Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ametembelea kambi ya kusaidia watu wenye ulemavu wa kusikia katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam asubuhi hii. Zaidi ya Watanzania 3500 wenye maradhi ya kusikia wanatarajiwa kunufaika kwa huduma ya tiba inayotolewa hiyo Taasisi hiyo ya Starkey Hearing Foundation yenye makao yake jijini Washington nchini Marekani.
Muasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing foundation Bwana Bill Austin Starkey amesema tayari huduma hiyo imeshatolewa katika hospitali ya Seliani mjini Arusha baada ya kutoa huduma hiyo katika miji ya Dar es Salaam na Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Nimefurahishwa sana na kutiwa moyo kwa kazi tuliyoifanya ya kuwahudumia watu na kuwawezesha kusikia ambapo wengine ndiyo wameweza kusikia kwa mara ya kwanza tangu walipozaliwa.Furaha yao ni kitu cha kutia moyo sana katika juhudi zetu.
Madaktari wa kitanzania walioshirikiana nao wamefanya kazi kubwa na nzuri” alisema Bwana Starkey ambaye ameambatana na timu ya wataalamu na watu mashuhuri kutoka nchini Marekani ambao wametoa misaada mbalimbali kugharamia kampeni hiyo.