Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akitoa salamu zake kwenye hafla ya Usiku wa Tarangire iliyokuwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani na pia kumuaga aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire Ndg. Martin Laiboki ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uhifadhi na Ekolojia TANAPA Makao Makuu, hafla hiyo ilifanyika katika Hifadhi ya Tarangire.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwilo (wa pili kulia) akimkabidhi Kamba Ndg. Martin Laiboki kama ishara ya zawadi ya Ng’ombe aliyozawadiwa na Uongozi na Wafanyakazi wa Hifadhi ya Tarangire kwenye hafla ya jioni ya kumuaga baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uhifadhi na Ekolojia TANAPA Makao Makuu, awali Ndg. Laiboki alikuwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire.
Mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia Nyoshi El – Saadat (katikati) akifungua Champaign kwenye hafla ya Usiku wa Tarangire iliyofanyika hifadhini hapo ambapo Bendi hiyo FM Academia ilitumbuiza na pia iliimba kibao maalumu kinachohamasisha utalii wa ndani kwa watanzania.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba/miwani), Mkuu wa Mkoa Manyara Elaston Mbwilo (kulia kwa Dr. Nchimbi) Uongozi na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Tarangire wakiserebuka kwa muziki wa Bendi ya FM Academia wakati wa hafla ya Usiku wa Tarangire iliyofanyika hifadhini hapo.
Wanamuziki wa Bendi ya FM Academia wakionesha vitu vyao wakati wa Hafla ya usiku wa Tarangire iliyofanyika kwenye hifadhi hiyo ya Taifa.