Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakiongozwa na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda kutembea hatua chache kabla ya kuzindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013. Barabara hiyo, yenye urefu wa kilomita 10.1 inaanzia makutano ya barabara za Rashid Kawawa na Bagamoyo hadi njia panda ya kwenda Africana karibu na uwanja wa kulenga shabaha wa JWTZ Mbezi Beach
Rais Mwai Kibaki wa Kenya akifunua pazia, akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda akizindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.
Vifijo na nderemo baada ya uzinduzi huo. |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi kabla ya kufanya mazungumzo rasmi(official talks)Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha kwa rais Mwai Kibaki baadhi ya Mawaziri waliohudhuria dhifa ya kitaifa ikulu jinni Dar es Salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa Ikulu kwa heshima ya Rais Kibaki aliyeko nchini kwa ziara yaka ya mwisho ya kiserikali.