Meneja uwanja wa Kigoma Elipid Tesha,wa pili kuli akifafanua jambo kwa ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM),uliofanya ziara fupi ya kuukagua uwanja huo na kujionea ujenzi wake unavyoendelea kwa kasi,kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh Issa Machibya akishuhudia tukio hilo adhimu, na shoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM,Martin Shigela,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye, pamoja na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na
Ujenzi ukiendelea.
Mafundi ujenzi wakipaka rangi sehemu ya barabara ya kurukia na kutua ndege mapema jana jioni.
Sehemu ya eneo ambalo linaendelea kupanuliwa ikiwa ni sehemu ya ongezeko ya marekebisho ya kiwanja hicho cha Kigoma
Pichani kati Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo akifafanua jambo mbele ya ujumbe wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa.
Sehemu ya kuruka na kutua ndege ikiwa katika hutua ya mwisho mwisho,Kwa mujibu wa Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo ameeleza kuwa unatarajiwa kukamilika mnamo juni mwaka huu,ambapo kwa asilimia 80 maeneo mengi yatakuwa yamekwishakamilika.
Pichani kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya,akimtambulisha Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana kwa baadhi ya wanachama wa CCM waliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot) kuwapokea,ambapo Mh Kinana na ujumbe wake waliwasili mapema jana jioni kuangalia maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje.
Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya,akipokea Ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana uliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot),kuangalia maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategemewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje.UJumbe huo umewasili mapema jana kutoka jijini Dar kwa njia ya Treni ( reli ya kati),ambako wamekuja kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.