Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

MAONYESHO YA MAVAZI YA KIMATAIFA LONDON KUHUSISHA WATANZANIA KWA MARA YA KWANZA LEO

$
0
0

Na Freddy Macha
Maonyesho maarufu ya mavazi ya kimataifa –London Fashion Week- yatamega kitengo chake cha kimataifa kusaidia kutangaza kazi za washoni wapya toka Tanzania ndani ya Ubalozi wetu leo Ijumaa mjini London.
Mada ya maonyesho haya yatakayoendelea kwa juma zima  ni “Swahili Flavour” (Ladha ya Kiswahili). Yametayarishwa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania London na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujenga vipaji na kazi za mavazi za washoni wasiofahamika duniani. 
 Kazi zitakazooyeshwa ni za washoni watatu Christine Mhando (anayetumia jina la ubunifu:  “Chichia London”),  Anna Lukindo ( “Anna Luks”) na Jacquleine Kibacha (“Heart 365”).
Mbunifu Christine Mhando
 Christine Mhando alihitimu chuo cha Usanii cha Kent mwaka 2002 na huhimiza mtindo wa Kanga na misemo na manen ya Kiswahili mathalan “Tongoza” na “Zungumza” kama wajihi wa kazi zake.  Anna Luks aliyesomea shahada yake chuo cha Middlesex, London hutumia vitambaa vya Kitanzania, kushona kwa mikono, kamba kamba, mavazi ya kike na dunia ya kisasa.  Baada ya kujiuzulu toka kazi ya kuajiriwa (kupanga sera)  Jaquileine Kibacha aliamua kufuata ndoto zake za kuwa msanii. Ubunifu wake unaochanganya desturi za kijadi na kisasa kutumia shanga shanga, manyoya ya ndege na mapambo imesanifiwa kutokana na safari aliyoifanya kuishi na Wamasai.
Kina  dada hawa  wanasisitiza kwamba  wana lengo la kukuuza sanaa na ubunifu, utamaduni wa Kitanzania, kutangaza taswira za Kiswahili na sura mbalimbali za Afrika Mashariki.
Kaimu Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga alisema kwamba maonyesho haya ya kimataifa yatakua nafasi kubwa kwa Tanzania kujenga jina  na ni sehemu mahsusi ya kujivunia utamadunina nchi  yetu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>