Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

DC KASESELA AKUTANA NA MASELA WA KIHESA, MJINI IRINGA, APIGA JALAMBA NA MGAMBO

$
0
0
Katika kupunguza kasi ya uhalifu na kuwawezesha Vijana wa Iringa, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alikutana na vijana wa kijiwe cha Kihesa, ambao wengi wao wanajishughulisha na kuosha magari na kuwaomba kusaidiana naye katika kutokomeza udokozi.

Vijana hao walimuomba Mkuu wa Wilaya awasaidie upatikanaji wa mashine ya kuoshea magari ambayo aliwahidi kuwatafutia ndani ya siku 2 ili mradi wajiunge kwenye kikundi na wafungue akaunti benki. Vijana hao walimsukuru sana mkuu wa wilaya na kuahidi kuwa watiifu wa sheria na kuchapa kazi. Kikundi hicho kina vijana 25.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akifanya mazungumzo na Kikundi cha vijana 25 wanaojishughulisha na uoshaji wa magari katika eneo la Kihesa, Mjini Iringa.
Kasesela akipitia taarifa ya Kikundi hicho aliyokabidhiwa.
Akitoka eneo hilo baada ya kumaliza kuzungumza na vijana hao.


MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WATENGENEZA AJIRA KWA WAJASILIAMALI VIJIJINI KUPITIA MRADI WA MADAWATI

$
0
0
Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Bulayanhulu Sara Teri (kulia)  na Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulayanhulu Elias Kasitila wakikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Nyangw’ale.
Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Geita ,Elias Kasitila akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na mgodi huo kwa ajili ya shule zilizoko katika wilaya ya Nyang'wale.
Utengenezaji wa Madawati ulitoa fursa ya ajira kwa fundi Deus Mlela aliyepewa tenda na Mgodi wa Bulyahulu ya kutengeneza madawati mia tano.

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NCHINI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh. Yahel Vilan alimpomtembelea Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akijadiliana jambo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh Yahel Vilan alimpomtembelea Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni Maafisa toka Wizara ya mambo ya nje waliongozana na Balozi huyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akisoma Nakala za machapisho alizopatiwa na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh . Yahel Vilan.

YANGA KUANZA KUJIFUA KESHO, KUIFUATA MAZEMBE JUMAPILI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KIKOSI cha Yanga  kesho kitaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Uhuru kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya TP Mazembe unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumanne  katika Mji wa Lubumbashi nchini Demokrasia ya  Congo.

Mchezo huo utachezwa saa nane na nusu mchana kwa saa za Congo na unatarajiwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka nchi tofauti wakiongozwa na mwamuzi wa kati kutoka nchini Angola.

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini siku ya Jumapili kuelekea Lubumbashi Congo. kikiwa na wachezaji 21 pamoja na benchi la ufundi huku kesho hiyo majibu ya daktari yatatoka juu ya wachezaji majeruhi waliopo kwneye kikosi hicho cha wanajangwani.

Majeruhi ni Obrey Chirwa, Juma Abdul, Ally Mustapha 'batez', Geofrey mwashiuya, Nadir Haroub 'Canavaro' Juma Mahadhi aliyeumia katika mchezo wao dhidiya Azam wa Ngao ya Hisani na Kelvin Yondani.

Waamuzi wa mchezo huo ni Ref. Helder Martins De Carvalho(Angola), A.I  Jean Claude Birumushashu(Burundi), A.II Arsenio Chadreque Marengula(Mozambique), R.R. Antonio Muachihuissa Caxala(Angola), M.C Gerges Rodolphe Bibi(Seylsius), R.A Ali Mohamed Ahmed(Somalia) na GC Russell Paul (Rep.of South Africa)

Yanga katika kundi lao wanashikilia mkia wakiwa na alama nne huku TP Mazembe akiongoza kwa kuwa na alama 10 akifuatiwa na ,edeama yenye alama nane na Mo Beajaia alama tano.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WAKADIRIAJI MAJENZI AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika.
Rais wa Chama Cha wakadiriajiMajenzi Afrika Prof. Robert Pearl akihutubia mkutano wa Wakadiriaji Majenzi uliofanyika kwenye hotel ya Golden Tulip.
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Viongozi wa Chama cha Wakadiriaji majengo mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
.......................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na waepuke vitendo vya rushwa katika mchakato wa ukadiriaji majengo nchini.Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 18-Aug-16 wakati anafungua mkutano wa mwaka wa wakadiriaji majenzi kutoka nchini mbalimbali za Afrika jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mchakato wa kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge) na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania na suala la kuhamia Makao Makuu Dodoma hivyo ni muhimu kwa wakadiriaji majenzi wakajipanga vizuri katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa kwa kuweka gharama nafuu kulingana na hali halisi ya mradi unaotakiwa kujengwa.

Amesema serikali inatambua mchango wa watalaamu wa ukadiriaji majenzi hivyo ni muhimu kwa wataalamu hao wakauongeza bidii katika utekelezaji wa kazi zao hasa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa.Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amehimiza ushirikiano kati wakadiriaji majenzi wa Tanzania na wa nchi nyingine za Afrika katika kubadilishana uzoefu kwenye kazi zao ili kuongeza ubunifu na ufanisi katika miradi wanayopata.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema serikali imetenga dola bilioni 2.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na bandari na viwanja wa ndege hivyo serikali inahitaji wakadiriaji majenzi waadilifu katika utekelezaji wa miradi hivyo na sio vinginevyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MKUU WA WILAYA KINONDONI,HAPI ATEMBELEA HOSPITALI MWANANYAMALA.

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi alipotembelea katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.

*Abaini gharama ya kadi ya wagonjwa kupandishwa hadi 10,000/= bila kufuata utaratibu.
*Aagiza kusitishwa mara moja
*Mganga mfawidhi kuchukuliwa hatua

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi leo asubuhi amefika katika hospitali ya Mwananyamala akiambatana na Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni na mganga Mkuu wa Kinondoni. Hapi amefika hospitalini hapo na kuongoza moja kwa moja kwenye dirisha la malipo ambapo imebainika kuwa gharama za kadi ya mgonjwa zimepandishwa bila kufuata utaratibu na kufikia shilingi 10,000 kwa mgonjwa kumuona daktari.  

Hapi ameyabaini hayo licha ya taarifa ya uongo iliyotolewa na msimamizi wa dirisha la malipo kuwa wamesitisha kutoza kiasi hicho .

Mkuu huyo wa wilaya alimuagiza mtaalam wa Max Malipo kufungua kompyuta yake na kuangalia ni kiasi gani ambacho wagonjwa waliofika saa 1 asubuhi leo walitozwa. Baada ya mtaalam huyo wa Max Malipo kufungua ikabainika kuwa wagonjwa wote walitozwa shilingi 10,000/=.

"Hivi wewe dada kwanini ulikua unanidanganya? Unadhani mimi ni mjinga? Unadhani nimekuja hapa kwa bahati mbaya? Najua kila kitu mnachofanya hapa. Ndio maana nikaitwa Mkuu wa Wilaya. Usirudie kunidanganya tena..." alisema Mh Hapi.

Baada ya kuzungumza na wagonjwa walioeleza kilio chao kuwa bei za vipimo pia zimepandishwa kinyemela, mkuu wa wilaya ameagiza Mkurugenzi na mganga mkuu kupitia maamuzi yote ya upandishwaji wa gharama bila kufuata utaratibu na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ili watu masikini wasishindwe kupata huduma.

"Wananchi masikini hawawezi kumudu gharama ya shilingi 10,000/= kwa kadi. Hii ni hospitali ya serikali na sio binafsi. Naagiza utaratibu ufuatwe na bei hii isitishwe kutumika mara moja. Badala yake bei ya awali iendelee. Huu ni uchonganishi mkubwa unaolenga kuwafanya wananchi waichukie serikali yao. Hatuwezi kuvumilia."

Naye Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni bwana Aron Kagurumjuli alieleza kuwa tayari amechukua hatua ya kumvua wadhifa wake mganga mfawidhi wa hospitali ya Mwananyamala kuanzia leo hii. Gharama mpya za daktari kuona mgonjwa zinatajwa kupandishwa kutoka shilingi 6,000 hadi 10,000/= kwa mgonjwa kuanzia tarehe 1 Ogasti mwaka huu.

SAMATTA KAZINI TENA LEO EUROPA LEAGUE na TIMU YAKE KRC Genk ya Ubelgiji

$
0
0
Kwa hisani ya Bin Zubeiry

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo anatarajiwa kuiongoza timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji katika mchezo wa kwanza hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya kuingia kwenye makundi ya Europa League dhidi ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia.

Genk wamesafiri hadi Zagreb kwa mchezo wa kwanza leo, wakati marudiano yatakuwa Alhamisi ya Agosti 25 Uwanja wa Luminus Arena, Genk na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi moja kwa moja, ambako atapangwa na vigogo wa Ulaya.
Genk imefika hatua hii baada ya kuitoa Cork City FC ya Ireland kwa ushindi wa jumla wa 3-1, baada ya kushinda 1-0 nyumbani na 2-1 ugenini.


Na Genk wataingia kwenye mchezo huo wakitoka kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Waasland-Beveren Jumamosi na kufungwa 1-0 ugenini na Gent Uwanja wa Ghelamco-Arena mjini Gent katika mfululizo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.

Samatta ambaye Desemba 13 mwaka huu atafikisha miaka 24, alijiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, iliyomtoa Simba SC ya Tanzania mwaka 2011.
Na baada ya mafanikio makubwa akiwa na klabu ya Lubumbashi ikiwemo kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo sambamba na kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, Samatta akahamia Ulaya Januari mwaka huu.
Na tangu atue Genk, Samatta amecheza jumla ya mechi 25 za mashindano yote, zikiwemo 18 za msimu uliopita na tatu za msimu huu hadi sasa, kati ya hizo nne ni za Europa League msimu huu.
Katika mechi hizo ni 10 tu ndiyo alianza, nyingine zote akitokea benchi na ameweza kufunga mabao saba, moja tu katika Europa League.

MHE. UMMY MWALIMU AMUAGA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUGHULIKIA IDADI YA WATU DUNIANI (UNFPA) LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni Dk. Natalia Kanem (wa pili kutoka kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) mara baada ya kufika Ofisini kwake kumuaga leo jijini Dar es salaam.Wengine alioambatana nao ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) kuhusu machapisho mbalimbali ya Umoja yanayoelezea Maendeleo ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa Shirika hilo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.)akiangalia moja ya chapisho la lenye Mipango ya Umoja wa Mataifa mwaka 2016 -2021 alilokabidhiwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (katikati) , Mwakilishi Mkazi wa UNFPA anayemaliza muda wake hapa nchini Dk. Natalia Kanem (wa pili kutoka kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionesha chapisho la lenye Mipango ya Umoja wa Mataifa mwaka 2016 -2021 leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.


Na. Mwandishi Wetu - Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) amemuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa Shirika hilo. 


Akizungumza na mwakilishi huyo Ofisini kwake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy ameeleza kuwa Serikali itaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Sera, miongozo na sheria mbalimbali zinazohusu usawa wa jinsia na haki za watoto hususan watoto wa Kike.

Amesema Serikali itaendelea kufanya kazi na kushirikiana na UNFPA pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya Tanzania.

Ameleza kuwa wizara yake itaendelea kuhakikisha kuwa tatizo la ukatili dhidi ya watoto linalohusisha ndoa na mimba za utotoni, ubakaji na ulawiti kwa watoto linamalizika katika jamii ya watanzania

Aidha,amesema kuwa wizara yake itaendelea na juhudi za kupunguza vifo vya mama wajawazito kwa kuweka miundombinu na mazingira bora ya kujifungulia huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuelimisha na kuhamasisha umma wa watanzania juu ya umuhimu wa kuzingatia uzazi wa mpango.

Kwa upande wake Dk. Natalia Kanem ambaye alikua ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliyompatia katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini na kuahidi kuendeleza kudumisha mashirikiano hayo atakapokuwa Makao Makuu ya Shirika hilo.

MAONESHO YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI 2016 KUFANYIKA ROCK CITY MALL JIJINI MWANZA.

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema (wa pili kushoto), akitoa ufafanuzi hii leo Jijini Mwanza kuhusiana na Maonesho ya Wafanyabiashara Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Agost 26,2016 hadi Septemba 04,2016 katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.


Wengine ni, Hassan Karambi ambaye ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza (wa kwanza kushoto), Tungu Misululu, Makamu Mwenyekiti TCCIA kitengo cha Biashara mkoani Mwanza (wa pili kulia) na Majid Igangula (wa kwanza kulia), kutoka bodi ya Washauri TCCIA.

Makampuni pamoja na wajasiriamali mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, yametakiwa kutumia Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki katika kutangaza na kuuza bidhaa zao.

Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema, ametoa rai hiyo leo Jijini Mwanza, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na Maonesho hayo.

"Maonesho haya yanatoa fursa kwa makampuni mbalimbali Afrika Mashariki kujitangaza, kukutana na wateja wao, kutafuta wabia wapya wa kibiashara pamoja na kufanya utafiti wa kimasoko". Ametanabaisha Lema.

Maonesho hayo yanatarajiwa kuanza agost 26,2016 hadi Septemba 04,2016 katika viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza na yanatarajiwa kushirikisha wafanyabiashara kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na nje ya Afrika Mashariki.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema (katikati), akiwa katika mkutano na wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na Maonesho ya Wafanyabiashara Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Agost 26,2016 hadi Septemba 04,2016 katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.

Wengine ni, Hassan Karambi ambaye ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza (kushoto), Tungu Misululu, Makamu Mwenyekiti TCCIA kitengo cha Biashara mkoani Mwanza (kulia).
Wanahabari Jijini Mwanza, wakiwa katika Mkutano wa TCCIA kuhusu Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki Jijini Mwanza, uliofanyika leo.
Wanahabari wakiwa katika mkutano huo
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari.
Taswira ya Mkutano wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA, na Wanahabari ulioketi hii leo Jijini Mwanza, kuhusu Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashari yanayotarajiwa kuanza Agost 26 mwaka huu viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza.

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG

Msimu wa pili wa kambi tiba ya GSM Foundation wafungwa rasmi Iringa, maisha ya watoto 37 yaokolewa

$
0
0

Kambi tiba ya GSM iliyokuwa imeingia katika msimu wake wa pili tangu Agosti mosi mwaka huu, imefungwa rasmi mkoani Iringa, huku watoto 37 wakiwa wamefanyiwa upasuaji, na wengine zaidi ya 300 wakipata ushauri nasaha kutokana na afya zao kutoruhusu kufanyiwa upasuaji, huku suala la uimara wa afya likiwa kipaumbele cha kwanza.

Awali akiongea kabla hajamkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Bi Amina Masenza kuongea, Msemaji wa Taasisi ya GSM, Khalfan Kiwamba alisema kila kukicha wanashukuru kuona maisha ya watoto ambao ilikuwa wapate mtindio wa ubongo ama kupoteza maisha yanaokolewa kupitia mchango wao pamoja na madaktari kutoka Taasisi ya ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili, MOI.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI kwa mwaka 2002, unasema zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na vichwa vikubwa na migongo wazi, na kati yao ni 500 tu wanaoweza kufika hospitali na kupata matibabu kutokana na changamoto kuu tatu.

Ya kwanza ni uhaba wa madaktari bingwa wa upasuaji wa vichwa vikubwa na vikubwa na migongo wazi ambapo kwa tanzania nzima, kwa sasa wamebaki saba tu, huku sita wakiwa ni waajiriwa wa Taasisi ya MOI na mmoja akiwa hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza.

Kutokana na uhaba huo wa madaktari, ambao wanapatikana katika mikoa miwili tu ya Tanzania, Mikoa mingine ambayo watoto wa aina hii huzaliwa wagonjwa hupata changamoto ya pili ya kusafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu ambapo hata hivyo, wakifika huko hupata changamoto ya kukuta foleni ya wagonjwa kutoka mikoa mingine wanaokuwepo kutoka mikoa mingine.

Kuna imani pia za kishirikina ambapo watoto wengi hupelekwa kwa waganga, wakihisi labda wamelogwa, wakati hili ni tatizo la kiafya ambalo mtoto akiwahishwa anaweza akawahishwa hospitali na akapona,

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa, Bi Amina Masenza amewaomba GSM Foundation warudi tena iringa kwani anahisi wagonjwa waliotibiwa kutoka mkoa wake ni wachache sana, ukilinganisha na idadi anayoijua ya watoto waliomo mkoani humo.

Mkuu huyo ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha kwamba wanajua idadi ya wagonjwa waliomo katika wilaya zao ili waeze kuwatayarisha kwa ajili ya matibabu kabla hajawasiliana na wataalamu ili kulimaliza tatizo hilo kama sio kulimaliza kabisa.

PICHANI JUU: Msemaji wa GSM Foundation, Khalfan Kiwamba `Kiwadinho',(Kulia) akiongea na wanahabari(Hawapo pichani), huku akishuhudiwa na Meneja wa Meneja wa Taasisi hiyo Shannon Kiwamba(Wa kwanza kushoto), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Robert Salim(wa Pili kutoka kushoto, na Kibwana Matukio kutoka GSM Foundation(Mwenye Miwani).
 Mkuu wa Mkoa wa iringa, akimjulia hali mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na Kambi tiba ya GSM Foundation.
Dk Mwanaabas Sued kutoka Taasisi ya MOI, akiongea na wanahabari(Hawapo pichani), huku akishuhudiwa na Afisa Miradi kutoka GSM Foundation Kibwana Matukio(wa Kwanza kushoto) Dk John Mtei kutoka MOI,(wa Pili kutoka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto).

Madaktari Bingwa waendelea kuwahudumia wananchi Singida

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amezindua rasmi huduma tembezi za madaktari bingwa Mkoani Singida, na kuwasihi wananchi Mkoani Singida kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa. 

Huduma hizo za kibingwa zilizozinduliwa Wilayani Iramba katika hospitali ya Kiomboi zitahusisha huduma za kibingwa za upasuaji, meno, macho, upasuaji wa mifupa, huduma za kibingwa za magonjwa ya watoto, wanawake na huduma za kibingwa za mionzi. 

Mhandisi Mtigumwe amesema matarajio ya Mkoa ni kuwa huduma tembezi za kibingwa zitasaidia kutambua na kutibu magonjwa mbalimbali kabla hayajafikia hatua ya usugu na kupunguza gharama za rufaa za wagonjwa kwenda nje ya mkoa. 

'Huduma tembezi za kibingwa zitawasaidia wananchi kutambua uwepo wa huduma za kibingwa katika mkoa wa singida na kupata matibabu kwa gharama nafuu' amengeza Mhandisi Mtigumwe. 

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki akisoma taarifa ya hali ya afya Mkoa wa Singida amesema wazo la kuanzisha huduma tembezi za kibingwa limetokana na idadi kubwa ya operesheni zilizofanyika kwa mwaka 2015/2016 na pia mkutano wa wadau wa afya mkoani hapa kuafiki wazo la kuanzisha huduma hiyo. 

"Kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 jumla ya operesheni kubwa na ndogo 4,836 zimefanyika katika hospitali mbalimbali mkoani hapa, aidha Idara ya macho katika hospitali ya Mkoa imefanya jumla ya operesheni kubwa na ndogo 2,020" ameongeza Dokta Mwombeki. 

Dokta Mwombeki amesema uwepo wa madaktari bingwa 11 mkoani Singida pia umekuwa chachu ya utekelezaji wa huduma hiyo huku Mkoa ukifanya jitihada za kuazima madaktari wengine katika mikoa jirani ya Dodoma na Manyara. 

Baadhi ya wagonjwa waliohudhuria katika siku ya kwanza ya zoezi hilo huku huduma hiyo ikitarajiwa kufanyika kwa muda wa siku tano wilayani hapo wameeleza shauku na furaha yao ya kusogezewa huduma za kibingwa katika halmashauri zao. 

"Nilikuwa naumwa jino ambalo limeota vibaya, niliambiwa nitaweza kufanyiwa operesheni katika hospitali kubwa kama Muhimbili lakini hawa madaktari wametusaidia , nimepata huduma haraka na kwa gharama nafuu, nawasihi wenzangu waje kwa wingi" amesema Bi Neema Josseph Mkazi wa Kijiji cha Kizaga Wilayani Iramba. 

Naye Mzazi wa mtoto Jonas Masaka amesema huduma za kibingwa zitamsaidia mtoto wake mwenye matatizo ya macho na hiyo kumpunguzia gharama ya kumpeleke katika hospitali kubwa kutibu tatizo la macho linalomsababisha mtoto huyo kushindwa kusoma vizuri. 

Huduma ya tembezi za kibingwa Mkoani Singida zitafanyika katika Wilaya zote tano za Mkoa nwa Singida na hvyo kupunguza wagonjwa wa rufaa watakaopelekwa hospitali za Bugando, KCMC na Muhimbili.
Baadhi ya wakazi wa Iramba waliojitokeza siku ya siku ya kwanza ya huduma tembezi za kibingwa.
. Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akihutubiwa wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma tembezi za madaktari bingwa Mkoani Singida.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida John Mwombeki akisoma taarifa ya hali ya afya Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi wa huduma tembezi za kibingwa
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho akimhudumia mteja siku ya kwanza ya huduma tembezi za kibingwa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Meno akimhudumia mteja siku ya kwanza ya huduma tembezi za kibingwa.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKABIDHI BAJAJ KWA MLEMAVU THOMAS KONE, 18 AUGUST 2016

$
0
0
Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsalimia  Bw. Thomas Kone (35) akiwa makao makuu ya TBC 1 alikuoitwa kukabidhiwa   Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alimuona kwneye kipindi cha TV   katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone.

 Kaimu Mnikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi funguo na nyaraka Bw. Thomas Kone (35) kwa ajili ya Bajaji mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumuona katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone. Hafla hii fupi imafanyika makao makuu ya TBC 1 Mikocheni jijini Dar es salaam leo Agosti 18, 2016
 Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimwangalia Bw. Thomas Kone (35) akipanda  Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alimuona kwneye kipindi cha TV   katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone. Hafla hii fupi imafanyika makao makuu ya TBC 1 Mikocheni jijini Dar es salaam leo Agosti 18, 2016
 Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimwangalia Bw. Thomas Kone (35) akiujaribu  Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alimuona kwneye kipindi cha TV   katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone. Hafla hii fupi imafanyika makao makuu ya TBC 1 Mikocheni jijini Dar es salaam leo Agosti 18, 2016.

Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

INTRODUCING "MISENGENYO" NEW JOINT KUTOKA KWA AT & Peter Msechu

GP MANGU AWAAGA ASKARI 14 WA KIKOSI MAALUM CHA POLISI (S.F.U)

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akimuuaga PC Prosper Yenda yenda wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi ( S.F.U) ambaye ni miongoni mwa askari 14 wanaokwenda nchini Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiwa katika picha ya pamoja na askari 14 wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi (S.F.U) ambao wanaokwenda nchini Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu. (Picha na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi).

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVIEHNI

$
0
0

SIMU.TV:  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Salumu Happy ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya Mwananyamala kwa kupandisha bei ya matibabu kinyume na utaratibu. https://youtu.be/S3ZIe2CIrTI

SIMU.TV:  Rais Dr John Pombe Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika mashariki amekutana na katibu mkuu wa jumuiya hiyo balozi Liberata Mfumukeko na kujadili namna ya kukabilina na matatizo ya jumuiya hiyo.https://youtu.be/bWf6alU0mFw

SIMU.TV:  Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa wilaya na maafisa elimu nchini kufanya ukaguzi wa wanafunzi katika shule zote ili kubaini udanganyifu wa idadi ya wanafunzi. https://youtu.be/9EVcmk2RaV0

SIMU.TV:  Wakazi wa mji mdogo wa Hydom wilayani Mbulu wamekua wakitaabika na upataikanaji wa huduma ya maji huku mkandarasi wa mradi wa maji akitokomea kusikojulikana. https://youtu.be/X6Qrb_yA94Y

SIMU.TV:  Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani likishirikiana na kampuni ya Makini Application wamezindua huduma ya kumuwezesha abiria kujua mwendo wa gari alilopanda kwa kutumia simu yake ya mkononi. https://youtu.be/hHr3rZsTyzI

SIMU.TV:  Chama cha wamiliki wa mabasi nchini TABOA kimesema kitasitisha huduma ya usafiri kuanzia agosti 22 kwa ajili ya kupisha zoezi la ukaguzi wa mabasi.https://youtu.be/dL1-laXQa_o

SIMU.TV:   Wafugaji wa jamii ya Kimang’ati wanaoishi katika wilaya ya Bagamoyo wameiomba serikali kukaa nao na wakulima ili kumaliza migogoro yao na wakulima.https://youtu.be/zD_WUjdiTtw

SIMU.TV:  Wafanyabiashara na wavunaji wa misitu nchini wametakiwa kufanya kazi hiyo kwa utaratibu wenye tija kwa taifa na kwa vizazi vijavyo. https://youtu.be/FmHbflWIgH8

SIMU.TV:  Wafanyabiashara wadogo wa mazao wameiomba serikali kusimamia bei za mazao kutokana na baadhi ya mazao kutokua na bei yenye msimamo.https://youtu.be/jfFsUvV76-4

SIMU.TV:  Mfuko wa hifadhi ya jamii wa LAPF imeeleza nia yake ya kuwekeza katika viwanda vidogo vyenye tija baada ya kufanya upembuzi yakinifu.https://youtu.be/TcbGX_0Hzts

SIMU.TV:  Klabu ya soka ya Ndada fc kutoka mkoani Mtwara inatarajia kusafiri kuja jijini Dar es Salaam kuivaa timu ya Simba siku ya jumamosi huku ikitanba kushinda katika mchezo huo. https://youtu.be/UX5iASdbTT4

SIMU.TV:  Bingwa wa mbio za mita 3000 na kuruka viunzi kutoka Kenya Ezekieli Kimboi aliyeshinda nishani ya shaba amenyang’anywa nishani hiyo baada ya Ufaransa kukata rufaa ya ushindi wake. https://youtu.be/1_5Kngkn1tw

SIMU.TV:  Chama cha mpira wa miguu wilayani Manyoni mkoani Singida MADIFA kinafanya maandalizi ya kufanya uchaguzi wa viongozi wa ngazi za juu za chama hicho.https://youtu.be/hBpmTx76Qdk

SIMU.TV:  Mchezaji Ryad Mahrez amesaini mkataba na klabu yake ya Leicester city na kukata mzizi wa fitina wakudhaniwa kuwa ataondoka katika klabu hiyo.https://youtu.be/J8dteeQZq_s

KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


AGIZO LA DKT. Kigwangalla Hamisi, NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KWA MA-DED NA MA-DMO WOTE NCHINI. KUTOKA MWANDOYA HEALTH CENTER, MEATU. SIMIYU.

$
0
0

Leo nimeamua kuchukua uamuzi wa kutoa agizo kali kabisa toka nimeteuliwa. 

Najua litazua maswali, lakini Kwa kuwa litaokoa maisha ya wanawake wajawazito wa nchi yetu (CEmOC) na wananchi wengine, nimelitoa. Nitalitetea. Nitalisimamia!


Nimeagiza maDED na maDMO wote nchini kuhakikisha wana theatres ZENYE KUFANYA KAZI IPASAVYO kwenye vituo vyote vya Afya kwenye maeneo yao. Wiki iliyopita nilitembelea Manispaa ya Ilala, kwenye vituo vya afya vitatu nilivyotembelea hakukuwa na theatre yenye kufanya kazi. 
Kwa mujibu wa sera ya afya ya Tanzania, 'kituo cha afya' kitakuwa na hadhi hiyo kama kina uwezo wa kufanya upasuaji. Vinginevyo hiyo ni zahanati. Mara nyingi watendaji hawa wamekuwa wakijificha kwenye kichaka cha 'hatuna fedha', wengine wakiomba fedha kutoka serikali kuu.
Nilimuuliza Mkurugenzi wa Ilala, unakusanya sh ngapi Kwa mwezi, akasema bilioni 6. Nikamuuliza unadhani ni sh ngapi kuwa na theatre yenye kufanya kazi? Akakosa jibu. Nikampa miezi 6 awe na theatre zenye kufanya upasuaji.
Leo nimefanya ziara yangu mikoa ya Shinyanga na Simiyu, nikitimiza mikoa 24. Huku pia nimekutana na tatizo hilo hilo nilipokuwa Kishapu, Shinyanga na Mwanhuzi, Simiyu. Hawa wa Meatu wenyewe wana kituo cha Afya Mwandoya, takriban Km 60 kutoka Hospitali ya Wilaya ya Meatu, pale Mwanhuzi. Wamekipa uwezo wa kufanya upasuaji. Wamenunua vifaa, wameajiri hadi Daktari (MD) kwa ajira ya muda kwa ajili ya kufanya kazi pale. Kituo kimefanya takriban operation 40, zote salama Kwa asilimia 100. Wamepunguza msongamano Mwanhuzi na wamepeleka huduma nyeti na za kuokoa maisha Karibu zaidi na wananchi, ukizingatia huku hakuna barabara za lami na hakuna ambulances. I was impressed.



Nikasema sababu za kuwa Halmashauri hazina pesa huku zinakusanya mamilioni ambayo wanayatumia bila ku-address matatizo ya msingi ya wananchi hazikubaliki. Leo iwe mwisho. Nimeagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini washirikiane na maDMO wajue watakavyofanya wahakikishe wanafungua huduma za upasuaji kwenye vituo vyote vya afya nchini ndani ya miezi sita (6).

Baada ya miezi hiyo sita mimi mwenyewe na timu yangu ya kurugenzi ya ukaguzi na uhakiki ubora wa huduma za afya (inspectorate and quality assurance) tutasambaa nchi nzima kukagua huduma hizi na pale ambapo hatutozikuta tutakishusha hadhi kituo hicho kutoka ngazi ya 'kituo cha afya' na kuwa ngazi ya 'zahanati' sambamba na kuwashauri wenzetu wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuwa wakuu hao wa idara wameshindwa kutekeleza majukumu yao na hivyo wawashushe vyeo.

Nitasimamia uamuzi huu Kwa nguvu zangu zote. Sababu ni kwamba ninajua faida yake. Ninajua Mungu atafurahi, atanibariki.



Wakati wa Bunge la bajeti wanaharakati wa haki za wanawake na Watoto waliwahamasisha Wabunge watushughulikie Kwa ajili ya suala hili. Wakawa-pump wabunge data kuwa kwa siku magnitude ya vifo vinavyotokana na sababu za uzazi ni sawa na 'coaster' moja ipate ajali na iue watu wote! Wabunge waligeuka mbogo. Japokuwa namba hizi zilikuwa exaggerated (zilizidishwa), walifikisha point kwetu. Kwamba lazima tufanye kitu tofauti kwenye eneo hili. Mimi naanza kuchukua hatua. Vifo vitokanavyo na uzazi havikubaliki!



Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB., NW-AMJW.
August 18th, 2016.

Benki ya CRDB imekanusha vikali habari kwamba imesimamisha mikopo kutokana na "hali tete ya uchumi wa nchi ".

$
0
0
Benki ya CRDB  imekanusha vikali habari iliyoandikwa leo Agosti 18, 2016 na  gazeti moja la kiswahili la kila siku na kunukuliwa na baadhi ya mitandao ya kijamii na  kumnukuu kimakosa Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Charles Kimei (pichani) kuwa Benki hiyo  “Sasa imesimamisha mikopo kutokana na "hali tete ya uchumi wa nchi ".

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB Bi. Tully Esther Mwambapa, amekanusha  vikali habari hiyo ambayo ameitaja kuwa  inalenga kuwatia hofu wateja wao  wapendwa na kuichonganisha Benki ya CRDB na dola.

“Nachukua fursa hii kuwatangazia wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla kuwa waipuuze taarifa hii na kuwajulisha kuwa Benki inatoa mikopo kama kawaida na tunawakaribisha kuja kukopa ili kwa pamoja tujenge uchumi wa taifa letu”, amesema Bi. Mwambapa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo.

Article 10

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AKUTANA NA MKURUGENZI WA BENKI YA DUNIA NCHINI.

$
0
0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini, Bi. Bella  Bird  kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 18, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Maajliwa akizungumza  na  Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini, Bi. Bella  Bird, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 18, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

INTRODUCING KITABU CHA UCHAWI NI UTUMWA

$
0
0
Ni  Simulizi  la  ukweli  na  lenye  kufundisha, kutoka  kwa  mwanadada  aitwaye  THEOFLIDA  WA  YESU. 
Kitabu  kinapatikana   nchi  nzima  kwenye  vibanda  vya  wauza  magazeti  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  TANO  TU..
Wahi  nakala  yako  mapema, kabla  hazijaisha. Kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  kitabu  hiki 

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images