Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

mbunge viti maalum ccm,Mh.Ritta Kabati apongezwa mkoani iringa kwa kuisaidia jamii.

$
0
0
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati akizungumza jambo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,Bwa. Athumani Mungi,mara Mbunge huyo alipokwenda kutazama maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha polisi kinachojengwa na Mbunge huyo,kilichopo maeneo ya Tumaini.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,Bwa. Athumani Mungi akipata maalezo mafupi kuhusiana na ujenzi wa kituo hicho kidogo cha polisi,pichani kati anaeshuhudia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati. 
 Baadhi ya Mafundi wakiendelaea na ujenzi wa kituo hicho kidogo cha polisi
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,Bwa. Athumani Mungi akimuelekeza jambo Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati. 
======  =======  =======

Viongozi mbalimbali mkoani Iringa wamekutana kujadili suala la uboreshaji wa miundombinu (barabara) katika kikao cha bodi ya barabara kwa kushirikiana na mamlaka ya barabara TANROADS mkoa wa Iringa akiwemo mkuu wa mkoa Dr.Christine Ishengoma ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho.

Viongozi hao wamefikia maadhimio kadhaa ili kuongeza ufanisi na ukarabati wa barabara katika mkoa wa iringa ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira na usafi,ikiwemo na kupitisha sheria ya kukaguliwa kwa magari yasiyokuwa na vyombo maalum kwa ajili ya utupaji taka na gari yoyote itakayokamatwa ikiwa haina kifaa hicho itachukuliwa hatua ili kuwa fundisho kwa wengine,.

Sambamba na hilo vingozi hao wamempongeza Mh.Ritta Kabati kwa kuwawakilisha vyema wanawake na wananchi wa mkoa wa Iringa hasa katika kupigania maendeleo ya mkoa,miongoni mwa mambo ambayo amekuwa akiyapigania ni pamoja na Ukarabati wa miundombinu,elimu pamoja na Benki ya akina mama iliyoko Dar es Salam pekee ikiwa ni benki ya akina mama wote nchini, hivyo amewataka viongozi wanaohusika na benki hiyo kuifikisha katika mkoa wa Iringa ili hata akina mama wa mkoa huo waweze kunufaika,



 kutokana na kilio cha wanachi wa maeneo ya Tumaini,Semtema na maeneo jirani kudai kituo kidogo cha Polisi ,Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati amejitolea kujenga kituo cha Polisi katika maeneo hayo ili kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo waliokuwa wakionelewa na watu wasio wema, hivyo amesema kituo hicho kitaweza kusaidia kupunguza idadi ya uharifu katika maeneo hayo kwani kituo hicho ni moja kati ya vituo vingi vinavyohitajika mkoani ha Iringa.



Akimuonesha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw.Athumani Mungi Mh.Kabati amemhakikishia kamanda kuwa ujenzi huo utakamilika mapema iwezekanavyo ili kuepusha adha kwa wananchi wa maeneo hayo.
Kwa upande wake kamanda wa Polisi mkoani Iringa,amempongeza Mbunge huyo kwa moyo wake wa kujitolea katika mambo ya jamii ambapo amesema Jeshi la Polisi linapenda kushirikiana na wadau wanaounga mikono jitihada za jeshi hilo katika kuboresha amani nchini huku akitoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo kwa umoja ni nguvu utengano ni Udhaifi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles