Wanachama wa timu ya Yanga kutoka sehemu mbalimbali wakitawanyika nje ya jengo la bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar mapema leo mchana mara baada ya kumalizika mkutano wao mkuu wa Mwaka,ambao kwa hakika umefanikiwa kwa kiasi kikubwa,Mkutano huo uliratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ya jijini Dar na kurushwa Live kupitia Clouds TV,aidha Mkutano huo ulionekana kunoga zaidi kufuatia timu hiyo ya Yanga kuifumua timu ya Black Leopards ya nchini Afrika kusini katika mechi yao ya kirafiki iliyofanyika hapo jana kwenye Uwanja wa Taifa bao 3-2.
Mwenyekiti Mpya wa Club ya Yanga Africans,Yusuf Manji akifafanua mambo mbalimbali kwenye mkutano huo,uliochanganua mambo mbalimbali zikiwemo changamoto za timu hiyo,maendeleo yao mbalimbali ikiwemo samabamba na ujenzi wa kiwanja kikubwa cha mpira maeneo ya Jangwani,jijini dar,Sahihisho la katiba yao,masuala mbalimbali ya yanayohusiana na wanachama wao,ustawi wa wanachama wao,mikataba baina yao na wadhamini wao na mambo mengine mbalimbali.
Sehemu ya meza kuu ya mkutano huo ilivyokuwa.
Makamu mwenyekiti wa timu ya Yanga,Clement Sanga akitolea ufafanuzi moja ya jambo lililoulizwa na wajumbe wa mkutano huo.
Pichani kulia ni mchezaji wa timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa akipeana mkono wa shukurani na Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mchezaji aliyedumu Yanga kwa muda mrefu miongoni mwa wachezaji waliopo hivi sasa,hivyo alizawadiwa barua ya shukurani na kitita cha shilingi milioni moja.
Pichani ni baadhi ya Wanachama wa Yanga waliofurika kwa wingi ndani ya mkutano mkuu wa timu hiyo uliofanyika ndani ya bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi na kumalizika mapema jioni ya leo.
Msanii mahiri wa kizazi kipya sambamba na wasanii wenzake kutoka THT wakitumbuiza kwenye mkutano huo.
Mtangazaji machachari wa kipindi cha michezo,Clouds FM/TV Mbwiga Mbwiguke akiwaweka sawa wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wao mkuu wa Mwaka.Picha zaidi bofya Jiachie Blog.