Meya wa jiji la Mwanza (pili shoto),Mh.Stanslaus Mabula akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu walioibuka katika mashindano ya kucheza,kwenye tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lililokuwa likifanyika kwa wiki nzima kwenye uwanja wa Nyamagana,jijini Mwanza.Mshindi wa kwanza pichani kati ni Laulencia Francis aliyejinyakulia kitita cha sh laki 2,Mshindi wa pilia ni Victoria Pascal (kwanza kulia) aliyeibuka na sh laki moja,na watatu ni Mariam Vincent aliyejinyakulia shilingi elfu hamsini.Pichani nyuma kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo,Mussa Kisoky wakiwa na wadau wengine wa jiji la Mwanza.Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
↧