My dear Michuzi,
Greetings, napenda kumrekebisha mwandishi wa habari aliyeandika habari kwamba gharama za kuunganisha umeme zilikuwa Sh milini mbili na sasa zimepunguzwa na kuwa sh laki nne na elfu arobaini. Hiyo si sahihi gharama halisi kwa sasa ni kama ifuatavyo;
Katika umbali usiozidi mita 30.,
Bei ya punguzo itakuwa ni shilingi 99,000/- kwa umeme wa njia moja na tatu. Hii ni tofauti na bei ya zamani ambayo ilikuwa ni shilingi 455,104.76 kwa njia moja na 912,104.74 kwa njia tatu.
Punguzo hili limetolewa na serikali ili kuhakikisha kuwa wananchi wengi katika mikoa hiyo wanapata huduma ya umeme ili kuharakisha maendeleo katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Badra Masoud
Msemaji TANESCO