Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

YALE YALEEEEEE....DAWASCO KINONDONI

$
0
0
Kaka Michuzi,
Pole na kazi,
Ninaomba kama kuna anayefahamu anifahamishe nini cha kufanya kuhusiana na DAWASCO kinondoni.
Mimi ni mteja wao Account 00505204, na ninaishi kwenye nyumba ya kawaida yenye idadi ya watu 7 na niliwekewa mita ya maji kama ilivyo wateja wengine.

Tangu mita ya maji ilipowekwa imekuwa inaleta matatizo kwa mwezi inaonyesha tunapaswa kulipa kati ya TZS 97,000 - 214,511, tumehangaika kuripoti ofisi za Dawasco kinondoni (ofisi iliyoko nyuma ya Airtel HQ) kwa muda mrefu sana na 2010 alikuwepo meneja mwanamke(sikumbuki jina) akaahidi kwa maandishi kwamba tungefungiwa test meter lakini haikufanyika na tulipozidi kufuatilia tukaambiwa amehama na sasa akawepo meneja (Bw. Mtowela) ikabidi tuanze upya story yetu ikachukuwa tena muda mrefu lakini test meter ikafungwa na wakagundua kwamba ni kweli mita  ina matatizo hivyo wakatwambia wataweka mita mpya hapo ilikuwa 2012.

Tukapewa maagizo kwamba wakati suala letu linashughulikiwa tuwe tunalipa angalau TZS 50,000 (elf 50).

Tulianza kulipahiyo elf 50 lakini bado walikuwa wakifika kukata maji wakisema tunadaiwa mamilioni ya pesa na wakishakata inabidi twende tena kwa meneja kujieleza ndipo turudishiwe maji.

25 October, 2012 tulifuatilia Meneja akasema mita ziliwaishia lakini zimeshawasili hivyo Jumatatu 29 October, 2012 watakuja kutubadilishia mita na tutakapopata ankara ya mwezi Novemba 2012 itaonyesha ni kiasi gani tunapaswa kulipa. Ankara ikaendelea kuletwa ikionyesha bado tunadaiwa mamilioni ya pesa (3,789,225.80).

Leo 25 January, 2013 tatizo bado linaendelea na baada ya kuona tumekatiwa maji kwa sababu tunadaiwa 3,789,225.80 (bill ya December 2012)  tumefika Dawasco kinondoni na tumeambiwa kwamba MENEJA AMEBADILISHWAna hayupo hivyo tufike kesho TUKAANZE TENA STORY UPYAAA!!!

Na aliyetupa jibu hilo billing officer nae ni mgeni anasema katika kazi alizokabidhiwa hii ya kwetu haipo.
Kama mteja kwa kweli nimechoka na sielewi nifanye nini maana nimeshakwenda sana kwenye hiyo ofisi lakini hakuna kinachofanyika.
Naomba kufahamishwa nifanye nini?? kwa sababu mpaka sasa sijui haswa napaswa kulipa kiasi gani ?? na pia wanapokuja kukata maji wananisumbua kwa sababu tatizo sio kulipa bali kama mteja nina haki ya kujua matumizi yangu halisi ni kiasi gani (najua haifikii hiyo elf 50)

Asante
Mdau Kinondoni

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>