Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

QChilla: Walionishusha walichangia kutumia na madawa ya kulevya

$
0
0
Q Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ilisababishwa na baadhi ya watu kuchangia kumrudisha chini na kujikuta yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipitia.

Huku akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu. Akiongea na Fina Mango kwenye kipindi cha Makutano, Qchilla amesema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha.

Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia madawa hayo.

Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye matumizi hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na kuishika dini.

Pia aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia alikuwa aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama aliemsaidia marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.

Q Chilla amesema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa zaidi akiwatolea mfano PSquare na kusema tatizo la wanamuziki wengi kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani tu na kumalizia hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa nyimbo kali.

Kusikiliza au Ku-download mahojiano yote na Qchilla bofya hapa: https://soundcloud.com/makutano-na-fina-mango/makutano-show-mahojiano-na-1
QChilla akiongea katika kipindi cha Makutano Magic FM
Fina Mango akimsikiliza QChilla wakati akijibu moja ya maswali katika kipindi.
Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango akiwa na QChilla na mwanae Nuru baada ya kipindi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>