Kaka issa
Heri ya Mwaka mpya 2013, Naomba kuwakilisha maoni yangu kuhusu hili la wizi wa fedha kwa kutimia mtandao
Kwa muda sasa wa wiki nzima, tumekuwa tukisoma kwenye vombo vya habari wizi wa fedha kwa mtandao au kwa kutumia kadi zinazotolewa na Bank, za ATM Card, Mastercard ama Visa. Kusema ukweli hili suala sijui kama benki za Kitanzania zinaichukua kwa umuhimu uliyonao, ni Hatari kuliko wanavyoichukulia.
Ukweli ni kwamba Benki pekee haziwezi kuhimili mapambano ya Cybercrime, kama kweli tunaelewa na kutambua kwa undani ukubwa wa hili tatizo. Mfano, katikati ya Mwaka 2012, Banki zote Marekani ziliwekwa kwenye ‘high alert’ na vyombo vya usalama kuwa kuna wahalifu wa kimtandao ambao walikuwa wakitaka kuiba fedha kwenye account za wateja wao. Kazi hiyo ilifanywa kwanza na FBI kuitercept uhalifu huo, kabla benki kuchukua hatua.
Hivi ni vita ambavyo vinapiganwa na vyombo vya usalama vya nchi. Cybercrime ni kubwa kuliko mabenki wanavyoifikiria, mwaka jana peke yake, wahalifu wa kimtandao walijaribu kuiba Paundi 2.5 Billion kutoka mabenki mbalimbali Ulaya peke yake achilia nchi zingine kama Asia na America. Ni vita ambavyo Tanzania peke yake hawawezi kuvipigania. Wakati Viongozi wetu wakifanya vikao vya kutaka kuwa kuwadhibit M23, hiyo kazi waichie drones za Obama, na waanze kupambana na Cybercrime ambayo miaka 20 ijayo itatufanya turudi kwenye ukoloni kwasababu tutakuwa tukiwategemea wazungu kutusaidia katika hivo vita.
Elimu ya usalama wa fedha za wateja unahitajika sana tena sana miongoni mwa wafanya kazi wa benki zetu. Usalama wa Banking System pia benki wanatakiwa kuangalia. Mfano, haiwezekani computer ya banki ambayo mfanyakazi wa benki hutumia kuangalia account za wateja, na akimaliza anaingi facebook kuchat. Mara nyingi mtu unaweza kuforwadiwa email ilikwisha pelekwa kwa zaidi ya watu Elfu na ukiangalia imetoka wapi usishangae ukaona john.idd@benkifulani.com. Huwezi kuingia kwenye website yoyote kwa kutumia mtandao wa Benki.
Kuna websites ambazo kazi zake ni kuwapatia hawa wahalifu taarifa zote za kila computer itakayoingia kwenye hiyo website. Benki zetu waache ubahiri waanze kuinvest kwenye security technology, na lazima wawe na cyberwatch team masaa 24 siku saba kwa wiki.
Mambo mengine ni uzembe wa mawazo na kwasababu ajira ni kwa kujuana inakuwa ngumu sana kudhibiti matatizo kwenye mabenki zetu kwasababu hatujui wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye maeneo nyeti kama haya wana uaminifu kiasi gani kwa pesa za wateja wao. Na inawekana hatuna huduma ya 'security clearance' kwenye kazi yenye kuhitaji uaminifu wa kiwango hiki.
Naomba kuwakilisha kaka.
Mdau US