Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waaandishi wa habari (hawapo pichani) madawa ya kulevya aina ya bangi yaliyokuwa kwenye moja ya viroba kati ya 20 vilivyokamatwa na Polisi,mkoa Arusha.
MNAMO TAREHE 31/01/2013 MUDA WA SAA 7:30 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA LOSOITI KIJIJI CHA KIMOKUWA WILAYANI LONGIDO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKISHIRIKIANA NA ASKARI MGAMBO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA AITWAYE MANDEGE S/O PAKASI (54) MFUGAJI NA NI MKAZI WA KITONGOJI CHA LOSOITI AKIWA NA MAGUNIA 20 YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI YANAYOKADIRIWA KUWA NA UZITO WA KILOGRAMU 50 KILA MOJA.
TUKIO HILO LILITOKEA MARA BAAADA YA ASKARI HAO KUPATA TAARIFA TOKA KWA RAIA WEMA, AMBAPO INAELEZWA KWAMBA MTUHUMIWA HUYO PAMOJA NA WENZAKE WAWILI WALIKUWA WANASAFIRISHA MADAWA HAYO KWA KUTUMIA WANYAMA AINA YA PUNDA AMBAO WALIKUWA KUMI AMBAPO KILA MMOJA ALIKUWA AMEBEBESHWA MAGUNIA MAWILI.
MARA BAADA YA WATU HAO KUWAONA ASKARI HAO WATUHUMIWA WAWILI WALIKIMBIA NA WAKAFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA MMOJA.
JESHI LA POLISI MKOANI HAPA BADO LINAENDELEA KUMHOJI MTUHUMIWA HUYO HUKU WATUHUMIWA WAWILI WALIOKIMBIA WANAENDELEA KUTAFUTWA. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) LIBERATUS SABAS