKAMATWA, WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI HUKU UCHUNGUZI KUHUSIANA NA KIFO HICHO UKIWA BADO UNAENDELEA,  PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU  UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA UCHUNGUZI.


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KWAMBA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMESIKITISHWA NA KIFO CHA ASKARI HUYU KWANI LIMEMPOTEZA ASKARI KIJANA AMBAYE BADO JESHI LILIKUWA LINAMTEGEMEA. LAKINI PIA ANAWATAKA WATU WENYE TABIA ZA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUWAPIGA WENGINE HADI KUFIKIA KUPOTEZA MAISHA KUWA WANAFANYA KOSA LA JINAI, NA KAMA WATU WANADAIANA WAFUATE TARATIBU ZA KISHERIA ZILIZOWEKWA ILI KUEPUSHA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA, HIVYO JESHI LA POLISI LINAWATAKA KUACHA TABIA HIYO MARA MOJA KWANI HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.


  IMETOLEWA NA:

  DCP: AHMED MSANGI


  KAMANDA WAPOLISI (M) MWANZA


  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa maagizo mazito kwa watendaji wa Wizara hiyo kesho tarehe 22 Agosti.2016 kuhakikisha wanamfikishia taarifa ya kina kuhusu upungufu wa chanjo nchini.
  Akiwa ziara ya kikazi Mkoani Geita, Ameagiza akute maelezo ya kina mezani kwake, kuwa ni nani haswa amesababisha chanjo kupungua kwenye maeneo mengi nchini? Na mpaka sasa amechukuwa hatua gani za kuwajibika?
  Je, changamoto ipo hazina ama kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Huduma za kinga? “Vyovyote vile, nataka utetezi uje ukiwa na vielelezo, kabla sijachukua hatua stahiki. Chanjo ni eneo pekee kwenye sekta ya Afya tulilofanikiwa kwa zaidi ya 95%! Haikubaliki kurudisha nyuma mafanikio haya."
  Alisema, Baadhi ya maeneo chanjo zipo na wana dozi za mwisho na baadhi hazipo kabisa. Mfano bohari ya chanjo Mkoa wa Geita hakuna chanjo za OPV, Rotavirus, BCG na Tetanus. Wangepaswa kuwa na akiba ya miezi mitatu mbele. Kwenye ngazi ya Taifa wanapaswa kuwa Na chanjo za miezi Sita mbele, hapo ndipo tunaweza kusema tuna chanjo za kutosha.
  DSC_6828Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Dk. Brayan Mawalla na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dk. Joseph Kisala.
  DSC_6843
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua sehemu ya dawa kwenye duka la Hospitali hiyo ya Mkoa wa Geita
  DSC_6845
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dk. Joseph Kisala akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla katika ziara hiyo
  DSC_6899
  Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   TBL Group remains committed to making a significant contribution to the Tanzanian economy. Speaking in Mwanza, the company’s Managing Director Roberto Jarrin who was presenting an overview of his company’s contribution to the country’s economy to journalists said.
  “In addition to contributing Tshs.384 Billion to the Government‘s revenue in 2015, we remain steadfast in our resolve to support all the industries that are linked to our business. 
   That is, from the farmers in the field to the consumers who buy our products.” In this regard, TBL Group will spend in excess of Tshs. 27billion/- in the agriculture sector through enabling thousands of Barley, Grapes, Sorghum and Maize farmers to grow in many ways. 
  This will include: providing them with seeds, extension services as well as facilitating them with access to credit. Banks that provide support to TBL’s partners in the agriculture sector include: CRDB, the National Microfinance Bank (NMB) and the Bank of Africa (BOA). 
   The company also plans to inject Tshs 150bn /- into the transportation sector this year for the collection and transporting of agricultural products from warehouses to its plants as well as the distribution of its finished products across the country. TBL Group’s financial year runs from April 1, 2016 to March 30, 2017.
   The managing director goes on to say that TBL Group will continue to play a key role in the development of the commercial farming of barley, sorghum and maize crops in the country. The company sources Barley, Sorghum (both red and white), Sifted Maize Flour and Grapes from local farmers which are then used in the manufacture of its products. Jarrin reiterated his company’s commitment to enhancing the lives of farmers through connecting them to organisations such as the World Food Programme which then buys their surplus cereals - mostly sorghum and maize - which TBL Group is unable to purchase.  For more CLICK HERE

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya  Kasulu Kanali  Martin Mkisi akiwa amekamata moja ya bunduki  mbele ya mmoja ya watuhumiwa ambao yeye kwa kushirikiana na timu yake ya Ulinzi na Usalama, wamefanikiwa kukamata watu watano wanaotuhumiwa kuwa wawindaji haramu na watekaji pamoja na silaha kadhaa walizokutwa nazo katika misitu ya wilaya hiyo. DC Mkisi amesema zoezi hilo ni endelevu na kwamba yeye na kamati yake hawatapumzika hadi vitendo vya ujangili na utekaji vimekomeshwa wilayani humo.


  0 0

  MAJALIWA: TUTAWANYANG’ANYA URAIA TULIOTOA KWA WAKIMBIZI WATAKAOBAINIKA KUTUUMIA VIBAYA

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania na kuitumia vibaya nafasi hiyo kwa kuingiza watu wengine  kinyume cha sheria watanyang’anywa na kurudishwa walikotoka.
   Aidha, Waziri Mkuu amewaomba viongozi wa dini wawe wanawaelimisha waumuni wao umuhimu wa kulinda amani na kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi husika. 
  Kauli hiyo imetolewa leo (Jumapili, Agosti 20, 2016) na Waziri Mkuu wakati akizungumza na waliokuwa wakimbizi wa Burundi ambao kwa sasa wamepewa uraia wa Tanzania wanaoishi katika Kata ya Katumba, Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mpanda. 
  “Wakimbizi waliopewa uraia wameendelea kuingiza ndugu zao. Naagiza kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ifanye ukaguzi katika kambi zote kwa sababu zimegeuzwa kuwa maficho ya kuwahifadhi watu wanaoingia nchini bila ya vibali,” amesema. 
  “Hakikisheni mnachukua hatua kwa wote watakaoingiza watu kinyemela katika kambi za wakimbizi za Mishamo na Katumba. Pia msiruhusu watu kuleta silaha kwenye maeneo haya. Tanzania watu wanaoruhusiwa kutembea na silaha ni askari tu,” amesisitiza. 
  Waziri Mkuu amesema lazima ulinzi uimarishwe katika maeneo ya mipakani na wasipofanya hivyo watu wengi wataingia nchini bila ya kuwa na vibali hivyo kusababisha ongezeko kubwa la idadi ya watu. 
  Wakati huo huo Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wasiwaudhi wakulima na wafanyabiashara wadogo kwa kuwatoza ushuru  kwenye mazao wanapotoka shambani kama debe moja la nafaka na wanaouza bidhaa ndogo ndogo. 
  “Mkulima ametoka shambani na debe moja la mahindi unamtoza ushuru maana yake nini? Halmashauri tusitafute mgogoro katika hili. Tafuteni biashara za kutoza ushuru, mkulima anatoka kijiji cha Kanoge anakwenda kijiji cha Ikongo ushuru wa nini? Waziri Mkuu amehoji. 
  Waziri Mkuu amesema “Tumewasisitiza mkusanye kodi lakini siyo hivyo. Mkiendelea kutoza ushuru kwa wakulima wanaotoka shambani na mahindi kidogo mtasababisha wakate tamaa ya kulima,”. 
  Akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Katavi jana jioni (Jumamosi, Agosti 20, 2016) mara baada ya Waziri Mkuu kuwasili mkoani hapa Mkuu wa mkoa, Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga alisema mkoa una jumla ya wakimbizi 6,918 wanaoishi katika kambi za Mishamo na Katumba ambapo kati yake wakimbizi 2,150 waliomba uraia wa Tanzania na kunyimwa. 
  Alisema wakimbizi 2,489 walichagua kurejea nchini kwao Burundi ila bado wapo katika kambi hizo huku wengine 653 waliomba uraia lakini majina yao hayakuonekana kwenye orodha ya waliokubaliwa wala kukataliwa uraia hivyo mkoa unaendelea kufuatilia ili kujua hatma yao. 
  Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa wakimbizi wengine sita walichagua kubaki nchini lakini hawakuomba uraia, 398 waliomba uraia ila fomu zao hazikukamilika,249 waliomba uraia ila majina yao hayakurudi huku wengine 973 hawakusajiliwa walipoingia nchini mwaka 2007/.2008.
   IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, AGOSTI 21, 2016.
                                              
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mnara uliojengwa na wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania ili kumshukuru Mungu kwa kupewa uraia huo wakati  alipokitembelea kijiji Katumba mkoani Katavi Agosti 21, 2016. Kushoto kwake ni mkewe Mary na kushoto i Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Mbuga.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakifurahia baada ya kuzindua mnara uliojengwa na wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania ili kumshukuru Mungu kwa kupewa urais huo wakati Waziri Mkuu alipokitembelea kijiji Katumba mkoani Katavi Agosti 21, 2016. Kushoto kwake ni mkewe Mary na kushoto i Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Mbuga.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzindua mnara uliojengwa na wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania katika kijiji cha Katumba  mkoani Katavi  Agosti 21, 2016 ili kumshukuru Mungu kwa kupewa uraia huo. Kushoto kwake ni mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Raphael Mbuga.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akionyesha Mpango wa Mafunzo ya Ujasiriamali katika jimbo la Nsimbo mkoani Katavi aliouzindua  kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Katumba akiwa katika ziara ya mkoa huo Agosti 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Katumba mkoani Katavi Agosti 21, 2016. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Arusha mteule 
  Bw. Gabriel Fabian Dagarro
  0 0

   Mwanariadha wa mbio ndefu wa Tanzania Alphonce Felix Simbu (24) leo ametia fora kwa kushika nafasi ya 5 kwenye siku
  ya mwisho ya michuano ya Olimpiki katika mashindano ya marathon jijini Rio de Janeiro nchini Brazil. Alitumia saa 2:11:15, sekunde 11 nyuma ya mshindi wa nne Ghirmay Ghebreslassie.
  Mkenya Eliud Kipchoge ndiye aliyeibuka mshindi na kunyakuwa medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa wanaume. Feyisa Lilesa wa Ethiopia alimaliza wa pili akiwa nyuma ya Kipchoge kwa sekunde 70 na  kushinda medali ya fedha huku Mmarekani Galen Rupp akimaliza wa tatu na kujishindia medali ya shaba.  0 0  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kagera, pindi alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, tayari kwa kukutana na Watumishi wa Umma mkoani Kagera, leo Jumatatu, Agusti 22, 2016.

  0 0

  Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi.

  Kufuatia vyombo vya habari mbalimbali nchini kutoa habari ambayo inamhusu Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi kuwa anatakiwa kufika mahakamani Agosti, 24 mwaka huu kujieleza kwanini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya kulipa Dola 598,750 (Bil. 1.20), wakili wa Dk. Mengi, Deogratias Ringia amekanusha habari hiyo.

  Katika taarifa ambayo imetolewa na wakili Ringia, amesema kuwa akiulizwa na watu mbalimbali kama ni kweli kuna hati imetolewa na Mahakama Kuu ikimtaka mteja wake Dk. Mengi kufika mahakamani kujieleza kwanini asifungwe baada ya vyombo mbalimbali kuripoti kuwa anatakiwa kufika mahakamani lakini jambo hilo halina ukweli.

  "Mhusika mkuu katika kesi hiyo ni kampuni Inayoitwa KM Prospecting Limited ambayo Dk. Mengi siyo mwanahisa wala mkurugenzi katika kampuni hiyo. Kampuni hiyo ndiyo iliingia kwenye mkataba na wadai iliyopelekea kesi hiyo ya madai," alisema Ringia.

  Ringia alisema hatua ya kumuunganisha Dk. Mengi katika kesi hiyo lilikuja baada ya mahakama kuamua hoja mbili zinazohusu kesi hiyo ndipo wadai ambao ni wafanyabiashara Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo kumuingiza Dk. Mengi katika kesi licha ya kuwa hausiki.

  Baadhi ya vyombo vya habari vilivyoandika habari hiyo ni pamoja na gazeti la Jambo Leo, Daily News, The Citizen na mtandao wa Habari Leo Online.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mh. Paul William Mtima Akikata utepe katika Uzinduzi Wa kampuni ya Mobisol kwa nyanda za juu kusini hivi katibuni iliyopo Soweto Block "C" Jijini Mbeya.

   

   Mobisol ni kampuni yenye asili ya Ujerumani inayoongoza kwa kutengeneza, kusambaza na kuuza Mitambo ya Umeme wa Jua (Sola) iliyo salama kiafya na mazingira katika ubora wa hali ya juu, Ikiwa mbadala wa nishati isiyo salama  kwa gharama nafuu kwa watu wa vipato vyote.

  Mchezaji wa timu ya Ilemi Fc, Rajabu Jezi ya bluu bahari akijaribu kuwatoka wachezaji wa timu ya Msumari wa Moto katika mchezo ulio chezwa hivi karibuni katika viwanja vya shule ya msingi mwenge na kutoka sare ya bila kufungana  ikiwa ni muendelezo wa ligi ya Mobisol inayo endelea hivi sasa mkoani mbeya kwa udhamini mkubwa wa Mobisol Mabingwa wa nishati ya umeme wa Jua "Sola" Tanzania.

  Kwakutambua na kupenda kuendelea kuenzi mahusiano mazuri na Wakazi wa Nyanda za juu kusini, Mobisol  Mobisol ambao ndio wadhamini wakuu wa Ligi ya Mobisol Cup iliyoshika Kasi jijini Mbeya Ikihusisha Timu 20 Kutoka Mbeya Jiji, Mbeya Vijijini  na Wilaya ya Chunya, Tarehe 13/08/2016  Ilifanya ufunguzi rasmi wa kuanza kufanya kazi Kanda ya nyanda za juu kusini uliofanyika Katika ofisi zao za kanda zilizopo Soweto Block C mkabala na jengo la Oilcom.

  Mtanange Ukiendelea kwa udhamini mkuu wa Mobisol

older | 1 | .... | 1327 | 1328 | (Page 1329) | 1330 | 1331 | .... | 3272 | newer