Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115013

MASHINDANO YA KOMBE LA MEYA KINONDONI YAFUNGULIWA RASMI, MIKOCHENI WALALA 3-1 DHIDI YA KAWE

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akiwakagua wachezaji wa timu ya Mikocheni Warriors na wachezaji wa timu ya Kawe Kombaini wakati wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Meya, Manispaa ya Kinondoni,jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meya wa Manispaa hiyo,Mh. Yusuph Mwenda.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yusuph Mwenda (kushoto) akimwongoza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara (katikati), Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Fortunatus Fwema na viongozi wengine mara baada ya ukaguzi wa timu.
Golikipa wa Kawe Kombaini Simon Adamu akiudaka mpira huku wachezaji wa timu ya Mikochezni Warriors wakijiandaa kupiga goli. Kawe ilishinda magoli 3-1.
Mshambuliaji wa Kawe Kombaini, Hassan Ngonyani (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka beki Ally Ramadhan wa Mikocheni Warriors wakati wa mechi ya ufunguzi ya Kombe la Meya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kawe walishinda kwa magoli 3-1.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akihutubia wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo. Kulia kwake ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordna Rugimbana (kuhoto kwake) na Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Songoro Mnyonge (kushoto).
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara (kulia) akibadilishana mawazo na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda wakati wa ufunguzi wa michuano ya kombe la Meya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na vyombo vya habari wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115013

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>