Na Swahili TV, Washington DC
Chuo Kikuu cha Howard alichokuwa akisoma mtanzania aliyeuawa mjini Washington Dc, marehemu Omary Adam Sykes kinataraji kuuaga mwili wake leo jioni, viongozi mbalimbali akiwemo meya wa jiji la Washington DC Bwana Gray nao wanatarajiwa kuhudhuria.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia Swahili TV shughuli za kumuaga marehemu zitafanyika katika ukumbi wa Andrew Rankin Memorial Chapel ulio katika kona ya 6th Street na Howard place na kufuatiwa sherehe za kukumbuka ya maisha yake zitakazofanyika katika ukum bi wa Blackburn ambao pia uko katika chuo hicho.
Shughuli za kuuaga mwili huo zimepangwa kuanza saa 12 jioni (takriban muda wa masaa mawili na nusu toka sasa kwa saa za Tanzania), ambazo habari hizo zinasema Mstahiki meya Vicent condol Gray atakuwa muongeaji mkuu akishirikia na rais wa chuo hicho Profesa Sidney A. Ribeau. Sherehe hizi pia zitashirikisha familia ya marehemu Omar ambaye baba yake mzazi mze Adam Sykes na baba yake mkubwa waliingia jana wakitokea nchini Tanzania.
Si jambo la kawaida kwa Meya wa jiji kubwa la Washington kuhudhuria sherehe za kuuga mwili, wachambuzi wa mambo ya siasa za Washington Dc wanasema hali hiyo huenda inatokana na umaarufu wa chuo hicho na mstuko mkubwa wa mauaji ya mwanafunzi huyo ambayo yamelistua jiji la Washington DC, ambalo licha ya kuwa na matukio ya mauaji ya hapa na pale lakini eneo la chuo hicho limekuwa salama kwa miaka mingi.
Taarifa ya chuo kwa Swahili TV inasema,Uongozi wa chuo uliamua kuanzisha mfuko maalum utakaosaidia wananchi mbalimbali wasio na uwezo kulipia ada zao, mfuko utatambulika kama Omar Scholarship Fund na tayari watu kadhaa wameshaanza kuchangia.Taarifa za namna ya sifa na uwasilisha wa maombi zitatangazwa baadaye.
Swahili TV itakuwepo katika shughuli za kuuaga mwili ili kukuletea habari za kina na uhakika.
Stay tuned for Exclusive story at www. swahilitv.blogspot.com