Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi kilichoko manispaa ya Mtwara/Mikindani yakoswa koswa kuchomwa moto hii leo kwa kile kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia pamoja na kituo kidogo cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara.
Vurugu hizo zilizoanza jana,leo zimehamia wilayani Masasi mkoani Mtwara ambapo Inasemekana Askari mmoja wa Upelelezi wa jeshi la Polisi Ameuawa baada ya kujiingiza katika kundi na kubainika akiwapiga picha ambapo pia alikutwa na bastola 2 huku Nyumba ya Mbunge wa Masasi(Mama Kasembe),Vifaa vya Mahakama ya mwanzo pamoja na magari ya Halmashauri nayo yateketezwa kwa Moto mchana wa leo katika vurugu za waandamanaji zilizoanzishwa na watu wa Bodaboda.
POLISI walianza kutuliza ghasia hizo na baadae wakazidiwa na kulazimika kupiga mabomu ya machozi na risasi za moto.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka yeyote hadi hivi sasa kufuatia simu za mkono za viongozi wa polisi kutopokelewa ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa katika mji huo ambapo Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki.
Na wameshateketeza nyumba ya mama Kassembe,Mbunge wa Masasi
Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea nguvu. Maaskari na makachero wamewasili Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.
Maandamano hayo ya Vurugu yalioongozwa na Madereva wa boda boda. Risasi za moto na mabomu ya machozi yanapigwa kutawanya watu na tayari nyumba moja imechomwa moto na baadhi ya magari huku Vijana wakizidi kusonga mbele