Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

TANAPA NA WADAU WAFANIKIWA KUDHIBITI MOTO KILIMANJARO

$
0
0
Shirika la Hifadhi za Taifa linashukuru ushirikiano ilioupata na kufanikiwa kudhibiti moto kwa asilimia 100 hadi sasa uliotokea Mlima Kilimanjaro siku ya Jumapili tarehe 7.7.2013. 

Juhudi mbalimbali zilizofanywa na wananchi pamoja na uongozi wa serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Mkuu wa Mkoa Leonidas Gama, zimeweza kudhibiti na kumaliza moto huo uliodumu kwa siku nne sasa.

Leo tarehe 10.7.2013 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alitembelea eneo la Horombo ambalo ni urefu wa mita 3,700 juu ya usawa wa bahari na kujionea jinsi moto ulivyounguza maeneo mbalimbali ya hifadhi.

Mkuu wa Mkoa akiwa eneo la tukio alitoa agizo kwa viongozi wa wilaya za Moshi na Rombo kushirikiana na TANAPA ili kuweza kubaini wale wote waliohusika na uharibifu huu pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha kuwa vitendo kama hivi havijitokezi mara kwa mara.

Taarifa hii inalenga pia kuujulisha umma kuwa shughuli za utalii zinaendelea vizurikama kawaida na hazikuweza kuathirika na moto huu kama ambavyo tumeshatoa katika taarifa zetu za awali kuwa maeneo wanayopita watalii hayakuathirika na moto huu.

Imetolewa na Idara ya Uhusiano
Hifadhi za Taifa Tanzania
10.07.2013

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>