Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

MAFUNZO YA KUTOA MAONI KWA WANAWAKE WALEMAVU YATOLEWA ZANZIBAR

$
0
0
MRATIBU wa Mradi wa kuimarisha ushiriki wa Wanawake wenye ulemavu katika kutoa maoni ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Bi. Mwandawa Khamis Mohd,akifungua mafunzo ya siku tatu ya Katiba kwa wanawake wenye ulemavu Zanzibar,kwa ajili ya kua tayari kutoa maoni katika Tume ya Taifa ya kukusanya maoni ya katiba ya Tanzania.kushoto ni Mwantatu Mbaraka Khamis na mwasilishaji kutoka ofisi ya Mwanasheria kutoka Dar es Salaam Jasani Akhamad Bungala.
MUWEZESHAJI Jasani Akhamad Bungala ambae ni Mwanasheria akionesha Katiba ya Tanzania wakati wa mafunzo kwa wanawake walemavu Zanzibar.
VIJANA wanaotoa tafsri ya lugha za alama kwa Viziwi,wakiwatafsiria wanawake wenye ulemavu mbalimbali,wakati wa mafunzo ya siku tatu kujua katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzani,mafunzo hayo yalifanyika ukumbi wa Jumuia ya watu wenye ulemavu Zanzibar,kwa ajili ya kushiriki kikamilifu wakati wa kutoa maoni kwenye tume ya kupokea maoni ya katiba mpya Tanzani.
BI Saada Hamad ambae NI MTAALAMU WA KUTOA TAFSIRI ZA ALAMA za Ishara kwa walemavu akimtafsiria kiziwi Salma Rajab katika mafunzo ya KATIBA kwa wajumbe wanawake wenye ulemavu.Picha na Abdallah Masangu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>