Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

POLISI MKOANI TABORA WAKABIDHIWA PIKIPIKI

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,ACP ANTHONY RUTHA akikabidhi pikipiki kwa mkaguzi msaidizi wa Polisi,Joseph Matui kwa niaba ya maafisa wote wa Polisi ngazi ya Tarafa Mkoani humo.

Na Juma Kapipi- Tabora

Jeshi la polisi mkoani Tabora limepokea pikipiki 13 kutoka kwa Inspekta Jenerali Said Mwema zitakazosaidia harakati za kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika mkoa huo.

Akikabidhi pikipiki hizo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, ACP Anthon Rutha amesema kuwa,pikipiki hizo zitagawiwa kwa wakaguzi wa kila tarafa wa wilaya za Igunga ,Uyui,Urambo ,Sikonge,Nzega na Tabora mjini kwa lengo la kusaidia ulinzi na usalama wa wananchi.

Kamanda huyo wa polisi wa mkoa wa Tabora ametoa wito kwa wakaguzi wa kila tarafa kuzitumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na si kuzitumia kwa matumizi binafsi na kuwataka wazitunze vizuri kwani kwa kufanya hivyo , kunaweza kusaidia kudhibit uhalifu kwa wakati na kuimarsha amani mkoani hapa.

Akipokea pikipiki hizo kwa niaba ya wakaguzi wa tarafa mkoani hapa mkaguzi msaidizi wa polisi Joseph Matui wa tarafa ya Tabora kaskazini amesema kuwa, pikipiki hizo zitawasaidia kufika maeneo ambayo wananchi wanahitaji kujua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na juu ya ulinzi na usalama wa mali zao.

Matui amewataka wananchi kuonesha ushirikiano wa dhati kwa askari polisi kuwafichua waharifu wanaosumbua katika maeneo yao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>