Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

JAMII YATAKIWA KUJIHADHARI NA MATAPELI WANAOPITA MAOFISINI KUWAHADAA VIONGOZI

$
0
0
Serikali inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hivi karibuni kumezuka kundi la Watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi waandamizi wa serikali na Taasisi nyeti ikiwemo Usalama wa Taifa kujipatia fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi hao.

Watu hao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa maofisa mbalimbali wa wizara, mashirika ya umma na Idara za Serikali zinazojitegemea kuomba pesa ili wawafanye mipango ya kupandishwa vyeo.

Utapeli huo umekuwepo nchini kwa kipindi kirefu sasa , ambapo watu huwapigia simu viongozi wa Taasisi za fedha , Mifuko ya Taasisi za Jamii na watu binafisi wakiomba fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi waandamizi Serikalini wakati si kweli.

Watu hao wamekuwa wakiwatapeli maofisa mbalimbali kuwa wanaweza kuwafanyia mipango ya kupandishwa vyeo endapo watawapatia kiasi cha fedha jambo ambalo halipo katika taratibu za utumishi wa umma.

Utumishi wa umma unazo taratibu zake za kuwapandisha vyeo watumishi wake kulingana na sifa za kada zao na wala haiwezekani kwa viongozi waandamizi kuwachangisha fedha kwa ajili ya kuwapandisha vyeo.

Serikali inawataka wananchi kuwapuuza matapeli hao na watoe taarifa katika vyombo vya dola na usalama mara wapatapo ujumbe wa aina hiyo ili hatua zichukuliwe dhidi yao.

IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI (MAELEZO) DAR ES SALAAM.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>