Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudentia Kabaka akiwa katika mazungumzo pamoja na Mke wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza,Bibi Cherie Blair wa Mkutano wao uliofanyika leo jijini Dar.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudentia Kabaka,kulia akimkabidhi zawadi ya kinyago cha kitanzania Bibi Cherie Blair baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu ya Mhe.Waziri wa kazi na Ajira Bibi Gaudentia Kabaka na Bibi Cherie Blair pamoja na maofisa wao walioshiriki katika mazungumzo ya pamoja.
Waziri wa Kazi na Ajira, Bibi Gaudentia Kabaka tarehe 2/07/2013 amekutana na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza Bibi Cherie Blair, katika mazungumzo ya kubadilishana uzoefu yaliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar-es-Salaam.
Katika mazungumzo hayo ,Viongozi hao walijadili changamoto mbali mbali zinazowakabili akina mama wa kitanzania katika kujikwamua kiuchumi. Katika mazungumzo hayo Bibi Cherie Blair ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ijulikanayo kama “Cherie Blair Foundation” alionyesha kuguswa sana na juhudi za kinamama nchini wanajishughulisha na masuala ya ujasiria mali na kujijengea fursa za kujiajiri,kupitia taarifa ya Mhe .Waziri Kabaka iliyoelezea juhudi za kinamama waliopo katika sekta isiyo rasmi.
Kina Mama hao wawili mashuhuri walikubaliana kushirikiana katika nafasi zao kuwasaidia kinamama hao wa Kitanzania.
Wizara ya Kazi na Ajira inahusika na kuratibu masuala ya ajira nchini na inawasaidia Wajasiria mali waliopo katika sekta isiyo rasmi kushiriki na kutangaza bidhaa zao wanazozizalisha kupitia Maonesho
Mashuhuri ya nchi za Afrika Mashariki yajulikanayo kama Nguvukazi/Jua kali, yanayofanyika kila mwaka kwa mzunguko katika nchi wanachama.