Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Kumbukumbu

$
0
0
Gadi Stephano Nkalang’ango
(11 July 1941-10 February 1980)



Miaka 33 imepita tangu alipotutoka baba Yetu mpendwa Gadi. Alipata ajali akiwa njiani kutoka Morogoro kwenda Dar-es-salaam. Alikuwa amemaliza kazi zake za ukaguzi wa mahesabu katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu ( Zilizopo Morogoro). Ndipo alipopata ajali sehemu ya mlandizi tarehe 08 Februari na kufariki siku mbili baadaye. Kwa kweli pengo lake halilizibiki.  Lakini Mungu ni Mwema ambaye amekuwa akitufariji na kututia nguvu siku hadi siku na sasa tu watu wazima.

Anakumbukwa na Mke wake mpenzi Hellena, Dada yake Magdalena (Mwalimu Kitururu) na wadogo zake Abasi, Naisai, Nambuyu, Nambua, Mwanahawa, Suni, Keto Bakari, Nkalang’ango, Sembua, Kosoni na Mtango.

Pia anakumbukwa sana na Wanawe Wapendwa sana Mramba (Baba Wawili), Neema (Mama Nyamaka), Ididi, Kighenda, Mshighwa (Emmanuel/Baba Alice), Nshighia (Tula/Mama Frida), Martha na Gadi Junior (Samweli) ambaye alizaliwa siku 9 baadaye baada ya baba Kufariki.  Na pia wakwe zake Wapendwa pia wanamkumbuka; Wanoga (Mama Wawili), Kosmas (Baba Nyamaka), Ansila (Mama Gadi) na Abraham (Baba Frida) na Alvin.

Wajukuu wamekuwa wakimtazama tu kwenye picha na kuangalia kaburi la Babu yao mpendwa. Wangependa leo hii wanataniana naye, wanacheza naye na kupewa hadithi za zamani lakini haikuwa mapenzi ya Mungu. Wajukuu hawa wataendelea kumi-miss kampani yake, Praise-God (PG), Praise-Jesus (PJ), Nyamaka, Gisela, Alice, Moses, Gadi, Msogoleka, Frida na Richard (Gadi).

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe [Ayub. 1:21]

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>