Mahmoud Ahmad Arusha
MTU mmoja anaedaiwa kuwa ni Jambazi afariki katika majibishano ya silaha na polisi katika tukio tofauti la kujibishana risasi na askari wa jeshi la polisi baada ya kumfyatulia askari risasi na kumkosa huko maeneo ya Sokon 1 jijini hapa jana majira ya jioni.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani hapa Kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa mnamo majira ya saa11;15 huko mtaa wa Onjaftian jeshi hilo lilifanikiwa kumuuwa baada ya majibishano ya risasi na askari wa jeshi hilo jambazi sugu aliyefahamika kwa jina la Lembris Taiko au kwa majina mengine doctor mbushii,general mwarusha, mwenye umri wa miaka32-35 mkazi wa sokon 1 jijini hapa.
Kamanda alisema kuwa awali walipata taarifa kwa wasamaria wema kuwa kuna watu3 wanaosadikiwa majambazi na kufuatilia maeneo ya tukio na kuizingira nyumba walipojaribu kuingia ndani na kuwataka watu wote kujisalimisha ghafla risasi zilianza kutoka ndani kupitia ukutani na kumkosa askari hali iliyowalazimu askari kujibu mapigo na kufanikiwa kumuua jambazi huyo.
Sabas alisema kuwa uchunguzi uliofanya na askari wa jeshi hilo umebaini kuwa ni jambazi sugu huyo alikuwa akitafuta na jeshi hilo na akishiriki kwenye matukio ya ujambazi maeneo mbali mbali ikiwemo Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam na alikutwa akiwa na bastola mmoja,aina ya bereta iliyofutwa namba risasi moja chemba,ganda moja la risasi iliyofyatuliwa,risasi 3za bunduki aina ya shortgun,na funguo mbali mbali 26 na mordem ya kampuni ya Airtel.
“Jambazi huyu alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi letu kwa kushiriki kwenye matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha za moto tukio ambalo lilitokea28\08\2012 huko maeneo ya olasiti jijini hapa ambapo walipora bastola yenye no.T0620-11J00491 aina ya tisas”alisema kamada sabas.
Katika tukio lingine jambazi huyo alijeruhiwa mguuni akafaniwa kutoroka lakini jeshi la polisi lilifanikiwa kumua jambazi aliefahamika kwa jina la peter Toshi katika majibizano hayo jambazi huyo alikutwa na bastola aina tisas inayoaminiwa kuwa ndio ilioporwa ikiwa imefutwa namba zake.
Kamanda sabas alisema kuwa kutoka eneo la tukio anabainisha kuwa mmiliki wa nyumba aliokuwa jambazi huyo anaefahamika kwa jina moja la Swalehe au baba Amiri ambaye hakuwepo wakati wa tukio hili jitihada za kumtafuta zinafanyika ili aweza kuhojiwa juu ya uhusiano wao na jambazi aliyeuwa na wapangaji wengine kwenye nyumba hiyo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.
Hata hivyo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount meru kwa uchunguzi zaidi na juhudi za kuasaka majmbazi wengine badao zinaendelea kufanyika.