Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

yale yaleee.....

$
0
0
Michuzi,

Mimi ni mdau wa blog hii tangu imefunguliwa nataka nipeleke ujumbe kwa wadau wote pale geti la kuingilia standi ya ubungo ni hatari sana kuna vibaka amabao ukiingia umebeba mizingo hasa miwili lazima wakusachi na watatimiza azma yao. Ngoja niwape kisa changu cha kusikitisha sana: Weekend iliyopita nikitokea dar kuja Arusha nilifika pale na bajaj mishale ya saa 12 kasorobo.

Hapa vibaka wanasoma kila anayeingia. Nililipa bajaji na kurudishiwa chenji nikafunga mfuko wangu wa nyuma vizuri nikaaza kuhangahika na mizingo yangu. Kumfikia anayekagua tiketi lilikuwa ni kosa nikahisi kupapaswa makalio kucheki mfuko umeshafunguliwa na pesa inachungulia niligeuka ghafla kijana aliyekuwa nyuma yangu akema kwa uungwana sana " angalia mzee kuwa makini" nikamwangalia anayekagua tiketi nikaona yupo attention anasikiliza nikawa na amani nikamwamini kijana na nikafunga mfuko wangu vizuri kabisa kwani wakati huo nikahisi kwamba labda nilisahau kufunga mfuko wakati natoa nauli ya bajaj nikaendelea mbele mara mtu (mmoja watu kwenye hiyo foleni) akaniambia kama kwa kunisaidia; pitia mlango wa kushoto; nikijaribu huku nasukumana na mizingo yangu mlango hauzunguki kufungua.

Mara sauti nyingine ikatoka nahisi hii ni ya mkaguzi pitia gei la mkono wa kulia.Kweli nikapita kiulaini kabisa. Kabla sijapiga hatua mbili mbele nikakumbuka je mfuko wangu bado uko salama? salaleeeeeeee! pesa yangu yote 155,000/= imeondoka!Baada ya kuomba wasamalia waiangalizie mizigo yangu nihangahike kutafuta hela ya nauli tena nilirudi pale geti nikwambia wamba nyie kama waangalizi wa hapa mmehusika kuibiwa hela zangu akanijibu...

kama uliona mfuko wa nyuma umefunguliwa kwanini usibadilishe mfuko mwingine nikagundua kuwa kumbe mechi yote jamaa alikuwa naishuhudia.

Wadau kaeni chonjo na hapo mlangoni usithubutu weka pochi au pesa mfuko wa nyuma na mbaya zaidi ukitoa nauli wanakuwa wanakuchora.Wakaguzi wa tiketi ubungo bus stand wanashirikiana na wezi.

Wako mdau,

Emma Kanindo
Arusha.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>