Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

MEYA JERRY SILAA AWATAKA WATANZANIA KUTUNZA NA KULINDA AFYA ZAO ILI KUJENGA FAMILIA NA JAMII YENYE AFYA BORA

$
0
0
IMG_2846
Wananchi wa Tanzania wameelezwa kuwa kazi ya kuboresha huduma za afya na afya ya mazingira na maji ni ngumu na kuwa inahitaji nguvu za pamoja kati ya jamii, halimashauri na wadau mbalimbali ili kupata mafanikio yaliyokusudiwa hasa ya uzuiaji wa magonjwa.
Akitoa nasaha wakati wa kufunga wa zoezi la utoaji wa huduma za afya kwa uwiano katika jamii kata ya Gombo la Mboto, Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa, Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala amesema huduma za afya na afya ya mazingira ni muhimu katika maisha ya kila siku ya binadamu.
Ameongeza kwa kuwapongeza sana wakazi wa Gomngo la mboto Markaz pamoja na viongozi wao kwa juhudi kubwa walioifanya katika kuhakikisha uwepo wa kituo cha tiba karibu na jamii na kuwa wanastahili kuwa mfano wa kuigwa na jamii zingine.
Aidha amesema hilo ni moja wapo katika utekelezaji wa agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika lengo lake la kupeleka huduma za tiba zikiwamo zile za zinazohitaji madaktari bingwa karibu na wananchi.
IMG_2798
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dr. Asha Mahita akielezea dhamira ya Idara katika kuendeleza Afya ya Jamii kwa kusogeza Huduma za Afya karibu na Jamii, Huduma hizo zinahusisha matibabu kwa magonjwa mbalimbali kama Magonjwa ya Moyo, Kisukari, Malaria, Macho, Meno, Afya ya Akili, Ushauri na kupima VVU kwa hiari, Elimu juu ya Uzazi wa Mpango na Afya ya Uzazi, Afya ya Mazingira, Lishe, na Jinsia, pia ametoa tathmini ya wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto Markaz waliopatiwa huduma za Afya bure kwa zoezi lililofanyika kwa muda wa siku tatu ikiwemo Afya ya Akili, Kifua Kikuu na matibabu ya Ujumla.
IMG_2869
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akipima Presha wakati wa kufunga zoezi la Utoaji wa Huduma za Afya kwa Uwiano katika jamii ikiwa ni ishara ya kuhamasisha watu kujenga utamaduni wa kupima Afya zao.
IMG_2882
Wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto wakipatiwa dawa za bure baada ya kufanyiwa vipimo wakati wa kutoa Huduma ya Upimaji Afya Bure kwa wakazi wa kata hiyo iliendehshwa kwa siku tatu.
IMG_2900
Mtaalamu wa Magonjwa ya Kisukari kutoka Kituo cha Afya Amana Dkt. Abushiri Rajabu akitoa maelezo kwa Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa kuhusu Elimu anayotoa kwa jamii kuhusiana na Ugonjwa huo.
IMG_2792
wakazi wa Gongo la Mboto wakimsikiliza Diwani wao ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati wa kufunga zoezi la utoaji wa Huduma za Afya kwa Uwiano katika Jamii kata ya Gongo la Mboto.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>