Mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa jengo la Uhuru Heights,Balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Tajammul Altaf akizungumza katika uzinduzi huo ambapo amasema amefurahishwa na jitihada zilizofanywa na mfanyabiashara kutoka nchini kwake na jinsi Tanzania ilivyoweza kumpa ushirikiano na hatimaye sasa matunda yameonekana kwa kuzaliwa jengo la Uhuru Heights lenye hadi ya Kimataifa.Aidha amesema huo ni mwanzo tu na kuwataka wafanyabiashara zaidi kutoka Pakistan kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu mahali ambapo ukiwekeza matunda yanaonekana kutokana na amani na utulivu uliopo na ushirikiano wa serikali.
Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights, Muhammad Owasi Pardesi akizungumza na wageni wakati wa uzinduzi wa jengo hilo na kutoa shukrani zake akisema sasa wakazi wa Dar es Salaam wataweza kununua nyumba kwa njia ya mkopo kutoka Benki ya International Commercial (ICB) na kulipa kwa muda wa miaka 10 na kuishi katika miongoni mwa majengo marefu ya makazi yaliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam lililojengwa kwa gharama ya Dola za Kimarekani Bilioni 40.
Amesema Malengo ya kampuni ya Cosmos Group ni kuboresha miundo mbinu na maisha ya watu na hayo yamezingatiwa kwa kujenga jengo la Uhuru Heights.
Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya EXIM Anthony Grant (kushoto) ikiwa ni ishara ya kuingia mkataba wa kufanya biashara pamoja baina ya Cosmos, IBC Benki na Exim.
MC katika uzinduzi wa Jengo la Uhuru Hegihts Taji Liundi.
Muonekano wa Jengo la Uhuru Heights lililopo barabara ya Bibi Titi Mohammed liking'arisha jiji la Dar nyakati za usiku.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
MC katika uzinduzi wa Jengo la Uhuru Hegihts Taji Liundi.
Muonekano wa Jengo la Uhuru Heights lililopo barabara ya Bibi Titi Mohammed liking'arisha jiji la Dar nyakati za usiku.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI