Mjumbe wa bodi kutoka Faraja Saccos Mafinga Macelina Mkini akiishukuru CRDB kwa mafunzo
|
Afisa ushirika mkoa wa Iringa John Kiteve
Na Francis Godwin WAJUMBE wa bodi za asasi za kifedha mkoani Iringa wameipongeza benk ya CRDB nchini Tanzania kwa kuanzisha utaratibu mzuri wa kutoa elimu kwa wajumbe wa bodi za asas za kifedha . i Pongezi hizo zimetolewa na wajumbe hao na mwakilishi kutoka faraja Saccos mjini Mafinga wilaya ya Mufindi Bi Macelina Mkini wakati akizungumza kwa niaba ya wajumbe wengine.
Amesema kuwa hatua ya CRDB nchini kuendelea kuzijali asasi za kifedha ni sawa na kuisaidia serikali ya Tanzania katika kuwajengea uchumi wananchi kupitia asasi za kifedha.
Hivyo alisema kati ya benk zote nchi ni CRDB pekee ambayo imeendelea kuwasaidia wanachama wa Asasi za kifedha vijijini jambo ambalo wao wanalipongeza zaidi.
Kwa upande wake afisa ushirika mkoa wa Iringa John Kiteve alisema kuwa mbali ya kuwapongeza CRDB kwa jitihada hizo ila bado yeye kama afisa ushirika hatawavumilia viongozi wazembe ambao wataonyesha kukwamisha ushirika mkoani Iringa .
Aliwataka viongozi wa asasi za kifedha mkoani Iringa na Mbeya kuendelea kujifunza namna ya utunzaji wa fedha za wanachama na iwapo hawatajifunza kwenda kisasa wanaweza kuyumba katika utunzaji wa fedha za wanachama.
Alisema kuwa suala la ubunifu na kujituma kwa wanachama ni mwanzo wa Asasi hizo kufanikiwa zaidi na kuwataka viongozi kuepuka kukata tamaa katika kuziendesha asasi hizo.
Hata hivyo amewataka wajumbe wa bodi za asasi za kifedha kuwa makini na matumizi ya fedha za wanachama na kuepuka kukimbilia maisha ya juu kupitia fedha za wanachama.
Alisema kuwa suala la uaminifu linahitajika zaidi kwa viongozi ikiwa ni pamnoja na viongozi hao kuendelea kujifunza na kutoa mafunzo kwa wanachama wake ili kuwajengea uwezo zaidi.
Kiteve aliwataka viongozi wa Asasi za kifedha kujenga utamaduni wa kujitegemea zaidi ili siku ambayo CRDB itasitisha mpango huo wa kuziwezesha Asasi hizo kuweza kusimama wenyewe kwa miguu yao. |