habari za leo,
naomba uniwekee mada yangu kwenye mtandao wako.
Naomba kuuliza wizara ya elimu watueleweshe kuhusu maana ya michango ya ushirikishi shuleni kila siku. maana katika shule ya msingi Boko wilaya ya kinondoni imekuwa ni kero kwa watoto na wazazi watoto wanapigwa kwa ajili hilo mfano darasa la saba kila siku asubuhi ni lazima waende na sh. 300 na wanaambiwa ni lazima vinginevyo wanapigwa sasa nimepiga mahesabu kama watoto ni 300 kila siku kila kipindi kinakusanya sh. 300 x 300 = 90,000/= hizo hela zinaenda wapi. ukiuliza wazazi wanasema kwenye kikao cha shule walisema sio lazima kwa hiyo aina maana mzazi asipompa mtoto hela lazima apigwe. Nawaomba Wizara ya Elimu watueleweshe kama ni kitega uchumi cha walimu? au inakuwaje?
Mdau