Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

HOJA YA MDAU KUHUSIANA NA TATIZO LA USALAMA KIGAMBONI

$
0
0

Naomba kuwasilisha mtazamo wangu juu ya suala la Usalama wa Raia kwa watu wa Kigamboni
 
Kufutatia kitendo cha wanafunzi wa IFM kuandamana na kusimamisha shughul;i za kivuko kwa muda, tatizo hili sasa limepata sura mpya, na limepata kufika kwenye masikio ya watu ambao wamepewa dhamana ya kulinda raia na mali zao. 

Wimbi la uhalifu kigamboni limekuwa kubwa sana na haswa suala la hawa vijana wanaoshinda Beach (Beach Boys) kufanya mambo ambayo kimsingi yangeweza kuzuiliwa na polisi wetu. Tatizo ni "business as usual attitude" kwa askari wetu. 

Tumeshuhudia watalii wakiibiwa vitu vyao na kujeruhiwa vibaya na vijana hawa, tumeshuhudia vijana hawa wakipora mabegi ya wanafunzi, wakiwa na malengo ya kuibia wanafunzi hawa laptop zao. Askari wanafahamau vyema kabisa mambio haya. Ni askari gani wa kigamboni asiyejua kijiwe cha minazi mikinda? 

Bhangi, unga na aina zzote za dawa za kulevya zinuzwa na kutumiwa hapo. Ni askari hawa hawa wanawahi kwenda huko pindi ukitokea uporaji wa vitu hivyo (nimepata kusikia wanawahi mgao!!!????). Sasa leo tunasikia wanafunzi wanavamiwa wakiwa vyumbani mwao, wanaporwa na kudhalilishwa.

 Ni nani asiyejua kuwa ili kuondoa wimbi hili ni lazima kuboresha doria kwenye fukwe hizi za kigamboni? Ni aibu kwa nchi kwa ujumla kufuga kundi kubwa la vijana wala unga nje tu ya uwanja wa Ikulu, pale karibu na soko la samaki? Nje ya ikulu vijana wanavuta unga. Je usalama wa kilometre 1000 kutoka ikulu ilipo ukoje?
 
Maandamano ya wanafunzi Kigamboni yafungue macho ya wahusika kuhusu hali halisi ya usalama kigamboni. Wananchi wa kibada wamepitia kipindi kigumu kiasi kwamba karibu kila mwanannchi aliishia kumiliki silaha, na sio moja kwani hali ilikuwa mbaya kupita kiasi. Walinzi wa Bar wanauwawa, madereva wa taxi wanauwawa. 

Nyumba zinavamiwa kila leo. nk. Tunaona polisi wakipita kufanya doria usiku, lakini basically doria hii hulenga bar ambazo hazijafungwa baada ya saa tano (saa sita weekends). Kweli nguvu hii ya kukamata wahudumu wa bar ikielekezwa kusaka wahalifu hatutapata nafuu ya kiusalama? Nadhani bado tuna nafasi kubwa sana ya kuboresha usalama kabla hali haijawa mbaya. 

Kila wakati polisi wanawakumbusha wananchi kuwa wasichukue sheria mkononi. Tunategemea nini kama wananch wanamawazo kuwa Polisi wanashirikiana na wezi?Unawezajae kuelewa unapoambiwa kuwa wezi walitumia zaidi ya saa mbili ndani ya hostel ya wanafunzi huku wanafunzi wakike wakipiga kelele kuomba msaada?
 
Ndugu zetu polisi, kodi zetu zinapaswa kutulinda, na si kushiriki katika vitendo viovu pamoja na waovu. Wezi wote wa ferry, na haswa hawa beach boys wanajulikana. Shukeni kule chini, fanyeni doria, tumieni mbinu zenu za kiupelelezi mlizofunzwa kwa kodi zetu kuwafichua na kuwafikisha waovu hawa sehemu inayostahili na sio huku mitaani. Huku sisi tunahitaji amani, na tunahitaji kufanya mipango ya maendeleo, na sio kulala na hofu kila siku.
 
Naomba mamlaka zitekeleze wajibu wao wa kikatiba, kulinda maisha ya raia na mali zao. Sio kulinda tu maisha ya watawala kwa misafara mirefu isiyo na sababu wala tija kwa taifa letu.
 
Naomba kuwasilisha

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>