Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wamepanga kufanya ziara ya kihistoria mkoani Morogoro mwezi wa tatu. Ziara hiyo ya siku tatu waliyoipa jina la Dom mpaka Moro (bata kwenda bata kurudi) inatarajiwa kufanyika sehemu mbalilmbali za mkoa wa Morogoro.
Mratibu wa ziara hiyo Mr AMANI KIZUGUTO ameuambia Mtandao huu ya kwamba taratibu za awali za maandalizi kwa upande mmoja zimekamilika kwani tayari wameshazungumza na mshauri wa wanafunzi (dean of students) katika maandalizi ya awali.
Alisema wanatarajia katika ziara hiyo kutembelea mbuga ya wanyama mikumi,maporomoko ya maji katika milima ya udizungwa huku mazungumzo ya kupitia katika vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo Mkoani Morogoro yakiendelea ili kwenda kufanya nao matukio mbalimbali ya kijamii.
Pamoja na kujadili mambo ya kielimu. haya sasa kazi kwenu wana udom kwa wale mtakaopenda kwenda wasilianeni na mratibu kwa simu namba 0717 3767350769 081122