Sehemu ya watuhumiwa wa vurugu za Mtwara wakikamatwa
mmoja baada ya mwingine
Hali ya utulivu inadaiwa kurejea katika wilaya ya Masasi mkoani Mtwara baada ya vikosi vya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na polisi kuungana kuweka ulinzi huku watu zaidi ya 40 wakikamatwa kuhusika na matukio ya vurugu za jana.
Mwandishi John Kasembe anaripoti kuwa kutokana na vurugu hizo waziri mkuu Mizengo Pinda na waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi usiku huu wapo Mtwara wakiendelea na vikao vya kurejesha amani na utulivu mkoani hapo.
Pia inadaiwa mida ya asubuhi leo polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya vijana ambao walikuwa wamefunga barabara na kuwatoza ushuru batili wa shilingi 5000 wenye magari kama sehemu ya kujipatia fedha kwa njia feki.
Mbali ya tukio hilo bado katika mitaa mbali mbali ya Mtwara kwa siku ya leo shughuli zote za uzalishaji mali zikiwemo biashara zimesimamishwa kwa muda ili kukwepa vurugu kama za jana japo shughuli za ibada zimeendelea kwa utulivu zaidi.