Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

SERIKALI YAFUNGUA GHALA LA KISASA LA KUHIFADHIA DAWA KATIKA MAKAO MAKUU YA BOHARI YA MADAWA

$
0
0
Picha na Habari na Dotto Mwaibale 
 RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi nchini kufanya msako na kuwafichua watu wote watakaopatikana na dawa za Serikali katika maduka binafsi. Maagizo hayo ylitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa niaba ya Rais Kikwete ambaye angekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za ufunguzi wa ghala la kisasa la kuhifadhia dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya Dawa jijini Dar es Salaam leo. 
 "Natambua kuwa lipo tatizo la dawa na vifaa tiba vya serikali kupatikana katika maduka ya dawa ya watu binafsi jambo ambalo linanikera sana nawaagizeni wachukukieni hatua za kisheria wale wote watakao patikana na dawa hizo" alisema Rais Kikwete. 
 Alisema Serikali haiwezi kuendelea kununua dawa kwa dharama kubwa na zikaishia katika mifuko ya watu wachache badala ya wananchi walio wengi hususani wa vijijini. Alisema Bohari ya dawa iliundwa mwaka 1994, ikiwa na dira ya kufikisha dawa na vifaa tiba karibu na wananchi ambapo tumeambiwa kuwa shughuli za MSD zimepanuka sana hususani uwezo wa maghala umefikia mita za mraba 51,800 na nusu ya hizo ni za kukodisha kwa watu binafsi. 
 "Natambua kuwa gharama za ukodishaji wa magahala ni kubwa sana na ni vema MSD ikawa na maeneo yake yenyewe bila kutegemea maghala binafsi" alisema Rais Kikwete. Rais Kikwete alizielekeza Halmashauri husika katika kanda za MSD kuisaidia Bohari ya dawa kupata maeneo mkakati ya uhifadhi wa dawa na maeneo waliyonayo tayari yaweze kupewa haki miliki. Alisema chanjo ni hatua muhimu kwa ajili ya ya afya za mama na mtoto ambapo mpango wa taifa wa chanjo ulianza mwaka 1975 ukiwa unatoa chanjo dhidi ya magonjwa kama KifuaKikuu, Polia, Surua, Dondakoo, kifaduro na Pepo Punda. 

 Alisema magonjwa mengine yaliyongezeka ni kinga dhidi ya Homa ya Ini, Homa ua Uti wa mgongo, nimonia na kinga dhidi ya magonjwa ya kuhara. Rais Kikwete aliongeza kuwa kinga ni haki ya kila mtoto hivyo mahitaji ya chanajo yamekuwa yanaongezeka kwaka hadi mwaka kutokana na ongezeko la idadi ya watu. "Ongezeko la idadi ya chanjo pamoja na ongezeko la aina za chanjo imesababisha kuwa na hitaji kubwa la maeneo ya kuhifadhi chanjo na kuzisambaza" alisema Kikwete. 

 Alisema Utunzaji wa chanjo unahitaji mfumo wa mnyororo baridi hivyo kuhitaji vyumba maalumu vyenye ubaridi, pamoja na gari lenye vifaa vya kutunza ubaridi huo ili kuhakikisha mnyororo baridi. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi alisema ufunguzi wa gahala hilo ni sehemu ya kutekeleza mpango mkakati wa MSD wa kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora unaokubalika na kwa bei nafuu.
 "Mpango huu umeandaliwa kwa kuzingatia Sera ya Afya ya kufikisha huduma bora za afya kwa kila Mtanzania" alisema Mwinyi. Alisema vyumba vya kuhifadhia chanjo na magari maalumu ya kusafirishia chanjo uliozinduliwa vitasaidia katika kutunza na kusafirisha chanjo katika hali ya ubaridi kwa mujibu wa miongozo ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ambayo Tanzania inatekeleza. 
 Alisema ghala hilo linauwezo wa kuhifadhi dawa na vifaa tiba lina mita za mraba 4,280 na kuwa limejengwa kwa msaada wa Serikali ya Marekani na Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na limegharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 4 sawa na takribani sh.bilioni 6.4 za Kitanzania. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani alisema ujenzi wa ghala hilo ni matunda yaliyotokana na safari za Rais Kikwete nje ya nchi hususan Marekani ambapo mei 2 mwaka 2009 akiwa katika ziara nchini Marekani Rais wa nchi hiyo Barack Obama aliahidi kuendelea kutoa misaada katika maeneo mbalimbali likiwemo la kuboresha huduma za kupambana na maradhi ya Ukimwi kupitia shirika la PEPFAR. 
 Alisema moja ya miradi inayoratibiwa na PEPFAR ni ujenzi wa maghala makubwa katika kanda za Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Tanga na Tabora. Mwaifwani alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Kikwete kwani matokeo ya juhudi zake zimeleta matunda ambayo yanaonekana kwa Taifa. 
 Alisema ukamilishwaji wa miradi hiyo utaisaidia Bohari ya Dawa kukomboa jumla ya shilingi za Tanzania bilioni 1 katika mwaka ujao wa fedha ambazo wamekuwa wakilipa kwa ajili ya kukodi maghala ya watu binafsi kwa ajili ya kuhifadhi dawa, vifaa tiba na vitendanishi kabla ya kusambazwa kwa walengwa. 
Alisema Bohari ya Dawa imeendelea kutekeleza jukumu lake la msingi la kusambaza dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya hapa nchini kwa niaba ya Serikali. Aliongeza kuwa katika kutekeleza majukumu hayo Bohari ya Dawa imefanikiwa kufanikisha upatikanaji wa dawa ambapo imefikia kati ya asilimia 70 hadi 75 ya mahitaji dhidi ya asilimia 44 wakati Taasisi hiyo ilipo anzishwa mwaka 1994. 
 Alisema mikoa 10 imeingizwa katika mfumo wa kufikisha dawa moja kwa moja hadi vituo vya afya na mikakati imewekwa ya kuingiza mikoa yote ya Tanzania katika mfumo huo kuanzia julai 2013 na kuwa mkakati huu unazihusu pia hospitali za Wilaya, Mikoa na Hospitali za Rufaa. Mwaifwani alisema MSD imefungua mfumo mpya wa kisasa wa TEHAMA (EPICOR) ili kurahisisha shughuli za usambaji ambao pia umefadhiliwa na USAID.

 Wafanyakazi wa Bohari ya Madawa (MSD), wakiwa kwenye hafla hiyo
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria upokeaji wa  magari  maalumu ya kusafirishia chanjo kwa kuzingatia mnyororo badiri. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF), DK. Jama Gulaid, Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt na Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu. Mbali na kupokea magari hayo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Dk. Mwinyi 
alifungua Jengo la Kisasa la ghala la kuhifadhi dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya dawa Dar es Salaam leo
 Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Donan Mmbando akihutubia kwenye sherehe hiyo.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi, akikata utepe kuashiria kupokea madawa na vifaa tiba vilivyotolewa na Madaktari wa Afrika kwa Serikali. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Tiba wa Madaktari Afrika, Dk.Dilan Ellegale na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani (kulia),akimuelekeza jambo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein 
Mwinyi (kushoto), juu ya ubora wa ghala  jipya la kisasa la kuhifadhia dawa, baada ya kulizindua katika Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mbunge Viti maalum Martha Mlata na Balozi wa Marekani nchini  Alfonso Lenhardt. 
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi  (wa tatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bohari ya madawa  (waliosimama nyuma). Kutoka kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando, Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt, Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani, Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungululile, Mwakilishi Mkazi 
wa Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF), DK. Jama Gulaid na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>