Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

MOTO MLIMA KILIMANJARO UMEDHIBITIWA

$
0
0
Askari mgambo wakiwa katika eneo la kifunika mlima Kilimanjaro wakiandaa chakula kwa ajili ya watu waliojitokeza kuzima moto katika eneo hilo.
Kundi la asakari mgambo lililopo katika eneo la Kifunika mara baada ya kufanikisha kuzima moto katika eneo hilo.
Sehemu ya eneo lililo athirika na moto mkubwa katika mlima Kilimanjaro.
Maeneo yaliyo athirika na moto mlima kilimanjaro.
Mwakilishi wa globu ya jamii akizungumza na mmoja wa wapagazi katika mlima Kilimanjaro Mathayo Kunkwa kuhusiana na tukio la moto uliozuka mlimani hapo.

Picha na habari na Dixon Busagaga 
wa Globu ya Jamii,  Moshi

JUHUDI za makundi mbalimbali yaliyokuwa yakishiriki katika zoezi la moto uliozuka mapema mwishoni mwa wiki iliyopita na kuteketeza zaidi ya ekari 40 katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro zimefanikiwa baada ya kuudhibiti moto huo sasa kwa asilimia 99%.

Hadi kufikia Juzi makundi hayo wakiwemo askari kutoka chuo cha taaluma ya Polisi cha Moshi (MPA),askari Mgambo kutoka wilaya za Rombo ,Moshi vijijini,Mwanga na Same wakiwemo maafisa kutoka hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) walikuwa wamefanikiwa kuzima moto huo huku kukiwa kumebakia na eneo dogo katika sehemu ya Kifunika.

Kwa takribani siku tano sasa eneo la mlima huo mrefu barani Afrika lilikuwa likiteketea kwa moto huku chanzo chake kikidaiwa kuwa ni shughuli za urinaji haramu wa asali uliokuwa ukifanywa na baadhi ya wananchi katika hifadhi hiyo.

Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA)Erastus Lufunguro katika taarifa yake kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alisema hifadhi ya mlima huo inaendeleza doria kudhibiti visiki vinavyotoa moshi ili usiwake tena.

Aidha mhifadhi Lufunguro alirejea kauli yake kwamba tukio la moto huo ulioteketeza zaidi ya Hekari 40 katika hifadhi yam lima huo,haujaathiri shughuli za watalii kupanda na kushuka katika mlima huo wenye urefu wa Futi 5895 kutoka usawa wa Bahari.

alisema pamoja na kuzimwa kwa moto huo,bado kambi za watu zaidi ya 400 zilizoundwa katika wilaya za Rombo na Moshi kuukabili moto huo,zinaendelea kukagua maeneo yote yaliyokuwa na moto na sasa yanafuka moshi ili kuudhibiti usianze upya.

“Kinachofanyika sasa ni doria za mara kwa mara katika maeneo yote ambayo moto ulikuwa ukiwaka ili kudhibiti iwapo utawaka tena kutokana na upepo mkali katika eneo hilo lililotawaliwa na vichaka na misitu mifupi”alisema Lufunguro.

“Baada ya moto kuripotiwa kuanza katika maeneo ya Amboni, Ushiri, Keryo, Kimori na Shimbi wilayani Rombo mnamo Julai 7, tuliunda kambi tano za Kilema, kifunika, Keryo, Maundi na Ujasiri zenye watu 467 ambao wamefanya kazi kubwa kuuzima moto” aliongeza Lufunguro .

Alisema pamoja na kambi za kuzima moto lakini pia hifadhi hiyo imeweka kambi mbili maalum kwa ajili ya kuhudumia wanaoshiriki zoezi la kuzima moto, ambapo moja ipo eneo la Nanjara wilayani Rombo ambapo ilikuwa na sehemu kubwa ya moto.

Lufunguro alisema kambi nyingine ipo katka eneo la Marangu kwa ajili ya kuhudumia eneo la Kilema juu ambapo zote kwa pamoja zilikuwa na askari mgambo 128 kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro sanjari na askari waliopo mafunzoni katika chuo cha polisi CCP.

Katika hatua nyingie mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Moshi,Ibrahimu Msengi pamoja na viongozi mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa walilazimika kupanda mlima Kilimanjaro hadi kituo cha Horombo kujionea hali halisi ya athari iliyotokana na moto huo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>