TAARIFA YA UHAKIKA KABISA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE,INAELEZA KUWA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA IMEUSIMAMISHA UCHAGUZI MKUU WA TFF,BAADA YA ALIEKUWA MGOMBEA WA NAFASI YA URAIS KWENYE KINYANG'ANYIRO HICHO,BW. RICHARD RUKAMBURA KUFUNGUA MASHTAKA KWENYE KESI NAMBA MOJA YA MWAKA 2013,KUPINGA KUENGULIWA KWAKE KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI ULIOPANGWA KUFANYIKA FEBRUARI 24,MWAKA HUU.
KESI HIYO ITAANZA KUSOMWA KWA MARA YA KWANZA FEBRUARI 19.
RUKAMBURA AMBAYE ALIENGULIWA KWENYE HATUA ZA AWALI KABISA ZA MCHAKATO WA UCHAGUZI NA KAMATI YA UCHAGUZI ILIYOKUWA CHINI YA NDUGU LYATO BAADA YA KUBAINIKA KUWA AMEJAZA FOMU MBILI ZA KUWANIA UONGOZI HUKU MOJA IKIWA NI YA KUWANIA URAIS NA NYINGINE UJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI.
LAKINI JANA RUKAMBURA ALIFUNGUA KESI TATU DHIDI YA TFF,MOJA IKIWA NI KUTAKA MAHAKAMA IZUIE UCHAGUZI NA KUPINGA KUENGULIWA KWAKE NA KUTAKA AREJESHWE KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI HUO.
KESI YA PILI AMBAYO BADO HAIJAPANGIWA TAREHE,ANATAKA MAHAKAMA IIZUIE TFF KUTUMIA KIGEZO CHA FIFA CHA KUWANYIMA HAKI WATU WENGINE.NA KESI YA TATU ANATAKA TFF IMLIPE FIDIA KWA SABABU IMEMDHALILISHA KWA KUMUENGUA KWA KIGEZO CHA KUJAZA FOMU MBILI WAKATI ANAEGOMBEA SHARTI AGOMBEE NAFASI MOJA.
''LAKI SABA YANGU WAMECHUKUA NA RISITI NINAZO,LAKI MBILI NILILIPA YA UJUMBE NA LAKI TANO YA URAIS,SASA KAMA SHARTI LAO NI KUGOMBEA NAFASI MOJA KWANINI WASISEME?" ALISEMA RUKAMBURA.
ALIENDELEA KUSEMA ''WAMENIDHALILISHA,MIMI NI MTU MZIMA NA NINA FAMILIA YANGU,NINA DIGRII TOKA MWAKA 2004 NA NILIGOMBEA NA TENGA MWAKA 2008 WAKANIENGUA,LAKINI SAFARI HII SIKUBALI.ALIMALIZA KUSEMA RUKAMBURA.