Mahmoud Ahmad - Globu ya Jamii,Arusha
Kauli mbiu ya kongamano la ulimwengu la Afya ya uzazi linaloendelea jijini hapa imepewa msisitizo na kuwa hakuna mama atakayekufa wakati akileta kiumbe duniani na pia Afya ya mama na mtoto ipewe kipaumbele.
Kauli hiyo imeendelea kutolewa na mke wa raisi mama Salma Kikwete wakati akiwasilisha na kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo jijini hapa na kuwataka watafiti na wataalamu hao kuja na majibu yatakayosaidia kupunguza vifo vya wamama wakati wa kujifungua.
Mama kikwete alisema kuwa takwimu zinaonyesha kupungua kwa kiasi kidogo tatizo la kujifungua na kupoteza maisha hapa nchini na kuwataka wataalamu humu nchini kuchukuwa uzoefu walioupata kuchangia kupunguza vifo vya wamama wakati wa kujifungua sanjari na watoto huku wajawazito zaidi ya 459 hufa kila mwaka wakati wakijifungua.
“Asilimia 90% ya nchi zilizoendelea wanaweza kupunguza ama kuokoa maisha ya kinamama na watoto huku hapa nchini wakiandaa mpango endelevu wa kuokoa maisha ya wamamawajawazito wakati wa kijifungua na kutoa rai kuwa wamama wasife kwa magonjwa ambayo yanaweza kupatiwa tiba”alisema mama Salma.
Mama Salma alisema kuwa suala la afya ya uzazi liwe mpango endelevu kwa serekali na asasi mbali mbali na kuitaka serekali kulipa kipaumbele suala la afya ya mama na mtoto licha ya majukumu mbali mbali iliyonayo.
Nae naibu waziri wa Afya na maendeleo ya jamii hapa nchini Seif Raishid alisema kuwa serekali kupitia wizara hiyo wameweka kipaumbele suala la mama afya ya uzazi na kuwa hakuna mama atakaeyekufa wakati akiwa analeta kiumbe duniani sanjari na watoto na wamejipanga kuongeza wigo wa kuwafikia wakinamama kwa kuongeza zahanati kuwa karibu na usafiri sanjari na huduma muhimu.
Rashid akwataka watanzania walioshiriki kongamano hilo kutoa uzoefu walioupata kutatua tatizo la afya ya mama na watoto ilikupunguza vifo ambvyo vinawezekana kuepukika kutokana na kukosa eidha huduma muhimu wakati wakujifungua.
Kwa upande wake mkurugenzi wa afya dkt dumilia chalamila alisema kuwa mkutano huo umewashirikisha zaidi ya wataalam na watoa maamuzi zaidi ya 800 kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni wakichangia uzoefu katika kulipatia ufumbuzi suala la afya ya uzazi.